Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa UWT na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mhe. Marry Chatanda, leo tarehe 22 Novemba 2023 ametembelea Hospitali ya Mji Kondoa ikiwa ni ziara yake kwa Halmashauri hiyo kujionea Miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita.
Akiwa Hospitalini, hapo Mhe. Chatanda amewajulia hali wagonjwa waliokuwepo kwenye jengo la dharura ambalo limejengwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 300 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu chini ya Mpango wa UVIKO.
Aidha, Mhe. Chatanda ametembelea jengo jipya la Mama na Mtoto ambalo lipo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake baada ya kupata fedha kiasi cha Shilingi Milioni 900 za ukarabati wa Hospitali ya Mji ambapo majengo matatu yamejengwa ikiwemo jengo la upasuaji, mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia Maiti (Mochwari).
Hata hivyo, ameagiza kufanyiwa marekebisho yaliyoonekana katika majengo hayo ikiwemo kumalizia jengo la mama na mtoto ili wananchi waanze kupata huduma katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na wahandisi kusaidia kutoa utaalam ili kujenga majengo yaliyo bora.
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
MWENYEKITI UWT TAIFA ATEMBELEA HOSPITALI YA MJI KONDOA
DARAJA LA BILLIONI 1.5 KUONDOA DARAJA LA KAMBA KONDOA.
Wananchi wa kijiji cha Hurui kata ya Kikore Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wamesema ujenzi wa daraja la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 linalotarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi Disemba 2023 litatatua kero ya muda ya mrefu ya kutumia daraja la kamba kuvuka mto na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watoto kutofika shule Pia wakazi wa Kijiji hicho kushindwa kuuza mazao yao kutokana na kukosekana kwa miundombinu hiyo.
Hayo yamebainishwa Leo Novemba 22,2023 baada ya Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Timu iloyoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Joketi Mwegelo na Wataalamu wengine wa Mkoa na Wilaya hiyo kufika katika daraja hilo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Aidha Ndg. Mwegelo wakati akitembelea mradi wa Maji katika Kata ya Kisese amemtaka mkandarasi anaye tekeleza mradi huo kuanza ujenzi wa tanki ndani ya siku saba awe ameshaanza utekelezaji wa mradi huo ili kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa mwiba mchungu kwa wananchi wa Kisese.Wito huo umetolewa baada ya kupita siku ishirini na moja ambazo mkandarasi alitakiwa awe eneo la mradi akiendelea na Ujenzi wa Mradi.
Hata hivyo Ndg. Mwegelo amesema licha ya Viongozi mbalimbali kuwachukulia hatua baadhi ya Viongozi ambao walikuwa wakitekeleza mradi huo lakini bado inaonekana kuendelea kusuasua jambo linalopelekea kucheleweshwa kwa ukamilishaji wa Mradi huo.
Pia, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Kikore na Kisese kupeleka watoto shule na kuachana na tabia ya kugeuza watoto kufanya kazi za ndani .
Mkoa wa Dodoma umekuwa wa 17 kufikiwa na ziara ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT ) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Mary Chatanda na Viongozi wengine ambapo wanatarajia kupita katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ikiwa tayari wamesha kamilisha ziara yao Wilaya ya Kondoa kwa kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) na maendeleo ya miundombinu mbalimbali pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa huo.
WANANCHI NTYUKA WAILALAMIKIA SERIKALI KULIPWA FIDIA YA BARABARA.
Na. Modern Rojas Dodoma
Wananchi wa mtaa wa ntyuka na chimalaa wailalamikia serikali kuwachelewesha kuwalipa fidia ya mradi wa barabara.
Michael Emily mkazi wa eneo hilo amesema wananchi wanaodai ni takribani 172 na tangu mwaka 2022 mwezi wa 8 waliahidiwa kabla ujenzi haujaanza watalipwa mafao yao lakini mpaka sasa hawajalipwa,kamati ilienda TANROAD lakini hakuna matokeo chanya yoyote mpaka sasa na wakati waliambiwa wasubiri wiki moja,baada ya hapo wakasema wanaotaka kubomolewa kwa hiari wajitokeze sasa wanashangaa imekuaje tofauti.
