WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha kuwa mikataba ya utekelezaji wa makubaliano ya uendeshaji wa maeneo ya bandari nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World itazingatia maslahi ya nchi na kuleta manufaa kwa Taifa letu.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 28, 2023) wakati akitoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo amesisitiza kuwa makubaliano yaliyoingiwa yanalenga kuweka msingi wa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa kuwa bandari ya Dar es salaam ndiyo kitovu cha huduma za bandari nchini Serikali iliamua kutafuta Kampuni yenye uwezo na uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa bandari duniani kwa teknolojia za kisasa ili kuiwezesha bandari hiyo kufanya kazi kwa ufanisi, kuongeza mapato ya nchi na kuchagiza sekta nyingine za kiuchumi.
Amesema Serikali za Tanzania na Dubai zimeingia makubaliano kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na wa kijamii katika uendeshaji wa maeneo ya bandari nchini kupitia Kampuni ya DP World, ambayo imeonesha kuwa na utaalamu, uwezo na uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa bandari 190 katika nchi 68 barani Afrika, Asia, Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini.
“Kuhusu umiliki wa bandari, nilihakikishie bunge lako na wananchi kwa ujumla kwamba, kupitia Sheria ya Bandari ya Mwaka, 2004, Mamlaka ya Bandari Tanzania imekasimiwa haki ya kuwa mmiliki wa maeneo yote ya bandari nchini na haina uwezo wa kutoa umiliki huo kwa kampuni nyingine. Haki iliyopewa kwa mujibu wa sheria hiyo ni kuingia mikataba ya ushirikiano wa kupangisha na kuruhusu sekta binafsi kuendesha sehemu ya maeneo hayo.”
Waziri Mkuu amesema wakati wote wa utekelezaji wa makubaliano hayo na mikataba itakayoingiwa, vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kutekeleza majukumu yao katika eneo la mradi kama vilivyofanya katika kipindi cha miaka yote 22 ya mkataba na mwekezaji wa awali (TICTS) aliyemaliza mkataba wake. “Kuhusu mapato, ninapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaendelea kusimamia masuala ya mapato ya Serikali kutoka kwa mwekezaji kwa mujibu wa sheria na mkataba.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kupokea mapendekezo, maoni na ushauri kutoka kwa waheshimiwa wabunge, wananchi na wadau mbalimbali. “Kwa msingi huo, niielekeze Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi iendelee kuratibu utoaji wa elimu na ufafanuzi wa hoja za wananchi.
“Nitumie fursa kutoa rai kwa Watanzania wenzangu tusiruhusu mgawanyiko wa aina yoyote ile tunapotoa maoni yetu kuhusu uwekezaji wa bandari, tuepuke kujadili itikadi za kisasa, udini, ukabila, ukanda au vyovyote vile, muhimu tuenzi tunu yetu ya amani na mshikamano wa Taifa letu iliyojengwa na waasisi wetu.”
Amesema Juni10, 2023 Bunge lilipata fursa ya kuchangia, kuishauri Serikali na kupitisha azimio la mapendekezo ya kuridhia makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari nchini, hivyo amewapongeza wabunge wote kwa michango yao na kwa kuona umuhimu na tija katika jambo hilo na kuamua kulipitisha azimio hilo.
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
MIKATABA YA UENDELEZAJI BANDARI ITAZINGATIA MASLAHI YA NCHI-MAJALIWA
BISHOP:KOMBA AMEWATAKA WAKRISTO KUWA NA TABIA YA KUMSHUKURU MUNGU
Na. Kadala Komba Dodoma
Bishop: Sylvanus Komba wa kanisa la Mlima wa Bwana Assemblies of God Tanzania Dodoma Amewataka Wakristo kuwa na Tabia ya kumshukuru Mungu kwa kujibu maombi yao .
Bishop Komba Alisema Hayo Jumapili iliyopita wakati akifundisha Somo la Shukrani kanisani hapo Alisema Wapendwa naomba tujifunze kitu kutoka kwa yule mmoja (msamalia) aliyekumbuka kurudi kushukuru, Kushukuru ni kutambua thamani ya fadhira ulizotendewa, Kushukuru ni Kumpa moyo yule aliyekusaidia , Kushukuru ni kuonyesha Utu, Kushukuru ni kutambua msaada iliofanyiwa.
Akinukuu Maandiko matakatifu ya Mungu kwenye Biblia Luka 17:12.19
"Kumbuka kuwashukuru waliokusaidia ulipoumwa, Ulipotingwa na jambo fulani, kumbuka kuwashukuru waliokulipia ada yako ya masomo, kumbuka kuwashukuru waliokupa mtaji wa biashara usiwasahau ukadhani ni ujanja wako au juhudi zako hapana bila wao usingefika kumbuka kuwashukuru Ipo Nguvu kwenye Kushukuru jifunze Kushukuru kwa kila jambo hata kidogo Alisema.
Bishop: Komba Alisema Kiwango ulichotumia kutafuta msaada Kiwango hicho hicho utatumia kurudi, Nguvu kubwa uliyotumia kutafuta msaada tumia hiyo Nguvu kurudi kushukuru,Bidii yako wakati wa kutafuta bidii hiyo hiyo hata wakati wa kutenda Tengeneza tabia ya kurudi kushukuru Luka 17:12-19
Amesema Kiwango unachotumia kutafuta msaada Kiwango hiyo hicho utatumia kurudi, Wakati wa kuomba WAKIIMBA KWA sauti kuu
"Bidii yako wakati wa kutafuta bidii hiyo hata wakati wa kutenda
Tengeneza tabia ya kurudi kushukuru
2Nyakati wa 32 :24.25
Hapo ulipo sio kwa bidii yako wala wazazi wako ni Mungu Daniel 4:28.34 kutokuwa na shukrani kunabadilisha hata Chakula waka ratiba ya Kumshukuru Mungu Zaburi 21: 1.5
Mwisho Bishop: Komba Alitoa Wito kwa waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Alisema waimbaji wengi Mungu Amewabariki kwa sauti nzuri lakini nyimbo zao nyingi hawamtaji Mungu unakuta mwimbaji amefakikiwa kuandaa Albam ya nyimbo tena akafanya na uzinduzi Watumishi wa Mungu wakaiwekewa mikono ya Baraka, cha kushangaza ukija kusikiliza hizo nyimbo hakuna hata wimbo Mmoja ametaja jina la Mungu , hiki ni chanzo kikubwa cha Anguko la waimbaji wa nyimbo za Injili Mjitafakali, Wewe kama ni mwimbaji basi Nyimbo zako ziwe nyimbo za sifa za Kumshukuru Mungu,
kama ni Mtumishi wa Mungu umeombea watu wamefunguliwa sifa hizo sio zako ni za Mungu Alisema "NENO LA KUSIMAMIA KWENYE HILI SOMO NI KUMSHUKURU MUNGU NI LAZIMA"
Bishop: Sylvanus Komba wa kanisa la Mlima wa Bwana Assemblies of God Tanzania Dodoma Akihubiri kanisani hapo
Washirika wa kanisa la Mlima wa Bwana Assemblies of God Tanzania Dodoma Wakisikiliza injili
Wachungaji Mlima wa Bwana Assemblies of God Tanzania Dodoma
DKT. KIKWETE AONGOZA MBIO ZA JKT MARATHON.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza Viongozi, Majenerali, Maafisaa, Askari, Vijana, Watumishi na Wananchi mbalimbali katika Mbio za JKT Marathon Zilizofanyika jana Juni 25, 2023, Jijini Dodoma. Mbio hizo za Kilomita 5, 10 na 21 ziliazia na kutamatika kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Katika hotuba yake, Dkt Kikwete amepongeza Kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Pamoja na kumshukuru Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) kwa kumwalika ili awe Mgeni rasmi wa shughuli hiyo.
