Home »
» WAZIRI WA ELIMU, PROF. MKENDA AMEZINDUA BODI YA TUME YA VYUO VIKUU 2023-2026
WAZIRI WA ELIMU, PROF. MKENDA AMEZINDUA BODI YA TUME YA VYUO VIKUU 2023-2026
Na. Kadala Komba Dodoma
WAZIRI Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Ameitaka Tume Ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) kushirikiana na Vyuo Vikuu Vyote Kwa kuwasikiliza, Kuwapa Muda Wa Kutosha, Kuhakikisha wanasaidiwa na Sehemu yenye Vikwazo wapewe Ushauri Wa haraka Kabla ya Kuchukua Sheria Nyingine Muhimu.
.
Mkenda Ameyasema hayo Leo January 19,2023 Alipokuwa kwenye Akizinduzi Bodi Ya Tume ya Vyuo Vikuu kuanzia mwaka 2023 hadi mwaka 2026 Jijini Dodoma.
.
Amesema wanahitaji Watanzania wengi waende Nje Ya Nchi Wakasome Na Sio Masomo ya Sayansi Tu hata Na Masomo Mengine Kwa Sababu hawawezi kutarajia Watu Ndani ya Nchi ikiwa Hawana Walimu Wa Kutosha.
.
Mkenda Ameitaka Pia TCU Kujaribu Kuvitambua Vyuo vinavyofundisha Nje Ya Nchi na Kuvielewa Vizuri Hasa Medicine.
.
Aidha, Mkenda Amesema Vyuo Vikuu ni Muhimu Sana kusimamia Ubora Wake Kwa Sababu vitakuwa Chachu Ya Kuwasaidia Kuongeza Ubora Kwa Ngazi ya Chini.
.
Nae Mwenyekiti Wa Bodi Ya Tume Hiyo Prof. Penina Mlama Amemuahidi Waziri Mkenda Kwamba watakuwa Began Kwa Bega Na wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Katika Juhudi zake Za Kupaisha Sekta Ya Elimu Juu Ili Watanzania Wote wanaopita Katika Vyuo Vyao Vikuu wapate Elimu Yenye Tija na Ya Viwango Vya Juu Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.
WAZIRI Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda,
0 Comments:
Post a Comment