Na Mwandishi wetu- Dodoma.
Naibu
Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu
Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa serikali imeendelea kufanya jitihada
za kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kwa
kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja na si kwa makundi kama ilivyokuwa
awali.
Amebainisha hayo
wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Vijana Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na
Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022
Dodoma. Ameongeza kuwa muongozo mpya uliotolewa umerahisisha sifa za
kukopa kwa vijana kulingana na mahitaji yao.
Naibu
Waziri Katambi amefafanua kuwa yapo maboresho ya mifumo katika kila
sekta zinazoshughulikia masuala ya vijana ambapo mifumo hiyo itasaidia
kuleta mazingira wezeshi kwa vijana kuweza kujikwamua kiuchumi na kuweza
kujiajiri.
Ameongeza
kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika kutoa
mafunzo kwa vijana ili kuweza kutatua changamoto za kiuchumi kwa vijana,
Aidha amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanasaidia kuongeza maarifa,ujuzi
na mipango thabiti kwa vijana kuweza kutambua vipaji vyao.
“Tunafurahi
kwamba leo katika mdahalo huu ulio tolewa na shirika AMDT (AGRICATURAL
MARKERT DEVELOPMENT TRUST) imetupa fursa ingine ya kusikiliza
changamoto, vipaumbele, uzoefu na matarajio toka kwa vijana wote wa kike
na kiume.wanaofanya shughuli zao za kiuchumi katika sekta ya kilimo.
Amesisitiza
kuwa vijana waliopata mafunzo hayo waendelee kushirikiana na vijana
wengine ili kubadili mitazamo na kushirikiana na Serikali kukabiliana na
changamoto zinazo wakabili.
MWISHO.
Naibu Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza jambo wakati ufunguzi wa
Mdahalo wa Vijana Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za
Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 katika ukumbi
uliopo Morena Hotel jijini Dodoma.
Sehemu ya vijana waliohudhuria Mdahalo ulioandaliwa na
shirika AMDT Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo
Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 katika ukumbi uliopo
Morena Hotel jijini Dodoma.
0 Comments:
Post a Comment