Dkt. Kikwete pia, amelitaka Jeshi, kupitia Wizara, lione uwezekano wa kufanya mbio za Marathon mara kwa mara Jijini Dodoma ili Wananchi waweze Kushiriki na kuimarisha afya zao.
Awali, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (Mb), amemshukuru na kumpongeza Dkt. Kikwete kwa kumuunga mkono Rais na Amri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyotoa hamasa kwenye Michezo nchini ikiwemo Jeshini.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, amepongeza kufaana kwa JKT Marathon 2023, aidha, alivutiwa na Kutoa zawadi kwa Mshiriki wa Mbio za Kilometa 5, aliyejitambulisha kwa Jina Mzee Mashaka, Kwa namna aliyokimbia na kumaliza ruti huku akiwahamasisha viongozi akiwemo Mgeni rasmi.
Nae, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda amesema Jeshi litaendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya michezo ndani na na nje ya Nchi.
Pamoja na mafanikio mengi kwa Wanamichezo Jeshini, Mkuu wa Majeshi pia ametumia fursa hio kuwapongeza Timu ya Jeshi ya Mashujaa fc, kwa kufuzu kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya kuifunga Mbeya City fc kwa uwiano wa magoli 4 kwa 1 baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini.
MAPOKEZI YA RAIS SAMIA KILIMANJARO
Mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan alipowasili Uwanja wa Ndege Kilimanjaro International Airport akiwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Kupiga vita Dawa za Kulevya ambayo Kitaifa yatafanyika Juni 25 mwaka huu katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Juni 24,2023
KAMATI YA UFUNDI YA SERIKALI MTANDAO YAFANYA KIKAO CHA KWANZA JIJINI DODOMA
Kamati ya ufundi ya serikali mtandao imefanya kikao cha kwanza na kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya utekelezaji wa majukumu yake, ili kuhakikisha jitihada za serikali mtandao zinaimarika na kuleta tija kwa Umma.
Kikao hicho kilifanyika jana, katika Ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) jijini Dodoma, na kuongozwa na Kaimu Mwenyekiti Bw. Eric Kitali Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Eric alisema kamati hiyo ipo kwa mujibu wa kifungu Na. 17 cha sheria ya Serikali Mtandao ya mwaka 2019, ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kutoa ushauri wa kitaalamu, ili kuhakikisha utekelezaji wa Serikali Mtandao unakuwa ni wenye tija na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma.
Alisema kuwa, kamati hiyo ina wajumbe wachache ikilinganishwa na idadi ya Wizara na Taasisi za serikali zilizopo, na kuwasihi wajumbe wote kutenda haki kwa kuwajibika na kuhakikisha wanatoa ushauri wenye tija katika eneo la TEHAMA ili kuhakikisha serikali mtandao inaimarika na kuleta tija kwa Serikali.
“Ikiwa kamati hii itafanikiwa kuifanya mifumo ya TEHAMA katika taasisi za umma izungumze tutakuwa tumeisaidia sana serikali, kwani itaokoa rasilimali fedha pamoja na rasilimali watu”, alisisitiza.
Akiyataja baadhi ya majukumu ya kamati hiyo kwa mujibu wa kifungu Na 17 (4) cha Sheria ya Serikali Mtandao ya mwaka 2019, Katibu wa Kamati hiyo Bw. Sylvani Shayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa TEHAMA e-GA alisema ni pamoja na; kupitia na kutoa mapendekezo juu ya Sera ya Serikali Mtandao itakayotekelezwa katika taasisi za umma, kupitia na kutoa mapendekezo juu mpango mkuu wa Serikali mtandao na mkakati wake utakaotekelezwa na taasisi zote za umma, kupitia na kutoa mapendekezo juu ya miradi na program za kitaifa za serikali mtandao, na kutoa miongozo ya kiufundi katika kutatua migogoro kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya TEHAMA katika taasisi za umma.
Majukumu mengine ni kuishauri kamati ya kitaifa ya serikali mtandao kuhusu masuala ya serikali mtandao, kuandaa ripoti za robo mwaka na kuziwasilisha katika kamati hiyo, pamoja na kutekeleza majukumu mbalimbali yatakayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao na kamati ya kitaifa ya Serikali Mtandao.
Aidha, kamati hiyo iliazimia kuweka mikakati ya kupunguza urudufu wa mifumo na kuhakikisha mifumo yote ya TEHAMA, katika taasisi za umma inawasiliana na kubadilishana taarifa kupitia Mfumo Mkuu wa ubadilishanaji taarifa serikalini (GoVESB).
Katika hatua nyingine, kamati ilimchagua Bi. Connie Francis Mkurugenzi wa TEHAMA Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Wajumbe wa kamati hiyo ni Wakuu wa TEHAMA kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti Bw. Priscus Kiwango kutoka Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Katibu Bw. Sylvani Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa TEHAMA Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).
Wajumbe wengine ni kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Uratibu na Bunge, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Wizara ya Maji, Mamlaka ya Serikali Mtandao (wajumbe 02), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), The Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Ufilisi na udhamini (RITA), Idara ya Uhamiaji, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, na Wizara ya Kilim
o.
BUI POWER AUTHORITY IMPROVES OPERATIONAL COVERAGE USING HUAWEI ELTE SOLUTION
[Accra, Ghana:
The International Renewable Energy Agency estimates that Africa’s renewable energy capacity could reach 310GW by 2030, catapulting the continent into the top tier of green energy production. The Bui Power Authority (BPA) hydro-solar hybrid power plant in Ghana is leading the way in Sub-Saharan Africa, with essential communication and operational management services provided across Huawei’s eLTE Broadband Network.
Ghanaian Energy Minister Dr. Matthew Opoku Prempeh underscored the importance of ICT systems in providing intelligent energy management critical for ensuring efficient power generation, power plant operations, and power distribution. They enable renewable energy to be integrated into the grid for the reliable, stable access and supply needed in order to achieve the country’s goal of universal electricity access by 2025.
Dr. Prempeh made the statement when the Bui Power Authority put into operation a broadband private network built by Huawei at its generating station at Bui.
“As Ghana is striding towards achieving universal electricity access by 2025, it is important for us to unleash the transformational power of ICT in optimizing the operations at power plants, increasing the efficiency of renewable energy use, and ensuring a stable and cost-effective electricity supply to many more households nationwide,” said the minister.
