Home »
» MKULIMA WA KARANGA NA MTAMA ANAYETUMIA VIFAA VYA KISASA KULIMA NA KUPANDA
MKULIMA WA KARANGA NA MTAMA ANAYETUMIA VIFAA VYA KISASA KULIMA NA KUPANDA
Na. Kadala Komba Dodoma
Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula amesema Hapa naendesha kilimo cha karanga na mtama kwa kutumia teknolojia mbalimbali katika kuandaa mashamba, kulima, kuvuna na sasa nategemea kuwa na teknolojia mpya ya mashine ya kuchambua karanga kulingana na madaraja na kutumia teknolojia rahisi," álisema
Alizungumza wakati wa mahojiano na Shinenews walipotembelea katika shamba lake lililopo katika eneo la Zinje, Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula álisema kuwa matumizi ya teknolojia yanafanya kilimo kiwe rahisi na uzalishaji kuwa mkubwa.
Álisema kuwa katika kuandaa mashamba anatumia trekta dogo la mkono (power tiller) ambapo hutumia lita mbili na nusu kulima shamba la ekari moja, jambo anbalo hupunguza gharama kwani unapolima kwa kutumia treka ekari moja hugharimu kati ya Sh 30,000 hadi Sh 50,000," álisema.
"Ukiwa na power tiller unatumia dizeli ya Sh 7,500 inapunguza gharama kwa kiasi kikubwa, wakati wa kupanda tunatumia mshine ambayo huchimba shimo na kufukiia mbegu, mashine hiyo niliinunua kwa Sh 350,000 ina uwezo wa kupanda eneo kubwa kwa muda mfupi"
Álisema kuwa wakati mashine hiyo ndogo ikiwa na kontena lililojaa mbegu za karanga mpandaji huipitisha pembeni ya Kamba ambapo ina uwezo wa kupanda karanga nmstari kwa mstari kwa sentiometa 50 na shimo kwa shimo ni sentimita 10.
“Unapoanza kupanda unatakiwa ukakikishe Kamba imefungwa kwa kunyooka hii hurahisisha hata wakati wa kuvuna karanga kwa kutumia mashine usiruke mstari,” alisema
Aidha alisema kuwa wakati wa kupalilia hutumia teknolojia ya kuua magugu na kuacha karanga ikiwa salama.
Álisema kuwa hata kwenye uvunaji wamekuwa wakitumia mashine na kwenye kupura mazao,' álisema. Aliwataka wakuliwa na wale wanaotaka kuingia kwenye kilimo kuwa ua utararibu wa kuwatembelea wakulima wanaotumia teknolojia ili kujifunza na kuboresha kilimo.
Alisema kuwa mpango wa Sserikali wa kuwezesha vijana kuingia kwenye kilimio utakuwa na manufaa makubwa kama vijana watakuwa na utayari wa kuingia kwenye kilimo.
“Tunatakiwa kuhakikisha vijana wanaelimishwa ili wafahamu kilimo ni nini nina amini kilimo cha teknolojia kitawavutia vijana wengi,” alisena.
Mmoja wa kibarua katika shamba hilo, Maneno Paulo alisema kuwa matumizi yam ashine yanmepelekea kazi yao kuwa nyepesi.
“Hapa tunapanda kwa kutumia mashine, tunavuna kwa mashine kazi yetu inakuwa rahisi tifauti na kufanya kazi kwa kutumia mikono.
Aliwataka vijana kujiajiri kupitia kilimo kwani kuna fursa nyingi.
Agostine Ng’ambi mkazi wa Zinje ambaye pia ni kibarua katika shamba hilo alisema kuwa upandaji ni rahisi na wanatumia muda mfupi katika kazi zao za kila siku.
mwisho
Ukiwa na power tiller
Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula
Akiwa na Power Tiller akiandaa shamba la Karanga
Agostine Ng’ambi mkazi wa Zinje ambaye pia ni kibarua katika shamba hilo
Mmoja wa kibarua katika shamba hilo, Maneno Paulo
mashine hiyo ndogo ikiwa na kontena lililojaa mbegu za karanga mpandaji huipitisha pembeni ya Kamba ambapo ina uwezo wa kupanda karanga nmstari kwa mstari kwa sentiometa 50 na shimo kwa shimo ni sentimita 10.
Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula Akitoa maelekezo kwa Vibarua
0 Comments:
Post a Comment