Na Moreen Rojas Dodoma
Mamlaka
inayoshughulika na utoaji wa vitambulisho vya Taifa NIDA wametakiwa
kuongeza kasi ya uzalishaji wa vitambulisho vya Utaifa ili kumsaidia
mwananchi kupata wepesi wa kutambulika anapokuwa na mahitaji mbalimbali.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Mjaliwa katika Kongamano la sita la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi jana
Jijini Dodoma ambapo ameitaka wizara ya mambo ya ndani ya nchi kuongeza
kasi ya utoaji wa vitambulisho vya Taifa huku akizitaka Taasisi za
kifedha kuendelea kutoa mikopo kwa riba nafuu
Sambamba
na hayo Waziri mkuu ameitaka mikoa ambayo haijaanzisha vituo vya
uwezeshaji wananchi kiuchumi waanzishe kwa mwaka huu wa fedha 2022-2023.
Akitoa
Taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya uwekezaji wananchi
kiuchumi katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi
Bengii Issa amesema jumla ya mifuko na programu za Uwezeshaji wananchi
kiuchumi zipo 85 ambapo mifuko na program 75 zinamilikiwa na serikali
huku mifuko 10 ikiwa inamilikiwa na sekta binafsi.
Kwa
upande wake Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji
amesema bado kuna changamoto ya watanzania kushindwa kuzalisha bidhaa
zenye ubora na kiwango cha kimataifa.
Akitoa
ufafanuzi Mkuu wa kitengo cha biashara Stanbic bank Kai Molel amesema
kama bank wanatoa huduma nyingi za kifedha kwa taasisi za umma na
wafanya biashara lakini pia kuwawezesha wananchi wa Tanzania kuweza
kufaidika na fursa zinazotokana na uwekezaji kama kauli mbiu inavyosema.
Kongamano la Sita la Uwezeshaji wananchi kiuchumi limebebwa na kauli mbiu isemayo ''uwezeshaji wananchi katika uwekezaji''
0 Comments:
Post a Comment