Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

WAZIRI PINDI CHANA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI TAWA



Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo tarehe 12 Oktoba, 2022 amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA aliyoiteua hivi Karibuni.

Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi iliyofanyika Makao Makuu ya TAWA Mkoani Morogoro, Dkt. Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kumteua Mwenyekiti wa Bodi  ya TAWA na kuwapongeza wajumbe Wote wa Bodi hiyo kuteuliwa  kuiongoza TAWA.

"Nichukue nafasi hii Kumshukuru sana Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kumteua "Chairman" (Mwenyekiti) wetu Mej. Jen.(Mstaafu) Hamis Semfuko asante sana ametuletea "Chairman" hodari kabisa na Kwakweli tuna matumaini makubwa sana na wewe" amesema

"Kwa dhati kabisa nawapongeza Wakurugenzi wa Bodi wote Kwa kuteuliwa kuiongoza Bodi hii ya TAWA" ameongeza.

Dkt. Pindi Chana amesema uteuzi wa bodi hiyo umefanyika Kwa umakini mkubwa na kuzingatia weledi  na uzoefu wa wakurugenzi hao ambao utaisaidia taasisi hiyo kufikia malengo hususani katika utekelezaji wa mikakati ya kuzuia ujangili, kuongeza idadi ya watalii na mapato na hivyo kuendeleza sekta ya Wanyamapori.

Aidha Waziri Pindi Chana ametoa rai Kwa bodi hiyo Kuweka mikakati ya Changamoto ya ongezeko la matukio ya Wanyamapori wakali na Waharibifu na uvamizi wa mifugo hifadhini.

Sambamba na hilo, Mhe. Dkt. Chana amewataka watu wenye tabia ya kuingiza mifugo ndani ya hifadhi kuacha vitendo hivyo mara moja.

"Nitumie nafasi hii kuushirikisha Umma kwamba maeneo ya hifadhi zetu siyo maeneo ya kulishia mifugo, haya ni maeneo ambayo tunapaswa kuyalinda Kwa maslahi ya Wote" amesema

Dkt. Chana ameongeza vitendo vya kuingiza mifugo hifadhini vinaleta athari kubwa  Kwa kukausha vyanzo vya maji, kuharibu mazingira na athari zake kuwa kubwa Kwa Taifa, hivyo amewaomba wananchi washirikiane na Serikali katika kuhifadhi maeneo yaliyohifadhiwa Kwa lengo la uhifadhi Kwa maslahi ya Nchi yetu.

Mbali na shughuli ya Uzinduzi wa Bodi, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alizindua mitambo mbalimbali iliyonunuliwa na TAWA Kwa fedha za UVIKO - 19 ambayo ni mashine za kuchima visima vya maji, matreka, "caterpillars", boti maalumu kwa ajili ya doria n.k

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Elaimani Sedoyeka amesema TAWA ina maeneo makubwa  takribani asilimia 10 ya maeneo yote Nchini, hivyo anatumaini kwamba itabuni mikakati mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuimarisha shughuli za Uhifadhi, kuboresha miundombinu ya Utalii, kujenga uwezo wa watumishi pamoja na matumizi ya teknolojia katika kuongeza ufanisi na tija kiutendaji.

Akielezea mikakati ya Bodi mpya ya TAWA, Mwenyekiti wa Bodi Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko amesema mkakati wa kwanza ambao Bodi itaupa kipaumbele ni kupunguza migongano kati ya watu na Wanyamapori "Human Wildlife Conflicts" Ili kuhakikisha TAWA inakuwa chombo ambacho kinakuwa na faida Kwa Serikali na Umma.

Kamishna wa Uhifadhi TAWA ambaye pia ni Katibu wa Bodi iliyozinduliwa leo, Mabula Misungwi Nyanda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Kwa kumteua Mej. Jen. Mstaafu Hamis Semfuko kwa awamu nyingine Ili aendelee kufanikisha kazi kubwa aliyokwisha ianzisha.