Bui Authority and Huawei have built an eLTE broadband private network that penetrates the substantial concrete barriers and infrastructure at Bui Power Plant, in Ghana. This is the first time that Huawei has deployed an eLTE-based solution in the hydroelectric industry. The network, which carries voice, video, and data services, enables instant communication between the control room and maintenance staff moving around the plant. It covers, without extensive cabling and installation, both indoor and outdoor working areas, including roadways inside the dam, generator rooms, and employee living areas within the Bui vicinity.
More digital applications to come
With features like “push-to-talk” and group calls for both voice and video, the private network makes routine maintenance and handling of emergencies easier and more efficient at the power plant.
“Now staff can communicate via video call to fix maintenance challenges in record time”, said a Huawei engineer. “Building modern networks also provide capacity for growth, enabling the intelligent digital transformation of the site in the future.”
Hydro-solar hybrid system
Clean energy is becoming increasingly important in Ghana's national energy mix, as Ghana's National Energy Plan aims to achieve a 10% penetration of renewable energy by 2030. The role of the Bui Generating Station as an important provider of hydroelectric power in the country has been further strengthened and complemented with a new installation of solar power generation capability.
In October 2019, construction commenced on the first phase of the 250MW project with the development of a Solar PV Facility. Additionally, the Bui Power Authority (BPA) has commissioned a 5MW Floating Solar Plant which is the first in the Sub-Saharan region and supplies power through the Bui Switchyard to the National Interconnected Transmission System (NITS).
Powering Development in Northern Ghana
The Bui Generating Station produces 404MW of hydropower. An additional 50MW of power is generated from the solar installations on site, with the total renewable power output contributing around 6-7% of the total power generated in-country. This is expected to reduce greenhouse gas emissions by more than 47,000 tons per year.
The country is keen to take advantage of the reservoir created by the Bui Generating Station to promote fishing in the reservoir and the irrigation of over 30,000 hectares of land for crops, including maize, cashew, and sugar cane.
The BPA is collaborating with strategic private investors for the running of a local cashew processing plant and sugar mill within the Bui vicinity. This intervention is aimed at developing agriculture in Ghana, boosting employment, and thus improving the lives of local people.
HUAWEI UNLEASHERS AFRICA'S DIGITAL FUTURE THROUGH FULL UTILISATION OF SUB-3GHZ DURING A BETTER AFRICA SPECTRUM PRACTICE ROUNDTABLE
Opening Ceremony: Jacob Munodawafa, Executive Secretary of Southern Africa Telecommunications Association (SATA)
...........
(MAPUTO, The critical annual Africa Spectrum Roundtable, one of the continent’s most important spectrum events, took place in Maputo, Mozambique recently. The event brought together regulators, operators and spectrum industry leaders from all over Africa.
Jacob Munodawafa, Executive Secretary of the Southern Africa Telecommunications Association (SATA) gave an overview of the key spectrum opportunities and challenges for lobbying investment and improving mobile service levels. He also spoke about what SATA believes should be the spectrum short, medium and long term targets for the region.
Mr. Munodawafa thanked all those who participated in the roundtable and encouraged stakeholders to look at the best way forward for the delivery of a spectrum strategy that works for Africa.
During the conference’s opening session, Mr. Yang, Vice President of Huawei Sub-Saharan Africa ICT Solution Department delivered a presentation titled “The unique potentials of Sub-3GHz to meet the realistic demand in the Africa region” in which he outlined Huawei’s latest spectrum concepts and unpacked successful digital transformation spectrum solutions.
“We experienced strong demand growth to improve the last-mile broadband infrastructure which bridges the digital divide between urban and rural areas. Sub-3GHz spectrum’s full utilisation will be the best way forward,” he added.
As Africa’s digital ship sails into the future, it will require a strong tailwind to propel it forward. Mr. Yang called for more favourable industrial spectrum policies in Africa in order to take full advantage of the Sub3-Ghz band.
Mr. Dick Sono, Chief Director: Radio Frequency Spectrum from South Africa’s Ministry of Communications and Digital Technologies shared the department’s best practice under the theme of “Mapping the potential evolution of the Sub-3GHz band in the Africa region”. Mr. Sono detailed South Africa’s achievements in the country’s progress towards the contribution of spectrum allocation to society for affordable, universal 4G mobile broadband and 4G FWA home broadband. Coverage for the South African population has improved, reaching over 98% with the full allocation of LTE FDD mid and low-band coverage, and boosting TDD band to uplift home broadband rates for households where there is no access to fibre.
Regulation experts from Mozambique also shared successful case studies which have contributed to the country’s ICT development. Mr. Lui-S CUMAIO said there is pressing demand for spectrum in Sub-3GHz, the most urgent requirement for 4G capacity. Currently there is only universal coverage with low band spectrum.
INCM encourages operators to use 2.6 GHz as the dedicated spectrum with the most cost-effective 4G FWA for HBB service because of the low home broadband penetration rate in Mozambique.
Following the discussion, an agreement on a common initiative was released which includes:
Ÿ Full allocation of FDD (Frequency Division Duplex) Sub-3Ghz for affordable and universal mobile broadband towards closing the digital gap and fueling Africa’s digital future.
Ÿ Full utilisation of 2.3/2.6G TDD Bands for further mobile broadband improvement.
Ÿ Adoption of defragmentation practices with win-win cooperation between ISP’s/regional MNOs and large MNOs (Mobile Network Operators).
Ÿ Overall development of 4G/5G FWA in order to uplift overall national broadband penetration rates.
Ÿ Tax incentives and rebates, affordability considerations for both devices and services, digital literacy for rural and underserved areas.
WAZIRI WA MAJI AWESO AMETENGUA UTEUZI WA MENEJA WA MAJI MKOA WA DODOMA
Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa H. Aweso (Mb) ametengua uteuzi wa Meneja wa Maji Mkoa wa Dodoma, (RUWASA) Mhandisi Godfrey Kabula Mbabaye kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Waziri Aweso amechukua hatua hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019,
Aidha, Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba kuunda timu ya Wataalam ya kufuatilia changamoto ya utekelezaji wa Miradi ya Maji kwa Mkoani Dodoma na kutoa suluhisho la kumaliza changamoto hizo mara moja.
Vilevile, ameelekeza timu hiyo ya Wataalam itakayoundwa na katibu Mkuu ifanye tathimini ya utendaji kazi wa Mameneja wa Wilaya zote wa Maji Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma.
Waziri Aweso amechukua hatua hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019,
KATAMBI AMEWATAKA WAKURUGENZI WAKUU WA MIFUKO YA PENSHENI KUHAKIKISHA MWANACHAMA ANALIPWA NDANI YA SIKU 60.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe.Patriobas Katambi amewataka Wakurugenzi wakuu wa Psssf na Nssf kuhakikisha kila mwanachama analipwa ndani ya siku 60 za kisheria kwa wanachama wote ambao nyaraka zao zimewasilishwa kwenye mfuko kwa ukamilifu.
Mhe.Katambi ameyasema hayo wakati akielezea changamoto wanazokutana nazo baadhi ya wanachama na wastaafu wanapofuatilia mafao kwenye mifuko ya pensheni katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dodoma.
