Home »
» *CCM YATOA AGIZO KUHUSU WALIMU KUPEWA VISHIKWAMBI*
*CCM YATOA AGIZO KUHUSU WALIMU KUPEWA VISHIKWAMBI*
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu kuanzia leo Januari 20, 2023, kuhakikisha vishikwambi vilivyotolewa na serika kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa.
CCM Imesema imepokea malalamiko ya kutotekelezwa kikamilifu kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji wa vishikwambi hivyo.
Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, alisema wakati akizundua ugawaji wa vishikwambi hivyo Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kuhakikisha vifaa hivyo vinakwenda kwa walengwa.
"Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivi ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini Chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo.
"Kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane wawili wanaachwa.
"Chama kinatoa maelekezo, kinaielekeza wizara husika (Wizara ya Elimu) kuhakikisha zoezi hili linakamilika na walengwa wote wanaostahili kuhakikisha wameipata vishikwambi hivyo, lakini so hivyo tu bali pia wahakikishe malalamiko haya hayapo na wasimamie zoezi kuona makundi yaliyopaswa kupewa yanafikiwa na wale ambao hawajapata wapate. Baada ya wiki moja tupate taarifa zoezi hili limekwendaje," amesema.
====
Related Posts:
MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 40 AMEKUTWA KANISANI BIRA NGUO ( MTUPU) Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni Mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye Madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambak… Read More
*CCM YATOA AGIZO KUHUSU WALIMU KUPEWA VISHIKWAMBI* CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu kuanzia leo Januari 20, 2023, kuhakikisha vishikwambi vilivyotolewa na serika kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa. CCM Imesema imepokea malalamiko ya k… Read More
PSPTB YACHUKUA HATUA KWA WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI UGAVINa. Kadala Komba Dodoma MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesem kuwa Bodi hiyo imekuwa ikichukua hatua katika madhaifu ambayo yanaweza kuleta hasara kwa serikali na kuat… Read More
WAZIRI MKENDA ANAYELETA UDANGANYIFU WA MITIHANI TUTAMKAMATA Na. Kadala Komba Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Amesema mitihani imekuwa ikienda vizuri kwenye Baraza la Mitihani la Tanzania isipokuwa inapokwenda shuleni wamekuwepo watu wachache sana… Read More
MWALIMU MWAKASEGE AINGILIA KATI VITA YA MCHUNGAJI KIMAROVITA YA MCHUNGAJI KIMARO: MWALIMU MWAKASEGE AMESEMA KATIKA SOMO LAKE LA “MAHAKAMA INAYOMPA MUNGU UHALALI WA KUHUKUMU MIUNGU” KWAMBA PAULO KATIKA UTUMISHI WAKE , KILA ALIPOKUWA AKIPINGWA AU AKIZUIWA, ALIKUWA NA UWEZO WA KUJU… Read More
0 Comments:
Post a Comment