Biblia inasema hivi
*Hosea 4:6(a) Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;*
Kwenye
hili andiko Mungu hasemi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWASABABU YA SHETANI
AU WACHAWI , isipokuwa anasema hivi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA
MAARIFA, kwahiyo kinachokuja kukuangamiza kwenye maisha yako
kinakuangamiza kwasababu hauna maarifa sahihi ndani yako, kinakuangamiza
kwasababu mitazamo yako si sahihi ndiyo maana ninasema KABLA YA
KUTAFUTA MCHAWI WA MAISHA YAKO, KABLA YA KUPAMBANA NA SHETANI NA
MAWAKALA WAKE BADILISHA KWANZA MITAZAMO YAKO YA NDANI....
*
Biashara yako inaweza ikawa haifanikiwi badala ya kuanza kupambana na
wachawi check kwanza kwenye moyo wako je mitazamo yako juu ya biashara
unayoifanya ni sahihi? Au unafanya kwa kuiga? Unaweza ukawa hauchumbiwi
na wanaume badala ya kukimbilia kukemea roho ya kukataliwa check kwanza
maisha yako jinsi yalivyo, unaweza ukawa hauchumbiwi kwasababu ya
ukorofi wako au una mienendo isiyopendeza machoni pa Mungu na wanadamu,
ndoa yako inaweza ikawa haina Amani badala ya kukimbilia kukemea roho ya
mafarakano jiangalie kwanza kibinafsi inaweza ikawa chanzo ni wewe
mwenyewe kwa kufanya mambo ambayo yanamkera mwenzako ukishajua hivi hata mchawi wako unayetakiwa kumshinda utamjua!*
Mtu
mmoja alimwona paka kwenye mlango wa nyumba yake akamkemea kwa maombi
akifikiri ni mchawi ile anamaliza tu kuomba akagundua kumbe aliyekuwa
anamkemea kwenye maombi ni paka wake aliyemfuga mwenyewe
shida nini? Mitazamo yake haikuwa sahihi, ndiyo maana nasisitiza kabla
ya kumpinga shetani kwenye maisha yako hakikisha ndani yako una mitazamo
sahihi juu ya changamoto mbalimbali unazozipitia kimaisha, kwasababu
kama hauna maarifa sahihi au mitazamo sahihi ndani yako unaweza
ukamkimbiza shetani kwenye maisha yako na akaondoka lakini matatizo yako
bado yakabakia pale pale
Mwisho...
*Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.*
Mungu wa mbinguni akubariki sana..
WhatsApp +255657117595
Mwl.Joseph Leonard
0 Comments:
Post a Comment