"Leo wanasema wanataka watu wachache sasa watu wa chache kivipi?hivyo tunamuomba Waziri wa Ujenzi Mhe.Innocent Bashungwa aje aangalie dhulma hii na Rais wetu Mama Samia atusikie" Amesema Ndg.Emily
"Tumekuwa tukifuatilia viongozi wa Mkoa wanatupiga danadana tufanye nini?chuo cha mwalimu Nyerere wamechukua maeneo ya wananchi hawalipa watu wa eneo husika,serikali jamani ituangalie na kama mradi huu umeshindikana usitishwe" Ameongeza Bwana Edward Lamale.
Muhanga mwingine wa barabara Bi.Eva Daniel amesema aliambiwa saa 9 mtendaji atakuwa ameshasaini karatasi kwaajili ya kupata hela lakini matokeo yake anazungushwa tu na kudanganywa na ameambiwa kwa vile nyumba yake iko karibu na barabara aibomoe ahame na hawezi kuhama kwa sababu hana hata mia na kama serikali imewachoka iwaambie wahame na watahama mpaka chama maana kila siku wakikusanyika wanaambiwa meneja yuko kwenye kikao.
"Kwa upande wa mtendaji wa kata kiukweli hayupo na sisi na tunaona kabisa hatufai yuko kinyume na sisi kunawatu wana wito wanataka kufanya kazi na leo waandishi mmekuja hataki kuongea Luna nini kilichojificha?mtendaji wa kata ni tatizo kawapa barua baadhi ya wananchi kwa nini?tunataka mtendaji mwingine sababu huyu hawezi kutumikia wananchi maana ofisi ya kata mara nyingi imefugwa" Amesisitiza Bi.Eva
Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya ufuatiliaji Atnas Matonya amesema miradi mingi ya serikali wanashangaa kwa nini? haina chanzo cha kulipa fidia na watakopowalipa wawalipe na muda kwa sababu wako nje ya makubaliano na mojawapo ya miradi ambayo imekuwa hailipwi ni pamoja na mradi wa mwalimu nyerere takribani hekari 50 waliahidi kulipa watu pamoja na mradi wa udom ujenzi ng'ong'ona.
Baada ya wananchi kutoa kero zao Injinia Colman Gaston ambaye alikuja kwa niaba ya meneja wa TANROAD Mkoa wa Dodoma amewaambia wananchi kuhusu malipo ya mradi wa barabara unaendelea kwani wananchi walifanyiwa uthamini lakini vitabu bado vinafanyiwa kazi hivyo ameagizwa awaambie kwamba suala lao linafanyiwa kazi.
"Hivyo niwaombe wananchi suala la fidia linafanyiwa kazi na niwaombe mvute subira hivyo siku ya leo ntapeleka maombi kwamba wananchi wanataka kumsikiliza na kila mtu apate haki yake kutokana na taratibu zinavyotakiwa" Amesema Injinia Gaston
Naye Yona Andrew Diwani wa kata hiyo amesema uwepo wa mgogoro huo umetokana na ucheleweshwaji wa fidia ya barabara lakini ni takribani miezi 6 sasa ambapo imepelekea wananchi kuwa na taharuki kutokana na mvua kubwa zinazokuja na kuleta maafa zaidi na yeye kama kiongozi alichukua hatua ya kuunda kamati ndogo ili kushughulikia huu mgogoro.
SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA MAWAZO, KUABUDU - DKT. BITEKO
ASA YAPONGEZWA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO
NEC YAKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI MKOANI TABORA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa wakazi wa maeneo yaliyoteuliwa kwa ajili ya majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo ambalo linalenga kupima utayari wa mifumo na vifaa vya uboreshaji wa Daftari.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Tabora leo tarehe 20 Novemba, 2023 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri amewapongeza wakazi wa mkoa huo kwa mkoa wao kuwa miongoni mwa mikoa miwili ambayo kata zake zimeteuliwa kufanya majaribio hayo ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.
Mhe. Mapuri amezitaja kata zitakazofanya majaribio hayo kuwa ni Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, ya mkoa wa Tabora na Kata ya Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, katika Mkoa wa Mara.
“Tume inawapongeza wakazi wa Mkoa wa Tabora kwa mkoa wenu kuteuliwa kuwa mwenyeji wa zoezi
RUSHWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO LIMEKUWA TATIZO SUGU.