Aidha amempongeza Mwenyekiti huyo Kwa kuendelea kuaminiwa na kuteuliwa kuiongoza TAWA na kumuahidi ushirikiano Wakati Wote wa utekelezaji wa majukumu ya Bodi Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
 
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi iliyofanyika Makao Makuu ya TAWA Mkoani Morogoro
 

 

SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KWA WATAALAMU WA NDANI WA MIFUMO

Na WAF - DSM

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwekeza kwa Wataalamu wa ndani wa mifumo ili kuhakikisha miradi yote inayoanzishwa na Wafadhili inaendelea kusimama siku Wafadhili wanapomaliza muda wao. 

Dkt. Shekalaghe ameeleza hayo, katika majadiliano ya pamoja yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya na OR TAMISEMI kwa kushirikiana na Wadau kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la PATH linalotekeleza mradi wa "matumizi ya sahihi ya takwimu" (Data Use Patnership - DUP) yaliyofanyika usiku wa Oktoba 12, 2022 Jijini Dar es Salaam. 

Amesema, Serikali inaendelea kuhimiza matumizi ya mifumo katika maeneo mbalimbali, hususan katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa wananchi kwani inasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji na itasaidia kupata takwimu sahihi na kwa wakati ambazo zitasaidia katika kupanga matumizi sahihi na udhibiti wa magonjwa. 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anaeshughulika na masuala ya Afya OR TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amesema, ili nchi ipige hatua kwa kasi ni muhimu mifumo ipewe kipaumbele kwani inasaidia kufanya ufuatiliaji na kuongeza utendaji katika maeneo ya kazi na kuepuka gharama zisizo za lazima. 

Aidha, Dkt. Magembe amesema, licha ya kazi kubwa kufanyika katika kuboresha mifumo nchini bado ipo haja ya kuongeza kasi ya uwekezaji katika eneo hilo ili mifumo iweze kuwasiliana baina ya mfumo wa hospitali moja kwenda hospitali nyingine (interoperability), jambo litalosaidia kupunguza gharama kwa mwananchi kwa kuepuka kurudia kufanya vipimo.

Aliendelea kusisitiza kuwa, ni muhimu Wadau kuendelea kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya nchini kupitia matumizi ya mifumo ili kupunguza matumizi ya taarifa za makaratasi, hali inayohatarisha usalama wa taarifa hizo na takwimu katika maeneo ya kutolea huduma. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa Data Use Patnership (DUP) Dkt. Seif Rashid amesema, matumizi sahihi ya takwimu yanasaidia kufanya maamuzi sahihi, hususan katika kutenga fedha na rasilimali watu kwa usahihi na kwa wakati kulingana na mahitaji. 

Nae, Mkurugenzi wa Tehama OR-TAMISEMI Bw. Eric Kitali amewataka Mashirika na Taasisi kutoka nchini kupenda kuwatumia Wataalamu wa ndani kutengeneza mifumo yao ili kutunza taarifa za taasisi zao, pia kufanya hivyo ni ishara ya uzalendo.

"Tupende vya nyumbani, tupende mifumo inayotengenezwa na Wataalamu kutoka ndani ya nchi, pia itasaidia kuongeza usalama."Amesema. 

Mwisho.
 
 
 

 
 

 

 

MCHUNGAJI AWATAKA WAGONJWA WANAONGUDULIKA NA TATIZO LA AFYA AYA AKILI WAPELEKWE HOSPITALI BADALA YA KWA WAGANGA WAKIENYEJI.

Na Peter Mkwavila CHAMWINO.

 

 

ASKOFU wa kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T) Kanda ya Kati Brayson Msanjila,amewashauri familia zinazogundulika kuwa na wagonjwa wa afya ya akili waache tabia ya kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji na wapiga ramli.badala yeke wawapeleke kwenye vituo vya afya ili wakapime afya zao kitaalamu zaidi.