Aidha amewataka Wakurugenzi Wakuu wa mifuko hiyo kuhakikisha mameneja wote wa mikoa wanasikiliza na kutoa elimu kuhusu taarifa za wanachama(michango na mafao)pamoja na kuhakikisha hakuna malalamiko ya wanachama katika mikoa wanayoongoza.
"Wakurugenzi wakuu nataka kuhakikisha waajiri wote wanalipa na kuwasilisha madeni ya michango ya watumishi wao kila mwezi,kila meneja wa mkoa awasilishe majina ya waajiri sugu wanaodaiwa michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku saba kuanzia leo"Amesisitiza Katambi
Aidha ameongeza kuwa Watumishi wa mifuko watapandishwa vyeo kwa kuzingatia utendaji na uwajibikaji katika kuwahudumia wateja(wanachama).
" Nafahamu Pssf na mamlaka za serikali za mitaa mko katika zoezi la kusaini mikataba ya kulipa madeni ya michango ya wanachama,hivyo ninaagiza mfuko na wahusika kukamilisha haraka zoezi hilo kabla ya tarehe 30 Juni 2023"
"Jana katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni nilitoa namba yangu ya simu, hadi kufikia leo asubuhi nimepokea jumbe za simu 28 ambapo zinahusu Nssf na Psssf 20 na tayari zimefanyiwa kazi na kukamilika" Amesema Katambi
Kupitia simu janja unaweza kujisajili na kwenye application ya mfuko na kuweza kuangalia michango yako kama inawasilishwa,kupata taarifa yako ya malipo ya pensheni na taarifa nyingine ya uanachama wako kwenye mfuko wa Psssf.
Sanjari na hayo Nssf taarifa kupitia simu janja mwanachama anaweza kujisajili kwenye mfuko application ya mfuko na kuweza kupata taarifa ya michango yako na kupata taarifa mbalimbali zinazomhusu mwanachama.
Aidha mifuko yote tayari ina dawati la malalamiko katika ofisi zake nchi nzima.
*TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI AFCON 2023, YAIFUNGA NIGER 1-0*
Na Eleuteri Mangi, WUSM Dar es Salaam
Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imeicharaza timu ya Niger goli 1-0 na kufufua matumaini ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 nchini Ivory Coast.
Saimon Msuva mfungaji wa goli hilo ndiye shujaa wa mchezo huo uliochezwa Juni 18, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewaongoza watanzania kuishangilia timu yao akiwa Mgeni Rasmi katika mchezo huo hatua iliyoongeza hamasa.
Mchezo huo umeshuhudiwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Wales Karia.
Tanzania ipo kundi F pamoja na timu za mataifa ya Algeria, Niger na Uganda kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA YOGA DUNIANI
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam
Tanzania imeadhimisha Siku ya Yoga Duniani huku Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikisisitiza kuunga mkono sherehe za kitamaduni za mataifa mbalimbali duniani kwa sababu zinasaidia kujenga jamii ya kimataifa kuwa wamoja.
Hayo yamsemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Yoga Duniani ambayo huadhimishwa Juni 18, kila mwaka ambapo kwa Tanzania yamedhuiriwa na watu mbalimbali ambao wamefanya mazoezi ya Yoga kwa pamoja katika viwanja vya Gym Kana jijini Dar es salaam.
“Huu ni mwaka wa tisa sasa tangu Umoja wa Mataifa ulipotambua na kuupa mchezo wa Yoga siku maalum, Ubalozi wa India umeandaa sherehe hizi ambazo zimehuidhuriwa na watu zaidi ya 1000 kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo India na Tanzania” amesema Bw. Yakubu
Mchezo wa Yoga asili yake ni India unaosaidia kuufanya mwili kuwa imara kwa kupata mazoezi kuanzia kichwani hadi miguuni hatua inayofanya mwili kuwa imara na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Miongoni mwa washiriki wa maadhimisho hayo ni Balozi wa India nchini Bw. Binaya Srikanta Pradhan na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini nchini Bw. Zlatan Milišić ambapo kwa Tanzania Siku ya Yoga imeadhimishwa katika mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Arusha, Zanzibar na Kilimanjaro.
WAZIRI UMMY AMETOA WITO KWA MADAKTARI BIGWA UPASUAJI KUFANYA KAZI MIKOA YOTE.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa wito kwa madaktari bigwa upasuaji kufanya kazi mikoa yote na kuhakikisha wanazalisha wataalamu wazuri kwani kuna uhaba wa madaktari bigwa wa upasuaji nchini.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa mkutano wa mwaka na kongamano la kisayansi linalohusisha chama cha madaktari wa upasuaji Tanzania lililofanyika St.Gasper Hotel jijini Dodoma.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wakati umefika wa madaktari kupangiwa vituo vya chini vya afya huku akihimiza kuwa hospitali kubwa za rufaa zisiwe sehemu za kuanzia ajira.
"Ningependa kuwashauri na kuwahimiza madaktari bigwa wa upasuaji kuanzia chini kabisa na sio kukimbilia hospitali za rufaa kwani huku chini ndio tuna wananchi wenye uhitaji zaidi kwani tumeshuhudia baada ya wananchi kukosa huduma hizi ndipo huamua kwenda hospitali za rufaa hivyo ningewaomba muanzie huku chini na sisi kama serikali tupo tayari kutoa ushirikiano pale mnapotuhitaji" Amesisitiza Waziri Ummy.
Aidha ameongeza kuwa kuhusu suala la kusambaza madaktari bigwa wa upasuaji mikoani watafatilia kazi na kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyakazi.
Kwa upande wake rais wa Chama cha madaktari bigwa wa upasuaji Tanzania Prof.Larry Akoko amesema kuwa wakati umefika serikali kuangalia namna ya kuboresha mikataba pamoja na kuipa kipaumbele tasnia ya udaktari pamoja na kusisitiza masuala ya maadili kwenye kazi kwa sababu wamekuwa wakiletewa malalamiko mengi.
Kauli mbiu ya mkutano na kongamano hilo la chama cha madaktari bigwa wa upasuaji Tanzania (TSA) ni kujenga mfumo wa utoaji huduma za upasuaji madhubuti unaofikika na wenye gharama nafuu Tanzania.
RC SENYAMULE VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA YA AFYA BONANZA KUPIMA AFYA ZAO.
Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa za Afya Bonanza ili waweze kupima afya zao na kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
Senyamule ametoa wito huo Juni,14,2023 katika ufunguzi wa Bonanza la Afya Mkoa wa Dodoma uliofanyika katika shule ya Msingi Chang’ombe na kufanikiwa jumla ya watu 721 hasa vijana kufikiwa na elimu kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
“Nikipiga hesabu za haraka haraka ,tunategemea katika bonanza hili kufikia vijana 6000 katika mkoa wa Dodoma kwa kata 28,tumieni fursa kuja kushiriki bonanza hili ili kupata elimu ya afya kwa vijana na huduma zinazotolewa kwa Jiji la Dodoma ,na kila mmoja akielimisha kijana tutafikia vijana 30,000”amesema Senyamule.