Rushwa kwenye miradi ya maendeleo limekuwa tatizo sugu,na wengine wamekuwa wakiliita kansa hivyo ni jukumu la kila mmoja hukakisha analeta usawa kwenye eneo hili.
Hayo yameelezwa na Mhe.George Simbachawene Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU).
Aidha ameongeza kuwa miradi iliyopo ni kwaajili ya kila mtanzania na kila mtu ana haki yakufanya kazi kwenye miradi hiyo lakini wasimamizi wa miradi wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya hivyo ni jukumu la watumishi wote wa sekta hii kuhakikisha wanakabiliana na watu hawa ambao wamekuwa miba kwenye jamii.
"Rushwa kwenye miradi ya maendeleo limekuwa tatizo sugu hivyo ni muhimu kushughulikia tatizo hili hasa kwa wale wasimamizi wa miradi wamekuwa wakitumia vyeo vyao vibaya kwa kuwanyanyasa wananchi hivyo watumishi wote wa sekta hii ni jukumu lenu kusimamia maadili ya kazi na kutenda haki" Amesisitiza Mhe.Simbachawene
Aidha ameongeza kuwa hatua nyingi zinafanywa dhidi ya mapambano ya Rushwa na Serikali imeipa(TAKUKURU) ajira mpya zaidi ya 600 ili kupambana na rushwa pamoja na watumishi kujituma kwa weledi katika mapambano dhidi ya rushwa hivyo suala la rushwa ni Agenda kubwa duniani.
Sanjari na hayo amesema kuwa kwa ulimwengu wa sasa katika kufanya kazi za kiuchunguzi watafakari nini cha kuboresha na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzipatia suluhu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)ambaye ni Kamishna wa Polisi C.P Salum Rashid Hamduni amesema mafanikio ya mwaka 2022 kupitia chaguzi mbalimbali bilioni 171 wameziokoa kupitia operesheni maana bila operesheni fedha hizo zingeishia mikononi mwa watu.
Naye Neema Mwakaliele Naibu Mkurugenzi Mkuu (TAKUKURU) amesema mkutano huo unalenga kujenga utendaji kazi wa watumishi wa taasisi hiyo pamoja na kuongoza mapambano dhidi ya rushwa ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa muadilifu na kutenda haki bila upendeleo.
Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU una jumla ya wajumbe 61 ambapo kauli mbiu inasema"Kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu Tutimize wajibu wetu".
WATENDAJI WA TARAFA NA KATA WATAKIWA KUONESHA ELIMU ZAO KWA VITENDO
Wito umetolewa kwa watendaji wa Tarafa na Kata za Mkoa wa Dodoma kuonesha thamani ya vyeti vyao vya Elimu kwenye utendaji wa kazi kwenye Tarafa na Kata zao kwani wao ndio wanatarajiwa kuiletea Serikali heshima kwa wananchi wake kwa. Hayo yamebainishwa leo Novemba 20, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa watendaji hao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Roma Complex Jijini Dodoma.
Mhe. Senyamule amesema watendaji wa Kata wanapaswa kufuata Sheria na kanuni za kiutendaji ili kuwapunguzia mzigo wa kero wananchi wa chini na sio kusubiri viongozi wa juu kufika kwenye maeneo yao kutatua kero.
"Serikali imeekeleza kila mtendaji asikilize kero na kuzitatua. Kazi kubwa ya mtendaji ni kuonesha njia kwenye Tarafa yako kwani changamoto kubwa iliyopo hapa ni mabadiliko bado ni madogo kulingana na matarajio ya Serikali. Mumewekwa pale kulinda heshima ya Serikali kwa kazi, maneno na matendo yenu. Jambo hili halifanyiki kwa uthabiti wa kutosha ndio maana munapewa mafunzo haya ili kuwakumbusha Sheria na kanuni mpya ili kuongeza maarifa kwa watumishi waweze kumudu majukumu yao" amesema Mhe. Senyamule.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurungenzi wa TAMISEMI Bi. Angelista Kihanga, amesema kuwa, mafunzo haya yamepewa umuhimu wa hali ya juu kwani yalianza awamu ya kwanza kwenye Mkoa wa Mbeya na Mikoa ya Magharibi na Sasa yanafanyika kwenye Mikoa ya Kanda ya kati kwa kuhusisha Maafisa Tarafa na Kata kwani ndio watekelezaji wa sera za nchi kwa wananchi.
