Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

JUKUMU LA KUWAANGALIA WAZEE SIO LA SERIKALI PEKEE.

Na Moreen Rojas Dodoma



Katika nchi nyingi Duniani,Wazee wamekuwa wakituzwa isipokuwa kwamba kila nchi ina namna yake ya kuwatunza wazee wao kwa kulingana na mila,desturi na tamaduni pamoja na hali za kiuchumi za nchi zao.

Hayo yamesemwa na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein wakati wa mjadala wa kitaifa kuhusu masuala ya uzee uliofanyika jijini Dodoma.

Dkt.Shein amesema kuwa kwa hapa nchini Tanzania suala la kuwaenzi na kuwatunza wazee ni utamaduni wa kale uliotokana na mila na desturi zetu.

Miongoni mwa mambo makubwa yaliyofanyika ni kuwajengea wazee hao nyumba imara za kuishi za ghorofa zilizokuwa na vifaa mbalimbali vya umeme vya kutumia,wazee hao waliwekwa pamoja na kuyaendeleza maisha yao vizuri.

Nyumba hizo za wazee zimejengwa huko Sebleni katika wilaya ya Mjini na Welezo katika Wilaya ya wete.

Ni jambo la kufurahisha kuona kwamba nyumba hizo zimekuwa zikifanyiwa matengenezo kila haja ya kufanya hivyo inapotokea na hadi leo zinaendelea kutumiwa na wazee.

Kadhalika wazee waliopatiwa makaazi katika nyumba hizo wanaendelea kuhudumiwa na Serikali katika mahitaji yao yote ya msingi.

Mbali na jitihada hizi, matamko ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ya kutangaza elimu bure kwa wote tarehe 23 Septemba,1964 na matibabu bure kwa wote tarehe 23 Machi,1965 yalisaidia sana katika kuwaendeleza wazee na kuwawezesha kukabiliana na uzee na maradhi.

Aidha ameongeza kuwa katika kuendeleza falsafa za waasisi wetu wa taifa la Tanzania,taifa letu limekuwa likichukua hatua zaidi kusaidia hali za wazee kwa kutatua changamoto zinazowakabili.

Katika miaka kadhaa iliyopita TanzaniaBara,Mpango wa TASAF II uliweka kima cha shilingi za Kitanzania 6000 kila mwezi kuwasaidia watu wenye mazingira magumu wakiwemo wazee.

Kadhalika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya Mpango wa Pensheni Jamii,ilianzisha utaratibu wa kuwasaidia wazee kwa kima cha Tsh.5,000 kila mwezi.

Kima hiki cha fedha hakikuwa kikikidhi mahitaji kwa wazee walioko TanzaniaBara na hata kwa wale wa Zanzibar,lakini hatua hiyo ilikuwa ni muhimu sana kama mwanzo wa kuelekea katika uundaji wa Sera na Sheria Madhubuti za hifadhi ya jamii kwa wote.

Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa idadi ya wazee ni asilimia 4.5 watu wote hapa nchini,hata hivyo matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika hivi karibuni yatatupa idadi halisi ya wazee tulionao kwa sasa,ili tuweze kutumia vizuri takwimu hizo katika kuweka mipango mizuri ya kuwaletea maendeleo.

Kauli mbiu ya mjadala wa kitaifa kuhusu masuala ya uzee ni "Miaka 60 ya Uhuru,Tuko wapi na tunakwenda wapi?
 
 

 

 

MAKAMU WA RAIS: SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA MADHEHEBU YOTE YA DINI



Imeelezwa kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan inathamini mchango wa Madhehebu ya dini kupitia mahubiri na kufundisha neno la Mungu kwa watu wote.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 75 ya Kanisa la Elimu Pentekoste Tanzania (KEPT) iliyofanyika Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Dkt. Biteko ametoa pongezi kwa niaba ya Serikali kwa mambo yanayofanyika ya kuhuburi kwa watu na Taifa kwa ujumla ikiwemo kufundisha neno la Mungu kwa watu wote.

Pia, amewapongeza kwa kutoa huduma za kijamii ikiwemo elimu na afya, kuendelea kuhimiza waumini wote kudumisha amani, upendo, mshikamano na utulivu kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na kutunza mazingira.

Dkt.Biteko amesema, Mhe. Rais Samia ameendelea kusisitiza kuwahudumia watanzania kwa heshima kubwa ili maisha yao yazidi kuwa bora kila wakati.

"Nitoe mfano kwa sekta ninayoiongoza ya Madini, tangu Mhe.Rais ameingia madarakani ametuelekeza kufuta baadhi ya kodi mbalimbali ambazo wachimbaji wadogo walikuwa wanaona ni kero katika shughuli zao.

Pia, Mhe. Rais amesisitiza kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji wa ndani na nje kwa kufuta baadhi ya vipengele vya Sheria na Kanuni ambavyo vilikuwa vinakwaza uwekezaji.

"Yote haya, Mhe. Rais anayafanya kwa sababu kiu yake ya kuona kila mwananchi ndani ya nchi hii anakuwa na furaha na maisha yake, na kufurahia kufanya kazi anayoifanya kwa ajili ya kuendeshea maisha yake," amesisitiza Dkt. Biteko.

Aidha, Dkt. Biteko kwa niaba ya Makamu wa Rais ameshiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo la kanisa na upandaji wa mti wa kumbukumbu.

Kwa upande wake, Baba Askofu Mkuu wa KEPT, Peter Konki amesema, kanisa lilianzishwa na Wamisionari kutoka Uingereza mwaka 1946 nchini Tanzania.

Amesema, walifungua makanisa ya kwanza wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma, Msolwa katika mkoa wa Pwani, Tanga na wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

Askofu Konki ametoa wito kwa jamii na watanzania kushiriki katika kudumisha amani na utulivu iliyopo kwa vitendo na kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuishi maisha mema.

