Subscribe Us

WAZIRI UMMY AMETOA WITO KWA MADAKTARI BIGWA UPASUAJI KUFANYA KAZI MIKOA YOTE.

 Na Moreen Rojas,
Dodoma.



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa wito kwa madaktari bigwa  upasuaji kufanya kazi mikoa yote na kuhakikisha wanazalisha wataalamu wazuri kwani kuna uhaba wa madaktari bigwa wa upasuaji nchini.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa mkutano wa mwaka na kongamano la kisayansi linalohusisha chama cha madaktari wa upasuaji Tanzania lililofanyika St.Gasper Hotel jijini Dodoma.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wakati umefika wa madaktari kupangiwa vituo vya chini vya afya huku akihimiza kuwa hospitali kubwa za rufaa zisiwe sehemu za kuanzia ajira.

"Ningependa kuwashauri na kuwahimiza madaktari bigwa wa upasuaji kuanzia chini kabisa na sio kukimbilia hospitali za rufaa kwani huku chini ndio tuna wananchi wenye uhitaji zaidi kwani tumeshuhudia baada ya wananchi kukosa huduma hizi ndipo huamua kwenda hospitali za rufaa hivyo ningewaomba muanzie huku chini na sisi kama serikali tupo tayari kutoa ushirikiano pale mnapotuhitaji" Amesisitiza Waziri Ummy.

Aidha ameongeza kuwa kuhusu suala la kusambaza madaktari bigwa wa upasuaji mikoani watafatilia kazi na kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyakazi.

Kwa upande wake rais wa Chama cha madaktari bigwa wa upasuaji Tanzania Prof.Larry Akoko amesema kuwa wakati umefika serikali kuangalia namna ya kuboresha mikataba pamoja na kuipa kipaumbele tasnia ya udaktari pamoja na kusisitiza masuala ya maadili kwenye kazi  kwa sababu wamekuwa wakiletewa malalamiko mengi.

Kauli mbiu ya mkutano na kongamano hilo la chama cha madaktari bigwa wa upasuaji Tanzania (TSA) ni kujenga mfumo wa utoaji huduma za upasuaji madhubuti unaofikika na wenye gharama nafuu Tanzania.




0 Comments:

Post a Comment