Home »
» TAHADHARI IMETOLEWA KWA WANANCHI KUJIKINGA NA MAJANGA YA MOTO
TAHADHARI IMETOLEWA KWA WANANCHI KUJIKINGA NA MAJANGA YA MOTO
Na Sifa Lubasi Dodoma
WANANCHI wametakiwa kuchukua tahadhari wanapotibu majeraha ya moto ili kupunguza uwezekano wa jeraha kuwa kubwa zaidi na kushindwa kutibika kwa wakati na hata kusababisha kifo
Akizungumza leo kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere square,Ofisa Muuguzi Msaidizi Mwandamizi daraja la pili David Mpaguke kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alisema majanga ya moto hutokea popote na wakati wowote
Alisema kuwa ulimwenguni kote kila mwaka takribani watu milioni moja hutafuta matibabu kutokana na kuungua moto.
Álisema kuwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka 2020 hadi 2022 imepokea na kulaza wagonjwa 225 walioungua mwa moto asilimia 87 walipona na asilimia 13 walikufa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kucheleweshwa kufikishwa hospitali, mika na desturi ya jamii,Imani na changamoto za Uchumi.
Álisema kuwa kitaalam mtu anapoungua amwagie jeraha maji safi ili kupunguza joto lisiathiri ngozi na misuli, Kisha apewe Panadol kwa ajili ya kutuliza maumivu na awahishwe hospitali
"Majeraha madogo ya moto, haraka mwaga maji baridi juu ya ngozi iliyoungua kwa dakika 15 hadi 30 husaidia kupunguza joti lisiathiri ngozi na misuli,,Álisema
Pia alisema kuwa ulaji wa vyakula vingi vyenye virutubishi vikiwemo protini ya ziada vinahitajika kusaidia kidonda cha moto kuponai
"Mgonjwa apatiwe vyakula vya profini ili Kujenga mwili ili nyama ziwe zinajengwa pia kufanya mazoezi ili kuzuia ulemavu unaoweza kutokea," alisema
Álisema kuwa kama majeraha ya Moto Ni makubwa mgonjwa hufanyiwa upasuaji wa kupandikizwa ngozi.
Álisema kuwa kumekuwa na njia mbalimbali za asili za kutibu majeraha ya Moto lakini nyingi so salama.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye moja ya mabanda kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere square Jijini
0 Comments:
Post a Comment