Hafla ya Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 75 ya KEPT imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati, Pauline Gekul, Maaskofu Wakuu kutoka Madhehebu mengine na waumini mbalimbali.

 

MKUU WA MKOA DODOMA AMEWATAKA WAAJIRI KUBAINI MBINU ZA KUPUNGUZA AJARI MAENEO YA KAZI

Na Moren Rojas Dodoma


Mkuu wa mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE amewataka waajiri kubaini mbinu za kupunguza ajali kwa wafanyakazi ili kupunguza ajali kazini.


Ameyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo kwa Madaktari juu ya tathmini ya ulemavu na magonjwa yatoka nayo na kazi yaliyofanyika jijini Dodoma huku akilitaka Shirika la Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi(WCF) kuhakikisha tathmini zinafanyika kwa usahihi na Wafanyakazi wanapata stahiki zao kwa wakati.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi JOHN MDUMA amesema mafunzo hayo yamelenga kuelimisha Madaktari namna ya kufanya tathmini ya ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi ili kuhakikisha wahanga hao wanapata stahiki zao.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE

 

VIONGOZI WA UVCCM BAHI WAMEONYWA KUTOBWETEKA

Na Peter Mkwavila BAHI.

VIONGOZI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana  (UVCCM) wa wilayani Bahi,wameonywa kutobweteka na kulewa na madaraka,badala yake wafanye kazi za kujiingizia kipato pamoja na kukisaidia chama cha Mapinduzi kimaendeleo.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti mstaafu Jumuiya hiyo Hassan Kidoke, ambaye aliyemaliza muda wake alipokuwa akizungumza na vijana wa wilaya kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa kuwapata viongozi watakaongoza kwa miaka mitano .

Mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma ulioshirikisha vijana kutoka kata zote za wilaya ya Bahi,Kidoke amewataka viongozi waliochaguliwa kushika nafasi ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo wafanye kazi za kujiingizia kipato pamoja na kukisadia chama kiendelee kudumu badala kulewa na kubweteka na madaraka.

“Jumuiya ya vijana kupitia Chama cha (CCM) vijana wanatarajiwa kuonekana wanafanya kazi za kujiingizia kipato cha kiuchumi pamoja na kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinafufaika kupitia kwao katika kutekeleza ilani zake”alisema

Naye Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mwankunda,akizungumza kwenye uchaguzi huo wa vijana wa (UVCCM) kwa upande wake amewataka  nafasi walizochanguliwa zitumike kwa kukemea maovu yakiwemo vitendo vya rushwa.

Alisema nafasi hizo walizochaguliwa watambue wamepewa thamana na vijana wezao ili waweze kuwatumikia na kuleta mabadiliko ndani ya chama na jumuiya hiyo huku wakikataa kutumika kwenye vitendo vya rushwa katika chaguzi mbalimbali za chama.

Mwankunda ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo,pia amewataka vijana hao wa wilaya kuendeleza mema yaliyofanywa na viongozi waliowatangulia.

“Jumuiya ya vijana wilaya ya Bahi wanamradi wa ujenzi wa nyumba,pia wanaplani ya kuweka uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo stendi ya mabasi hivyo siyo vema juhudi hizi zikafa wakati nyinyi mkiwa madarakani”alisema.

Pia wametakiwa vijana hao kututumika na wagombea wa jumuiya zingine kwa kuwafanyia kampeni zinazoashiria kuwepo kwa rushwa,Chama cha Mapinduzi kinawataka viongozi wenye uadilifu na sifa ya kuongoza.

Katika uchaguzi huo Mwenyekiti aliechaguliwa kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Hassani Kidoka ni Jastin Sangula huku nafisi mbalimbali za uwakilishi zikiwapata viongozi wake.

Mwisho


 

 

MITAA ISIYO NA UMEME IFIKAPO DESEMBA 2022 IWE IMESAMBAZIWA UMEME

Imeelezwa kuwa, Mitaa 28 ambayo bado haina umeme katika Jimbo la Handeni mjini ipo katika mpango wa kupatiwa umeme kupitia mradi wa umeme vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato wakati akijibu swali la Mbunge wa Handeni Mjini, Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa ambaye aliuliza kuhusu mpango wa Serikali wa kupeleka umeme katika mitaa 28 ya Jimbo la Handeni Mjini ambayo bado haijapata umeme.

Naibu Waziri alisema kuwa, mitaa hiyo inapelekewa umeme na mkandarasi kampuni ya DERM ELECTRICS TANZANIA ambae yupo katika eneo la kazi na anaendelea na ujenzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Handeni.

Naibu Waziri aliongeza kuwa, Jimbo la Handeni Mjini lina jumla ya mitaa 60 ambapo kati ya mitaa hiyo, 32 ina umeme sawa na asilimia 53.3 na mitaa 28 haina umeme sawa asilimia 46.7.

Alisema kuwa kazi ya kupeleka umeme kwenye mitaa hiyo itakamilika Mwezi Desemba, 2022. 


 

*KABLA YA KUPAMBANA NA MCHAWI WA MAISHA YAKO BADILISHA KWANZA MIND-SET YAKO, BADILISHA KWANZA MITAZAMO YAKO YA NDANI*

Biblia inasema hivi

*Hosea 4:6(a) Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;*

Kwenye hili andiko Mungu hasemi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWASABABU YA SHETANI AU WACHAWI , isipokuwa anasema hivi WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA, kwahiyo kinachokuja kukuangamiza kwenye maisha yako kinakuangamiza kwasababu hauna maarifa sahihi ndani yako, kinakuangamiza kwasababu mitazamo yako si sahihi ndiyo maana ninasema KABLA YA KUTAFUTA MCHAWI WA MAISHA YAKO, KABLA YA KUPAMBANA NA SHETANI NA MAWAKALA WAKE BADILISHA KWANZA MITAZAMO YAKO YA NDANI....