Mafunzo kwa Maafisa wa Tarafa na Kata yaliyoandaliwa na Wizara ya TAMISEMI, yanagusia mada mbalimbali zikiwemo mwongozo wa ushughulikiaji malalamiko ya wananchi katika utumishi wa umma na huduma kwa wateja, ununuzi wa umma, nafasi ya Afisa Tarafa na Mtendaji wa Kata katika mafanikio ya Serikali, kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma na Sera na Sheria za uendeshaji wa Serikali za Mitaa.
MASHIRIKA YASIYO TAKA KUSHIRIKI MICHEZO YACHUKULIWE HATUA KALII.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ayaandikie Barua Mashirika ambayo hayajapeleka Wafanyakazi Kushiriki michezo ya SHIMUTTA Mwaka 2023 na kueleza sababu zakutoshiriki ili Serikali ione hatua zakuchukua.
Dk Biteko ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa wiki mbili.
Aidha ameongeza kuwa watumishi wa Umma wafanye kazi kwa Weledi na kutoa huduma Bora kwa watanzania pamoja na kuondoa hali ya watanzania kuona taasisi zao ni kero kwa Wananchi hivyo watatue kero hizo kwakutimiza wajibu wao.
"Tumekubaliana kufanya jambo fulani basi tulifanye, na kama tunaona halifai basi bora tuliache, kuliko tunakubaliana kufanya kitu halafu hatukifanyi; haiwezekani viongozi wote hapa wanalalamika, Katibu Mkuu analalamika, Naibu Waziri analalamika na mimi nilalamike?, hapana sijaumbwa hivyo, sioni sababu yoyote ya kutamkika au ya kuandikika, kwamba kuna mashiriki ya umma 248 na hapa yapo mashirika 57 tu; haiwezekani." Amesisitiza Dkt.Biteko
Aawali, Mwenyekiti wa Kamati ya SHIMMUTA, Roselyne Massama amemweleza Naibu Waziri Mkuu kuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya muitikio mdogo wa Mashirika ya Umma kushiriki mashindano hayo jambo ambalo linazorotesha mashindano hayo.
Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Charles Maguzu amesisitiza michezo maofisini na serikali ya awamu ya sita inasisitiza michezo ambapo watumishi wawe na muendelezo wa michezo maeneo ya kazi ili kutokomeza magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Kwa upande wake Naibu Waziri,Sanaa na Michezo Hamisi Mwijuma amesema
serikali itoe tamko juu ya Mashirika ambayo hayawaruhusu Wafanyakazi kushiriki michezo kwani michezo ni njia nzurii ya kudumisha uhusiano na haswa kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kwani kwa kipindi hichi cha serikali ya awamu ya sita michezo imeenda kimataifa zaidi kupitia sekta ya michezo haswa mpira wa miguu haswa timu kongwe simba na yanga na Tanzania kujulikana kimataifa kupitia sekta hii.
Kwa upande wake Afisa uhifadhi mwandamizi Carlos Ernest Mbilo kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania(TAWA) amesema mashindano hayo yatadumisha uhusiano na taasisi mbalimbali na kwa upande wao mchezo mpira wa miguu wanafanya vizuri na upande wa netiboli wamepoteza mechi 1 na wanafanya vizuri kujituma lakini kikubwa ni nidhamu ili kuhakikisha wanapata vikombe vyote.
Naye Patrick Gandye Mwenyekiti wa michezo kutoka mfuko wa taifa wa jamii(NSSF) amesema michuano ilianza tangu jumamosi umuhimu mkubwa wa mashindano haya ni kujenga ukaribu na mashirika mengine ya serikali na taasisi ambazo hazijashiriki kama mgeni rasmi inabidi wafanye hima waweze kushiriki kwenye haya mashindano ikiwemo taasisi binafsi pamoja na mashirika ya serikali.
