Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

WAZAZI KUWAJIBIKA KWENYE MALEZI YA MTOTO Ndg , KINGWANDE

 Na. Kadala Komba Dodoma


Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.Mary Chatanda  Novemba 24,2023  umeendelea na ziara yake  Halmashauri ya Wilaya ya Bahi.

Uongozi huo ukiwa katika ziara yake umegawanyika katika timu mbalimbali ambapo  Naibu Katibu Mkuu Ndg , Riziki Kingwande amefanikiwa  kutembelea Kata ya
Ibugule kijiji cha  Mapanga
Kata Chibelela
Kijiji Isangha
Kata ya Mtitaa na Kukagua mradi ya  madarasa matano (5) ya shule ya msingi Isangha Kukagua nyumba ya mtumishi two ni One Kukagua matundu 10 ya choo Yenye Gharama za Tsh.  233,800,000/= Pamoja na kusikiliza kero za wananchi .

Akizungumza na wananchi wa Kata ya  Mtitaa    amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao na kuwalinda  kwani maadili yameporomoka hivyo amewasihii kundokana na desturi ya  kuamini watu kwa urahisi kwani Dunia imeharibika .

"Wazazi naombeni tuwajibike katika kuwalea watoto wetu kwenye msingi mzuri kwani ndio viongozi wa leo na kesho yao hatuwezi kukaa kimya na kulifumbia macho hii hali ya sasa hivi ambayo watoto wetu wanaharibiwa kwa kukatishwa ndoto zao tumechoka kusikia mara mtoto amelaitiwa mara kabakwa hizi tabia tuzikomeshe " Amesisitiza Ndg. Kingwande .

Sambamba na hilo, Ndg  .Kingwande Amewahimiza viongozi wa Chama cha Mapinduzi kutekeleza majukumu yao kwa nafasi zao kuanzia ngazi ya shina , matawi kata kwa lengo la kuwaaminisha wananchi waone kazi vinazofanywa na viongozi wa chama cha Mapinduzi, hivyo viongozi wenzangu tujitume katika kazi ya kuwasaidia wananchi tufanye ziara pamoja na mafunzo kwa viongozi hili kuwajengea uwezo.

Naibu Katibu Mkuu Ndg , Riziki Kingwande Akizungumza na Wananchi wa kata ya Mtitaa
 



 MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA












Na Mwandishi wetu.

Imeelezwa kwamba uwekezaji wa hoteli kubwa na za kisasa unasaidia katika kuchochea shughuli za utali na kuongeza thamani ya Mji wa Mbinga, kwa sababu ya upekee wa vivutio vyake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Hotel ya One Pacific yenye hadhi ya nyota tatu katika wilaya ya Mbinga.

Waziri Mhagama amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan amejipambanua kwa kuwa balozi kinara wa sekta ya utalii na uwekezaji kwa ujumla katika sekta ya utalii.

“Mkakati wa Taifa wa ROYAL TOUR na kuifungua nchi yetu Tanzania katika sekta ya utalii ni mkakati mkubwa sana, na uliotukuka na tunaungana na wawekezaji katika kutafsiri ROYAL TOUR ndani ya wilaya yetu ya Mbinga,” Alifafanua

Akieleza kuhusu vivutio vinavyopatikana, Waziri amesema, wilaya ya Mbinga inavivutio vya kutosha; kama safu za milima zilizojipanga kwa kuvutia, zenye maporomoko ya maji, uoto wa asili, unaopendezesha madhari ya milima hiyo.

Aidha hapa ndio mahali ambapo kuna mapango ya kale katika eneo la Litembo, na inaaminika wazee wetu wa zamani waliishi katika mapango hayo.

“Hii historia kama itawekezwa vizuri, ni kivutio na utalii wa kutosha sana katika eneo letu,” Alibainisha.

Kwa upande wake Dkt. Erasmo Nyika akizungumza kwa niaba ya bodi ya wawekezaji wa mradi wa Hotel hiyo amesema wamesukumwa kuja kuwekeza Mbinga kutokana na Msukumo wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejenga mazingira rafiki ya uwekezaji.

“Tumuwekeza miradi miwili ndani ya wilaya ya Mbinga yenye thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 4, na tumeona fursa zipo na tunashukuru Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbinga kwa kutushawishi kuwekeza Mbinga, mradi umelenga kuzalisha ajira nyingi kwa wazawa,” Alisema

Awali, Mhandisi Selemani Kinyaka katika taarifa yake amesema Ujenzi wa Majengo ya mraadi wa One Pacific Hotel; unavyumba vya kawaida 14, vyumba vya daraja la juu 23 vyumba vya hadhi ya kiutawala 3, Ukumbi mdogo wa mikutano, Migahawa 2, sehemu ya mazoezi, eneo la kuogelea na eneo la kufulia nguo.

 

Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi tumetoa ajira zaidi ya 250 ambapo 30 zilikuwa ajira za kudumu, na nyingine ni ajira zilizojitokeza kila siku.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kulshoto akizindua) Mradi wa Hotel ya One Pacific katika ziara yake ya Kikazi wilayani Mbinga.
 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo wakitembelea baadhi ya maeneo ya mradi wa Hotel One Pacific kabla ya uzinduzi rasmi kufanyika.

 

WANAFUNZI CHUO CHA MIPANGO WATAKIWA KUTUMIA TAFITI ZAO KWA MANUFAA YA JAMII.

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Wanafunzi Chuo cha Mipango ya  Maendeleo Vijijini wametakiwa kutumia tafiti zao kwa manufaa ya jamii ili kuleta tija na matokeo chanya ya tafiti zao.

