Na. Kadala Komba Dodoma
Kilimo ni sekta inayotegemewa sana Tanzania kwa ajili ya kutoa malighafi kwa ajili ya taifa letu.
Tarehe
16 mwaka 2021 mwezi wa 2 Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango
iliingia mkataba wa kutekeleza na kuimarisha Afya ya mimea na jumuiya ya
Umoja wa ulaya.
Mradi
huu ni wa miaka 3 na miezi 6 na umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na
Shirika la Kimataifa la Kilimo na chakula ambapo FAO ni msimamizi wa
mradi na utekelezaji umefanywa na serikali kupitia mamlaka ya mimea na
viatilifu uliochini ya Wizara ya Kilimo.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde wakati
akizindua mradi uboreshaji wa huduma za afya ya mimea Tanzania kwa
usalama wa chakula uliofanyika katika ukumbi wa St.Gasper jijini Dodoma.
Aidha
ameongeza kuwa mradi huu unalenga kuhakikisha usalama wa chakula nchini
kwa kuimarisha mfumo wa ukaguzi wa utoaji wa vyeti na usafi wa mazao
yanayo safirishwa nje ya nchi.
Mradi
huu unalenga kuthibiti vizimbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao
yanayonaingia au yanayotoka nchini yanakuwa na ubora unaokidhi viwango
vya soko la kimataifa.
Mhe.Mavunde
amewashukuru Umoja wa jumuiya ya ulaya na shirika la umoja wa mataifa
Kilimo na Chakula (FAO) kwa kufadhili na kusimamia fedha za mradi huu
ambao ni mradi muhimu kwenye sekta ya kilimo nchini kwani utachochea
uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kamati ya bunge Sekta ya Kilimo,Mifugo na
Maji Dkt.Christine Ishengoma amesema kuwa mradi huu utawasaidia wakulima
kwani walikuwa wanapata shida hivyo kupitia mradi huu mazao na mimea
itakuwa salama na tutapata chakula kingi cha kuweza kulisha taifa pamoja
na nchi za nje.
Aidha
ameongeza kuwa kama kamati watakuwa wanatembelea mradi ili kuukagua na
kuangalia namna gani wakulima wanafikiwa kwa wakati ili kuwasaidia
wakulima kupata mazao yaliyo bora ma kwa wakati.
Dkt.Ishengoma
ameishukuru Serikali na kuomba mradi kusimamiwa vizuri pamoja na kuwa
nao bega kwa bega ili kuweza kutekelezwa ipasavyo.
Naye
Naibu Katibu Mkuu Sera na Mipango Obadia Nyagiro amesema kuwa mradi huu
umelenga kuimarisha mfumo wa kidijitali wa kufanya takwimu pamoja na
kuwajengea uwezo wataalamu kuhusu maswala ya mimea.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde akizindua mradi uboreshaji wa huduma za afya ya mimea Tanzania kwa usalama wa chakula
0 Comments:
Post a Comment