"Tuna mechi moja dhidi ya WCF tunaamini tutafuzu katika hatua inayofuata,tunaamini mwaka huu tutafanya vizuri licha ya kukutana na magwiji wa mchezo hivyo tunaamini tutachukua ubigwa,changamoto ni kwamba hatupati muda wa kutosha wa kufanya mazoezi,kama unavyojua kama mtumishi wa serikali muda ni mchache mno lakini haituzuii kutimiza majukumu yetu ya kimichezo" Amesisitiza Nora Mwidunda Meneja timu ya netiboli NSSF.
Naye Raymond Nyarufugo Mtumishi wa bandari ya Tanzania(TPA) amesema anawasihi taasisi zingine ziweze kuleta wanamichezo,kwa sababu michezo inasaidia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na magonjwa ya saratani lakini pia kuimarisha uhusiano katika taasisi za umma,kwenye taasisi yao kwa mwaka jana walikuwa washindi wa pili na walifanya vizuri.
UZALENDO WAHIMIZWA UTUNZAJI MIRADI BAHI
Na. Mwandishi wetu Bahi
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dodoma Ndg.Jawadu Mohammed ametoa Rai kwa wasimamizi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuitunza ili wananchi wanufaike zaidi na maendeleo yanayoletwa na kiongozi wao Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika kila Halmashauri ili idumu kwa muda mrefu.
Amesema kila mwanachi anapaswa kuwa mwangalifu Katika matumizi ya miradi hii kwani huo ndio uzalendo wa nchi kwa kila mtu kujali na kuzingatia miradi inayoletwa kwenye Halmashauri zao.
“Ni lazima kuzingatia na kuona umuhimu wa kila mradi unaoletwa na kutumia njia zote kuhakikisha kila huduma muhimu inafika kwenye kila Kata ikiwemo huduma ya maji, umeme, N.k.
“Halmashauri ni lazima kuendelea kufanya jitihada za kimaendeleo ili angalau baadhi ya maeneo yenye changamoto zozote za kijamii ziweze kutatuliwa kwa haraka" Amesema Ndugu Mohammed.
Vile vile, amesisitiza suala la upandaji miti kwenye mazingira yanayowazunguka ili kuondoa changamoto za majanga kama mafuriko na kusababisha ukame hivyo, kila mwananchi anajukumu la kupanda mti.
Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Ndg. Maranyingi Matukuta amesema miradi inakuja kwenye Mkoa wetu ili tuweze kunufaika nayo hivyo miradi hiyo itunzwe vizuri kwani ni miradi yenye thamani nyingi na ni mizuri.
“Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Halmashauri inayofanya vizuri kwenye miradi hivo, Rais wetu mpendwa Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ana lengo zuri kwa wananchi wake wa Bahi, hivyo, isimamiwe kwa weledi na watumiaji waitunze” Amesisitiza Ndugu Matukuta
Pia ziara ya kamati hiyo iliweza kutembelea Mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Chiona ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 493, Mradi wa Maji Chali Makulu, Chali Isangha na Chali Igonga inayogharimu kiasi cha Bilioni 02 na kumalizia kwenye Ujenzi w Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Chali inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 544.
WILAYA YA KONGWA KUJA NA MBIO ZA KIHISTORIA.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini imeandaa mbio za Marathon kwa lengo la kuutangaza mchango wa Wilaya hiyo na Tanzania kwa ujumla katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.
Kupitia mbio hizo Ofisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuyatambua maeneo ya kihistoria, kuyalinda, na kuyaendeleza ili kuenzi historia yataifa na kuyafanya sehemu ya utalii wa kihistoria katika maeneo ya urithi wa ukombozi yaliyopo nchini.
Hayo yameelezwa leo November 15,2023 Jijini hapa na Mkuu wa Wilaya hiyo Remidius Mwema wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya kuitangaza wilaya hiyo kupitia mbio za marathon zitakazoanza November 25,2023 wilaya ya Kongwa mkoani hapa.
Amesema mbio hizo za marathon ambazo zimepewa jina la "Kongwa African liberation Marathon"imezingatia taratibu zote za marathon na kwamba zimegawanywa kwenye makundi ya Km 5,Km 10 na Kilometa 21 huku mgeni rasmi wa mbio hizo akitarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro.
Amesema Wilaya ya Kongwa imegusa ukombozi na historia ya harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika zikiwemo Afrika ya Kusini,Zimbabwe,Angola na Msumbiji na hivyo kuwa na nafasi ya kujitangaza kama sehemu ya vivutio vya utalii.