* Biashara yako inaweza ikawa haifanikiwi badala ya kuanza kupambana na wachawi check kwanza kwenye moyo wako je mitazamo yako juu ya biashara unayoifanya ni sahihi? Au unafanya kwa kuiga? Unaweza ukawa hauchumbiwi na wanaume badala ya kukimbilia kukemea roho ya kukataliwa check kwanza maisha yako jinsi yalivyo, unaweza ukawa hauchumbiwi kwasababu ya ukorofi wako au una mienendo isiyopendeza machoni pa Mungu na wanadamu, ndoa yako inaweza ikawa haina Amani badala ya kukimbilia kukemea roho ya mafarakano jiangalie kwanza kibinafsi inaweza ikawa chanzo ni wewe mwenyewe kwa kufanya mambo ambayo yanamkera mwenzako ukishajua hivi hata mchawi wako unayetakiwa kumshinda utamjua!*

Mtu mmoja alimwona paka kwenye mlango wa nyumba yake akamkemea kwa maombi akifikiri ni mchawi ile anamaliza tu kuomba akagundua kumbe aliyekuwa anamkemea kwenye maombi ni paka wake aliyemfuga mwenyewe  shida nini? Mitazamo yake haikuwa sahihi, ndiyo maana nasisitiza kabla ya kumpinga shetani kwenye maisha yako hakikisha ndani yako una mitazamo sahihi juu ya changamoto mbalimbali unazozipitia kimaisha, kwasababu kama hauna maarifa sahihi au mitazamo sahihi ndani yako unaweza ukamkimbiza shetani kwenye maisha yako na akaondoka lakini matatizo yako bado yakabakia pale pale

Mwisho...

*Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.*

Mungu wa mbinguni akubariki sana..

WhatsApp +255657117595

Mwl.Joseph Leonard


EURO BILIONI 10.1 ZATUMIKA MRADI UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA MIMEA TANZANI.

Na. Kadala Komba Dodoma

Kilimo ni sekta inayotegemewa sana Tanzania kwa ajili ya kutoa malighafi kwa ajili ya taifa letu.


Tarehe 16 mwaka 2021 mwezi wa 2 Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliingia mkataba wa kutekeleza na kuimarisha Afya ya mimea na jumuiya ya Umoja wa ulaya.

Mradi huu ni wa miaka 3 na miezi 6 na umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Shirika la Kimataifa la Kilimo na chakula ambapo FAO ni msimamizi wa mradi na utekelezaji umefanywa na serikali kupitia mamlaka ya mimea na viatilifu uliochini ya Wizara ya Kilimo.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde wakati akizindua mradi uboreshaji wa huduma za afya ya mimea Tanzania kwa usalama wa chakula uliofanyika katika ukumbi wa St.Gasper jijini Dodoma.


Aidha ameongeza kuwa mradi huu unalenga kuhakikisha usalama wa chakula nchini kwa kuimarisha mfumo wa ukaguzi wa utoaji wa vyeti na usafi wa mazao yanayo safirishwa nje ya nchi.

Mradi huu unalenga kuthibiti vizimbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao yanayonaingia au yanayotoka nchini yanakuwa na ubora unaokidhi viwango vya soko la kimataifa.

Mhe.Mavunde amewashukuru Umoja wa jumuiya ya ulaya na shirika la umoja wa mataifa Kilimo na Chakula (FAO) kwa kufadhili na kusimamia fedha za mradi huu ambao ni mradi muhimu kwenye sekta ya kilimo nchini kwani utachochea uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya bunge Sekta ya Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma amesema kuwa mradi huu utawasaidia wakulima kwani walikuwa wanapata shida hivyo kupitia mradi huu mazao na mimea itakuwa salama na tutapata chakula kingi cha kuweza kulisha taifa pamoja na nchi za nje.

Aidha ameongeza kuwa kama kamati watakuwa wanatembelea mradi ili kuukagua na kuangalia namna gani wakulima wanafikiwa kwa wakati ili kuwasaidia wakulima kupata mazao yaliyo bora ma kwa wakati.

Dkt.Ishengoma ameishukuru Serikali na kuomba mradi kusimamiwa vizuri pamoja na kuwa nao bega kwa bega ili kuweza kutekelezwa ipasavyo.

Naye Naibu Katibu Mkuu Sera na Mipango Obadia Nyagiro amesema kuwa mradi huu umelenga kuimarisha mfumo wa kidijitali wa kufanya takwimu pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu kuhusu maswala ya mimea.
 
 

 
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde akizindua mradi uboreshaji wa huduma za afya ya mimea Tanzania kwa usalama wa chakula
 

 

GLOBAL FUND YAUNGA MKONO SERIKALI KUKABILIANA NA MAGONJWA NCHINI.

Na mwandishi wetu- Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja Mkaguzi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kupiga Vita UKIMWI, TB na Malaria (GLOBAL FUND) Bwa. Andrew Hammond ofisini kwake Jijini Dodoma.

Dkt. Jingu amesema mazungumzo hayo yalilenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya afya katika maeneo yao.

Ameongeza kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kushirikana na mfuko huo kwani umekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha vifaa tiba kama ilivyo azima ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia  Suluhu  Hassan  ya kujenga miundo mbinu ya  na kuboresha masuala ya tiba kwa wananchi.

Naye Meneja Mkaguzi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa kusaidia mapambano  dhidi ya  UKIMWI, TB na Malaria (GLOBAL FUND) Bwa. Andrew Hammond ameishukuru Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko huo katika kupiga vita maradhi ya Kifua Kikuu, Malaria na Ukimwi.

Ameahidi kuwa Mfuko wa Dunia utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na magonjwa hayo hapa nchini kwa kuelekeza rasilimali fedha kwa ajili ya kununua dawa pamoja na kuboresha mifumo ya utoaji huduma ya afya.

MWISHO

 



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizungumza alipokutana na kufanya mazungumzo na Meneja Mkaguzi kutoka (GLOBAL FUND) Bwa. Andrew Hammond Ofisini kwake Jijini Dodoma.