Hayo yamesemwa na Bwana. Moses Dulle   Mkurugenzi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye amemwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Omolo Mgeni rasmi katika kongamano la kitaaluma ambapo wanafunzi wamepewa tuzo mbalimbali kutokana na tafiti zao ili kuwapa motisha na wengine kuendelea kufanya tafiti hizo ambapo tukio hilo limefanyika ukumbi wa  miyuji North jijini Dodoma.


Aidha ameongeza kuwa tafiti nyingi hazitangazwi kutokana na udhaifu kutoka kwa wahitaji na wazalishaji kwa kawaida jamii inabidi iwe na uhitaji wa tafiti fulani kwa ajili ya ubunifu na wakati mwingine inawezekana jamii yenyewe hawana uhitaji hivyo kuwapa ugumu watafiti kutumia tafiti zao lakini jamii inapaswa kuwa na muamko wa kufanya uwekezaji kwenye tafiti hizo.

"Maendeleo ni hatua na hayawezi kuja ghafla ni jukumu la wanafunzi na walimu kuweza kutangaza tafiti zao pamoja na waandishi wa habari kuuliza taasisi zinazofanya tafiti kujua namna wanavyofanya tafiti zao na kuzitangaza kwa wananchi lakini pia ni jukumu la jamii yote kwa ujumla wake kuhamasisha namna watu wanaweza kupata taarifa za utafiti" Amesisitiza Bwana Dulle

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof.Hozen Mayaya amesema chuo kinakuwa na wamewapongeza watu wao mbalimbali na kuwafikishikia umma kwamba wanajenga uwanja wa watu wao,hivyo pamoja na kwamba wanawaleta wanafunzi na kwa sasa hivi wanataaluma 79 ambao wanasoma katika maeneo mbalimbali kati yao 45 walikuwa wanasoma vyeo vya PHD ambao ni vyeo vya juu zaidi.

"Hii maana yake ni kwamba miaka michache ijayo chuo hiki kitakuwa kinatoa wasomi wenye elimu ya juu lakini kwa upande wa kuwapa tuzo wanafunzi ni kuwajengea hamu ambao wanaendelea kusoma ili kufanya vizuri zaidi na kuwa bora kwenye masomo yao na kujifunza kutoka kwa wingine" Amesisitiza Prof.Mayaya

Naye Dorcas Samson ambaye ni mhitimu wa chuo hicho amesema anashukuru kuwa miongoni mwa wahitimu kwani kupitia chuo hicho ameweza kuwa mjasiriamali na hivi sasa anajishughulisha na uongezaji wa thamani kwenye bidhaa za chakula anatengeneza unga wa lishe pamoja na soya ambapo ndoto yake kubwa ni kuwa mjasiriamali mkubwa kutokana na ujuzi alionao na kuajiri wengine.

"Kwa wanafunzi ambao hawajajiunga na chuo cha mipango nawashauri wajiunge na chuo hiki kwani mbali na masomo watafundishwa elimu ya ujasiriamali na kuweza kujiajiri wenyewe na kupunguza wimbi kubwa la kutegemea kuajiriwa na serikali ili kuendana na kasi ya uchumi wa kati na nchi yetu kupunguziwa lawama kutoka kwa vijana lakini kwa upande wa serikali tunaomba ihakikishe inawasapoti wajasiriamali wadogo na wanaochipukia hasa hasa vijana" Ameongeza Tabitha Yusuph ambaye ni mhitimu na mjasiriamali.



MWENYEKITI UWT TAIFA ATEMBELEA HOSPITALI YA MJI KONDOA

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa UWT na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mhe. Marry Chatanda, leo tarehe 22 Novemba 2023 ametembelea Hospitali ya Mji Kondoa ikiwa ni ziara yake kwa Halmashauri hiyo kujionea Miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita.

Akiwa Hospitalini, hapo Mhe. Chatanda amewajulia hali wagonjwa waliokuwepo kwenye jengo la dharura ambalo limejengwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 300 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu chini ya Mpango wa UVIKO.

Aidha, Mhe. Chatanda ametembelea jengo jipya la Mama na Mtoto ambalo lipo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake baada ya kupata fedha kiasi cha Shilingi Milioni 900 za ukarabati wa Hospitali ya Mji ambapo majengo matatu yamejengwa ikiwemo jengo la upasuaji, mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia Maiti (Mochwari).

Hata hivyo, ameagiza kufanyiwa marekebisho yaliyoonekana katika majengo hayo ikiwemo kumalizia jengo la mama na mtoto ili wananchi waanze kupata huduma katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na wahandisi kusaidia kutoa utaalam ili kujenga majengo yaliyo bora.










DARAJA LA BILLIONI 1.5 KUONDOA DARAJA LA KAMBA KONDOA.

 
Wananchi wa kijiji cha Hurui kata ya Kikore Wilayani Kondoa  Mkoani Dodoma wamesema ujenzi wa daraja la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 linalotarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi Disemba 2023 litatatua  kero ya muda  ya mrefu ya kutumia daraja la kamba kuvuka mto na  kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii  hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watoto kutofika shule Pia   wakazi wa Kijiji hicho kushindwa kuuza mazao yao kutokana na kukosekana kwa miundombinu hiyo.

Hayo yamebainishwa Leo Novemba 22,2023 baada ya Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Timu iloyoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Joketi Mwegelo na Wataalamu wengine wa Mkoa na Wilaya hiyo kufika katika daraja hilo  kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.

