Subscribe Us

WANAWAKE 15 WAMEFANYIWA UPASUAJI WA UGONJWA WA FISTULA

Na. Mwandishi wetu Mbeya Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi Amezindua Rasmi kambi ya matibabu ya Fistula katika Hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya ,amesema Ugonjwa wa Fistula unawasababishia maumivu makali wanawake huku ukiwahathiri kisikolojia hasa pale wanaponyanyapaliwa na jamii pamoja kukimbiwa na wenza. Aidha Naibu Waziri amesema tangu kuanzishwa kwa kambi hiyo Januari 16 mwaka huu mpaka sasa ni wanawake 15 pekee ndio waliofanyiwa upasuaji kati ya wanawake 60 wanaolengwa kunufaika na huduma hiyo ambayo inatolewa bure. “Kambi hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Hospital kanda ya Mbeya na Ofisi ya Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Kwaupande wake mwakilishi wa chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania ,Dk.Peter Majige amesema wanawake 3000 huugua kila mwaka ugonjwa huo nchini huku 1500 pekee wakitibiwa kutokana na matatizo mbalimbali . Amesema matibabu ya ugonjwa huo huwa yana gharama kubwa hali ambayo wananchi wengi wanashindwa kumudu na hivyo kukilazimu chama hicho kuomba ufadhili kutoka kwenye mashirika mbalimbali ya kitaifa. Ameiomba serikali kusamehe baadhi ya gharama za matibabu ya ugonjwa huo ili kuwasaidia wagonjwa wengi Zaidi kupata matibabu na kuondokana na tatizo hilo. Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Francis Rwegoshora amesema Hospital hiyo inatoa huduma ya matibabu ya ugonjwa huo lakini wagonjwa wengi wanashindwa kufika kutokana na uchumi mdogo pamoja na kutopata Taarifa . Amesema kambi hiyo iliyopelekwa katika Hospitali hiyo itasaidia kuwatambulisha matibabu hayo kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ili waende wakatibiwe.
Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi Akiwa na mwakilishi wa chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania
MATUKIO KATIKA PICHA YA UZINDUZI RASMI WA KAMBI YA MATIBABU YA FISTULA MBEYA

0 Comments:

Post a Comment