 

Msanjila amesema hayo alipokuwa apokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Chalinze nyama wilaya ya Chamwino kwenye ibada iliyoandaliwa kwa ajili ya kumpongeza mchungaji Saimon Sandiya aliyetimiza  miaka 40 toka awe kwenye utumishi wake,

 

Ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa la   Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T) Usharika wa Yerusalemu Chalinze Nyama Chamwino.

 

Askofu ameziomba familia hizo pindi zinapotokea kuwepo kwa mgonjwa wa afya ya akili,ni vizuri akapelekwa hosptalini badala ya huko kwa waganga na kwa wapiga ramli.

 

Alisema kuwa tatizo la afya ya akili likipatiwa matibabu haraka kwa asilimia kubwa linatibika haraka tofauti kama mgonjwa huyo akipelekwa kwa waganga wa kienyeji.

 

“Hivyo niziombe familia hususah huku vijijini pindi mnapogundua kuna tatizo hilo miongoni mwenu acheni kumkimbiza mgonjwa huyo kwa mganga wa kienyeji na wapiga ramli,bali wapelekeni hospitalini wakapatiwe matibabu ya kitaalam zaidi.

 

Alisema serikali kupitia hospitali zake kuna wataalamu wa kutosha kwa ajili ya magonjwa ya afya ya akili,hivyo hakuna sababu ya kuwapeleka watu wanaongudulika kuwa na tatizo hilo.

Awali akizungumza na wakazi hao wa kijiji hicho pia amewashauri wakulima kuhakikisha wanaandaa mashamba yao mapema ikiwemo na kuweka mbolea kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mbegu kwa wakati.

 

Naye Mchungaji Saiman Sandiya ambaye kiongozi wa kanisa hilo la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania PHAM (T) Usharika wa Yerusalemu Chalinze Nyama Chamwino.

 

Kwa upande wake amewataka wazazi na walezi ambao wana wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi kuwaendeleza kielimu zaidi badala ya kuwaweka majumbani.

 

Sandiya ambaye ametimiza miaka 40 ya uchungaji kwa kumtumikia Mungu,alisema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuwaendeleza kielimu ikiwemo na kwenye vyuo vya ufundi na kwa kufanya hivyo watakuwa wamewawekezea taaluma.

 

Alisema kuwa watoto hao wakianchwa bila kuendelezwa taifa litakuwa na tabaka la vijana wanaoweza kujikuta wakijiingiza kwenye makundi maovu kama vile panya road na mengineyo.

Mwisho.


 

 

WADAU WA MAENDELEO WAHIMIZWA KUCHANGIA VIFAA VYA MISAADA YA KIBINADAMU WAKATI WA MAAFA.

 

Na Mwandishi wetu- Kilimanjaro

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewahimiza wadau wa maendeleo na watu binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuchangia vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa.

Mhe. Ummy aliyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa Kanda ya Kaskazini  lililopo maeneo ya Chekereni, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.

Alisema uungwaji mkono wa serikali kutoka kwa wadau unasadia wananchi kufikiwa na huduma kwa haraka kutokana na majanga yaliyojitokeza ambayo husabababisha madhara kama vifo, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika pamoja na miundombinu.

“Nitoe wito kwa wadau na watu mbalimbali ambao wanaguswa kushirikiana na serikali kwa kutoa vifaa wafanye hivyo pengine ngaji ya Wilaya, Mkoa na hata kijiji ili tuwe navyo vya kutosha ili yanapotokea tunatoa msaada kwa haraka,” alihimiza Mhe. Ummy.

Pia Mhe. Ummy alisisitiza utunzwaji wa magahala hayo hatua itakayosaidia vifaa hivyo kudumu kwa muda mrefu na kuwa tayari kutumika pindi vinapohitajika katika maeneo yenye maafa.

Aidha aliupongeza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa utayari wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa wananchi wanaokumbwa na maafa kwa lengo la kuwasaidia kurejea katika hali yao ya awali.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni Afisa Mifugo katika Mkoa huo  Bwa. James Shao alisema ghala la Kanda ya Kasikazini linahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.