Aidha,Mkuu huyo wa Mkoa amesema mada zinazotolewa ikiwemo elimu ya afya ya uzazi,lishe, ukatili wa Kijinsia ina umuhimu mkubwa katika makundi mbalimbali ya watu hususan Vijana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Watoto na Vijana kutoka Wizara ya Afya Dkt.Felix Bundala amesema kama Wizara wameamua kuwekeza nguvu zaidi kufikisha elimu ya afya na huduma kwa vijana ikiwemo namna ya kujikinga na UKIMWI na Mimba za Utotoni.
“Tumeamua kuangalia namna ya kufikisha elimu kwa vijana ikiwemo mimba za utotoni,ukatili wa kijinsia,Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza ,lishe ,Madhara ya dawa za kulevya,afya ya akili”amesema.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.Best Magoma amesema Bonanza hilo litaleta tija kubwa kubwa kwa Vijana
Nao baadhi ya vijana wa Chang’ombe akiwemo Furaha David, Juma Athuman, pamoja na Mwajuma Hassan wamesema bonanza hilo limekuwa na manufaa makubwa kwao huku wakiiomba Wizara ya Afya kuendelea kuwezesha mabonanza kama hayo mara kwa mara .
“Kwa kweli kupitia bonanza hili la Afya nimeipongeza Wizara ya Afya kwanza imenipunguzia gharama Kwenda hospitalini lakini hapa vipimo nimepata bure na elimu ya afya imekuwa na msaada kwangu kujua namna cha kufanya”amesema Furaha David.
Ikumbukwe kuwa katika bonanza hilo la Afya mbali na utoaji wa elimu na huduma, michezo mbalimbali imefanyika kwa vijana ikiwemo mpira wa miguu,pete,kukimbiza kuku huku jumla ya watu 721 kata ya Chang’ombe wakifikiwa elimu ya afya kupitia bonanza hilo .
Kuhusu masuala ya lishe jumla ya watu 71 wamepimwa huku asilimia 15% wakigundulika kuwa na utapiamlo, 22% uzito uliozidi, magonjwa yasiyo ya kuambukiza jumla ya watu 68 wamepimwa ambapo Shinikizo la Juu la damu wamebainika watu watano(5),shinikizo la chini la damu wakibainika watu 2 na afya ya akili wakibainika watu watatu(3).
Katika ushauri nasaha jumla ya watu 66 wamepata ushauri nasaha na kuweza kupima Virusi vya UKIMWI ambapo hakuna hata mmoja aliyebainika kuwa na maambukizi huku katika suala la ukatili wa kijinsia(Gender Based Violence- GBV vilevile watu 66 wamepatiwa elimu hiyo huku mmoja akibainika kufanyiwa vitendo vya kikatili .
Halikadhalika, katika bonanza hilo la afya kupitia Wizara ya Afya ,Idara ya Huduma za Mzazi, Mama na Mtoto kwa kushirikiana na Elimu ya Afya kwa Umma,Ofisi ya Rais-TAMISEMI, chini ya uwezeshaji wa Mfuko wa Dunia( Global Fund) linafanyika katika mikoa mitano(5)halmashauri 18 lengo ni kufikia watu 15,000 katika mikoa hiyo,watu 833 kila Halmashauri na watu 208 katika kila kata .
Kwa mkoa wa Dodoma malengo ni kufikia watu 500 kila kata ambapo Kata ya Chang’ombe imevuka lengo na kufikia watu 721 na siku ya Juni 15.2023 bonanza litaendelea katika kata ya Kikuyu.
MWISHO.
SERIKALI KUJENGA KIWANJA KIPYA CHA MICHEZO JIJINI ARUSHA
Na Eleuteri Mangi, WUSM, ARUSHA
Mkoa wa Arusha umepewa dhamana kubwa ya kitaifa ya kujengwa kiwanja kipya cha michezo na kufanya Tanzania kuwa na viwanja vitatu vinavyokidhi vigezo na mahitaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili kuandaa mashindano ya AFCON 2027 katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Akikagua eneo kitakapojengwa kiwanja hicho kata ya Olmoti jijini Arusha la Juni 13, 2023, Mkuu wa mkoa huo Bw. John Mongela amesema mkoa umepokea mradi huo kwa mikono miwili na watatekeleza azma ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa barani Afrika.
“Tunamshukuru Rais kwa moyo wake wa uzalendo wa kuwaletea watanzania maendeleo makubwa, Uwanja huu utabadilisha sana sura ya Mkoa wa Arusha na kuiweka kwenye ramani ya dunia, tutatekeleza maelekezo ya Wizara yetu ya michezo, maelekezo ya TFF, mwongozo wa Mhe. Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na mamlaka zote. Sisi kama mkoa tutafanya linalowezekana jambo hili lifanikiwe” amesema Bw. Mongela.
Ili kufikia azma ya Tanzania kuwa wenyeji wa AFCON 2027 kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda, tayari Kiwanja cha Benjamin Mkapa cha Dar es salaam kimeanza kufanyiwa ukarabati mkubwa pamoja na Kiwanja cha Amani Zanzibar hatua itakayofanya Tanzania kuwa na viwanja vitatu vinavyokidhi ubora kulingana na Sharia na Kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na mashindano mengine duniani.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua eneo kitakapojengwa kiwanja cha kisasa cha michezo katika jiji la Arusha ambayo ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON 2027.
“Huu ni ukaguzi wa awali wa eneo utakapojengwa uwanja wa michezo hapa Arusha, Sisi Wizara tunawaahidi wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na Watanzania kwa ujumla kuwa tutajenga kiwanja cha kisasa chenye uwezo wa kuchukua watu 30,000,000 ambacho kina uwezo wa kuchezwa mechi za CAF na mechi ambazo zinatambuliwa na FIFA” amesema Bw. Yakubu.
Aidha, ziara hiyo imeshirikisha Uongozi wa mkoa wa Arusha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw. Wales Karia pamoja na viongozi wa taasisi zote ambazo zitakuwa na miundombinu muhimu ya kuhudumia kiwanja hicho.
𝗧𝗔𝗔𝗦𝗜𝗦𝗜 𝗭𝗔 𝗨𝗠𝗠𝗔 𝗭𝗔𝗛𝗜𝗠𝗜𝗭𝗪𝗔 𝗞𝗨𝗘𝗡𝗗𝗘𝗦𝗛𝗔 𝗩𝗜𝗞𝗔𝗢 𝗞𝗪𝗔 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗧𝗔𝗡𝗗𝗔𝗢 𝗞𝗨𝗣𝗨𝗡𝗚𝗨𝗭𝗔 𝗚𝗛𝗔𝗥𝗔𝗠𝗔
Meneja Mawasiliano Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Bi. Subira Kaswaga, amezitaka Taasisi za Umma nchini kuendesha vikao kidijitali kwa kutumia mfumo wa e-Mikutano ili kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao.
Kaswaga alitoa rai hiyo jana, alipofanya mazungumzo na mwandishi wetu ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu faida zitokanazo na mfumo wa e-Mikutano.
