Na Masala Komba Dodoma
Naibu waziri wizara ya nishati Steven Byabato ameagiza shirika la umeme Tanzania kuwa na kitengo cha masuala ya jinsia (dawati la jinsia).
Mhe.Byabato ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habati pamoja na wadau mbalimbali ambapo amezindua programu ya usawa kazini katika ukumbi wa morena jijini Dodoma.
Aidha amesema ni wajibu wa shirika kuweka mazingira rafiki na kuboresha mazingira kwa vijana wa like na wanawake ili kuweza kuwarahisishia kufanya kazi kwa urahisi bila kupata changamoto yoyote pindi wanapokuwa kazini.
Aidha amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo chama kitahakikisha kinaisimamia serikali katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
"Ili kufikia hadma hii chama kitaelekeza serikali kuhakikisha sekta zote zinazingatia masuala ya jinsia katika shughuli zao pamoja na kuimarisha madawati ya kijinsia ili kuzuia ukatili wa kijinsia,kubuni,kuendeleza na kutekeleza mikakati ya ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi ya kiuchumi hadi kufikia 50/50" Amesisitiza Naibu waziri Byabato.
Aidha amesema kifungu cha 230 cha ilani ya chama cha mapinduzi(CCM) ya 2020_2025 inasema chama kinatambua kuwa na usawa wa kijinsia kama sehemu ya utekelezaji wa ilani yake kwa binadamu wote sawa na wanastahili heshima na fursa sawa.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2015_2020 miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuweka na kuimarisha mifumo ya haki za wanawake kwa kuanzisha madawati ya jinsia na watoto 420 katika vituo vya polisi pamoja na kuanzisha madawati hayo vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu madawati ya jinsia 162 yameanzishwa katika jeshi la magereza.
"Kumekuwa na juhudi za kupambana na vitendo vya rushwa ya ngono kupitia kampeni ya VUNJA UKIMYA iliyoratibiwa na taasisi ya kupambana na rushwa takukuru" Amesema Naibu waziri Byabato.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji Tanesco Ndg.Maharage chande amesema suala ya usawa wa kijinsia liko juu sana ambapo kipaumbele chao kama taasisi ni kuhakikisha wanawake wanaongezeka kwa kasi katika shirika lao.
Aidha amesema maeneo ya kimkakati yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kuiboresha sera ya shirika na kujenga uwezo ili sera iende sambamba na masuala ya kijinsia,kuwepo na taarifa sahihi zinazohusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye taasisi,kuruhusu fursa ya ukuzaji wa taaluma kwa wafanyakazi wanawake hasa wanaofanya kazi kwenye miradi pamoja na kuwepo kwa nafasi ya mafunzo kwa vitendo(intership)kwa wafanyakazi wanawake waliopo kazini ili kuwajengea uwezo kuelekea kwenye ajira kamili.
Naye Balozi Mwanaidi Sinare Maajar ambaye ni makamu mwenyekiti wa bodi amesema kuwa ni kweli kwamba masuala ya haki za jinsia inawahusu wanaume na wanawake yako katika nyanja mbalimbali ya serikali yetu.
Sanjari na hayo amesema kuwa hatutafikia maendeleo kama hatutazingatia wanawake has wa kwa kuzingatia sensa ya watu na makazi ambayo inaonyesha idadi kubwa ya wanawake ili kuleta usawa kazini.
Ameongeza kuwa ni wajibu wa kula mtu kuhakikisha kuwa hakuna vitendo vya kumdhoofisha mwanamke akashindwa kufanya kazi yake na pia kuhakikisha mifumo yote ni rafiki kwa wanawake ili kuwapa morali na wengine kuwa sekta ya nishati wanawake nao wanaweza na sio sekta ya nishati pekee bali nyanja zote.
Programu ya usawa kazini (Gender work program) kwa miaka minne 2023_2026 ni mradi uliofadhiliwa na benki ya Tanzania kupitia mkopo wa dunia wa gharama nafuu.
0 Comments:
Post a Comment