 


*DKT. KIRUSWA AIAGIZA GST NA STAMICO KUFANYA TAFITI ZA MADINI MUFINDI NA KILOMBERO*



 
Na. Mwandishi wetu Dodoma 
 
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kufanya tafiti za madini katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro na wilaya ya Mufindi mkoani Njombe kwa lengo la kubaini aina ya madini yaliyopo katika wilaya hizo.

Hayo yamebainishwa na Dkt. Kiruswa wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abubakari Asenga katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameainisha maeneo mbalimbali yenye madini ya dhahabu na vito katika wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Akijibu swali hilo amesema, Taasisi ya GST imefanya utafiti wa awali sambamba na kuchora ramani kwenye maeneo yote yaliyopo katika Jimbo la Kilombero katika mfumo wa Quarter Degree Sheet (QDS).

Dkt. Kiruswa amesisitiza kuwa, tafiti za awali zilizofanyika  katika wilaya ya Kilombero, zilionesha uwepo wa madini ya dhahabu na madini ya vito katika Kata ya Chisano.

Ameongeza kuwa, GST ilifanya utafiti wa awali na kuchora ramani ya eneo la Hifadhi ya Milima Udzungwa na maeneo jirani ambapo utafiti wa madini uliofanyika katika maeneo hayo hauoneshi taarifa zozote za uwepo wa madini ya thamani katika milima hiyo.

Mkoa wa Morogoro umebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini ikiwemo dhahabu, Shaba, Kinywe, madini ya viwandani (Ulanga, Kaoline),  madini ya ujenzi (mchanga, kifusi) na madini ya vito ( Rubi, Rodolite).



WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO KWA NIDA KUONGEZA KASI UZALISHAJI WA VITAMBULISHO

Na Moreen Rojas Dodoma

Mamlaka inayoshughulika na utoaji wa vitambulisho vya Taifa NIDA wametakiwa kuongeza kasi  ya uzalishaji wa vitambulisho vya Utaifa ili kumsaidia mwananchi kupata wepesi wa kutambulika anapokuwa na mahitaji mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa  katika Kongamano la sita la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi jana Jijini Dodoma ambapo ameitaka wizara ya mambo ya ndani ya nchi kuongeza kasi ya utoaji wa vitambulisho vya Taifa huku akizitaka Taasisi za kifedha kuendelea kutoa mikopo kwa riba nafuu 


Sambamba na hayo Waziri  mkuu ameitaka mikoa ambayo haijaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi waanzishe kwa mwaka huu wa fedha 2022-2023.



Akitoa Taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya uwekezaji wananchi kiuchumi katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bengii Issa amesema jumla ya mifuko na programu za Uwezeshaji wananchi kiuchumi zipo 85 ambapo mifuko na program 75 zinamilikiwa na serikali huku mifuko 10 ikiwa inamilikiwa na sekta binafsi.



Kwa upande wake Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema bado kuna changamoto ya watanzania kushindwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na kiwango cha kimataifa.

Akitoa ufafanuzi Mkuu wa kitengo cha biashara Stanbic bank  Kai Molel amesema kama bank wanatoa huduma nyingi za kifedha kwa taasisi za umma na wafanya biashara lakini pia kuwawezesha wananchi wa Tanzania kuweza kufaidika na fursa zinazotokana na uwekezaji kama kauli mbiu inavyosema.



Kongamano la Sita la Uwezeshaji wananchi kiuchumi limebebwa na kauli mbiu isemayo ''uwezeshaji wananchi katika uwekezaji''
 
Wazir Mkuu Kassim Majaliwa akizindua taarifa ya utekelezaji wa Sera ya Taifa uwezeshaji Kiuchumi



 

 

CHANZO KIKUBWA CHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA NI HIKI.



Mwanzilishi na mwasisi wa kwanza wa  Ndoa ni Mungu,

Mungu alipomuumba Adam alimpa kazi  2 kubwa  kulima bustani na kuitunza,pia akampa kazi  ya kuwapa wanyama wote majina.

Baada ya yote hayo Mungu alimwangalia Adam na akaona siyo vyema Adam awe peke yake,akamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 

Alimfanya mwanamke kutoka  kwenye Ubavu wa Adam,Kwa kumpa Adam Usingizi mzito akaondoa ubavu mmoja akaufanya mwanamke,

 Ndipo Mungu akamletea Adam akamkabidhi mkewe,Ndipo Adam akasema hakika huyu ni nyama katika nyama yangu na mfupa katika mifupa yangu.

Mungu alipomuunganisha Adam na Hawa kuwa mwili mmoja aliwabariki akawaambia zaeni mkaongezeke.

Kwa maana kwamba kila watakachoenda kufanya  kama wanandoa kitazaa na siyo kuzaa tu kitaongezeka kwa sababu Mungu ndiye amewaunganishankwa KUSUDI lake.

Mithali 18:22
[22]Apataye mke apata kitu chema; 
Naye ajipatia kibali kwa BWANA. 

Wanaume unapompata mke umepata kitu Chema alafu umepata kibali kwa Mungu,huko nje unataka kwenda kutafuta nini tena?

Sasa kinachoua Ndoa Nyingi na kwa kasi kubwa sana sasa hivi ni Hiki;

1.TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA.

Vijana wengi ambao wapo kwenye mahusiano,hawana mahusiano masafi mbele za Mungu,Mahusiano yao yameanza kwenye Misingi ya ngono na siyo Mungu.

Hawatafuti Misingi imara kwa Mungu bali katika miili yao,jambo ambalo linapelekea mahusiano hayo kutawaliwa na shetani zaidi kuliko Mungu.

Mahusiano yanapotawaliwa na shetani zaidi,huwa yana uharibifu siku za usoni, hautatokea kwenye mahusiano bali utakusubiri mpaka uingie kwenye ndoa.