Alibainisha kuwa, mfumo wa e-Mikutano unawawezesha watumishi wa Taasisi za umma kufanya vikao kidijitali mahali walipo bila kulazimika kukutana mahali pamoja na hivyo kusaidia kupunguza gharama za uandaaji na uendeshaji wa vikao.
“Mfumo huu wa e-Mikutano unazisaidia taasisi za umma kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao, kwani watumishi hawalazimiki kusafiri na kukutana mahali pamoja ili kufanya vikao na badala yake wanaweza kufanya vikao mahali walipo”, alisisitiza.
Aliongeza kuwa, mfumo wa e-Mikutano huokoa muda ambao watumishi wangeutumia kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa ajili ya kufanya vikao na hivyo kutumia muda huo kutekeleza majukumu yao mengine hali inayopelekea kuongeza ufanisi.
“Mfumo huu pia unasaidia kupunguza au kuondoa kabisa gharama za kulipia leseni zinazohitajika ili taasisi za umma ziweze kutumia mifumo ya uendeshaji wa vikao kidijitali iliyojengwa na makampuni binafsi”, alifafanua.
Alisema, Mamlaka ya Serikali Mtandao ilitengeneza Mfumo wa e-Mikutano, baada ya kuona uhitaji mkubwa wa matumizi ya TEHAMA kwenye eneo la kuratibu mikutano kwa watumishi wanaokuwa katika mazingira tofauti.
Mfumo wa e-Mikutano ni rahisi na rafiki kutumia kwani mtumishi yeyote wa umma mwenye barua pepe ya serikali (GMS), anaweza kuandaa kikao na kualika washiriki wengine, na pia mfumo unawezesha kuwasiliana kwa njia ya sauti na video, alifafanua.
Mfumo wa e-Mikutano umetengezwa na wataalamu wazawa kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na pia ni mfumo salama kwakuwa, umetengezwa kwa kuzingatia usalama mkubwa kwa watumiaji.
UCHUNGUZI WA KIIKOLOJIA KUHUSU UGONJWA WA VIRUSI VYA MARBURG WAANZA KAGERA.
Na Mwandishi wetu - Kagera
Wataalam kutoka Wizara za kisekta chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameanza uchunguzi wa Kiikolojia kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Marburg baada ya ugonjwa huo kutokomezwa Nchini.
Wataalamu wanaounda timu wanatoka ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ofisi ya Waziri Mkuu ( Menejimenti ya Maafa), Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori (TAWIRI), na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI)
Watalam hao ambao wamekutana Mkoani Kagera wanalenga mufanya uchunguzi wa kiikolojia ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kimataifa ya kufanyika kwa shughuli mbalimbali za ufuatiliaji baada ya ugonjwa huo kutoweka.
Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Prudence Constantine amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imeratibu sekta na Taasisi mbalimbali kufanya uchunguzi wa kiikolojia ili kubaini uwepo wa Wanyama wanaoweza kuhifadhi Virusi vya Marburg na mwingiliano wao na wanadamu ambapo Uchunguzi huu ni moja kati ya juhudi za pamoja za kuendelea kujua chanzo cha tatizo, kujiandaa, kukabiliana na dharura za kiafya ikiwemo endapo zitajitokeza.
"Wizara ya Afya imeainisha uchunguzi huu kati ya kazi muhimu zinazotakiwa kufanyika ndani ya mpango wa siku 90 wa kurejesha hali Mara baada ya mlipuko wa Marburg ulipotangazwa kuisha".ameeleza Mkurugenzi Prudence
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera ,Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Issessanda Kaniki amesema baada ufuatiliaji wa mbinu za utafiti na vipimo ndani ya siku 42 tumeweza kuudhibiti ugonjwa huo hivyo hadi sasa hakuna Mgonjwa hata mmoja.
"Baada ya Ufuatiliaji lakini pia na mbinu mbalimbali za Utafiti Mkoa wa Kagera pamoja na Nchi tunazopakana nazo kwa sasa mlipuko wa Ugonjwa wa Marburg haupo tena".Amesema Dkt. Kaniki.
Uchunguzi huu wa Kiikolojia utakaofanyika kati ya tarehe 12 na 24 Juni, 2023 utahusisha uchukuaji wa sampuli za Wanyamapori, wanyama wa kufugwa pamoja na kufanya utafiti shirikishi jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Muleba na Kyerwa.
Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Prudence Costantine akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Ziara ya kufanya uchunguzi wa kiikolojia ili kubaini uwepo wa Wanyama wanaoweza kuhifadhi Virusi vya Marburg na mwingiliano wao na wanadamu katika Mkoa wa Kagera
MEJA JENERALI MBUGE “TUIMARISHE USHIRIKIANO KUKABILI MAJANGA”
Na Mwandishi wetu- Singida
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta mbalimbali katika kukabiliana na maafa ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira salama.
Kauli hiyo imetolewa Juni 12, 2023 mkoani Singida na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge wakati akifungua kikao kazi cha Watalam waliokutana kwa lengo la Kuhuisha na Kutafsiri Mwongozo wa Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja.
Meja Jenerali Mbuge amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la mwingiliano wa binadamu, wanyama na mazingira ambao husababisha kutokea kwa magonjwa mbalimbali yanayotoka kwa wanyama na kwenda kwa binadamu hivyo ipo haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa sekta mbalimbali katika kujiandaa, kuzuia na kukabiliana na majanga hayo.
“Tunahuisha mwongozo huu kwa sababu ya mabadiliko ya sheria na kanuni za usimamizi wa Maafa. Mwongozo huu ni muhimu katika kurahisisha ushirikiano wa kisekta ili kujenga na kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya milipuko ya magonjwa na dharura zingine zenye madhara kwa afya ya binadamu, wanyama na mazingira,” Amesema Meja Jenerali Mbuge.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa husisitiza yakiwemo Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Wanyama (WOAH) na Programu ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa (UNEP) kwa pamoja husisitiza ushirikiano wa sekta mbalimbali ili kuwa na mikakati na sera za pamoja katika kuimarisha afya ya wanadamu, wanyama na mazingira.
“Ili kutekeleza dhana ya Afya moja, ni muhimu kuwa na miongozo mbalimbali ili kurahishisha uratibu na utendaji katika ngazi zote. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru FAO ambao walianzisha mchakato wa kutengeneza mwongozo huu ambao katika kikao hiki utauhuishwa na kutafsiriwa,” Ameeleza.
Aidha amebainisha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa ina wajibu wa kuratibu utekelezaji wa dhana ya Afya Moja kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ya 2004, Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya Mwaka 2022 na kanuni zake za mwaka 2022 pamoja na Mkakati wa Afya Moja 2022-2027.
Baadhi ya Wataalam kutoka sekta mbalimbali wakifuatilia kikao kazi cha Watalam waliokutana kwa lengo la Kuhuisha na Kutafsiri Mwongozo wa Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja mkoani Singida.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watalam waliokutana kwa lengo la Kuhuisha na Kutafsiri Mwongozo wa Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja mkoani Singida.
