Na. Mwandishi wetu Dodoma
Naibu
Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na
Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) kufanya tafiti za madini katika wilaya ya Kilombero mkoani
Morogoro na wilaya ya Mufindi mkoani Njombe kwa lengo la kubaini aina ya
madini yaliyopo katika wilaya hizo.
Hayo
yamebainishwa na Dkt. Kiruswa wakati akijibu swali la msingi la Mbunge
wa Jimbo la Kilombero Abubakari Asenga katika kipindi cha maswali na
majibu Bungeni jijini Dodoma.
Aidha, Dkt. Kiruswa ameainisha maeneo mbalimbali yenye madini ya dhahabu na vito katika wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
Akijibu
swali hilo amesema, Taasisi ya GST imefanya utafiti wa awali sambamba
na kuchora ramani kwenye maeneo yote yaliyopo katika Jimbo la Kilombero
katika mfumo wa Quarter Degree Sheet (QDS).
Dkt.
Kiruswa amesisitiza kuwa, tafiti za awali zilizofanyika katika wilaya
ya Kilombero, zilionesha uwepo wa madini ya dhahabu na madini ya vito
katika Kata ya Chisano.
Ameongeza
kuwa, GST ilifanya utafiti wa awali na kuchora ramani ya eneo la
Hifadhi ya Milima Udzungwa na maeneo jirani ambapo utafiti wa madini
uliofanyika katika maeneo hayo hauoneshi taarifa zozote za uwepo wa
madini ya thamani katika milima hiyo.
Mkoa
wa Morogoro umebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini ikiwemo
dhahabu, Shaba, Kinywe, madini ya viwandani (Ulanga, Kaoline), madini
ya ujenzi (mchanga, kifusi) na madini ya vito ( Rubi, Rodolite).
0 Comments:
Post a Comment