Home »
» WAZIRI MKENDA ANAYELETA UDANGANYIFU WA MITIHANI TUTAMKAMATA
WAZIRI MKENDA ANAYELETA UDANGANYIFU WA MITIHANI TUTAMKAMATA
Na. Kadala Komba Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Amesema mitihani imekuwa ikienda vizuri kwenye Baraza la Mitihani la Tanzania isipokuwa inapokwenda shuleni wamekuwepo watu wachache sana ambao wanajihusisha na udanganyifu na kwamba Serikali haitavumilia udanganyifu huo.
“Anayeleta udanganyifu kwenye mitihani tutamkamata, walimu hakikisheni mnakataa kujiingiza katika udanganyifu huo na kuwa makini zaidi kwenye masuala ya mtihani,” amesisitiza Waziri Mkenda.
Waziri Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 17 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA) ambapo amesema kwa kufanya hivyo ni kuandaa taifa ambalo litashindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Amesema Shule zitakazofungiwa Kwa Udanganyifu Wa Mitihani Sio za Watu Binafsi Peke Yake Bali hata Zile Za Umma Endapo Tu Mtu atabainika amehusika Kufanya Jambo Hilo na Atafukuzwa Kazi na Kushtakiwa Mahakamani" Waziri Mkenda amekemea vikali udanyanyifu wa mitihani unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu na kuwataka Wakuu wa shule kutojiingiza katika udanganyifu huo.
Na kuongeza kuwa "Kwa sasa kuna kesi zinaendelea kwa wale ambao walituhumiwa kwa kuvujisha mitihani na nawaahidi pindi hukumu zao zitakopotolewa na Mahakama, tutaweka majina yao hadharani ili kila mmoja asijaribu kujihusisha na udanganyifu huo."
Akizungumzia suala la malezi shuleni Waziri Mkenda amewataka walimu kufuata Mwongozo wa Malezi, Unasihi na Ulinzi wa Mtoto katika Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu wa 2020 na kwamba kama kuna changamoto zibainishwe.
“Tushirikiane kufanya ulinzi wa watoto, hakikisheni shuleni hawalali watoto wawili kitanda kimoja na kama kuna changamoto ya vyoo toeni taarifa kwa Mkurugenzi kuhusu changamoto hizo, lengo ni kuhakikisha kunakuwepo na mazingira salama ya utoaji elimu na kuwalinda watoto,” amesisitiza Waziri Mkenda.
Amewataka Walimu kuangalia maudhui ya vitabu vinavyoingia shuleni ili visiharibu wanafunzi lakini pia kutumia Skauti na Viongozi wa dini katika kuendeleza malezi mazuri ya watoto shuleni.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Dkt. Charles Msonde amewataka Wakuu wa Shule kufuatilia utendaji wa walimu shuleni ili kuondoa alama F kwenye masomo wanayofundisha.
“Naendelea kusisitiza kufuatilia utendaji wa walimu, lakini pia wanafunzi wanapoingia shuleni tuanze na kuhakikisha wanakuwa vizuri katika lugha, wanapoilewa na kuweza kuiandika inakuwa rahisi kwao kuelewa masomo,” amesisitiza Dkt. Msonde.
Kwa upande wake Rais wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA), Frank Mahenge ameishukuru Serikali kwa namna inavyoshirikiana na Umoja huo na kuiomba pamoja na kazi nzuri wanayoifanya ya kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu nchini kujenga pia nyumba za walimu.
Awake
Aidha Katibu wa Elimu Jimbo Mkuu Katoliki la Dodoma Father Chrisant Mganga,amezitaka taasisi kuwa makini na vitu vinavyoletwa na Haki za Binadamu kunavitu vya hovyo vinaingizwa kwetu na baadhi wanatete vitu hivyo ambavyo vimetufikisha hapa tulipo leo , vijana wanafanya mambo ya hovyo mashuleni utasikia maadili ya memomonyoko hayo yote yamesababishwa na baadhi ya watu kuto kuwa waaminifu na kushindwa kujitambua wenyewe.
@wizara_elimutanzania
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Akizungumza na Wadau wa Elimu
Katibu wa Elimu Jimbo Mkuu Katoliki la Dodoma Father Chrisant Mganga,
Khamis Ali Naibu Mkurugenzi Elimu (BAKWATA)
Waziri Mkenda na Wadau wa Elimu
Related Posts:
MWENYEKITI UWT TAIFA ATEMBELEA HOSPITALI YA MJI KONDOA Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa UWT na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mhe. Marry Chatanda, leo tarehe 22 Novemba 2023 ametembelea Hospitali ya Mji Kondoa ikiwa ni ziara yake kwa Halmashauri hiyo kujionea … Read More
ASA YAPONGEZWA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMONa Mwandishi wetu- Tabora Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameupongeza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa kukamilisha Awamu ya Kwanza ya Mradi wa miundombinu ya Umwagiliaji kati… Read More
DARAJA LA BILLIONI 1.5 KUONDOA DARAJA LA KAMBA KONDOA. Wananchi wa kijiji cha Hurui kata ya Kikore Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wamesema ujenzi wa daraja la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 linalotarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi Disemba 2023 litatatua… Read More
WANANCHI NTYUKA WAILALAMIKIA SERIKALI KULIPWA FIDIA YA BARABARA. Na. Modern Rojas DodomaWananchi wa mtaa wa ntyuka na chimalaa wailalamikia serikali kuwachelewesha kuwalipa fidia ya mradi wa barabara.Michael Emily mkazi wa eneo hilo amesema wananchi wanaodai ni takribani 172 na tangu… Read More
SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKOSTORY SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKO Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Serikali itaendelea kulinda kwa nguvu na gharama zote uhuru wa wananchi wa k… Read More
0 Comments:
Post a Comment