Mwanzilishi na mwasisi wa kwanza wa Ndoa ni Mungu,
Mungu alipomuumba Adam alimpa kazi 2 kubwa kulima bustani na kuitunza,pia akampa kazi ya kuwapa wanyama wote majina.
Baada ya yote hayo Mungu alimwangalia Adam na akaona siyo vyema Adam awe peke yake,akamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Alimfanya mwanamke kutoka kwenye Ubavu wa Adam,Kwa kumpa Adam Usingizi mzito akaondoa ubavu mmoja akaufanya mwanamke,
Ndipo
Mungu akamletea Adam akamkabidhi mkewe,Ndipo Adam akasema hakika huyu
ni nyama katika nyama yangu na mfupa katika mifupa yangu.
Mungu alipomuunganisha Adam na Hawa kuwa mwili mmoja aliwabariki akawaambia zaeni mkaongezeke.
Kwa
maana kwamba kila watakachoenda kufanya kama wanandoa kitazaa na siyo
kuzaa tu kitaongezeka kwa sababu Mungu ndiye amewaunganishankwa KUSUDI
lake.
Mithali 18:22
[22]Apataye mke apata kitu chema;
Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
Wanaume unapompata mke umepata kitu Chema alafu umepata kibali kwa Mungu,huko nje unataka kwenda kutafuta nini tena?
Sasa kinachoua Ndoa Nyingi na kwa kasi kubwa sana sasa hivi ni Hiki;
1.TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA.
Vijana
wengi ambao wapo kwenye mahusiano,hawana mahusiano masafi mbele za
Mungu,Mahusiano yao yameanza kwenye Misingi ya ngono na siyo Mungu.
Hawatafuti
Misingi imara kwa Mungu bali katika miili yao,jambo ambalo linapelekea
mahusiano hayo kutawaliwa na shetani zaidi kuliko Mungu.
Mahusiano
yanapotawaliwa na shetani zaidi,huwa yana uharibifu siku za usoni,
hautatokea kwenye mahusiano bali utakusubiri mpaka uingie kwenye ndoa.
Inapofika
suala la kufunga ndoa,Vijana hao hawatubu mbele za Mungu na kuomba
Rehema kwa maisha machafu waliyoishi kwenye kipindi cha UCHUMBA, ili
Mungu awarehemu na kuanza nao safari ya ndoa yao bali wanafunga hivyo
hivyo tu kwa mazoea na kwa kujidanganya.
Nyumba inayoanzaga na msingi mbovu huwa haikai muda Mrefu na wala hainaga uimara wowote.
2.KUKOSA UAMINIFU KWENYE NDOA
(MICHEPUKO).
Mwanaume
au mwanamke ambaye yupo kwenye ndoa anapotoka nje ya ndoa yake
kingono(Sex na mtu mwingine) ni kwamba amekaribisha uharibifu kwenye
ndoa yake yeye mwenyewe.
Mtu
anapotoka nje ya ndoa kwa uzinzi,huko nje Kuna mbwa mwitu ambao
walikuwa wanakusubiri kwa hamu kubwa ili wairarue ndoa yako na isipone
tena.
Unapokutana kimwili
na mtu mwingine ambaye siyo mke au mume wako ina maana umekuwa mwili
mmoja na huyo kahaba,kwa maana nyingine umemuunganisha mke au mume wako
na huyo Kahaba,maana mlipofunga ndoa nyinyi mlikuwa mwili mmoja.
Mithali 23:27-28
[27]Kwa maana kahaba ni shimo refu;
Na malaya ni rima jembamba.
[28]Naam, huotea kama mnyang’anyi;
Huwaongeza wenye hila katika wanadamu.
Sasa
umeunganisha tena nafsi yako kwa mchepuko ukijua utatuliza akili
mawazo,na maisha yawe safi kumbe umekimbilia kwenye Shimo refu.
1 Wakorintho 6:16
[16]Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
Sasa
ukute mchepuko kama mchepuko kabeba roho za ukahaba,ni mzinzi roho za
umasikini,laana za huko kwako,katawaliwa na Mizimu ua huko kwao,tabia
chafu za huko kwao,ukute ni muumini mzuri wa waganga na wachawi basi
ujue ya kwamba unazoa vya kuzoa unapeleka wewe mwenyewe kwenye ndoa
yako,
Dalili zinazojitokea ni Hizi;
KUMBUKA shetani akiingia kwenye ndoa haji kuleta amani,Ni anachinja,anaharibu na kuua.
1.Mtu
ataanza kumuona mke au mume wake Hafai,hana thamani tena mbele
yake,siyo bora tena,anamchukia sana ,hakuna upendo tena,hakuna Amani
tena kama mwanzo,hakuna maelewano tena ndani ya familia,kama kuna
watoto,watoto nao wanaanza kuingia kwenye matatizo.
2.Uchumi
wa familia unaanza kuyumba,mali zinapukutika,biashara zinakufa,huna
wateja tena,roho ya madeni inaikumba familia,kwa sababu umeenda
kushikamana na kahaba,umeenda kuzoa roho za umasikini umezileta ndani
mwenyewe.
Mithali 29:3
[3]Apendaye hekima humfurahisha babaye;
Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.
Mahali
ambapo hakuna upendo tena Uchungu huwa unazalika kwenye Moyo,Hasira
zinajaa kwenye kifua ndipo kisasi kinazalika hapo,mtu anaamua kuvunja
ndoa,kuua mume au mke au kufanya chochote kibaya ili mradi tu ndoa ife.
Mithali 19:14
[14]Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;
Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
Kama
una mke mzuri anakupenda,anakutii na kukuheshimu basi Tafadhali usije
ukafanya ujinga wa kukaribisha michepuko kwenye ndoa yako,utajuta.
Kama una mume mzuri,anakupenda,anakujali, anakuheshi anatunza familia kwa ujumla, Muombee ili Mungu amtawale na kumlinda kwa nguvu zake.
Kutoka
kwenye changamoto hii ya ndoa Kuvunjika hovyo au migogoro isiyoisha
siyo kujifunza mbinu mpya za kitandani,siyo kuhudhuria semina nyingi za
ndoa,siyo kumvuta kwa dawa za waganga wa kienyeji,siyo kumuita majina
mazuri,
KUMBUKA ni wapi ulipoanguka ukatubu mbele za Mungu.
Kama
ulishawai kutoka Nje ya Ndoa yako au Misingi yako huko nyuma ulianza na
uzinzi kabla ya kufunga ndoa na imekupelekea majuto makali sana na
unaona maisha yamefika mwisho kwa sababu hukujua kama maisha yako
yatakuwa hivyo baada ya ndoa basi Kaa mbele za Mungu kuomba
Rehema,Samehe kabisa walisababisha maimivu kwenye moyo walo na mpe Mungu
nafasi aingilie kati maisha yako na familia yako.
2 Wakorintho 7:10
[10]Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
YESU ANAKUPENDA NA ANAPENDA WATU WAFURAHIE NDOA NA MAISHA YA NDOA.
0 Comments:
Post a Comment