Aidha Ndg. Mwegelo wakati akitembelea mradi wa Maji katika Kata ya Kisese amemtaka mkandarasi anaye tekeleza mradi huo kuanza ujenzi wa tanki ndani ya  siku saba awe ameshaanza utekelezaji wa mradi huo ili kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa mwiba mchungu kwa wananchi wa Kisese.Wito huo umetolewa baada ya kupita siku ishirini na moja ambazo mkandarasi alitakiwa awe eneo la mradi akiendelea na Ujenzi wa Mradi.

Hata hivyo Ndg. Mwegelo amesema licha ya Viongozi mbalimbali kuwachukulia hatua baadhi ya Viongozi ambao walikuwa wakitekeleza mradi huo lakini bado inaonekana kuendelea kusuasua jambo linalopelekea kucheleweshwa kwa ukamilishaji wa Mradi huo.

Pia, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Kikore na Kisese kupeleka watoto shule na kuachana na tabia ya kugeuza watoto kufanya kazi za ndani .

Mkoa wa Dodoma umekuwa wa 17 kufikiwa na  ziara ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT ) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Mary Chatanda na Viongozi wengine ambapo wanatarajia kupita katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ikiwa tayari wamesha kamilisha ziara yao Wilaya ya Kondoa kwa  kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) na maendeleo ya miundombinu mbalimbali pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa huo.





WANANCHI NTYUKA WAILALAMIKIA SERIKALI KULIPWA FIDIA YA BARABARA.

 Na. Modern Rojas Dodoma


Wananchi wa mtaa wa ntyuka na chimalaa wailalamikia serikali kuwachelewesha kuwalipa fidia ya mradi wa barabara.

Michael Emily mkazi wa eneo hilo amesema wananchi wanaodai ni takribani 172 na tangu mwaka 2022 mwezi wa 8 waliahidiwa kabla ujenzi haujaanza watalipwa mafao yao lakini mpaka sasa hawajalipwa,kamati ilienda TANROAD lakini hakuna matokeo chanya yoyote mpaka sasa na wakati waliambiwa wasubiri wiki moja,baada ya hapo wakasema wanaotaka kubomolewa kwa hiari wajitokeze sasa wanashangaa imekuaje tofauti.

"Leo wanasema wanataka watu wachache sasa watu wa chache kivipi?hivyo tunamuomba Waziri wa Ujenzi Mhe.Innocent Bashungwa aje aangalie dhulma hii na Rais wetu Mama Samia atusikie" Amesema Ndg.Emily

"Tumekuwa tukifuatilia viongozi wa Mkoa wanatupiga danadana tufanye nini?chuo cha mwalimu Nyerere wamechukua maeneo ya wananchi hawalipa watu wa eneo husika,serikali jamani ituangalie na kama mradi huu umeshindikana usitishwe" Ameongeza Bwana Edward Lamale.


Muhanga mwingine wa barabara Bi.Eva Daniel amesema aliambiwa saa 9 mtendaji atakuwa ameshasaini karatasi kwaajili ya kupata hela lakini matokeo yake anazungushwa tu na kudanganywa na ameambiwa kwa vile nyumba yake iko karibu na barabara aibomoe ahame na hawezi kuhama kwa sababu hana hata mia na kama serikali imewachoka iwaambie wahame na watahama mpaka chama maana kila siku wakikusanyika wanaambiwa meneja yuko kwenye kikao.


"Kwa upande wa mtendaji wa kata kiukweli hayupo na sisi na tunaona kabisa hatufai yuko kinyume na sisi kunawatu wana wito wanataka kufanya kazi na leo waandishi mmekuja hataki kuongea Luna nini kilichojificha?mtendaji wa kata ni tatizo kawapa barua baadhi ya wananchi kwa nini?tunataka mtendaji mwingine sababu huyu hawezi kutumikia wananchi maana ofisi ya kata mara nyingi imefugwa" Amesisitiza Bi.Eva


Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya ufuatiliaji Atnas Matonya amesema miradi mingi ya serikali wanashangaa kwa nini? haina chanzo cha kulipa fidia na watakopowalipa wawalipe na muda kwa sababu wako nje ya makubaliano na mojawapo ya miradi ambayo imekuwa hailipwi ni pamoja na mradi wa mwalimu nyerere takribani hekari 50 waliahidi kulipa watu pamoja na mradi wa udom ujenzi ng'ong'ona.

Baada ya wananchi kutoa kero zao Injinia Colman Gaston ambaye alikuja kwa niaba ya meneja wa TANROAD Mkoa wa Dodoma amewaambia wananchi kuhusu malipo ya mradi wa barabara unaendelea kwani wananchi walifanyiwa uthamini lakini vitabu bado vinafanyiwa kazi hivyo ameagizwa awaambie kwamba suala lao linafanyiwa kazi.


"Hivyo niwaombe wananchi suala la fidia linafanyiwa kazi na niwaombe mvute subira hivyo siku ya leo ntapeleka maombi kwamba wananchi wanataka kumsikiliza na kila mtu apate haki yake kutokana na taratibu zinavyotakiwa" Amesema Injinia Gaston


Naye Yona Andrew Diwani wa kata hiyo amesema uwepo wa mgogoro huo umetokana na ucheleweshwaji wa fidia ya barabara lakini ni takribani miezi 6 sasa ambapo imepelekea wananchi kuwa na taharuki kutokana na mvua kubwa zinazokuja na kuleta maafa zaidi na yeye kama kiongozi alichukua hatua ya kuunda kamati ndogo ili kushughulikia huu mgogoro.



SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKO

STORY SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKO Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Serikali itaendelea kulinda kwa nguvu na gharama zote uhuru wa wananchi wa kutoa mawazo, imani na uchaguzi katika dini, hivyo itahakikisha kunakuwa na amani na utulivu ili uhuru huo wa kuabudu na kutoa mawazo uwepo muda wote. Dkt.Biteko amesema hayo tarehe 19 Novemba, 2023 wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kumpongeza Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul Ruzoka na kumpokea rasmi Askofu Mkuu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa. Sherehe zilizofanyika katika Jimbo Kuu Kanisa Katoliki Tabora. "Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan muda wote amekuwa akisisitiza haki kwa wananchi wote, na ili kuishi katika misingi ya utangamano haki lazima itawale. Rais anataka wananchi wasikilizwe; tunaweza kutofautiana katika maoni na mitazamo lakini kamwe tusivunje umoja wa kitaifa, tuwaunganishe watanzania na tupambane kuwaondoa wananchi katika umaskini na kuwaletea nafuu kubwa ya maisha." Amesema Dkt.Biteko Dkt. Biteko amesema kuwa, Mheshimiwa Rais, msisitizo wake ni kupeleka maendeleo kwa wananchi wote bila kuangalia tofauti zao, ikiwemo maji, barabara, umeme, shule na pia lengo lake ni kuendelea kuwaunganisha wananchi ili kuleta umoja nchini. Vilevile, Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt.Samia yupo tayari muda wote kushirikiana na taasisi za kidini nchini kuwaletea maendeleo wananchi. Ameendelea kusema kuwa, Serikali itaendelea kuhubiri haki na maridhiano kama msingi wa amani wa nchi na pia itaendelea kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujiletea maendeleo kwani bila kazi hakuna Taifa. Katika hatua nyingine, Dkt.Biteko amesema kuwa, Rais ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Askofu Mkuu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa kama ambavyo amekuwa akitoa ushirikiano kwa mtangulizi wake Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul R. Ruzoka. Kwa upande wa Askofu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa na Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul R. Ruzoka wameshukuru kwa ushirikiano ambao Serikali imeendelea kuutoa kwao na wameahidi kutoa pia ushirikiano kwa Serikali. Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Batilda Burian na Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamis Kigwangala. Pia walihudhuria Viongozi mbalimbali wa Madhehebu ya Dini kutoka ndani na nje ya nchi, na Waumini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Tabora. Regards, Henry KIlasila

ASA YAPONGEZWA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO

Na Mwandishi wetu- Tabora Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameupongeza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa kukamilisha Awamu ya Kwanza ya Mradi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la mbegu Kilimi lililopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora. Mhe. Ummy ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika shamba la mbegu Kilimi linalotekelezwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kupitia Mradi wa Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ambapo amesema Taasisi hiyo iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo imepiga hatua kwa utekelezaji wa vitendo kwa ujenzi wa miundombinu ya kisasa na imara ya Umwagiliaji katika shamba hilo. Amesema matarajio ya Serikali ni kuona uzalishaji wa mbegu unaongezeka kwa wananchi ili kupunguza uagizwaji wa mbegu kutoka Nchi jirani ambapo baadhi ya wakulima hushindwa kumudu gharama. “Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha tufanya kilimo cha kisasa na kupata fedha za kuendeleza sekta hii muhimu lengo la ziara hii ni kuona Mradi unavyoendelea hivyo nampongeza Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe anafanya kazi kubwa sana akishirikiana na ASA. Pia nimefurahi kuona fedha inayokuja katika mradi inafanya kazi iliyokusudiwa kuongeza tija katika uzalishaji wa mbegu,”Alisema Mhe. Ummy. Ameeleza kwamba Wizara ya Kilimo imejipambanua kwa kuweka miundombinu ya Umwagiliaji, kuhamasisha vijana kukipenda kilimo tofauti na awali kilichukuliwa kama adhabu. “Tunawashauri watanzania waendelee kuiamini Serikali wakati tunafanya mapinduzi ya kilimo watumie fursa hii hasa waliopo katika maeneo haya na hata tutakapoanzisha vituo hivi katika maneno mengine basi wakulima watumie fursa hiyo kuboresha kilimo wajikwamue kiuchumi,”Ameeleza. Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt. Sophia Kashenge amesema maelekezo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri yatafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mbegu ili kukidhi mahitaji ya wakulima hapa Nchini huku akisema kuwa wataendelea kuweka mikakati ya kuimairisha usalama katika mashamba kuepuka uharibifu unaotokana na uingizwaji wa mifugo katika mashamba hayo. “Awali kulikuwa na changamoto kubwa ya mifugo kuingia katika mashamba lakini tumejitajidi kutoa elimu kwa vijiji vilivyopo katika maeneo haya na tunaendelea kuongeza ulinzi kimsingi mifugo ina madhara makubwa kwa mashamba ya mbegu na uzalishaji wa chakula pale mifugo inapoleta magugu kupitia kinyesi, wanaharibu rutuba ya udongo, kuongezeka kwa magonjwa kwa mazao hali inayoongeza gharama za matunzo,” Alifafanua Dkt. Sophia. Naye Katibu Tawala Wilaya ya Nzega Bi. Winfrida Funto amemshukuru Mhe. Ummy kwa kufanya ziara katika Mkoa huo ambayo imetoa hamasa katika sekta ya kilimo hususan kilimo cha umwagiliaji ambacho hongeza tija kwa wakulima na kuondokana na kilimo cha mazoea. Aidha mmoja wa wakazi katika Kijiji cha Bukamba Mpya Bi. Joyce Masanja ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuratibu Mradi wa AFDP ambao kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) imewasaidia wakulima kupata mbegu bora za asili kutokana na uwepo wa mashamba ya uzalishi wa mbegu na kupatikana kwa urahisi. ==MWISHO==
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga akikagua mifumo ya maji inayosambaza maji katika shamba la mbegu Kilimi linalotekelezwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kupitia Mradi wa Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) alipofanya ziara hiyo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