 


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati alipotembellea na kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya msaada  wa kibinadamu wakati wa maafa lililopo mkoani Kilimanjaro.

 

Afisa Ugavi Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro Bwa. Claude Kilala akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Ummy Nderiananga alipotembelea ghala hilo.    
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (aliyeinama) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu (kulia)

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akikagua ghala la kuhifadhi vifaa vya msaada wakati wa maafa lililopo mkoani Kilimanjaro.
      

 
 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkoa huo.
   

SERIKALI YAOMBA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

 

NA MWANDISHI WETU

Serikali imetoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea  kuhimiza jamii kuepuka uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya na kujenga uelewa kuhusu madhara ya madawa ya kulevya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Mjini Dodoma.

 “Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za kulevya, itaendelea kushirikiana na Wizara nyingine katika kuona namna nzuri ya kuandaa maudhui ya mtandaoni ili kuelimisha vijana kuhusu athari ya dawa za kulevya kama ambavyo Tume ya Kudhibiti   UKIMWI inavyofanya”.

Tupo kwenye utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imetoa maelekezo mahususi kuhusu kushughulikia dawa za kulevya, Amesema Naibu Waziri.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Dkt. Alice Karungi ameipongeza serikali kwa kiwango cha fedha kilichopelekwa kwenye Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kinachoendana na kwa kiwango cha fedha kilichokadiriwa wakati wa bajeti.

“Zoezi la kuwasaidia vijana wetu waliopata nafuu ya uraibu wa dawa za kulevya kwa kupatiwa mafunzo ya kukuza ujuzi; kama sehemu ya jitihada za Mamlaka, katika  kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, liwe endelevu”.

Naye Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Musabila amesema mamlaka imeweka msukumo mkubwa katika kukabiliana dawa zinazotoka nje ya nchi, Heroin, Cocaine na Methamphetamine.

 “Bangi imekuwa ikitumika kwa wingi kwa sababu inapatikana kwa bei nafuu na zinalimwa katika maeneo ya kujificha sana”.

Tamaa ya kupata fedha imekuwa ikichochea wananchi kulima bangi kulinganisha na mazao mengine hata hivyo udhibiti unaendelea.

“Tunashirikiana na wenzetu wa Wizara ya Klimo waweze kushauri Mwananchi badala ya kulima bangi walime zao gani ambalo litawasaidia kupata fedha nyingi.”

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Dkt. Leonard Maboko ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya kwamba fedha za Global Fund zitatoka robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/23.

 

“Mradi wa Umoja wa Mataifa wa Kuhusisha UKIMWI kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa katika bajeti 2022/23 iliyoidhinishwa ya shilingi 2,132,610,000.00, tayari kiasi cha shilingi 1,090,849,597.00 zimepokelewa. Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF) katika bajeti 2022/23 iliyoidhinishwa ya shilingi 1,880,000,000.00 fedha za ndani, tayari kiasi cha shilingi 469,992,000.00  zimepokelewa mwishoni mwa mwezi Septemba 2022 hivyo zitatumika katika robo ya pili ya mwaka (Oktoba – Desemba, 2022)”.

Naye Mhe. Asia Halamga ameomba serikali kubadili baadhi ya Sheria zinazowazuia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya iweze kufanya kazi zake kikamilifu.

“Fedha tunazotumia kutibu ni vyema tukazitumia kudhibiti ili tusiendelee kuumiza taifa na hasa vijana”.

 


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya alipokuwa akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23.

 



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Dkt. Alice Karungi akizungumza wakati wa kupokea taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23.

 



Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Mhe. Neema Mwandabila akizungumza jambo wakati wa kupokea taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23 kwa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu.

 



Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana  na Dawa za Kulevya Gerald Musabila (Kulia) katika picha wakati wa kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022/23.

