Imeelezwa kuwa, Mitaa 28 ambayo bado
haina umeme katika Jimbo la Handeni mjini ipo katika mpango wa
kupatiwa umeme kupitia mradi wa umeme vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa
Pili unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Hayo
yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili
Stephen Byabato wakati akijibu swali la Mbunge wa Handeni Mjini,
Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa ambaye aliuliza kuhusu mpango wa
Serikali wa kupeleka umeme katika mitaa 28 ya Jimbo la Handeni Mjini
ambayo bado haijapata umeme.
Naibu Waziri alisema kuwa, mitaa
hiyo inapelekewa umeme na mkandarasi kampuni ya DERM ELECTRICS TANZANIA
ambae yupo katika eneo la kazi na anaendelea na ujenzi wa miundombinu ya
umeme katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Handeni.
Naibu
Waziri aliongeza kuwa, Jimbo la Handeni Mjini lina jumla ya mitaa 60
ambapo kati ya mitaa hiyo, 32 ina umeme sawa na asilimia 53.3 na mitaa
28 haina umeme sawa asilimia 46.7.
Alisema kuwa kazi ya kupeleka umeme kwenye mitaa hiyo itakamilika Mwezi Desemba, 2022.
Home »
» MITAA ISIYO NA UMEME IFIKAPO DESEMBA 2022 IWE IMESAMBAZIWA UMEME
0 Comments:
Post a Comment