Inapofika suala la kufunga ndoa,Vijana hao hawatubu mbele za Mungu na kuomba Rehema kwa maisha machafu waliyoishi kwenye kipindi cha UCHUMBA, ili Mungu awarehemu na kuanza  nao safari ya  ndoa yao bali wanafunga hivyo hivyo tu kwa mazoea na kwa  kujidanganya.

Nyumba inayoanzaga na msingi mbovu huwa haikai muda Mrefu na wala hainaga uimara wowote.

2.KUKOSA UAMINIFU KWENYE NDOA
(MICHEPUKO).

Mwanaume au mwanamke ambaye yupo kwenye ndoa anapotoka nje ya ndoa yake kingono(Sex na mtu mwingine) ni kwamba amekaribisha uharibifu kwenye ndoa yake yeye mwenyewe.

Mtu anapotoka nje ya ndoa kwa uzinzi,huko nje Kuna mbwa mwitu ambao walikuwa wanakusubiri kwa hamu kubwa ili wairarue ndoa yako na isipone tena.

Unapokutana kimwili na mtu mwingine ambaye siyo mke au mume wako ina maana umekuwa mwili mmoja na huyo kahaba,kwa  maana nyingine umemuunganisha mke au mume wako na huyo Kahaba,maana mlipofunga ndoa nyinyi mlikuwa mwili mmoja.

Mithali 23:27-28
[27]Kwa maana kahaba ni shimo refu; 
Na malaya ni rima jembamba. 
[28]Naam, huotea kama mnyang’anyi; 
Huwaongeza wenye hila katika wanadamu. 

Sasa umeunganisha tena nafsi yako kwa mchepuko ukijua utatuliza akili mawazo,na maisha yawe safi kumbe umekimbilia kwenye Shimo refu.

1 Wakorintho 6:16
[16]Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 

Sasa  ukute mchepuko kama mchepuko  kabeba roho za ukahaba,ni mzinzi roho za umasikini,laana za huko kwako,katawaliwa na Mizimu ua huko kwao,tabia chafu za huko kwao,ukute ni muumini mzuri wa waganga na wachawi basi ujue ya kwamba unazoa vya kuzoa unapeleka wewe mwenyewe kwenye ndoa yako,

Dalili zinazojitokea ni Hizi;

KUMBUKA shetani akiingia kwenye ndoa haji kuleta amani,Ni anachinja,anaharibu na kuua.

1.Mtu ataanza kumuona mke au mume wake Hafai,hana thamani tena mbele yake,siyo bora tena,anamchukia sana ,hakuna upendo tena,hakuna Amani tena kama mwanzo,hakuna maelewano tena ndani ya familia,kama kuna watoto,watoto nao wanaanza kuingia kwenye matatizo.

2.Uchumi wa familia unaanza kuyumba,mali zinapukutika,biashara zinakufa,huna wateja tena,roho ya madeni inaikumba familia,kwa sababu umeenda kushikamana na kahaba,umeenda kuzoa roho za umasikini umezileta ndani mwenyewe.

Mithali 29:3
[3]Apendaye hekima humfurahisha babaye; 
Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali. 

Mahali ambapo hakuna upendo tena Uchungu huwa unazalika kwenye Moyo,Hasira zinajaa kwenye kifua ndipo kisasi kinazalika hapo,mtu anaamua kuvunja ndoa,kuua mume au mke au kufanya chochote kibaya ili mradi tu ndoa ife. 

Mithali 19:14
[14]Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; 
Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA. 

Kama una mke mzuri anakupenda,anakutii na kukuheshimu basi Tafadhali usije ukafanya ujinga wa kukaribisha michepuko kwenye ndoa yako,utajuta.

Kama una mume mzuri,anakupenda,anakujali,anakuheshi anatunza familia kwa ujumla, Muombee ili Mungu amtawale na kumlinda kwa nguvu zake.

Kutoka kwenye changamoto hii ya ndoa Kuvunjika hovyo au migogoro isiyoisha siyo kujifunza mbinu mpya za kitandani,siyo kuhudhuria semina nyingi za ndoa,siyo kumvuta kwa dawa za waganga wa kienyeji,siyo kumuita majina mazuri,

KUMBUKA ni wapi ulipoanguka ukatubu mbele za Mungu.

Kama ulishawai kutoka Nje ya Ndoa yako au Misingi yako huko nyuma ulianza na uzinzi kabla ya kufunga ndoa na imekupelekea majuto makali sana na unaona maisha yamefika mwisho kwa sababu hukujua kama maisha yako yatakuwa hivyo baada ya ndoa basi Kaa mbele za Mungu kuomba Rehema,Samehe kabisa walisababisha maimivu kwenye moyo walo na mpe Mungu nafasi  aingilie kati maisha yako na familia yako.

2 Wakorintho 7:10
[10]Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti. 

YESU ANAKUPENDA NA ANAPENDA WATU WAFURAHIE NDOA NA MAISHA YA NDOA.


 

By Glory Kwayu 
Youth/Author.
 

 

DUWASA KUMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI NZUGUNI


Na. Mwandishi wetu Dodoma.
 
 
KATIKA kukabiliana na suala la upungufu wa maji katika Jiji la Dodoma, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inaendelea na uchimbaji wa visima pembezoni wa mji ili kukabiliana na changamoto hiyo.

DUWASA mpaka sasa imekwisha chimba jumla ya visima vitano katika maeneo ya Nzuguni A visima vinne na Nzuguni B kisima kimoja.

Akizungumza wakati wa zoezi la kupima wingi wa maji katika mtaa wa Nzuguni A jijini Dodoma, Fundi Pampu DUWASA, Fadhili Mahonya amesema kazi inayoendelea kwa sasa ni upimaji wa pampu ili kujua uwezo wa kisima na kupata pampu sahihi itakayotumika.

“Kisima hiki kinaurefu wa mita 134 kwenda chini na kinauwezo wa kuzalisha maji lita 65000 kwa saa”. Amesema Mahonya

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzuguni A, Onaeli Mathias amesema ni muda mrefu sana tangu uhuru eneo la Gogwa na Dundulu kumekuwa na shida ya maji.

