NA WAF, BUNGENI DODOMA.
NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha juhudi zinazofanywa na Wizara ya Afya katika mapambano dhidi ya changamoto ya utoaji mimba usio salama ikiwemo, kutoa elimu juu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike ambao wapo chini ya umri wa kuzaa.
Dkt. Mollel amesema hayo leo Juni 2, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Judith Salvio Kapinga katika Bunge la kumi na mbili Mkutano wa kumi na moja kikao cha 39, Jijini Dodoma.
Ameendelea kusema, Wizara kupitia vitengo vyake imeendelea kutoa elimu kwa klabu za vijana na vijana balehe kutojihusisha na ngono zembe (abstinence) ili kuepuka kupata mimba zisizotarajiwa ambazo hupelekea kuongezeka vitendo vya utoaji mimba usio salama.
Aidha, Dkt. Mollel amesema, Wizara inaendelea kusimamia utoaji wa huduma za uzazi wa mpango katika vituo vya huduma bila malipo ili kuwawezesha wanawake na wanaume kuzuia mimba zisizotarajiwa.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, ametoa wito kwa jamii kuhakikisha mimba zote zinapatikana kwa mpango ili kuondokana na changamoto ya utoaji mimba usio salama unaoweza kuathiri afya za wajawazito.
Pia, amewataka wajawazito kuhudhuria katika kliniki za uzazi wa mpango ili waweze kupatiwa elimu ya afya ya uzazi ikiwemo jinsi ya kuepukana na mimba zisizotarajiwa ili kuondokana na uavyaji wa mimba usio salama.
Mwisho.
Home »
» SERIKALI YABAINISHA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA UTOAJI WA MIMBA USIO SALAMA.
SERIKALI YABAINISHA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA UTOAJI WA MIMBA USIO SALAMA.
Related Posts:
SABABU ZA MAKATO YA BIMA YA AFYA KWA VITUO HIZI HAPA,Na WAF, Bungeni, Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel amebainisha sababu zinazopelekea upotevu wa fedha katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoka kwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini.Dkt… Read More
MCHUNGAJI DANIEL MGOGO HIZI NDOA HAZIWEZI KUDUMU Mchungaji na Mhubiri maarufu kutoka Tanzania Pastor Daniel Mgogo ametaja aina ya ndoa ambazo kwa mujibu wa mafundisho yake ndoa hizo haziwezi kudumu hata iweje.Kwa mujibu wa Mchungaji Mgogo amesema ndoa lazima zibarikiw… Read More
NAIBU WAZIRI NISHATI AMEWATAKA TANESCO KUWA NA KITENGO CHA MASUALA YA JINSIA. Na Masala Komba Dodoma Naibu waziri wizara ya nishati Steven Byabato ameagiza shirika la umeme Tanzania kuwa na kitengo cha masuala ya jinsia (dawati la jinsia).Mhe.Byabato ameyasema hayo wakati akizung… Read More
MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMEWAAMBIA WAKRISTO "MIMI SIYO YESUMwigizaji Robert Powell, mtu aliyeigiza uhusika wa"Yesu" katika filamu maarufu ya Yesu wa Nazareti amewasihi wanaoabudu Picha yake wakiamini kuwa yeye ndiye Yesu waache. anasema “ACHENI KUNIABUDU MIMI SIYO YESU” Tan… Read More
TASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI MTWARA.Na Mwandishi Wetu,Mtwara.SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC)limetoa elimu kwa wananchi kuhusu namna Shirika linavyotekeleza Majukumu yake kwa Mujibu wa Sheria.Elimu hiyo imetolewa katika maonesho ya Bishara, Uwekezaji … Read More
0 Comments:
Post a Comment