"Serikali itashirikiana na nchi tulizozipa hifadhi wakati wa harakati za ukombozi kwa kukarabati majengo yaliyotumika na wapigania uhuru wa Afrika ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wao na kuitunza historia hiyo kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae” amesema
Amesema kupitia Marathon Wilaya hiyo itatangaza fursa kiuchumi na Uwekezaji zilizopo ikiwemo Kilimo,Viwanda,Ranchi ya taifa,Soko la kimataifa la mahindi Kibaigwa na Hoteli za kitalii .
"Kwa kuwa Kongwa ni lango la kuingia makao makuu ya nchi tunategemea kuwa sehemu ya kivutio cha utalii na uhifadhi wa historia,hivyo tumetenga eneo la Pandambili kwa ajili ya Uwekezaji wa Viwanda,tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza, " Amesema na kuongeza;
"Niwaombe wana Dodoma na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu
kuendelea kutangaza fursa zetu
kama ambavyo Serikali yetu imekuwa ikijitolea fedha kukarabati baadhi ya maeneo muhimu ya kihistoria kupitia wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo, "amesema
Kwa upande wake Kelvin Msumule Makamu mwenyekiti wa kamati amesema kama kamati wamejipanga kuhakikisha kila kitu kiko sawaa na wanawakaribisha watanzania wote kushiriki katika jambo hilo la kihistoria na kuongeza kuwa wamejipanga namna ambavyo watapokea wageni kutoka sehemu tofauti tofauti na kuwasihi watu wote wahakikishe wanafika kongwa ili kuweza kunufaika na fursa zinazopatikana wilayani hapo ambazo ni za tofauti na za kipekee ambazo huwezi kuzipata popote pale isipokuwa wilayani hapo.
Mbio hizo zimebeba dhima inayosema " kuthamini nchi na mchango wa wilaya ya kongwa kwa nchi za kusini mwa afrika"ambapo mbio hizi zitazinduliwa rasmi mwaka huu na kufanyika kila mwaka wilayani hapo.
WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA INALENGA KUWAFIKIA WADAU MBALIMBALI.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Wiki ya huduma za fedha inalenga kuwafikia wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa umma,wanafunzi,wakufunzi,wanawake,vijana,watu wenye mahitaji maalumu,wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs),waendesha boda boda,machinga,asasi za kiraia,wahariri na waandishi wa vyombo vya habari,watoa huduma za fedha,watoto na umma kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na kamishna wa maendeleo ya sekta ya fedha kutoka wizara ya fedha Dk.Charles Mwamwaja wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa wizara hiyo jijini Dodoma kuelezea maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa tarehe 20 hadi 26 novemba 2023 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid Arusha.
Aidha ameongeza kuwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi watashiriki na wanaendelea kualikwa kushiriki katika maadhimisho haya ikiwa ni pamoja na Wizara,idara na wakala wa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
"Wasimamizi wa Sekta ya fedha,taasisi za fedha,asasi zisizo za kiserikali,sekta binafsi,bodi za wataalamu,vyama vya wafanyakazi,vyombo vya habari,taasisi za elimu na utafiti,washirika wa maendeleo,vyama vilevile vya sekta ya fedha,makundi ya watoaji wa huduma za fedha na taasisi za dini zinazotoa huduma hizo" Ameongeza Dk.Mwamwaja.
Aidha amesema njia mbalimbali zitakazotumika katika kutoa elimu ya fedha kwa umma ikiwemo,machapisho(vipeperushi na mabango madogo),uandishi wa insha,gari la matangazo,semina,maonesho ya bidhaa za fedha,majukwaa ya kidigitali(mfano,simu za kiganjani),mitandao ya kijamii,vyombo mbalimbali vya habari(Tv,Radio,Magazeti)pamoja na burudani.
