March 13, 2023 Staa wa muziki wa Injili nchini Christina Shusho alifika Kanisani kwa Nabii Mkuu Geordavie jijini Arusha kwa ajili ya Ibada, lakini akiwa katikati ya mazungumzo Shusho alianza kum-mwagia sifa Nabii huyo na baadae akamuomba kiasi cha pesa ili zimsaidie kwenye shughuli yake ya uzinduzi wa Album yake mpya itakayozinduliwa April 9, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City akiwa yeye Rose Muhando, Martha Mwaipaja na wanainjili wengine.
Naye Nabii Mkuu Geordavie bila kupepesa macho aliinuka upesi ambapo kabla ya kutoa dau aliloombwa alimuomba Shusho aimbe kionjo cha wimbo wa "Nipe macho nione" ili asikie umwororo wa sauti yake, na baada ya Shusho kutii maamuzi hayo papohapo alipewa milioni 10 huku akisifiwa kuwa kilichomsukuma zaidi nabii kukubali kukwapuliwa pesa hizo ni sauti nyororo ya mwanainjili huyo.
"Wewe ni Mfalme, wewe ni Baba na si kwamba ni kujifanya wala kujipendekeza ila mimi ni mtoto wako mimi ni binti yako ninasikia Fahari nazungumza maneno haya kwa baba na nasikia nina nguvu ninaposema kitu kwa baba, siyo kitu kingine ni kazi ileile uliyotutia moyo kuendelea ndo hiyo tunaifanya, Baba natamani unipe nguvu"- alisema Christina Shusho.
Home »
» CHRISTINA SHUSHO AZIKWAPUA MILIONI 10 ZA NABII MKUU GEORDAVIE, AMUITA MFALME.
CHRISTINA SHUSHO AZIKWAPUA MILIONI 10 ZA NABII MKUU GEORDAVIE, AMUITA MFALME.
Related Posts:
SERIKALI YABAINISHA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA UTOAJI WA MIMBA USIO SALAMA. NA WAF, BUNGENI DODOMA. NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha juhudi zinazofanywa na Wizara ya Afya katika mapambano dhidi ya changamoto ya utoaji mimba usio salama ikiwemo, kutoa elimu juu ya afya ya uzaz… Read More
TANZANIA NA JAPAN KUSHIRIKIANA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI Na Eleuteri MangiKatibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) katika sekta ya michezo nchini ili kuendelea kutoa … Read More
TUKUMBUKE KULIOMBEA TAIFA - SIMBACHAWENE Na. Mwandishi Wetu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amewataka viongozi wa dini zote nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, utulivu … Read More
“SERIKALI KUJENGA VITUO MAALUM VYA UREKEBU” WAZIRI MHAGAMANa; Mwandishi Wetu – DodomaWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amesema Serikali imejenga vituo maalum vya urekebu na ufundi stadi ili kuwasadia vijana … Read More
WAHALIFU WOTE MKONO WA SHERIA UTAWAANDAMA" NAIBU WAZIRI SAGINI Na Mwandishi WNN, Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Sagini amewataka Wananchi wa Mkoa wa Mara Wilaya ya Butiama kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na ku… Read More
0 Comments:
Post a Comment