Subscribe Us

HALMASHAURI 7 ZATHIBITIKA KUWA NA MLIPUKO WA UGONJWA WA SURUA.

Na Moreen Rojas.Dodoma

HALMASHAURI  7 ZATHIBITIKA KUWA  NA  MLIPUKO  WA UGONJWA   WA SURUA.

Hayo yamesemwa na Waziri wa afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ikiwa ni kutoa taarifa kwa umma kuhusu ongezeko la wagonjwa wa surua nchini.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wagonjwa thelathini na nane(38) walithibitika katika halmashauri za bukoba sampuli (3),Handeni DC sampuli(4) Kilindi sampuli (3) Mkuranga sampuli(4) Manispaa ya kigamboni sampuli (8)Manispaa ya temeke sampuli (12)na Manispaa ya Ilala sampuli (4).

Uchambuzi huo pia ulionesha uwepo wa ugonjwa wa Surua katika halmashauri za Arusha (1)Chalinze (2) Igunga(1) Kahama(1) Kalambo(1) Kigoma DC (2) Kwimba DC (1) Masasi (1) Mvomero DC(2) Rorya DC (2) na Manispaa ya Ubungo (2),hata hivyo halmashauri hizi hazikukidhi vigezo vya kuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Surua.

Waziri Ummy ameongeza kuwa jumla ya wagonjwa wote waliothibika kuwa na maambukizi ya Surua imefikia (58) kwa kipindi cha Julai hadi Agosti 2022.

Waziri Ummy amemaliza kwa kutoa rai kwa Umma kupeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ili wapatiwe chanjo ya Surua/Rubella kulingana na umri wao.

Chanjo ya Surua/Rubella hutolewa kwa mtoto anapofikia umri wa miezi 9 kwa dozi ya kwanza na miezi 18 kwa dozi ya pili ili kupata kinga kamili.
Waziri wa afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma

 

0 Comments:

Post a Comment