Afisa Kiungo wa Afya Moja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Justine Assenga akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mratibu wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Valentina Sanga akiwasilisha Mwongozo wa Utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja .
(OFISI YA WAZIRI MKUU)
SERIKALI YAWATAKA WAFUGAJI WA KUKU KIJISAJILI
Hayo yamesemwa na Bi. Afsa Milandu Kaimu Meneja wa Idara ya Usajili na Udhibiti Ubora kutoka Bodi ya Nyama Tanzania wakati akifungua warsha ya siku moja ya wafugaji wa kuku wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa niaba ya Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Bw. John Chasama. Warsha hiyo imefanyika Leo tarehe 09/06/2023 jijini Dar es Salaam.
Bi. Milandu amesema Wadau wa Ufugaji kuku wamekutanishwa kwenye warsha hiyo ili kuwapa elimu itakayowawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi Ubora.
"Tumewakutanisha ili kutoa elimu na pia kuwapa taarifa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika utakaofanyika mwezi Septemba. Elimu tuliyoitoa leo itawasaidia wafugaji wa kuku wa nyama kufahamu taratibu za kusajiliwa na Bodi ya Nyama ili kutambulika na kuwezeshwa kupata mafunzo ili kuzalisha bidhaa bora na salama na kuzingatia vigezo vya ufugaji" amesema Bi. Milandu.
Bi. Milandu ameongeza kuwa mfugaji aliyesajiliwa na Bodi ataweza kupata taarifa kuhusu masoko au sehemu sahihi za kununua vifaranga vitakavyomzalishia bidhaa bora na kumwezesha mfugaji kuuza Nyama ya kuku iliyo salama.
Naye, Dkt. Mwajuma Chaurembo kutoka Ofisi ya Huduma za Magonjwa ya Mifugo (ZBC) amesisitiza kuwa ni wajibu wa mfugaji wa kuku kujisajili na kuhakikisha anapata kifaranga bora na kutoka kampuni gani ili kumwezesha pale anapopata changamoto kusaidiwa kirahisi na Bodi ya Nyama Tanzania.
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa kuku Tanzania Bw. Agusta Mrema ameishukuru Bodi ya Nyama Tanzania Kwa kuandaa warsha hiyo na kutoa rai kwa wafugaji wa kuku kujisajili ili kupata fursa na msaada hususan wa kisheria kutoka Bodi ya Nyama Tanzania pale wanapopata changamoto za kiufugaji.
Bw. Mrema amesema "Wadau wote tujiunge, tujisajili kwenye Bodi na vyama vya ufugaji ili tusipitwe na fursa kama hizi za kupatiwa elimu ya ufugaji.
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Bodi ya Nyama Tanzania imehudhuriwa na wafugaji wa kuku zaidi ya 150 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
SENYAMULE ATETA NA WAFANYABIASHARA
Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekutana na wafanyabiashara wa Mkoa wake kwa lengo la kujadili changamoto za biashara kwa ujumla na kuweka maazimio yenye tija katika kukuza masoko kwa kutumia fursa zilizopo ndani na nje ya nchi.
Kikao hicho kimefanyika Juni 8, 2023 katika Ukumbi wa jiji Mkoani humo na kuhudhuriwa na wafanyabiashara wakubwa, wakati na wadogo wakiwemo viongozi wa masoko, wamiliki wa shule, wamiliki wa Nyumba za wageni, Viongozi wa makampuni mbalimbali, wauza vipodozi na wafanyabiashara wa Mbao. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na TANROADS, TRA, OSHA, TBS, LATRA, BRELA na Tanzania Commercial Bank (TCB).
Awali wafanyabiashara walifanikiwa kutoa changamoto mbalimbali zinazowakabili ndani ya masoko zikiwemo ulipishwaji wa kodi ya pango ikiwa siyo wamiliki wa nyumba, wingi wa kodi kwa wafanyabiashara, ubovu wa miundombinu ikiwemo barabara, upungufu katika kaguzi za risiti, mfumo wa ulipaji kodi usio rafiki na changamoto za uzoaji wa taka na maji taka.
"Sisi Mkoa wa Dodoma tuna dhamira ya kuhakikisha wafanyabiashara wanakaa katika Mazingira mazuri na tunajipanga kufanyia kazi changamoto na maazimio ili kuendelea kuboresha huduma katika nyanja zote "amesema Senyamule
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa huyo ametoa rai kwa wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi kwa Serikali na kuwahakikisha uwepo wa Mazingira rafiki ya biashara ikiwa ni utekelezaji wa agizo na maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amewataka kuunda umoja kulingana na biashara wanazofanya ili iwe rahisi kuratibu hoja zinazojitokeza na kuziwasilisha Serikalini.
Nae, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amewapongeza wafanyabiashara kwa kujumuika pamoja katika kuwasilisha changamoto zilizopo ndani ya masoko na kuweka kwa pamoja mikakati ya ufumbuzi na amewasisitiza kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu.
"Serikali itahakikisha eneo letu la Makao Makuu ni sehemu sahihi na wezeshi kwa wafanyabiashara, lazima kuwa na mahali sahihi pakufanya biashara eneo ambalo halitakuwa na changamoto ili biashara ziweze kushamiri na kuweza kupata faida ninyi kwa mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla" Amesema Gugu
Kikao hicho, kiliazimia maazimio ambayo yataboresha biashara zao ikiwa ni pamoja na Halmashauri kuchukua hatua madhubuti kwa wanaomiliki vizimba na kutofanya biashara, kuundwa kwa timu itakayopitia Sheria ya kodi ili kuunganisha Serikali na sekta binafsi na kuundwa kwa kamati ya utatuzi wa changamoto za masoko kama ilivyokuwa kwa soko la Machinga.
Maazimio mengine yaliyokubalika ni pamoja na kuwepo kwa taasisi moja ya kukusanya tozo, Jiji kukamilisha miundombinu kwenye baadhi ya masoko na kutoa elimu kwa umma hususan wafanyabiashara kuhusu matumizi ya mfumo wa TAUSI.
SAKATA LA BANDARI MSUKUMA AWATOA HOFU WATANZANIA.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amewatoa hofu watanzania kuhusiana na kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya viongozi wa siasa kuhusu mkataba wa bandari unaotarajiwa kupitishwa na wabunge.
Msukuma ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kilimani jijini Dodoma.
"Nataka niwaambie watanzania mimi nilienda dubai tulifanya ziara ya siku 9 kiukweli wao wameendelea kuliko sisi,sasa tumepata hii fursa tunaanza kuponda,tunaanza kutukana hii sio sawa na hao wanaotangaza mitandaoni walishiriki kufanya maovu huko nyuma" Amesema Msukuma.
Aidha amewataka watanzania kuendelea kuunga mkono serikali yao na wabunge kuendelea kuchakata na kupitisha na kama kuna mapungufu yakasimame kwenye mkataba wenyewe.