"Malengo ya wiki ya huduma za fedha ni kujenga uelewa na weledi kwa umma katika matumizi sahihi ya huduma za fedha zinazotolewa ili kujenga uchumi na kuondoa umaskini,kuimarisha ufanisi wa masoko ya fedha kupitia elimu ya fedha,kuongeza upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha,kutoa elimu ya kumlinda mtumiaji wa huduma za fedha,kuwezesha wananchi kusimamia vizuri rasilimali fedha,kuwezesha wajasiriamali wadogo kuongeza ujuzi na matumizi sahihi ya huduma za fedha katika kukuza biashara zao,kuimarika kwa utamaduni wa kujiwekea akiba,kukopa na kulipa madeni na kuongeza kwa mchango kwa mchango wa sekta ya fedha kwenye ukuaji wa uchumi" Amesisitiza Dk.Mwamwaja.
Sanjari na hayo utekelezaji wa wiki ya huduma za fedha unatarajiwa kuwa na matokeo chanya kwa mtu binafsi,kaya,jamii na taifa kwa ujumla kwa kuongezeka kwa idadi ya watu wenye kiwango cha ufahamu wa elimu ya fedha na maarifa juu ya upatikanaji na utumiaji wa bidhaa na huduma rasmi za kifedha,kuimarika kwa uelewa na matumizi ya masoko ya fedha,kusogeza huduma za fedha karibu zaidi na wananchi,kuimarisha matumizi ya huduma hizo pamoja na kupata maoni na ushauri wa kuboresha huduma hizo,kuwawezesha watumiaji wa huduma za fedha kuelewa haki na wajibu wao,kuwawezesha wananchi kupata maarifa kuhusu namna bora ya kusimamia vizuri rasiliamali fedha,kuwaunganisha wajasiriamali na fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta ya fedha katika kukuza na kuimarisha biashara zao,wananchi kupata maarifa na uelewa wa masuala ya fedha na hivyo kuwezesha kujenga utamaduni wa kutumia huduma rasmi za kifedha na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
Kauli mbiu itakayotumika katika wiki ya huduma za fedha kitaifa ni "ELIMU YA FEDHA,MSINGI WA MAENDELEO YA KIUCHUMI".
"TUMERIDHISHWA NA UTEKELEZAJI NA UBORA WA MIRADI YA CHEMBA " -JAWADU
Kamati ya siasa ya Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Katibu Wa Itikadi na uenezi (NEC ) Mkoa wa Dodoma Bw.Jawadu Mohammed imewapongeza wasimamizi wa miradi inayotekelezwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ikiwemo Miradi ya Shule na Hospitali kwa kuzingatia ubora na ufanisi unaotakiwa.
Akizungumza na baadhi ya viongozi walioshiriki katika ziara ya ukaguzi wa Miradi hiyo Bw. Mohammed amewataka watumishi wa Umma kuitangaza na kuwa Mabalozi Wazuri wa Miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema "ni lazima tuwe na watu makini wa kufuatilia miradi inayoletwa na Rais wetu ili wananchi wasiwe na changamoto katika kupata huduma na ndio maana zimejengwa shule na Hospitali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na zinazostahili.
“Serikali ipo imara na imedhamiria kuhakikisha wananchi wanapata huduma za umeme, maji, mabweni, madarasa na majengo yote yanakua kwenye ubora na uimara wa Hali ya juu.Ni lazima miundombinu zote zikamilike kwa wakati kama mikataba inavyotaka hatufikirii kuona miradi inavuka muda wake wa utekelezaji,” Amesema Bw. Mohamed.
Pia Bw. Mohamed amesisitiza suala la upandaji Miti kwa Kila mradi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa bora na imara hivyo kudumisha Sera ya Serikali ya Mkoa ya "Kijanisha Dodoma".
Kamati hiyo ilipata fursa ya kutembelea mradi wa Barabara kwa kiwango cha lami uliogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 599, ujenzi wa kituo cha afya Farkwa uliopokea kiasi cha Shilingi Milioni 500, Ujenzi wa Shule ya Msingi na awali Sankwaleto uliopokea kiasi cha shilingi Milioni 396, ujenzi wa Zahanati ya Sankwaleto ambao umepokea kiasi cha Shilingi Milioni 97, na ujenzi wa Mradi wa maji Babayu uliopokea kiasi cha shilingi Milioni434.
Ukaguzi wa Miradi mbalimbali unaofanywa na Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wa Kamati Bw. Mohhamed ni muendelezo wa ziara ya kikazi wanayoifanya katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Dodoma.













