 



 

 

 
 

MALALAMIKO YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI BARRICK YAPATIWA UFUMBUZI

 Na. Kadala Komba Dodoma
 
 
 
Malalamiko ya wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji Madini BARRICK ambao waliachishwa kazi Kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 2007 Serikali imebainisha hatua zilizochukuliwa katika kushughulikia malalamiko hayo.

Malalamiko hayo yalihusiana na wafanyakazi kutopimwa afya wakati wa kuachishwa kazi, kutopatiwa huduma ya matibabu na kutopewa malipo ya fidia kutokana na ajali au magonjwa waliyoyapata kutokana na kazi. 

Akizungumza na na waandishi wa habari Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana Ajira na wenye ulemavu Prof.Juma Katundu amesema kuwa Malalamiko hayo yameshughulikiwa katika hatua mbali mbali, kupitia Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Idara ya Kazi. Hata hivyo, wafanyakazi hao waliendelea kuwasilisha malalamiko katika mamlaka mbalimbali za Serikali wakidai kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa. 

"Kutokana na hali hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ilichukua hatua mbalimbali za kiutawala (administrative measures) ili kuyapatia ufumbuzi malalamiko hayo,

"Hatua hizo ni pamoja na kuunda Timu Maalum mwaka 2021 na 2022 zilizojumuisha wataalam kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa lengo kufanya uchambuzi wa kina wa malalamiko ya wafanyakazi hao na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuyahitimisha,"amesema.

Aidha amesema kuwa timu husika zimeshughulikia jumla ya walalamikaji 427, kati yao walalamikaji 150 walishughulikiwa mwaka 2021 na 277 mwaka 2022, hata hivyo, kati ya walalamikaji 277 wa mwaka 2022, walalamikaji 47 walishashughulikiwa na timu ya mwaka 2021.

"mwaka 2022, kabla ya timu kuanza kazi, mwezi Mei, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ilitoa tangazo kupitia Vyombo vya Habari kuwataka waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Barrick wenye malalamiko ambayo hayajawahi kuwasilishwa na kutolewa maamuzi na vyombo vya Serikali, kuwasilisha malalamiko yao ili yafanyiwe kazi,

Timu iliyoundwa imekamilisha uchambuzi na kuwasilisha taarifa kwangu,Katika taarifa hiyo imeainishwa kuwa wapo walalamikaji waliobainika kuwa na magonjwa yanayotokana na kazi na hivyo mwajiri atawajibika kuwapatia matibabu, wapo wenye magonjwa yatokanayo na kazi na wamefikia ukomo wa kuimarika afya zao na hivyo mwajiri atatakiwa kuwafanyia taratibu za kuwalipa fidia. Vilevile, wapo waliobainika kuwa na magonjwa yasiyotokana na kazi,"alifafanua.

Pia amesema kuwa Kwa kuzingatia matokeo hayo, walalamikaji wote waliowasilisha malalamiko yao watapatiwa majibu yao kwa barua ndani ya siku kumi za kazi baada ya kutoka tangazo hili. 

Amesema barua hizo zitatolewa kupitia Ofisi za Idara ya Kazi za Mikoa au Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama kwa kutumia anuani walizobainisha katika barua zao za malalamiko,Aidha, yeyote ambaye atapenda kupata barua kwa njia tofauti na zilizoelezwa, awasiliane na Ofisi ya Kamishina wa kazi kupitia namba ya simu 0655 544 489.

"Ninapenda kutoa taarifa kuwa nimemtaka mwajiri kuweka Dawati/Ofisi maalum kwa ajili ya kusikiliza na kutatua malalamiko na kero za wafanyakazi,

 Nimearifiwa kuwa Mwajiri ameshatekeleza agizo hilo, ambapo amefungua Ofisi maalum katika eneo la Boomgate Bulyankulu (Nje ya mgodi). Hivyo, niwatake wale wote wenye malalamiko dhidi ya Kampuni ya Barrick kufika katika Dawati/Ofisi hiyo kuwasilisha malalamiko yao ili yaweze kufanyiwa kazi,Aidha, Uongozi wa Kampuni uandae utaratibu wa namna ya kupokea malalamiko kwa kutoa namba ya simu maalum na watumishi ambao watashughulikia malalamiko,"amesema.

