Na. WAF - Ziara Mkoani Kagera, Bukoba
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea katika Kijiji cha Ntoma Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera kwa lengo la kujionea hali inavyoendelea baada ya kutangazwa kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Mkoani humo.
Katika Ziara hiyo, Waziri Ummy ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Zabron Yoti pamoja na Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Bi. Shalini Bahuguna.
Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa hali ni salama na kuwataka Wananchi wa kijiji hicho na watanzania kwa ujumla kuondoa hofu kwa kuwa Serikali inawajali Wananchi wake.
“Niwatoe hofu Watanzania tuendelee kufanya kazi zetu lakini tuzingatie maelekezo ya Serikali ya kujikinga na ugonjwa huu kwa kuepuka kushikana mikono hususan kipindi hiki lakini pia tujitahidi kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.” amesema Waziri Ummy
Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na juhudi za kuhakikisha ugonjwa huo unamalizika na hautatokea tena katika maeneo hayo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kanyangele Bw. Hamim Hassan ameishukuru Serikali kwa kufanya juhudi kubwa ambapo hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeongezeka kwa kuthibitika kuwa na ugonjwa huo.
“Hatua za Serikali kupitia Wizara ya Afya zilizochukuliwa za kuwaweka sehemu maalumu waliokuwa karibu na wagonjwa imesaidia sana kutoendeleza maambukizi kwingine na hali ni shwari kwa sasa.” amesema Bw. Hassan
Home »
» KAGERA NI SHWARI HAKUNA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA MARBURG
KAGERA NI SHWARI HAKUNA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA MARBURG
Related Posts:
MKUU WA MKOA DODOMA AMEWATAKA WAAJIRI KUBAINI MBINU ZA KUPUNGUZA AJARI MAENEO YA KAZI Na Moren Rojas DodomaMkuu wa mkoa wa Dodoma ROSEMARY SENYAMULE amewataka waajiri kubaini mbinu za kupunguza ajali kwa wafanyakazi ili kupunguza ajali kazini.Ameyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo kwa Madaktari juu ya ta… Read More
MAKAMU WA RAIS: SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA MADHEHEBU YOTE YA DINIImeelezwa kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan inathamini mchango wa Madhehebu ya dini kupitia mahubiri na kufundisha neno la Mungu kwa watu wote.Hayo yamebainish… Read More
WATOTO YATIMA WAIOMBA BAKWATA KUWAWEKEA UZIO Na Peter Mkwavila KONDOAWATOTO wa Kituo cha yatima kinachomilikiwa na taasisi ya All Hafidhu Islamic Orphans Centre kilichopo Bicha wilaya ya Kondoa.Wameliomba Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuwajengea uzio … Read More
BODI YA FILAMU TANZANIA IMEUNDA KAMATI MAALUM YA KURUDISHA UTAMADUNI WA KUTAZAMA FILAMU KATIKA KUMBI ZA SINEMANa Moreen Rojas Dodoma Hatua hiyo inatarajiwa pia kutoa mchango stahiki katika uchumi wa wadau wa Sekta na Taifa kupitia viingilio vya mlangoni. Kwa upande wa usambazaji Serikali ina makubaliano ya kimataifa Televi… Read More
JUKUMU LA KUWAANGALIA WAZEE SIO LA SERIKALI PEKEE.Na Moreen Rojas DodomaKatika nchi nyingi Duniani,Wazee wamekuwa wakituzwa isipokuwa kwamba kila nchi ina namna yake ya kuwatunza wazee wao kwa kulingana na mila,desturi na tamaduni pamoja na hali za kiuchumi za nchi zao.Ha… Read More
0 Comments:
Post a Comment