Subscribe Us

SEKTA YA UTALII INACHANGIA ASILIMIA 17% PATO LA TAIFA NA 20% FEDHA ZA KIGENI.

Na Moreen Rojas, Dodoma. Kamishna msaidizi mwandamizi Jeshi la uhifadhi ofisi ya kiunganishi TANAPA Dodoma Dkt.Noelia Myonga amesema sekta ya utalii inachangia asilimia 17% ya pato taifa na asilimia 20% ya fedha za kigeni. Dkt.Noelia ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapo na kutoa ufafanuzi kuhusiana na TANAPA na namna gani waandishi wanaweza kutumia kalamu zao vizuri ili kuelimisha jamii juu ya sekta nzima ya utalii. "Tujitahidi sana kwenye kalamu zetu kuandika habari zinazotuletea tija na Mungu atawabariki mkitumia kalamu zenu vizuri kwa kuandika ukweli na sio kupotosha kwani mkipata elimu nyie nawanachi wataelimika kupitia nyie kama kioo cha jamii" Aidha amesema kuwa malengo yao kama TANAPA ni hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania iwe imeshatembelewa na watalii milioni tano(5) ikiwa pia ni lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluh Hassan ambaye amefungua njia kwa watalii kuja Tanzania na kuonyesha nia ya dhati na sekta hii ya utalii. "Tunatoa elimu ya uhifadhi na kutoa elimu ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa jamii kila mtu kwa nafasi yake anatakiwa avisemee vivutio vyetu ili wananchi waweze kuvijua kwa maana ya watalii wa ndani na watalii wa nje"Amesema Dkt.Noelia Aidha amesema kazi yao ni kuhifadhi rasilimali zote zilizopo chini ya TANAPA huku TFS wenyewe wamejikita kwenye mambo ya misitu,kuna sheria inayotutofautisha na hizo mamlaka nyingine lakini hawa wote TAWA na TFS tunafanya nao kazi kwa ukaribu,kushirikiana pamoja na kushauriana. " Niwapongeze waandishi wa habari kwa kuweza kujitoa kufanya habari za utalii,kutangaza vivutio vyetu tena kwa kuamua kujilipia wenyewe kwenda kujionea vivutio vyetu jambo ambalo halijawahi kutokea nawapongeza sana" Amesisitiza Dkt.Noelia Aidha Dkt.Noelia ametaja baadhi ya hifadhi zinazopatikana Tanzania na sifa zake;Serengeti ni hifadhi maarufu kwa wanyama wa hamao nyumbu na wanyama wanaoonekana kwa urahisi kwani ni uwanda mpana,Ziwa Manyara inasifika kwa kuwa na simba wanaopanda miti pamoja na ndege ni hifadhi pekee inayopatikana bonde la ufa,Tarangire inasifika kuwa na tembo wengi pamoja na mibuyu mingi,Arusha national park inasifika kwa kuwa na mlima meru pamoja na utalii wa kupiga picha,Kilimanjaro Mlima mrefu afrika kivutio kikubwa kwa watalii mbalimbali,Mkomazi imepandishwa daraja kutoka pori la akiba,faru na wanyama wengine wanapatikana,Saadani Pwani hii inasifa ya kipekee kwani kuna kivutio ambacho hakiko kwenye vivutio vyovyote Tanzania ni kasa wa kijani,Mikumi inasifika kuwa na nyati wengi lakini na wanyama wengine wapo pia,Zuri kuwa na mbega wazuri wanaovutia,Ruaha wanyama wengi na idadi ya watalii wanaoenda ni wachache kwahiyo husababisha watalii wengi kwenda,Kitulo kuwa na maua mengi sana na madhari nzuri,Katavi wanyama wengi na watalii ni wachache,Bonde mahale Sokwe mtu wanapatikana kwa wingi pembezoni mwa ziwa Tanganyika,Rubondo kumekuwepo na samaki aina mbalimbali wapo wanyama wote kama tembo,sokwe mtu pamoja na ndege aina nyingi. "Shughuli za utalii zinasaidia kukuza pato la wananchi kwani wenye mahoteli wanapata wageni pamoja na kununua bidhaa kwenye maduka hivyo kuchangia pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla" Hifadhi zinazoongoza kwa utalii wa ndani ni pamoja na Saanane,Saadani,Mikumi,Manyara,Kilimanjaro na nyingine zinajitahidi. MWISHO.
Dkt.Noelia Myonga Kamishna msaidizi mwandamizi Jeshi la uhifadhi ofisi ya kiunganishi TANAPA Dodoma
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Dodoma

0 Comments:

Post a Comment