Subscribe Us

WAFANYABIASHARA WANAOANZA BIASHARA WAMERUSIWA KUFANYA BIASHARA MIEZI 6 BIRA KULIPA KODI

Na Kadala Komba , Kondoa WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji amésema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kibali cha kuruhusu wafanyabiashara wanaoanza biashara kutokulipa kodi kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka moja "Rais ametoa kibali ,wale wanaoanza biashara kufanya biashara miezi sità hadi mwaka moja ndipo waanze kulipa Kodi," alisema. Álisema hayo Jana wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma Álisema kuwa jambo hilo linaonesha ni jinsi gani Rais Samia Suluhu Hassan anawajali wananchi wake Ni vyema kila mmoja akäuunga mkono juhudi za Rais katika kuwaletea wananchi maendeleo. . Pia aliwataka wananchi kuachana na mikopo umiza na Ile ya kausha damu kwani imekuwa ikiumiza wananchi. kutokana na kuwa na riba kubwa. "Halmashauri zimekuwa zikitoa mikopo ya asilimia nne, wananchi Muende mkope huko pia Rais ametoa fedha kwenye Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) ambapo mikopo hutolewa kwa riba ya asilimia tisa, Muende Sido mkachukue mikopo na kupatiwa mafunzo ya biashara," alisema. Álisema kuwa mikopo yenye riba kubwa imekuwa ikiumiza wananchi huku wakiwa hawapati faida yoyote. Pia aliwataka wanawake wanaofanya biashara mipakani kufuata sheria na taratibu. "Kama unataka kufanya Biashara mpakani kachukue hati ya kusafiria ili kufanya biashara kihalali,Kuna malalamiko ya wanawake wanaokamatwa kwa kufanya biashara mipakani bila kuwa na vibali"alisema. kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pili Mbanga alisema kuwa Sasa Kuna janga kubwa kwa watoto wa kiume na ndoa za jinsia moja. " Tujitahidi kuwalea watoto katika mazuri bila hivyo tutakuwa tunatengeneza taifa chenye kizazi cha ajabu , tusiwe bize na biadhara na kazi tuangalie pia malezi ya watoto" alisema. Jaji Mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mathew Maimu alisema kuwa palipo na mwanamke Kuna amani pia kuna uwepo wa Mungu . aliwataka wanawake kuendelea kupigania haki zao . "Tuendelee kumuunga mkono Rais na viongozi wote, tusrudi nyuma tuendelee kukaza buti badala ya kutembea tukimbie," alisema. . Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule Álisema bado wanawake ni wachache katika ngazi mbalimbali za uongozi. Pia aliwataka wanawake kutumia fursa za kiuchumi zilizopo katika mkoa wa Dodoma ili kujiongezea kipato mwisho.

0 Comments:

Post a Comment