Meneja Mawasiliano Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Bi. Subira Kaswaga, amezitaka Taasisi za Umma nchini kuendesha vikao kidijitali kwa kutumia mfumo wa e-Mikutano ili kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao.
Kaswaga alitoa rai hiyo jana, alipofanya mazungumzo na mwandishi wetu ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu faida zitokanazo na mfumo wa e-Mikutano.
Alibainisha kuwa, mfumo wa e-Mikutano unawawezesha watumishi wa Taasisi za umma kufanya vikao kidijitali mahali walipo bila kulazimika kukutana mahali pamoja na hivyo kusaidia kupunguza gharama za uandaaji na uendeshaji wa vikao.
βMfumo huu wa e-Mikutano unazisaidia taasisi za umma kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao, kwani watumishi hawalazimiki kusafiri na kukutana mahali pamoja ili kufanya vikao na badala yake wanaweza kufanya vikao mahali walipoβ, alisisitiza.
Aliongeza kuwa, mfumo wa e-Mikutano huokoa muda ambao watumishi wangeutumia kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa ajili ya kufanya vikao na hivyo kutumia muda huo kutekeleza majukumu yao mengine hali inayopelekea kuongeza ufanisi.
βMfumo huu pia unasaidia kupunguza au kuondoa kabisa gharama za kulipia leseni zinazohitajika ili taasisi za umma ziweze kutumia mifumo ya uendeshaji wa vikao kidijitali iliyojengwa na makampuni binafsiβ, alifafanua.
Alisema, Mamlaka ya Serikali Mtandao ilitengeneza Mfumo wa e-Mikutano, baada ya kuona uhitaji mkubwa wa matumizi ya TEHAMA kwenye eneo la kuratibu mikutano kwa watumishi wanaokuwa katika mazingira tofauti.
Mfumo wa e-Mikutano ni rahisi na rafiki kutumia kwani mtumishi yeyote wa umma mwenye barua pepe ya serikali (GMS), anaweza kuandaa kikao na kualika washiriki wengine, na pia mfumo unawezesha kuwasiliana kwa njia ya sauti na video, alifafanua.
Mfumo wa e-Mikutano umetengezwa na wataalamu wazawa kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na pia ni mfumo salama kwakuwa, umetengezwa kwa kuzingatia usalama mkubwa kwa watumiaji.
Home Β»
Β» π§πππ¦ππ¦π ππ π¨π π π πππππ πππͺπ ππ¨ππ‘πππ¦ππ π©ππππ’ ππͺπ π‘πππ π¬π π π§ππ‘πππ’ ππ¨π£π¨π‘ππ¨ππ ππππ₯ππ π
π§πππ¦ππ¦π ππ π¨π π π πππππ πππͺπ ππ¨ππ‘πππ¦ππ π©ππππ’ ππͺπ π‘πππ π¬π π π§ππ‘πππ’ ππ¨π£π¨π‘ππ¨ππ ππππ₯ππ π
Related Posts:
MCH.MARKO AMEWATIA MOYO WAKRISTO MSIKATE TAMAA Na. Kadala Komba ,DodomaWakiristo wametakiwa kuachana na hali ya kukata tamaa na kuishiwa nguvu hasa pale wanapokutana na changamoto mbalimbali katika maisha yao kwa maana tumaini lipo katika Mungu.Hayo yamebainishwa na⦠Read More
*MHE.KAPINGA AZINDUA JUKWAA LA UZIDUAJI 2023* # Asema vyanzo vya umeme hasa Sekta ya Gesi ina uhusiano wa moja kwa moja na Sekta ya UziduajiNaibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga asema kuwa vyanzo vya kuzalisha umeme vina uhusiano wa moja kwa moja na Sekta ya⦠Read More
SERIKALI IMETUTUPA,HAITUTAMBUI WANANCHI ZEPISA WATEMA NYONGO. Na Moreen Rojas,Dodoma.Wananchi wa kijiji cha ZEPISA Dodoma jiji wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwatimizia huduma muhimu kama maji,umeme,miundombinu ya barabara pamoja na kituo cha afya.Pendo Wilson ambaye ni mw⦠Read More
KAMATI YA SIASA YA MKOA WA DODOMA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MPWAPWA Na. Mwandishi wetu MpwawaKamati ya siasa ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa Ndg. Pili Mbaga, imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kat⦠Read More
WAZAZI NA WALEZI WAKUMBUSHWA KUPELEKA WATOTO SHULE. Na Mwandishi Wetu- KilimanjaroWazazi na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha watoto wao waliofikia umri wa kwenda shule wanapelekwa ili kupata elimu itakayowawezesha kuwa wataalam wa fani mbalimbali pamoj⦠Read More
0 Comments:
Post a Comment