Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amewatoa hofu watanzania kuhusiana na kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya viongozi wa siasa kuhusu mkataba wa bandari unaotarajiwa kupitishwa na wabunge.
Msukuma ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kilimani jijini Dodoma.
"Nataka niwaambie watanzania mimi nilienda dubai tulifanya ziara ya siku 9 kiukweli wao wameendelea kuliko sisi,sasa tumepata hii fursa tunaanza kuponda,tunaanza kutukana hii sio sawa na hao wanaotangaza mitandaoni walishiriki kufanya maovu huko nyuma" Amesema Msukuma.
Aidha amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono serikali yao na wabunge kuendelea kuchakata na kupitisha na kama kuna mapungufu yakasimame kwenye mkataba wenyewe.
"Hakuna mradi mkubwa uliotengenezwa hapa Tanzania bila kuwa na makelele,wenzetu dubai wanategemea bandari na airport,tunahitaji kutafuta watu wenye uwezo na kuendesha hivi vitu mfano mzuri ukilinganisha bandari ya dar es salaam na wenzetu jirani Kenya bandari ya mombasa utaona kabisa utofauti mkubwa hivyo wananchi wanapaswa kuangalia suala hili kwa manufaa ya vizazi vijavyo" Amesisitiza Msukuma.
Aidha amesema ataendelea kupambana na wanaoendelea kuiponda serikali na kusambaza uzushi kwenye mitandao ya kijamii na kuamua kutengeza uongo na kuzua taharuki kwa watanzania na wengine kudai amehongwa ili kutumika kwenye sakata hili la bandari.
"Naomba niwaonye wale wote wanaoendelea kusambaza maneno kwenye mitandao ya kijamiii na hao baadhi ya wanasiasa wanaosema nimehongwa ili kutetea hili suala niwaambie tu mimi nimeanza kumiliki magari na vitu vya thamani kabla hata sijawa mbunge na serikali inapoleta jambo zuri siwezi kupingana nalo haswa ukizingatia suala la bandari nilienda mwenyewe dubai nikashuhudia hivyo wasinichokoze kwani nina mengi sana yakuzungumza lakini nimeamua kukaa kimya lakini wakitaka nizungumze nitazungumza tu maana sina cha kuogopa na kwenye ukweli lazima tuseme ukweli hii nchi ina wasome wengi ambao wamekaririshwa badala yake wanashindwa kuchanganua mambo hivyo ningewaomba wasomi wanchi kutumia elimu zao vizuri na sio kupotosha watanzania"
Ameongeza kuwa kwa upande wake amesoma mkataba huo na hajaona sehemu iliyoandikwa miaka 100 na kama ni miaka 100 ina maana Rais Dkt.Samia Suluh Hassan yuko tayari watanzania wateseke ilihali yeye mwenyewe baada ya kumaliza urais anakuwa mtanzania wakawaida,hivyo amewataka watanzania kuchambua na kuelewa mambo na sio kumezeshwa sumu na baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao hawana maslahi na taifa hili.
Aidha amesema kuwa anaiomba serikali kama waliweza kuwapeleka wabunge zaidi ya 60 basi waangalie namna ya kuwapeleka waandishi 100 kutoka sehemu tofauti tofauti Tanzania nzima ili kwenda kushuhudia na kuja kuwa mashahidi kwa watanzania.
0 Comments:
Post a Comment