Subscribe Us

WAZIRI MKUU AMEWATAKA MAWAKILI WOTE KUFANYA KAZI KWA BIDII.

 Na Moreen Rojas,
Dodoma.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka mawakili wote wa serikali kufanya kazi kwa bidii pamoja na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia kanuni ili kuepuka migogoro.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa  mawakili wa serikali ikiwa ni maadhimisho ya miaka 5 ya ofisi ya wakili mkuu wa serikali yaliyofanyika katika ukumbi wa jakaya convention jijini Dodoma.

Aidha amezitaka taasisi zote za serikali kutoa ushirikiano kwa ofisi ya wakili mkuu wa serikali.

"Hakikisheni mfumo wa kieletronic unatumika ili kuhakikisha serikali inaimarisha sekta ya uchumi"

"Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ofisi hii na kutoa ushirikiano hivyo wakili mkuu wa serikali kaa mkao wa kula kwani serikali iko nyuma yenu kuhakukisha kila kitu kinakuwa sawa"Amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.

Kwa upande wake Waziri wa katiba na sheria Dkt.Damas Ndumbaro amesema ofisi ya wakili mkuu wa serikali kwa miaka 5 wameweza kumaliza mashauri mengi kwa njia ya ushuluhishi pamoja na amani na kufanikiwa kuokoa fedha ambazo serikali ingelazimika kulipa na ingeshindwa katika kesi hiyo.

"Mashauri 65 na kwa usuluhishi mashauri 7 na katika mashauri hayo yote tumeweza kuikolea serikali shilingi Trilioni 7.5"Amesema Dkt.Ndumbaro

Naye Wakili Mkuu wa Serikali Boniphace Luhende  amesema mafunzo hayo yataleta uandaaji wa mikataba pamoja na utatuzi wa migogoro mbalimbali.



Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeongeza uwanda wa utoaji huduma katika mikoa 17 kwa kufungua ofisi za masijala.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali,Tulipotoka,Tulipo na Tunapoelekea".


0 Comments:

Post a Comment