Subscribe Us

VIONGOZI WA UVCCM BAHI WAMEONYWA KUTOBWETEKA

Na Peter Mkwavila BAHI.

VIONGOZI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana  (UVCCM) wa wilayani Bahi,wameonywa kutobweteka na kulewa na madaraka,badala yake wafanye kazi za kujiingizia kipato pamoja na kukisaidia chama cha Mapinduzi kimaendeleo.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti mstaafu Jumuiya hiyo Hassan Kidoke, ambaye aliyemaliza muda wake alipokuwa akizungumza na vijana wa wilaya kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa kuwapata viongozi watakaongoza kwa miaka mitano .

Mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma ulioshirikisha vijana kutoka kata zote za wilaya ya Bahi,Kidoke amewataka viongozi waliochaguliwa kushika nafasi ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo wafanye kazi za kujiingizia kipato pamoja na kukisadia chama kiendelee kudumu badala kulewa na kubweteka na madaraka.

“Jumuiya ya vijana kupitia Chama cha (CCM) vijana wanatarajiwa kuonekana wanafanya kazi za kujiingizia kipato cha kiuchumi pamoja na kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinafufaika kupitia kwao katika kutekeleza ilani zake”alisema

Naye Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mwankunda,akizungumza kwenye uchaguzi huo wa vijana wa (UVCCM) kwa upande wake amewataka  nafasi walizochanguliwa zitumike kwa kukemea maovu yakiwemo vitendo vya rushwa.

Alisema nafasi hizo walizochaguliwa watambue wamepewa thamana na vijana wezao ili waweze kuwatumikia na kuleta mabadiliko ndani ya chama na jumuiya hiyo huku wakikataa kutumika kwenye vitendo vya rushwa katika chaguzi mbalimbali za chama.

Mwankunda ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo,pia amewataka vijana hao wa wilaya kuendeleza mema yaliyofanywa na viongozi waliowatangulia.

“Jumuiya ya vijana wilaya ya Bahi wanamradi wa ujenzi wa nyumba,pia wanaplani ya kuweka uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo stendi ya mabasi hivyo siyo vema juhudi hizi zikafa wakati nyinyi mkiwa madarakani”alisema.

Pia wametakiwa vijana hao kututumika na wagombea wa jumuiya zingine kwa kuwafanyia kampeni zinazoashiria kuwepo kwa rushwa,Chama cha Mapinduzi kinawataka viongozi wenye uadilifu na sifa ya kuongoza.

Katika uchaguzi huo Mwenyekiti aliechaguliwa kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Hassani Kidoka ni Jastin Sangula huku nafisi mbalimbali za uwakilishi zikiwapata viongozi wake.

Mwisho


 

 

0 Comments:

Post a Comment