Home »
» PSPTB YACHUKUA HATUA KWA WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI UGAVI
PSPTB YACHUKUA HATUA KWA WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI UGAVI
Na. Kadala Komba Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesem kuwa Bodi hiyo imekuwa ikichukua hatua katika madhaifu ambayo yanaweza kuleta hasara kwa serikali na kuathiri Miradi mikubwa kwa wakuu wa vitengo vya Ununuzi na Ugavi.
Akizungumza jijini hapa leo Januari 19,2023 wakati wa kutoa taarifa ya matokeo ya mitihani ya 25 ya Bodi hiyo Mkurugenzi huyo amesema wanachosisitiza ni somo la hebabu na ni dhana ambayo imejengwa tangu chini kuwa somo hilo ni gumu kitu ambacho sio sahihi hesabu inafaulika.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mtaalamu wa manunuzi ni vizuri ajue hesabu ambayo itamsaidia kujianini na kuandika ripoti katika shughuli zake na kwamba Ununuzi na Ugavi unaakisi zaidi katika uelewa wa manunuzi,uelewa wa dhana nzima mtambuka katika ule mzunguko wa shughuli za kimanunuzi kwa kuwa anatakiwa kupiga hesabu katika uwiano mbalimbali.
"Tunachukua hatua pale tunaona kuna madhaifu ambao yanaweza kuleta hasara kwa serikali na pia inaweza kuathiri utoaji huduma kwa watu hasa katika miradi mikubwa," amesema Mbanyi.
Ameongeza kuwa kumekuwa na mamalamiko kwa baadhi ya wanunuzi na kwamba wao kama Bodi mwaka wa fedha uliopita waliamru Wakuu wa vitengo 20 kuondolewa kwenye nafasi zao baada ya kutathimini taarifa ya matumizi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari wameshatuma barua 73 kuwaeleza makosa waliyoyafanya,udhaifu na makosa yaliyoonekana kwenye maunuzi na wanunuzi 68 kupeleka utetezi wao katika Ofisi ya Bodi.
Akizungumzia matokeo hayo amesema jumla ya watahiniwa 1,216 walisajiliwa kufanya mitihani ambapo watahiniwa 1,135 sawa na asilimia 93.3 walifanya mitihani hiyo na kwamba kumekuwa na ongezeko la watahiniwa 1,031, ikilinganishwa na msimu uliopita.
"Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 452 ni wapya na waliobaki 683 ni watahiniwa waliokuwa wanarudia baadhi ya masomo," amesema Mkurugenzi huyo.
Mbanyi ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 613 sawa na asilimia 54.0 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 474 sawa na asilimia 41.8 watarudia baadhi ya masomo kuanzia moja hadi masomo matatu kutegemeana na idadi ya masomo aliyofeli na watahiniwa 48 sawa na asilimia 4.2 wamefeli masomo yote katika ngazi mbalimbali.
"Katika masomo 34 waliyopimwa watahiniwa, masomo 18 yalifanywa vizuri, masomo 10 yalifanywa kwa wastani na matokeo ya masomo 6 yalikuwa mabaya kwa maana ya kuwa chini ya wastani. Huku watahiniwa watatu wakiibuka kama watahiniwa bora katika ngazi za mitihani za Professional I,iii na CPSP," amesema.
Mwisho
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi
Related Posts:
SHAKA AWASILI MKOANI TABORAKatibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka amewasili mkoani Tabora kwa ziara ya siku tano kuanzia tarehe 16-20 Agosti, 2022 yenye lengo la kuimarisha uhai wa chama, kufuatilia na kukagu… Read More
MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI DODOMA Na. Kadala Komba Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akipokea Mwenye wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba tayari kuanza kukimbizwa mkoani humo kuanzia leo Jumanne Agosti 16, 2022. Wak… Read More
JINSI YA KUEPUKA KUCHELEWA KANISANI 1. Piga pasi nguo zako zote kabla ya kulala. 2. Safisha na andaa viatu kabla ya kulala. 3. Tayarisha Biblia yako, Notebook, Kalamu, n.k mahali pamoja. 4. Tayarisha zaka na sadaka yako.(Kisha sema na Mungu unataka akufanyi… Read More
NBS IDADI YA WATALII WALIOINGIA NCHINI YAONGEZEKA HADI ASLIMIA 62.7. Na.Kadala Komba Dodoma OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema kuwa idadi ya watalii walioingia nchini kuanzia Januari hadi Julai yaongezeka hadi kufikia 742,133 ikilinganishwa na 456,266 kwa kipindi Cha mwaka 2021, saw… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 17, 2022… Read More
0 Comments:
Post a Comment