Na. Mwandishi wetu Dodoma.
KATIKA
kukabiliana na suala la upungufu wa maji katika Jiji la Dodoma, Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inaendelea na
uchimbaji wa visima pembezoni wa mji ili kukabiliana na changamoto hiyo.
DUWASA mpaka sasa imekwisha chimba jumla ya visima vitano katika maeneo ya Nzuguni A visima vinne na Nzuguni B kisima kimoja.
Akizungumza
wakati wa zoezi la kupima wingi wa maji katika mtaa wa Nzuguni A jijini
Dodoma, Fundi Pampu DUWASA, Fadhili Mahonya amesema kazi inayoendelea
kwa sasa ni upimaji wa pampu ili kujua uwezo wa kisima na kupata pampu
sahihi itakayotumika.
“Kisima hiki kinaurefu wa mita 134 kwenda chini na kinauwezo wa kuzalisha maji lita 65000 kwa saa”. Amesema Mahonya
Naye
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzuguni A, Onaeli Mathias amesema ni muda mrefu
sana tangu uhuru eneo la Gogwa na Dundulu kumekuwa na shida ya maji.
“Kwa
mradi huu wa DUWASA ni jambo la kushukuru sana, namshukuru Rais na
Waziri wa Maji na uongozi wa DUWASA kwakweli hili tatizo lilikuwa sugu
tangu uhuru walikuwa wanatumia maji ya kisima”. Amesema Mwenyekiti
Amesema
watu wamepata maradhi hasa homa ya matumbo kutokana na kunywa maji
yasiyosalama. Pia ameongeza maji yakipatikana hata eneo hilo linaweza
kuimarika kwani kwa sasa limekuwa kame sana.
Kwa upande wa Wananchi wa Nzuguni A wameishukuru Serikali kupitia DUWASA kwa kuwapelekea huduma ya maji katika eneo hilo.
Rehema
Simon amasema tunashukuru wanawake kwa kutuliwa ndoo kichwani kwani
tulikuwa tunachota maji mbali huku mtoto akiwa mgongoni.
“Tunamshukuru
Mungu na Serikali pia kupitia DUWASA, kwa kutuletea maji, kwani kwa
sasa gharama ya kupata maji ni kubwa unalipia maji pamoja na usafiri kwa
gharama ya elfu sita au tano”. Alisema Loveness Abdul
Wakazi
hao pia wamesema ujenzi kwa maeneo hayo utaendelea kwani awali walikuwa
wanatumia gharama kubwa sana katika ujenzi hasa katika upatikanaji wa
maji.
“Tulikuwa tunafuata
maji kama kilomita nne, lakini kwa maji haya kusogea karibu itakuwa
imeturahisishia”. Amesema Prosper Mnyoli
Kukamilika
kwa visima hivi kutaongeza kiwango cha maji eneo la Nzuguni hivyo
kupunguza au kuondoa kabisa kero ya maji katika eneo hilo na maeneo ya
jirani kama Ilazo.
0 Comments:
Post a Comment