NEC YAKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI MKOANI TABORA

 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa wakazi wa maeneo yaliyoteuliwa kwa ajili ya majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo ambalo linalenga kupima utayari wa mifumo na vifaa vya uboreshaji wa Daftari.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Tabora leo tarehe 20 Novemba, 2023 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri amewapongeza wakazi wa mkoa huo kwa mkoa wao kuwa miongoni mwa mikoa miwili ambayo kata zake zimeteuliwa kufanya majaribio hayo ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

Mhe. Mapuri amezitaja kata zitakazofanya majaribio hayo kuwa ni Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, ya mkoa wa Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, katika Mkoa wa Mara.

“Tume inawapongeza wakazi wa Mkoa wa Tabora kwa mkoa wenu kuteuliwa kuwa mwenyeji wa zoezi




RUSHWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO LIMEKUWA TATIZO SUGU.

 

Rushwa kwenye miradi ya maendeleo limekuwa tatizo sugu,na wengine wamekuwa wakiliita kansa hivyo ni jukumu la kila mmoja hukakisha analeta usawa kwenye eneo hili.

Hayo yameelezwa na Mhe.George Simbachawene Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU).

Aidha ameongeza kuwa miradi iliyopo ni kwaajili ya kila mtanzania na kila mtu ana haki yakufanya kazi kwenye miradi hiyo lakini wasimamizi wa miradi wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya hivyo ni jukumu la watumishi wote wa sekta hii kuhakikisha wanakabiliana na watu hawa ambao wamekuwa miba kwenye jamii.

"Rushwa kwenye miradi ya maendeleo limekuwa tatizo sugu hivyo ni muhimu kushughulikia tatizo hili hasa kwa wale wasimamizi wa miradi wamekuwa wakitumia vyeo vyao vibaya kwa kuwanyanyasa wananchi  hivyo watumishi wote wa sekta hii ni jukumu lenu kusimamia maadili ya kazi na kutenda haki" Amesisitiza Mhe.Simbachawene

Aidha ameongeza kuwa hatua nyingi zinafanywa dhidi ya mapambano ya Rushwa na Serikali imeipa(TAKUKURU) ajira mpya zaidi ya 600 ili kupambana na rushwa pamoja na watumishi kujituma kwa weledi katika mapambano dhidi ya rushwa hivyo suala la rushwa ni Agenda kubwa duniani.

Sanjari na hayo amesema kuwa kwa ulimwengu wa sasa katika kufanya kazi za kiuchunguzi watafakari nini cha kuboresha na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzipatia suluhu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)ambaye ni  Kamishna wa Polisi C.P Salum Rashid Hamduni  amesema mafanikio ya mwaka 2022 kupitia chaguzi mbalimbali bilioni 171 wameziokoa kupitia operesheni maana bila operesheni  fedha hizo zingeishia mikononi mwa watu.

Naye Neema Mwakaliele Naibu Mkurugenzi Mkuu (TAKUKURU) amesema mkutano huo unalenga kujenga utendaji kazi wa watumishi wa taasisi hiyo pamoja na kuongoza mapambano dhidi ya rushwa ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa muadilifu na kutenda haki bila upendeleo.

Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU una jumla ya wajumbe 61 ambapo kauli mbiu inasema"Kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu Tutimize wajibu wetu".


WATENDAJI WA TARAFA NA KATA WATAKIWA KUONESHA ELIMU ZAO KWA VITENDO

 
Wito umetolewa kwa watendaji wa Tarafa na Kata za Mkoa wa Dodoma kuonesha thamani ya vyeti vyao vya Elimu kwenye utendaji wa kazi kwenye Tarafa na Kata zao kwani wao ndio wanatarajiwa kuiletea Serikali heshima kwa wananchi wake kwa. Hayo yamebainishwa leo Novemba 20, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa watendaji hao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Roma Complex Jijini Dodoma.

Mhe. Senyamule amesema watendaji wa Kata wanapaswa kufuata Sheria na kanuni za kiutendaji ili kuwapunguzia mzigo wa kero wananchi wa chini na sio kusubiri viongozi wa juu kufika kwenye maeneo yao kutatua kero.

"Serikali imeekeleza kila mtendaji asikilize kero na kuzitatua. Kazi kubwa ya mtendaji ni kuonesha njia kwenye Tarafa yako kwani changamoto kubwa iliyopo hapa ni mabadiliko bado ni madogo kulingana na matarajio ya Serikali. Mumewekwa pale kulinda heshima ya Serikali kwa kazi, maneno na matendo yenu. Jambo hili halifanyiki kwa uthabiti wa kutosha ndio maana munapewa mafunzo haya ili kuwakumbusha Sheria na kanuni mpya ili kuongeza maarifa kwa watumishi waweze kumudu majukumu yao" amesema Mhe. Senyamule.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurungenzi wa TAMISEMI Bi. Angelista Kihanga, amesema kuwa, mafunzo haya yamepewa umuhimu wa hali ya juu kwani yalianza awamu ya kwanza kwenye Mkoa wa Mbeya na Mikoa ya Magharibi na Sasa yanafanyika kwenye Mikoa ya Kanda ya kati kwa kuhusisha Maafisa Tarafa na Kata kwani ndio watekelezaji wa sera za nchi kwa wananchi.