“Kwa mradi huu wa DUWASA ni jambo la kushukuru sana, namshukuru Rais na Waziri wa Maji na uongozi wa DUWASA kwakweli hili tatizo lilikuwa sugu tangu uhuru walikuwa wanatumia maji ya kisima”. Amesema Mwenyekiti

Amesema watu wamepata maradhi hasa homa ya matumbo kutokana na kunywa maji yasiyosalama. Pia ameongeza maji yakipatikana hata eneo hilo linaweza kuimarika kwani kwa sasa limekuwa kame sana.

Kwa upande wa Wananchi wa Nzuguni A wameishukuru Serikali kupitia DUWASA kwa kuwapelekea huduma ya maji katika eneo hilo.

Rehema Simon amasema tunashukuru wanawake kwa kutuliwa ndoo kichwani kwani tulikuwa tunachota maji mbali huku mtoto akiwa mgongoni.

“Tunamshukuru Mungu na Serikali pia kupitia DUWASA, kwa kutuletea maji, kwani kwa sasa gharama ya kupata maji ni kubwa unalipia maji pamoja na usafiri kwa gharama ya elfu sita au tano”. Alisema Loveness Abdul

Wakazi hao pia wamesema ujenzi kwa maeneo hayo utaendelea kwani awali walikuwa wanatumia gharama kubwa sana katika ujenzi hasa katika upatikanaji wa maji.

“Tulikuwa tunafuata maji kama kilomita nne, lakini kwa maji haya kusogea karibu itakuwa imeturahisishia”. Amesema Prosper Mnyoli  
Kukamilika kwa visima hivi kutaongeza kiwango cha maji eneo la Nzuguni hivyo kupunguza au kuondoa kabisa kero ya maji katika eneo hilo na maeneo ya jirani kama Ilazo.
MWISHO.
Wananchi mtaa wa Nzuguni A jijini Dodoma, “Tunamshukuru Mungu na Serikali pia kupitia DUWASA, kwa kutuletea maji
 

 

KATAMBI- MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA UMEANZA KUTOA MIKOPO KWA KIJANA MMOJA MMOJA.


Na Mwandishi wetu- Dodoma.

Naibu Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa serikali imeendelea kufanya jitihada za kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja na si kwa makundi kama ilivyokuwa awali.

Amebainisha hayo wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Vijana Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 Dodoma. Ameongeza kuwa muongozo mpya uliotolewa umerahisisha sifa za kukopa kwa vijana kulingana na mahitaji yao.

Naibu Waziri Katambi amefafanua kuwa yapo maboresho ya mifumo katika kila sekta zinazoshughulikia masuala ya vijana ambapo mifumo hiyo itasaidia kuleta mazingira wezeshi kwa vijana kuweza kujikwamua kiuchumi na kuweza kujiajiri.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika kutoa mafunzo kwa vijana ili kuweza kutatua changamoto za kiuchumi kwa vijana, Aidha amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanasaidia kuongeza maarifa,ujuzi na mipango thabiti kwa vijana kuweza kutambua vipaji vyao.

“Tunafurahi kwamba leo katika mdahalo huu ulio tolewa na shirika AMDT (AGRICATURAL MARKERT DEVELOPMENT TRUST) imetupa fursa ingine ya kusikiliza changamoto, vipaumbele, uzoefu na matarajio toka kwa vijana wote wa kike na kiume.wanaofanya shughuli zao za kiuchumi katika sekta ya kilimo.

Amesisitiza kuwa vijana waliopata mafunzo hayo waendelee kushirikiana na vijana wengine ili kubadili mitazamo na kushirikiana na Serikali kukabiliana na changamoto zinazo wakabili.

MWISHO.
 

 
 Naibu Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza jambo wakati ufunguzi wa Mdahalo wa Vijana Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 katika ukumbi uliopo Morena Hotel jijini Dodoma.
 

Sehemu ya vijana waliohudhuria Mdahalo ulioandaliwa na shirika AMDT Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 katika ukumbi uliopo Morena Hotel jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa shirika la AMDT (AGRICATURAL MARKERT DEVELOPMENT TRUST) akichangia jambo wakati wa Mdahalo wa Vijana Kuhusu Upatikanaji wa Mitaji na Kukuza Shughuli za Kilimo Biashara kwa Vijana, tarehe 15 Septemba, 2022 katika ukumbi uliopo Morena Hotel jijini Dodoma.
 


 
 
 
 
 


 

HALMASHAURI 7 ZATHIBITIKA KUWA NA MLIPUKO WA UGONJWA WA SURUA.

Na Moreen Rojas.Dodoma

HALMASHAURI  7 ZATHIBITIKA KUWA  NA  MLIPUKO  WA UGONJWA   WA SURUA.

Hayo yamesemwa na Waziri wa afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ikiwa ni kutoa taarifa kwa umma kuhusu ongezeko la wagonjwa wa surua nchini.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wagonjwa thelathini na nane(38) walithibitika katika halmashauri za bukoba sampuli (3),Handeni DC sampuli(4) Kilindi sampuli (3) Mkuranga sampuli(4) Manispaa ya kigamboni sampuli (8)Manispaa ya temeke sampuli (12)na Manispaa ya Ilala sampuli (4).

Uchambuzi huo pia ulionesha uwepo wa ugonjwa wa Surua katika halmashauri za Arusha (1)Chalinze (2) Igunga(1) Kahama(1) Kalambo(1) Kigoma DC (2) Kwimba DC (1) Masasi (1) Mvomero DC(2) Rorya DC (2) na Manispaa ya Ubungo (2),hata hivyo halmashauri hizi hazikukidhi vigezo vya kuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Surua.

Waziri Ummy ameongeza kuwa jumla ya wagonjwa wote waliothibika kuwa na maambukizi ya Surua imefikia (58) kwa kipindi cha Julai hadi Agosti 2022.