Pia Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya kazi, Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) zitaendelea kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi nchini kwa mujibu wa Sheria za Kazi. 

Aidha, Ninapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha Waajiri wote nchini kuwa Wakala wa Afya na Usalama Mahali Pa Kazi (OSHA) ndiyo yenye mamlaka kwa mujibu wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Na. 5 ya 2003 ya kupima afya za wafanyakazi ili kubaini endapo wana madhara yaliyosababishwa na kazi wanazofanya.

"Ninatoa rai kwa waajiri na wafanyakazi katika Sekta ya Madini kutekeleza wajibu na majukumu yenu kwa Uadilifu na kufuata misingi ya kitaaluma kwa lengo la kudumisha Mahusiano mema pahala pa kazi na hivyo kuepuka kuwepo kwa malalamiko na migogoro isiyo ya lazima ili kujenga nguvu kazi shindani na Maisha bora,"ameeleza.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana Ajira na wenye ulemavu Prof.Juma Katundu  Akizungumza na na waandishi wa habari


 

BILION 22 ZIMETENGWA KWAJILI YA UJENZI WA MITAMBO NA VIFAA VYA KISASA VYA KIMAABARA KWA MWAKA WA FEDHA 2022-2023.

Na.Kadala Komba 
Dodoma

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema majibu ya vipimo vya vinasaba (DNA) hutolewa ndani ya siku 21 huku uchunguzi hufanyika kwenye kuangalia uhalali wa wazazi na masuala ya jinai ikiwamo ubakaji na ulawiti.

Pia, katika  mwaka huu wa fedha serikali  imetenga sh.biliom 22 kwa ajili ya ujenzi na ununuzi wa mitambo na
vifaa vya kisasa vya kimabaara ili kuboresha huduma

Akizungumza 
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2021/22 na vipaumbele vya bajeti ya 2022/23, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk.Fidelice Mafumiko, alisema gharama ya kipimo hicho ambayo imedumu kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 10 ni sh.100,000 kutokana na serikali kubeba mzigo wa gharama zingine.


Alisema kwa uhalisia kipimo hicho gharama yake ni sh.700,000 hadi 800,000 kutokana na ughari wa kemikali lakini kwa muda mrefu serikali imebeba gharama hizo ili wananchi wapate huduma.


“Zile kemikali zinazosaidia kufanyika kipimo ni za ghari na kuna kemikali moja huwa tunanunua kila baada ya miezi mitatu ni Dola za Marekani 6,000 lakini ikitokea suala la janga huisha kabla ya muda huo,”alisema.


Alisema kama mtu anataka kupima vinasaba vya baba, mama na mtoto ni Sh.300,000 na wamepeleka mapendekezo serikalini iongezeke kidogo ili kusaidia kuhudumia watu bila kuathiri uendeshaji wa mitambo na gharama za kemikali.

“Sehemu kubwa ya DNA inatumika kwenye masuala ya jinai kama masuala ya ulawiti, ubakaji, au hata wizi, kwa hiyo sio kwamba DNA inatumika kuonesha wazazi halisi lakini inasaidia kwenye masuala hayo ya jinai,”alisema.
Kuhusu uchunguzi wa jinsi tata, alisema mamlaka hiyo inapofanya uchunguzi huo huwasilisha matokeo kwa madaktari bigwa walioomba ufanyike.

“Kama inatokea wasiwasi mtu anasema haelewi jinsi yake kama ni ya kike au ya kiume sisi tuna uwezo huo wa kuona hii ni ya kiume au ya kike mara moja, kwa hiyo tunafanya uchunguzi wenye weledi unaotawaliwa na kutunza siri kwa anayefanyiwa uchunguzi na kupeleka majibu kwa aliyeomba kifanyike kipimo,”alisema.

