Home »
» TUIMARISHENI UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI – DKT. YONAZI
TUIMARISHENI UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI – DKT. YONAZI
Na. Mwandishi Wetu – Dodoma.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kuimarisha ufanisi katika utendaji kazi wa kila siku ili kufanikiwa katika kufikia malengo ya Serikali.
Ameyasema hayo mapema leo Machi 9, 2023 katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum.
“Endelezeni ushirikiano katika maeneo yenu ya kazi na naamini kuwa, kila mtumisi ni kiongozi katika eneo lake, na hili linaweza kuleta tija katika utendaji na kuwaletea Faraja watanzania tunaowahudumia katika nchi yetu.” Alisistiza Dkt. Yonazi
Dkt. Yonazi aliendelea kuwaasa wafanyakazi hao, kufanya kazi kwa ushirikiano, upendo na amani ili kuleta matokea chanya.
“Naamini tutaendelea kushirikiana namimi na mnipe mawazo yenu katika utendaji wetu, tuweke juhudi zetu, kwani tuna kazi ambayo Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ametupa nafasi na tuitumie kwa ushindi.”alisisitiza.
Kwa hatua nyingine akizungumza na wajumbe wa menejimenti ya ofisi hiyo mara baada ya makabidhiano rasmi ya ofisi aliwaasa kuwa vielelelezo na kuwaongoza wengine kwa upendo, umoja, amani huku wakitumia nafasi zao katika kujali kila mtumishi katika nafasi yake pasipo kuwabagua.
“Niwaombe viongozi wote, tuchukie kuongoza watumishi wasio na furaha, wapeni watu nafasi na kuwaheshimu kwa kuelewa tabai zao na kuchukuliana mapungufu tukiamini kuwa umoja ni nguvu utengano ni dhaifu,”alisema Dkt. Yonazi.
Awali, akiongea katika makabidhiano hayo aliyekuwa katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu, ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, aliwashukuru Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana naye vizuri kwa kipindi chote alichotumikia Serikali katika Ofisi hiyo na kuwaomba kuendelea na moyo huo wa ushirikiano.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa TUGHE katika Ofisi Hiyo Bi. Numpe Mwambenja akitoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wa Ofisi hiyo alimshukuru Katibu Mkuu Dkt Jingu kwa kuwajengea ujasiri na kuondoa uwoga katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
=MWISHO=
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na watumishi
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi Ofisi Hiyo Bi. Numpe Mwambenja akitoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wa Ofisi hiyo alimshukuru Katibu Mkuu Dkt Jingu kwa kuwajengea ujasiri na kuondoa uwoga katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Aliyekuwa katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. John Jingu (kushoto) ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum akizungumza wakati wa kuwaaga wajumbe wa menejimenti wa Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya hafla ya makabidhiano ya ofisi.
Sehemu wa wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. John Jingu.
Related Posts:
TIMU YA MBEYA CITY YAKABIDHI ZAWADI KWA WAGONJWA KATIKA KITENGO CHA WAZAZI META.Na.Mwandishi wetu Mbeya Katika kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka, ikiwemo Krismas na Mwaka mpya timu ya Mpira wa Miguu ya Mbeya City ikiongozwa na viongozi wake wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Kitengo c… Read More
MKUU WA MKOA DODOMA MHE. ROSEMARY SENYAMULE AMEPOKEA HATI YA PONGEZI KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI GEITA Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea hati ya pongezi kutoka kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita kwa kutambua mchango wake na kuleta mageuzi katika kipindi ambacho amekua Mkuu wa Mkoa huo. Hati … Read More
UONGOZI DOREFA WAAGIZWA KUFUTILIA MAENEO YALIYOTENGWA KWAJILI YA MICHEZO Na Kadala Komba Dodoma Wanamichezo nchini waaswa kupambania tasnia ya michezo ikiwa ni agenda ya kuhakikisha tasnia hiyo inapewa thamani na kipaumbele kama sekta zingine. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa michezo N… Read More
MKULIMA WA KARANGA NA MTAMA ANAYETUMIA VIFAA VYA KISASA KULIMA NA KUPANDA Na. Kadala Komba Dodoma Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula amesema Hapa naendesha kilimo cha karanga na mtama kwa kutumia teknolojia mbalimbali katika kuandaa mash… Read More
WAZIRI WA ELIMU, PROF. MKENDA AMEZINDUA BODI YA TUME YA VYUO VIKUU 2023-2026 Na. Kadala Komba Dodoma WAZIRI Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Ameitaka Tume Ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) kushirikiana na Vyuo Vikuu Vyote Kwa kuwasikiliza, Kuwapa Muda Wa Kutosha, Kuhakikisha wanas… Read More
0 Comments:
Post a Comment