Home »
» MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 40 AMEKUTWA KANISANI BIRA NGUO ( MTUPU)
MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 40 AMEKUTWA KANISANI BIRA NGUO ( MTUPU)
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni Mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye Madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe huku sababu zikiwa bado hazijajulikana.
Katibu wa Kanisa hilo, Elias Ngailo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Mwanaume huyo amekutwa akiwa mtupu amelala na kulazimika kumsaidia kumvalisha nguo na kumpeleka Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako huku wakiwa hawajui kama anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili.
"Tumemuhoji baadhi ya maswali amesema yeye ni wa Morogoro sasa umekujaje huku hawezi kujieleza ila tulifadhaika tukaona walau tumsaidie kwa kumtafutia nguo asitiri mwili wake baada ya hapo tukampeleka kwenye Vyombi vya Usalama ili wajue namna ya kumsaidia"
Mwinjilisti wa Kanisa hilo John Kisogo amesema awali baada ya kumkuta Mtu huyo katika madhabahu walilazimika pia kumfanyia maombi "Huyu Mtu alisema alijikuta tu yupo Madhabahuni tukamuuliza ulikuwa peke yako akasema nilikuwa na mwenzangu"
Credit: Millard Ayo
Kwa habari kemkem za kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha tembelea Shine News kila wakati hakika hutopitwa na chochote saa 24.
Related Posts:
RC SENYAMULE MAANDALIZI YA SENSA YAMEKAMILIKA ASILIMIA 98 Na.Kadala Komba Dodoma MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema ili kuhakikisha zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23,2022 linafanyika kwa ufasaha Mkoa wa dodoma umezindua namba maalum… Read More
MATUKIO KATIKA PICHA ;BAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WANASIASA WALIOHUDHURIA JUBILEI YA MIAKA 50 MATUKIO KATIKA PICHA: Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wanasiasa waliohudhuria adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya miaka 50 ya Jimbo Katoliki Singida pamoja na Miaka 25 ya Upadre wa Mhashamu Edward Elais Mapunda Askofu … Read More
MBUNGE DITOPILE TUNAKUSHUKURU RAIS KWA KUTUPATIA WAKULIMA MBOLEA YA RUZUKU Na. Kadala Komba Dodoma MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkulima, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa aliyoyafanya katika sekta ya Kilimo ambapo kwa mara ya kwanza b… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 22, 2022… Read More
MCHUNGAJI CHARLES PROSPERITY KUHESABIWA HAKUNA MAHUSIANO NA MAMBO YA GIZA KISHETANIWA YA USHETANINa. Kadala Komba Dodoma MCHUNGAJI kiongozi Charles A. Prosperity wa kanisa la The Covenant Place lililopo kisasa Relini Dodoma amewataka watanzania kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa ya watu na makazi ambalo linatal… Read More
0 Comments:
Post a Comment