"Hakuna mradi mkubwa uliotengenezwa hapa Tanzania bila kuwa na makelele,wenzetu dubai wanategemea bandari na airport,tunahitaji kutafuta watu wenye uwezo na kuendesha hivi vitu mfano mzuri ukilinganisha bandari ya dar es salaam na wenzetu jirani Kenya bandari ya mombasa utaona kabisa utofauti mkubwa hivyo wananchi wanapaswa kuangalia suala hili kwa manufaa ya vizazi vijavyo" Amesisitiza Msukuma.
Aidha amesema ataendelea kupambana na wanaoendelea kuiponda serikali na kusambaza uzushi kwenye mitandao ya kijamii na kuamua kutengeza uongo na kuzua taharuki kwa watanzania na wengine kudai amehongwa ili kutumika kwenye sakata hili la bandari.
"Naomba niwaonye wale wote wanaoendelea kusambaza maneno kwenye mitandao ya kijamiii na hao baadhi ya wanasiasa wanaosema nimehongwa ili kutetea hili suala niwaambie tu mimi nimeanza kumiliki magari na vitu vya thamani kabla hata sijawa mbunge na serikali inapoleta jambo zuri siwezi kupingana nalo haswa ukizingatia suala la bandari nilienda mwenyewe dubai nikashuhudia hivyo wasinichokoze kwani nina mengi sana yakuzungumza lakini nimeamua kukaa kimya lakini wakitaka nizungumze nitazungumza tu maana sina cha kuogopa na kwenye ukweli lazima tuseme ukweli hii nchi ina wasome wengi ambao wamekaririshwa badala yake wanashindwa kuchanganua mambo hivyo ningewaomba wasomi wanchi kutumia elimu zao vizuri na sio kupotosha watanzania"
Ameongeza kuwa kwa upande wake amesoma mkataba huo na hajaona sehemu iliyoandikwa miaka 100 na kama ni miaka 100 ina maana Rais Dkt.Samia Suluh Hassan yuko tayari watanzania wateseke ilihali yeye mwenyewe baada ya kumaliza urais anakuwa mtanzania wakawaida,hivyo amewataka watanzania kuchambua na kuelewa mambo na sio kumezeshwa sumu na baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao hawana maslahi na taifa hili.
Aidha amesema kuwa anaiomba serikali kama waliweza kuwapeleka wabunge zaidi ya 60 basi waangalie namna ya kuwapeleka waandishi 100 kutoka sehemu tofauti tofauti Tanzania nzima ili kwenda kushuhudia na kuja kuwa mashahidi kwa watanzania.
TANZANIA, UINGEREZA KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA
Na WMJJWM, Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekubaliana na Kamisheni ya Uingereza kushirikiana ili kuimarisha usawa wa kijinsia nchini.
Hayo yamebainika wakati wa kikao cha Wizara na Kamisheni hiyo kilichofanyika jijini Dodoma Juni 7, 2023, kwa lengo la kutambulisha Programu na mkakati mpya wa kusaidia wanawake na wasichana kufikia ndoto zao (International Women and Girls strategy) utakaotekelezwa kati ya mwaka 2023 hadi 2030.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, amesema, lengo la Serikali ni kuhakikisha elimu ya usawa wa kijinsia inatolewa kuanzia ngazi ya malezi ya awali huku akiwaomba wadau hao kuongeza ushirikiano kwenye maeneo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kamisheni ya Uingereza Nchini Kemi William, amebainisha kuwa, Kamisheni ipo tayari kuunga mkono jitihada za Serikali kupitia Programu za Elimu hasa mradi wa Shule Bora unaotekelezwa na Wizara ya Elimu kwa kuzingatia na kuhusisha makundi yote ndani ya jamii.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ambapo wamejadili ushirikiano bora wa kimaendeleo kwa lengo la kuwalinda Watoto na kuwawezesha wanawake na katika suala zima la utoaji wa elimu ya Afya ya uzazi kwa Wanawake na Wanaume ndani ya jamii.
Wakati wa Ziara hiyo, Kemi alifuatana na Wataalamu Waandamizi wa Elimu kutoka Kamisheni hiyo, Colin Bangay na John Lusingu.
MWISHO
NHC KUSHIRIKI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah ambapo wamejadiliana namna kuendeleza ushirikiano baina ya pande mbili ili kuendeleza miundombinu ya michezo nchini.
Kikao hicho kimefanyika Juni 07, 2023 katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatekeleza miradi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwemo jengo la ofisi za Wizara linalojengwa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma pamoja na eneo la changamani la michezo Kawe jijini Dar es Salaam.
WAKAGUZI WA NDANI WATAKIWA KUTOA USHAURI WENYE TIJA
Bw. Mwamnyasi aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo maalum kwa Wakaguzi wa Ndani kutoka halmashauri na Tawala za Mikoa 13 za Tanzania Bara.
Alisema kuwa, mafunzo ya ukaguzi wa mifumo na miradi ya TEHAMA Serikalini ni muhimu kwa Wakaguzi wa Ndani kwa kuwa yanawajengea uwezo katika utendaji kazi na kurahisisha shughuli za ukaguzi sambamba na kutoa ushauri wenye tija kwa serikali.
“Ukielewa namna mifumo inavyofanya kazi, unaweza kukagua ipasavyo, na tutaepuka kutaja majina ya watu katika taarifa zetu za ukaguzi badala ya mifumo, sisi Wakaguzi tunatambua kuwa miongozo ya ukaguzi inaeleza kutokagua sehemu ambayo hauna uelewa nayo kwa kuwa unaweza kutoa maoni na ushauri kwa Serikali ambao hauna tija” aliongeza.
Aidha, Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa TEHAMA Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bw. Sylvani Shayo, aliwasisitiza Wakaguzi wa Ndani kutumia Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao wakati wa kusimamia na kufanya ukaguzi wa miradi na mifumo ya TEHAMA katika taasisi zao.
Alibainisha kuwa, e-GA kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wanaendelea na jitihada za kutoa mafunzo kwa Wakaguzi wa Ndani ili waweze kufanya ukaguzi katika eneo la TEHAMA kwa ufanisi.
“Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao ni nyenzo muhimu katika ukaguzi wa miradi na mifumo ya TEHAMA katika taasisi za umma, na ikiwa wakaguzi wa ndani mtazingatia vema miongozo na sheria hizo mtafanya ukaguzi wenye tija na maslahi kwa taifa”, alisema Bw. Shayo.
Naye Meneja wa Udhibiti wa Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao Bi. Sultana Seiff alisema, e-GA haitaki kuacha kada yoyote nyuma katika matumizi ya TEHAMA kwakuwa dunia ya sasa inaendeshwa kidijitali, hivyo wakaguzi wa ndani wanapewa mafunzo hayo ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa njia ya kidijitali.
Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani Morogoro yameanza Juni 05 mwaka huu yanahusisha wakaguzi wa ndani 110 kutoka Halmashauri na Tawala za Mikoa ya Dodoma, Tabora, Singida, Kigoma, Mara, Dar es Salaam, Morogoro, Shinyanga, Rukwa, Kagera, Geita, Simiyu na Katavi. Awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yalifanyika Machi mwaka huu ambapo jumla ya Wakaguzi wa Ndani 133 kutoka Halmashauri na Tawala za Mikoa 13 za Tanzania Bara, walishiriki.