Mafunzo kwa Maafisa wa Tarafa na Kata yaliyoandaliwa na Wizara ya TAMISEMI, yanagusia mada mbalimbali zikiwemo mwongozo wa ushughulikiaji malalamiko ya wananchi katika utumishi wa umma na huduma kwa wateja, ununuzi wa umma, nafasi ya Afisa Tarafa na Mtendaji wa Kata katika mafanikio ya Serikali, kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma na Sera na Sheria za uendeshaji wa Serikali za Mitaa.



MASHIRIKA YASIYO TAKA KUSHIRIKI MICHEZO YACHUKULIWE HATUA KALII.

 
Na Moreen Rojas,
Dodoma.


Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta  Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ayaandikie Barua  Mashirika ambayo hayajapeleka Wafanyakazi Kushiriki michezo ya SHIMUTTA Mwaka 2023 na  kueleza sababu zakutoshiriki ili Serikali ione hatua zakuchukua.

Dk Biteko ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa wiki mbili.

Aidha ameongeza kuwa watumishi wa Umma wafanye kazi kwa Weledi na kutoa huduma Bora kwa watanzania pamoja na kuondoa hali ya  watanzania kuona taasisi zao ni kero kwa Wananchi hivyo watatue kero hizo kwakutimiza wajibu wao.

"Tumekubaliana kufanya jambo fulani basi tulifanye, na kama tunaona halifai  basi bora tuliache, kuliko tunakubaliana kufanya kitu  halafu hatukifanyi; haiwezekani  viongozi wote hapa wanalalamika, Katibu Mkuu analalamika, Naibu Waziri analalamika na mimi nilalamike?, hapana sijaumbwa hivyo, sioni sababu yoyote ya kutamkika au ya kuandikika, kwamba kuna mashiriki ya umma 248 na hapa yapo mashirika 57 tu; haiwezekani." Amesisitiza Dkt.Biteko


Aawali, Mwenyekiti wa Kamati ya SHIMMUTA, Roselyne Massama amemweleza Naibu Waziri Mkuu kuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya muitikio mdogo wa Mashirika ya Umma kushiriki mashindano hayo jambo ambalo linazorotesha mashindano hayo.



Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Charles Maguzu amesisitiza michezo maofisini na serikali ya awamu ya sita inasisitiza michezo ambapo watumishi wawe na muendelezo wa michezo maeneo ya kazi ili kutokomeza magonjwa yasiyoyakuambukiza.

Kwa upande wake Naibu Waziri,Sanaa na Michezo Hamisi Mwijuma amesema
serikali itoe tamko juu ya Mashirika ambayo hayawaruhusu Wafanyakazi kushiriki michezo kwani michezo ni njia nzurii ya kudumisha uhusiano na haswa kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kwani kwa kipindi hichi cha serikali ya awamu ya sita michezo imeenda kimataifa zaidi kupitia sekta ya michezo haswa mpira wa miguu haswa timu kongwe simba na yanga na Tanzania kujulikana kimataifa kupitia sekta hii.


Kwa upande wake Afisa uhifadhi mwandamizi Carlos Ernest Mbilo kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania(TAWA) amesema mashindano hayo yatadumisha uhusiano na taasisi mbalimbali na kwa upande wao mchezo mpira wa miguu wanafanya vizuri na upande wa netiboli wamepoteza mechi 1 na wanafanya vizuri kujituma lakini kikubwa ni nidhamu ili kuhakikisha wanapata vikombe vyote.


Naye Patrick Gandye Mwenyekiti wa michezo kutoka mfuko wa taifa wa jamii(NSSF) amesema michuano ilianza tangu jumamosi umuhimu mkubwa wa mashindano haya ni kujenga ukaribu na mashirika mengine ya serikali na taasisi ambazo hazijashiriki kama mgeni rasmi inabidi wafanye hima waweze kushiriki kwenye haya mashindano ikiwemo taasisi binafsi pamoja na mashirika ya serikali.

"Tuna mechi moja dhidi ya WCF tunaamini tutafuzu katika hatua inayofuata,tunaamini mwaka huu tutafanya vizuri licha ya kukutana na magwiji wa mchezo hivyo tunaamini tutachukua ubigwa,changamoto ni kwamba hatupati muda wa kutosha wa kufanya mazoezi,kama unavyojua kama mtumishi wa serikali muda ni mchache mno lakini haituzuii kutimiza majukumu yetu ya kimichezo" Amesisitiza Nora Mwidunda Meneja timu ya netiboli NSSF.

Naye Raymond Nyarufugo Mtumishi wa bandari ya Tanzania(TPA) amesema anawasihi taasisi zingine ziweze kuleta wanamichezo,kwa sababu michezo inasaidia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na magonjwa ya saratani lakini pia kuimarisha uhusiano katika taasisi za umma,kwenye taasisi yao kwa mwaka jana walikuwa washindi wa pili na walifanya vizuri.





UZALENDO WAHIMIZWA UTUNZAJI MIRADI BAHI

Na. Mwandishi wetu Bahi

Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dodoma Ndg.Jawadu Mohammed ametoa Rai kwa wasimamizi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuitunza ili wananchi wanufaike zaidi na maendeleo yanayoletwa na kiongozi wao Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika kila Halmashauri ili idumu kwa muda mrefu.

Amesema kila mwanachi anapaswa kuwa mwangalifu Katika matumizi ya miradi hii kwani huo ndio uzalendo wa nchi kwa kila mtu kujali na kuzingatia miradi inayoletwa kwenye Halmashauri zao.

“Ni lazima kuzingatia na kuona umuhimu wa kila mradi unaoletwa na kutumia njia zote kuhakikisha kila huduma muhimu inafika kwenye kila Kata ikiwemo huduma ya maji, umeme, N.k.