Waziri Ummy amemaliza kwa kutoa rai kwa Umma kupeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ili wapatiwe chanjo ya Surua/Rubella kulingana na umri wao.

Chanjo ya Surua/Rubella hutolewa kwa mtoto anapofikia umri wa miezi 9 kwa dozi ya kwanza na miezi 18 kwa dozi ya pili ili kupata kinga kamili.
Waziri wa afya Mhe.Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma

 

KENYA; AJIUA KISA KANYIMWA TENDO LA NDOA

Polisi katika kijiji cha Ebungaya, kaunti ya Kakamega nchini Kenya wanachunguza kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 50, anadaiwa kukatiza maisha yake baada ya mzozo wa kifamilia mnamo Jumatatu, Septemba 5,2022.


Mwili wa Ezra Skim ulipatikana ukining'inia kwenye mti ukiwa na kamba shingoni mnamo Jumanne, Septemba 6,2022. Marehemu anaripotiwa kutoweka nyumbani kwake mnamo Jumatatu, Septemba 5, kabla ya mwili wake kupatikana na wapita njia.
Akithibitisha kisa hicho, Afisa Mkuu wa Polisi wa Khayega, Elizabeth Kagehi aliomba kutafuta njia bora ya kusuluhisha migogoro yao badala ya kujitoa uhai.

Akizungumza na waandishi wa habari, dada yake marehemu Jetina Tegeno alisema kaka yake amekuwa akilalamikia kudhulumiwa katika ndoa kabla ya kifo chake. 
Alisema mke wa marehemu amekuwa akimtesa kaka yake na kumyima haki zake za ndoa kila mara.

"Katika siku zake za mwisho, yeye (Skim) alionekana kuwa na msongo wa mawazo. Amekuwa akimtuhumu mke wake kwa kumdhulumu," Tegeno alisema.

Akisimulia matukio hayo, mke wa mwendazake Maximila Anyika, alisema walikuwa wamelala wakati Skim akitoka nje ya nyumba bila kurejea.

 "Ghafla alitoka kitandani tulipokuwa tumelala, bila maelezo alitoka nje na kugonga mlango nyuma yake. Tulishtuka kukuta mwili wake ukining'inia kwenye mti," Anyika alisimulia. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Mukumu ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

*YALIYOJIRI SEPTEMBA 1, 2022 JIJINI DODOMA WAKATI SERIKALI IKITOA UFAFANUZI KUHUSU TOZO*

*Aliyosema Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba* #Chimbuko la tozo lilikuwa ni kwa ajili ya kuunganisha nguvu kama Watanzania ili tuweze kutekeleza baadhi ya mahitaji ya lazima ambayo yamekuwa yakikosa bajeti kutokana na bajeti zinazopangwa. #Katika nchi za Afrika Mashariki na SADC, hakuna nchi inayotekeleza kwa mara moja miradi mikubwa kama Tanzania, hii inapelekea uhitaji wa bajeti yetu kuongezeka kwa sababu ya miradi mikubwa inayotekelezwa. #Katika mwaka 2021, kati ya tozo zilizokusanywa, Shilingi bilioni 221 zilienda kwenye mikopo ya elimu ya juu, Shilingi bilioni 117 zilitumika kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na fedha zingine zilienda kwenye ujenzi wa madarasa. #Tozo hii sio kodi ya biashara wala haitokani na faida ya biashara bali chimbuko lake ni ushirikiano wa pamoja, ilivyokuwa inafanyika mwanzo ilitamkwa kama kodi ya miamala ya simu, kwa sababu tunataka kushirikisha watu wengi tuliona tuwashirikishe hata wanaofanya miamala ya kibenki. #Tumeendelea na tozo mwaka huu kwa sababu mbali na madarasa na vituo vya afya, kuna mambo mengine ya msingi yenye umuhimu wa kuchukuliwa hatua kwa haraka ikiwemo shughuli za uzalishaji ili zisaidie watanzania wapate ajira. #Kuanzia sasa mpaka mwezi Januari, 2023 kupitia tozo, tumepanga kujenga madarasa yasiyopungua 8,000, kumalizia vyuo vya VETA katika wilaya 72 zilizobakia pamoja na vitendea kazi katika vituo vya afya. #Tumesikia maoni ya wananchi na tumeyapokea na tumekutana na wataalam na makundi mbalimbali, ikiwemo kutozwa tozo mara mbili pale unapotoa benki kwenda kwenye simu na ukiituma kwenye simu kwenda kwa mtu mwingine, tumepokea na tunafanyia kazi. Tutatoa majibu ya utekelezaji wake hivi karibuni. #Maoni mengine ni kuhusu tozo iliyokusanywa kutoka kwenye mabenki ambayo ilitakiwa kuanza tarehe 1, Serikali imejiridhisha kwamba kuna baadhi ya taasisi za fedha zimeanza kukusanywa tarehe tarehe 15 lakini zimekata fedha kuanzia tarehe moja. Tumeona mantiki kwenye jambo hili nalo tutalifanyia kazi. #Kodi ya upangishaji majengo sio Sheria mpya isipokuwa utekelezaji wake ndio umeanza wakati huu, anayepaswa kulipa kodi ya kupangisha ni mwenye nyumba. Kuhusu mpangaji kukusanya kodi hiyo badala ya TRA wenyewe. Serikali imepokea maoni hayo na inafanyiwa kazi. #Watu wanaostahili kulipa kodi na hawalipi, wanasababisha wengine wanaolipa kodi kubeba mzigo mkubwa ndio maana kodi zetu zinakuwa juu. #Tumeweka timu zinaendelea kuchambua kuhusu mifumo yetu ya kodi, mtu ambaye ana mapato ni lazima alipe kodi iliyo sahihi. *Aliyosema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa* #Hadi kufikia Disemba, 2020, Serikali imejenga Hospitali za Wilaya 102, Vituo vya Afya 487, Zahanati 1,198, kwa kipindi cha mwaka na miezi mitano ambao Rais Samia amekuwa madarakani, katika Tarafa 570 tumeshajenga Vituo vya Afya kwenye tarafa 207. Kupitia tozo za miamala ya simu, tumejenga vituo vya afya 234 kwa Shilingi bilioni 117. #Serikali imetuwezesha Shilingi bilioni 149.5 kwa ajili ya manunuzi ya vifaa tiba vya kisasa kwenye vituo hivyo vilivyojengwa kupitia fedha za tozo. #Tusingeweza kufikia katika hatua hii kwenye sekta ya afya kama zisingekuwa tozo hizi, nawahakikishia kuwa tutaendelea kusimamia vyema makusanyo tutakayoendelea kuyapata kupitia tozo hizi ili kuhakikisha huduma katika sekta ya afya zinaendelea kuwa bora. *Aliyosema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu* #Nawahakikishia wafanyakazi kuwa kuhusu maoni yao yanayohusu tozo, wasiwe na mashaka na uwakilishi wa vyama vyao vya wafanyakazi kwenye suala hilo. *IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO*

