Subscribe Us

MCHUNGAJI WAKRISTO TUMEZIDIWA MAARIFA NA WACHAWI

 Na. Kadala Komba Bahi

Daniel David Kikunile Mchungaji Kiongozi Mchungaji Daniel Kikunile wa Kanisa la Ufunuo na Uzima lililopo karibu na shule ya Msingi Bahi Misheni  Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma  Amesema Sisi wakristo ni wazembe tunazidiwa maarifa na wachawi, Mfano Mchungaji,Mwinjilisti Ametumika kikamilifu katika huduma au karama aliyupowe na Mungu kwa Kazi aliyotumwa hapa Dunia tatizo linakuja pale Kazi yake ikiisha anakufa bila kuacha Mrithi wa huduma au karama aliyonayo.


 hayo alipokuwa Akihubiri kanisani hapo Jumapili wakati Akifundisha Somo la Fimbo ya Enzi ya Kitaifa ya Kichawi Sambamba na kuhitimisha Mfungo wa siku Saba wa kuombea Wilaya ya Bahi na vijiji vyake. UFUNUO 12:5

Mchungaji Kikunile Alisema njia pekee ya kufurahia wokovu na karama tulizopewa na Mungu ni kuwarithisha watu wetu wa karibu kile ulichopewa na Mungu amekupa bure na wewe toa bure, Maono ya Viongozi wengi wa Dini wamebeba Maono mengi juu ya huduma namna ya kufanya Kazi ya Mungu tatizo linakuja wanapotwaliwa basi na Maono yamekufa hakuna mtu wa kuyaendeleza wanaobaki wanashindwa sababu ahakufundishwa, kama ni huduma inayumba nyingine zinakufa kabisa na kusaulika kama kulikuwa na huduma ya namuna hiyo.
"Tofauti na Wachawi mchawi kabla ajafa anatafuta mtu wa kumrithi Kazi aliyokuwa anafanya ya kuloga watu, kama ni Mganga anatafuta mtu wa kumwachia tunguli, Mikoba yake na irizi zake Ili kile alichokuwa anakufa ya yeye kuendelee kufanyika hata kama yeye hayupo Tena katika Dunia Kazi aliyokuwa nayo ya kuharibu maisha ya watu inaendelea kufanywa na warithi wake Tena na kuzidi Alisema .

Aidha Mchungaji Kikunile Alisema Wakristo Mungu ametupa Neema Kubwa katika huduma zetu,tunacho chakula cha kutosha kulisha kondoo zetu sababu sisi ni Wachungaji ni haki yetu kulisha kondoo waliopo kwenye Zizi letu hata tukitwaliwa na Bwana leo tunakuwa hatuna mashaka kwa kile tulichokianzisha kinaendelea,Mavuno hayatakauka Shambani mwa Bwana maana Watendakazi wanafanya Kazi ile ile kama miujiza inaendelea kutendeka uponyaji unaendelea kama Yesu Kristo alivyofanya kwa Wanafunzi wake Aliwafundisha hata Yesu alipowaacha Wanafunzi waliendeleza Kazi ile ile aliyokuwa Anafanya Yesu.
" Viongozi wezangu Ambao tumepewa Neema ya kuchunga Kondoo nawakumbusha tuache Urithi kwajili ya Ukombozi wa Kizazi hiki na kijacho kama sisi tulivyo rithishwa kutoka kwa Adamu na Musa kwa jili ya Utukufu wa Bwana na Kazi yake Alisema .

Mwisho kabisa Mchungaji Kikunile Alitoa Wito kwa Wakristo wote nchini Kumpokea Bwana kama Kiongozi wa Maisha yao, Alisema Wakristo wengi wa sasa wanaabudu Dini wameacha upendo wa kweli wanasahau kwamba Dini yako haita kupeleka Mbinguni, Mbinguni atuendi na Dini zetu Dini ni utaratibu tu wa hapa Duniani kwamba tuwe na Dini lakini Mbinguni hakuna Dini usingangane na Dini Mpendwa icho sio cheti cha kuingia Mbinguni,  Wewe Ng'a ng'ania kumjua Mungu


 

a Yesu kupata wokovu Ili uende Mbinguni Alisema .

Picha Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Akifundisha Somo la Fimbo ya Enzi ya Kitaifa ya Kichawi.

Washarika wa Kanisa hilo wakipiga makofi wakionekana kupendezwa na Somo hilo

0 Comments:

Post a Comment