“Halmashauri ni lazima kuendelea kufanya jitihada za kimaendeleo ili angalau baadhi ya maeneo yenye changamoto zozote za kijamii ziweze kutatuliwa kwa haraka" Amesema Ndugu Mohammed.

Vile vile, amesisitiza suala la upandaji miti kwenye mazingira yanayowazunguka ili kuondoa changamoto za majanga kama mafuriko na kusababisha ukame hivyo, kila mwananchi anajukumu la kupanda mti.

Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Ndg. Maranyingi Matukuta amesema miradi inakuja kwenye Mkoa wetu ili tuweze kunufaika nayo hivyo miradi hiyo itunzwe vizuri kwani ni miradi yenye thamani nyingi na ni mizuri.

“Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Halmashauri inayofanya vizuri kwenye miradi hivo, Rais wetu mpendwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ana lengo zuri kwa wananchi wake wa Bahi, hivyo, isimamiwe kwa weledi na watumiaji waitunze” Amesisitiza Ndugu Matukuta

Pia ziara ya kamati hiyo iliweza kutembelea Mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Chiona ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 493, Mradi wa Maji Chali Makulu, Chali Isangha na Chali Igonga inayogharimu kiasi cha Bilioni 02 na kumalizia kwenye Ujenzi w Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Chali inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 544.







WILAYA YA KONGWA KUJA NA MBIO ZA KIHISTORIA.

 

Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini imeandaa mbio za Marathon kwa lengo la kuutangaza mchango wa Wilaya hiyo na Tanzania kwa ujumla katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Kupitia mbio hizo Ofisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuyatambua maeneo ya kihistoria, kuyalinda, na kuyaendeleza ili kuenzi historia yataifa na kuyafanya sehemu ya utalii wa kihistoria katika maeneo ya urithi wa ukombozi yaliyopo nchini.

Hayo yameelezwa leo November 15,2023 Jijini hapa na Mkuu wa Wilaya hiyo Remidius Mwema wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya kuitangaza wilaya hiyo kupitia mbio za marathon zitakazoanza November 25,2023 wilaya ya Kongwa mkoani hapa.

Amesema mbio hizo za marathon ambazo zimepewa jina la "Kongwa African liberation Marathon"imezingatia taratibu zote za marathon na kwamba zimegawanywa kwenye makundi ya Km 5,Km 10 na Kilometa 21 huku mgeni rasmi wa mbio hizo akitarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro.

Amesema Wilaya ya Kongwa imegusa ukombozi na historia ya harakati za ukombozi wa nchi za  kusini mwa Afrika zikiwemo Afrika ya Kusini,Zimbabwe,Angola na Msumbiji na hivyo kuwa na nafasi ya kujitangaza kama sehemu ya vivutio vya utalii.

"Serikali itashirikiana na nchi tulizozipa hifadhi wakati wa harakati za ukombozi kwa kukarabati majengo yaliyotumika na wapigania uhuru wa Afrika ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wao na kuitunza historia hiyo kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae” amesema

Amesema kupitia Marathon Wilaya hiyo itatangaza fursa kiuchumi na Uwekezaji zilizopo ikiwemo  Kilimo,Viwanda,Ranchi ya taifa,Soko la kimataifa la mahindi Kibaigwa na Hoteli za kitalii .

"Kwa kuwa Kongwa ni lango la kuingia makao makuu ya nchi tunategemea kuwa sehemu ya kivutio cha utalii na uhifadhi wa historia,hivyo tumetenga eneo la Pandambili kwa ajili ya Uwekezaji wa Viwanda,tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza, " Amesema na kuongeza;

"Niwaombe wana Dodoma na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu
kuendelea kutangaza fursa zetu
kama ambavyo Serikali yetu imekuwa ikijitolea  fedha kukarabati baadhi ya maeneo muhimu ya kihistoria kupitia wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo, "amesema

Kwa upande wake Kelvin Msumule Makamu mwenyekiti wa kamati amesema kama kamati wamejipanga kuhakikisha kila kitu kiko sawaa na wanawakaribisha watanzania wote kushiriki katika jambo hilo la kihistoria na kuongeza kuwa wamejipanga namna ambavyo watapokea wageni kutoka sehemu tofauti tofauti na kuwasihi watu wote wahakikishe wanafika kongwa ili kuweza kunufaika na fursa zinazopatikana wilayani hapo ambazo ni za tofauti na za kipekee ambazo huwezi kuzipata popote pale isipokuwa wilayani hapo.

Mbio hizo zimebeba dhima inayosema " kuthamini nchi na mchango wa wilaya ya kongwa kwa nchi za kusini mwa afrika"ambapo mbio hizi zitazinduliwa rasmi mwaka huu na kufanyika kila mwaka wilayani hapo.


WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA INALENGA KUWAFIKIA WADAU MBALIMBALI.

 
Na Moreen Rojas,
Dodoma.

Wiki ya huduma za fedha  inalenga kuwafikia wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa umma,wanafunzi,wakufunzi,wanawake,vijana,watu wenye mahitaji maalumu,wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs),waendesha boda boda,machinga,asasi za kiraia,wahariri na waandishi wa vyombo vya habari,watoa huduma za fedha,watoto na umma kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na kamishna wa maendeleo ya sekta ya fedha kutoka wizara ya fedha Dk.Charles Mwamwaja wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa wizara hiyo jijini Dodoma kuelezea maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa tarehe 20 hadi 26 novemba 2023 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid Arusha.