FAHAMU MAENEO YA KUOMBEA KWENYE NYUMBA UNAYOISHI

FAHAMU MAENEO YA KUOMBEA KWENYE NYUMBA UNAYOISHI 1️⃣Ombea chumba unacholala na ufunike kwa damu ya Yesu. ✅Kama ni hotel omba toba kwa kila kilichofanyika nje ya mapenzi ya Mungu. ✅Nguo zinabeba roho kwahiyo, ombea mashuka kwa damu ya Yesu. 2️⃣Ombea nyumba nzima *Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko* (Isaya 13:21) 3️⃣Ombea ardhi unayolala..na kama kuna madhabahu nyingine,vunja Hiyo madhabahu kabsa *Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu* (Mambo ya Walawi 26:6) ✅Mtu mmoja alipita kwenye Ardhi anasikia vitu vinagonga chini... ✅Na mwingine aliomba Mungu naomba ardhi kama imebeba kitu kisicho cha kwako.. na akasema naomba itapike kila kitu hapo na akatoka nyoka. Hivi ni vitu vya kweli 4️⃣Ombea mbingu iliyoko juu maana ina sauti ya kiroho.. ✅Yesu alipotoka juu ya maji na mbingu zilimfunukia *Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake* (Mathayo 3:16) ✅ Mbingu zina siri ya ajabu sana.. ✅Mbingu zinatatandaza utukufu wa Bwana. 5️⃣Ombea watu wanaoingia mahali hapo.. ✅Tamari alipobakwa alienda mahali kwa kaka yake.. na ukiwa wa Tamari ulimshika kaka yake ulileta hasira ya kuua. ""Huyo Absalomu nduguye akamwambia, je! Amekuwa nawe Amnoni nduguyo? Ila sasa tulia, dada; ni nduguyo; usilitie moyoni jambo hili. *Basi Tamari akakaa hali ya ukiwa nyumbani mwa nduguye Absalomu* (2 Samweli 13:20) ✅Kama ni mgeni amekuja kwako omba kwa ajili yake na vichujwe vitu alivyokuja navyo kwako.. ✅Kama unaombea nyumba yako hata kama mtu anavuta sigara hiyo hamu itaondoka akiwa kwako.. na ombea sana hivi vitu. ✅Ni vitu vya kawaida kabisa, anakuja mtu kuwatembelea nyumbani na mnaanza kuota ndoto ngumu ngumu. Mungu awabariki Sana Sana SHALOM 🙏 ONLY CHRIST CAN ACCOMPLISH IT WITHIN US!FAHAMU MAENEO YA KUOMBEA KWENYE NYUMBA UNAYOISHI 1️⃣Ombea chumba unacholala na ufunike kwa damu ya Yesu. ✅Kama ni hotel omba toba kwa kila kilichofanyika nje ya mapenzi ya Mungu. ✅Nguo zinabeba roho kwahiyo, ombea mashuka kwa damu ya Yesu. 2️⃣Ombea nyumba nzima *Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko* (Isaya 13:21) 3️⃣Ombea ardhi unayolala..na kama kuna madhabahu nyingine,vunja Hiyo madhabahu kabsa *Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu* (Mambo ya Walawi 26:6) ✅Mtu mmoja alipita kwenye Ardhi anasikia vitu vinagonga chini... ✅Na mwingine aliomba Mungu naomba ardhi kama imebeba kitu kisicho cha kwako.. na akasema naomba itapike kila kitu hapo na akatoka nyoka. Hivi ni vitu vya kweli 4️⃣Ombea mbingu iliyoko juu maana ina sauti ya kiroho.. ✅Yesu alipotoka juu ya maji na mbingu zilimfunukia *Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake* (Mathayo 3:16) ✅ Mbingu zina siri ya ajabu sana.. ✅Mbingu zinatatandaza utukufu wa Bwana. 5️⃣Ombea watu wanaoingia mahali hapo.. ✅Tamari alipobakwa alienda mahali kwa kaka yake.. na ukiwa wa Tamari ulimshika kaka yake ulileta hasira ya kuua. ""Huyo Absalomu nduguye akamwambia, je! Amekuwa nawe Amnoni nduguyo? Ila sasa tulia, dada; ni nduguyo; usilitie moyoni jambo hili. *Basi Tamari akakaa hali ya ukiwa nyumbani mwa nduguye Absalomu* (2 Samweli 13:20) ✅Kama ni mgeni amekuja kwako omba kwa ajili yake na vichujwe vitu alivyokuja navyo kwako.. ✅Kama unaombea nyumba yako hata kama mtu anavuta sigara hiyo hamu itaondoka akiwa kwako.. na ombea sana hivi vitu. ✅Ni vitu vya kawaida kabisa, anakuja mtu kuwatembelea nyumbani na mnaanza kuota ndoto ngumu ngumu. Mungu awabariki Sana Sana

MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa September 02 2022