Aidha ameongeza kuwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi watashiriki na wanaendelea kualikwa kushiriki katika maadhimisho haya ikiwa ni pamoja na Wizara,idara na wakala wa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

"Wasimamizi wa Sekta ya fedha,taasisi za fedha,asasi zisizo za kiserikali,sekta binafsi,bodi za wataalamu,vyama vya wafanyakazi,vyombo vya habari,taasisi za elimu na utafiti,washirika wa maendeleo,vyama vilevile vya sekta ya fedha,makundi ya watoaji wa huduma za fedha na taasisi za dini zinazotoa huduma hizo" Ameongeza Dk.Mwamwaja.

Aidha amesema njia mbalimbali zitakazotumika katika kutoa elimu ya fedha kwa umma ikiwemo,machapisho(vipeperushi na mabango madogo),uandishi wa insha,gari la matangazo,semina,maonesho ya bidhaa za fedha,majukwaa ya kidigitali(mfano,simu za kiganjani),mitandao ya kijamii,vyombo  mbalimbali vya habari(Tv,Radio,Magazeti)pamoja na burudani.


"Malengo ya wiki ya huduma za fedha ni kujenga uelewa na weledi kwa umma katika matumizi sahihi ya huduma za fedha zinazotolewa ili kujenga uchumi na kuondoa umaskini,kuimarisha ufanisi wa masoko ya fedha kupitia elimu ya fedha,kuongeza upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha,kutoa elimu ya kumlinda mtumiaji wa huduma za fedha,kuwezesha wananchi kusimamia vizuri rasilimali fedha,kuwezesha wajasiriamali wadogo kuongeza ujuzi na matumizi sahihi ya huduma za fedha katika kukuza biashara zao,kuimarika kwa utamaduni wa kujiwekea akiba,kukopa na kulipa madeni na kuongeza kwa mchango kwa mchango wa sekta ya fedha kwenye ukuaji wa uchumi" Amesisitiza Dk.Mwamwaja.


Sanjari na hayo utekelezaji wa wiki ya huduma za fedha unatarajiwa kuwa na matokeo chanya kwa mtu binafsi,kaya,jamii na taifa kwa ujumla kwa kuongezeka kwa idadi ya watu wenye kiwango cha ufahamu wa elimu ya fedha na maarifa juu ya upatikanaji na utumiaji wa bidhaa na huduma rasmi za kifedha,kuimarika kwa uelewa na matumizi ya masoko ya fedha,kusogeza huduma za fedha karibu zaidi na wananchi,kuimarisha matumizi ya huduma hizo pamoja na kupata maoni na ushauri wa kuboresha huduma hizo,kuwawezesha watumiaji wa huduma za fedha kuelewa haki na wajibu wao,kuwawezesha wananchi kupata maarifa kuhusu namna bora ya kusimamia vizuri rasiliamali fedha,kuwaunganisha wajasiriamali na fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta ya fedha katika kukuza na kuimarisha biashara zao,wananchi kupata maarifa na uelewa wa masuala ya fedha na hivyo kuwezesha kujenga utamaduni wa kutumia huduma rasmi za kifedha na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.

Kauli mbiu itakayotumika katika wiki ya huduma za fedha kitaifa ni "ELIMU YA FEDHA,MSINGI WA MAENDELEO YA KIUCHUMI".


"TUMERIDHISHWA NA UTEKELEZAJI NA UBORA WA MIRADI YA CHEMBA " -JAWADU



Kamati ya siasa ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Katibu Wa Itikadi na  uenezi  (NEC ) Mkoa wa Dodoma Bw.Jawadu Mohammed imewapongeza   wasimamizi wa miradi inayotekelezwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ikiwemo Miradi ya Shule na Hospitali kwa kuzingatia ubora na ufanisi  unaotakiwa.

 Akizungumza na baadhi ya viongozi walioshiriki katika ziara ya ukaguzi wa Miradi hiyo Bw. Mohammed amewataka watumishi wa Umma kuitangaza na kuwa Mabalozi Wazuri wa Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema "ni lazima tuwe na watu makini wa kufuatilia miradi inayoletwa na Rais wetu ili wananchi  wasiwe na changamoto katika kupata huduma na ndio maana zimejengwa shule na Hospitali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na zinazostahili.

“Serikali ipo imara na imedhamiria kuhakikisha wananchi wanapata huduma za umeme, maji, mabweni, madarasa na majengo yote yanakua kwenye ubora na uimara wa Hali ya juu.Ni lazima miundombinu zote zikamilike kwa wakati kama mikataba inavyotaka hatufikirii kuona miradi inavuka muda wake wa utekelezaji,” Amesema Bw. Mohamed.

Pia Bw. Mohamed amesisitiza suala la upandaji Miti kwa Kila mradi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa bora na imara hivyo  kudumisha Sera ya Serikali ya Mkoa ya "Kijanisha Dodoma".

Kamati hiyo ilipata fursa ya kutembelea mradi wa Barabara kwa kiwango cha lami uliogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 599, ujenzi wa kituo cha afya Farkwa uliopokea kiasi cha Shilingi Milioni 500, Ujenzi wa Shule ya Msingi na awali Sankwaleto uliopokea kiasi cha shilingi Milioni 396, ujenzi wa Zahanati ya Sankwaleto ambao umepokea kiasi cha Shilingi Milioni 97, na ujenzi wa Mradi wa maji Babayu uliopokea kiasi cha shilingi Milioni434.

Ukaguzi wa Miradi mbalimbali unaofanywa na Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wa Kamati Bw. Mohhamed ni muendelezo wa ziara ya kikazi wanayoifanya katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Dodoma.