Awali, alisema katika Mwaka wa Fedha 2021/22 vibali vya uingizaji wa kemikali viliongezeka kufikia 63,588 ikilinganishwa na vibali 49,234 vilivyotolewa mwaka wa fedha 2020/21 ikiwa ni ongezeko la vibali 14,354.


“Mbali na utoaji vibali vya kemikali, Mamlaka katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2021/22 imefanikiwa kusajili wadau wanaojihusisha na shughuli za kemikali 1087 ikilinganisha na wadau 1057 waliosajiliwa kwa mwaka fedha 2020/21 ikiwa ni ongezeko la wadau 30,”alisema.


Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha huduma na sheria wa mamlaka hiyo, Daniel Ndiyo, alisema mahakama zimekuwa zikitumia ushahidi wa vinasaba na kutoa wito kwa jamii inapotokea mtu amefanyiwa ubakaji au ulawiti asikimbilie kunawa ili kurahisisha upimaji wa kipimo hicho.

“Huwa zinachukuliwa mbegu za kiume na kuletwa kwa Mkemia ili zipimwe, na kwa wengine ambao huwa wanasababisha ujauzito kwa hiyo mtoto akizaliwa huwa tunaletewa sampuli kwa ajili ya kumpima mama baba na mtoto na kama matokeo hutumika kama ushahidi,”alisema.

Alisema kipimo hicho hutumika kwenye kesi nyingi za mirathi, jinai na ndoa.
Mwisho.
 
 
 
 

 
 Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk.Fidelice Mafumiko,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.

 

FILAMU YA ROYAL TOUR IMEENDELEA KULETA MATOKEO MAKUBWA KATIKA UWANJA WA KIA

Na. Kadala Komba Dodoma.



IMEBAINISHWA kuwa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kuitangaza nchi pamoja na vivutio vilivyomo kupitia filamu maalum ya  Royal Tour matokeo chanya ya filamu hiyo yameanza kushuhudiwa katika mwaka wa fedha wa 2021/22 katika kiwanja Cha Kilimanjaro International Airport (KIA).

Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la abiria kutoka  laki 347,757 mwaka 2020/21 na kufikia abiria  laki 654,159 mwaka 2021/22 ni sawa na ongezeko la asilimia 88.

Hayo yameelezwa  Leo Oktoba 11 jijini Dodoma  na  Mtendaji Mkuu wa  kampini ya uendelezaji na uendeshaji wa kiwanja Cha ndege Cha Kilimanjaro (KIA) wakati akitoa taarifa ya utekelezaji  wa shughuli za KADCO kwa vyombo vya habari.

Amesema kuwa mafanikio mengine ni kupitia shirika jipya la ndege la Eurowings Discover(part of Lufthansa Group)iliyoanza safari zake kutoka Frankfurt,Ujerumani kwenda KIA kuanzia mwezi Juni mwaka huu,shirika hilo linachangia kuongeza idadi ya abiria na mizigo.

"Kuendelea kuwa na mashirika mbalimbali ya ndege za kukodi(charter flights)ambayo yameendelea kutumia KIA kwa kuleta makundi maalumu ya watalii kutoka sehemu mbalimbili duniani,

Kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi kuwekeza KIA katika maeneo tofauti ikiwemo hotel za kisasa,maeneo ya biashara mchanganyiko(business Complex)na jengo la wageni mashuhuri(CIP lounge facility),"Ameeleza.

Kadhalika amesema kuwa jali ya uendeshaji uliendelea kuimarika hadi mwaka wa fedha 2020/21 ambapo Dunia ilikumbwa na janga la Uviko 19 lililoathiri sekta nyingi za kiuchumi Duniani ikiwa ni pamoja na sekta ya usafiri wa anga.

Amesema katika kipindi hicho shughuli za uendeshaji KIA zilishuka kwa kiasi kikubwa kutokana na nchi nyingi kufunga anga ikiwa ni njia moja wapo ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo,hii ilipelekea idadi ya abiria kushuka kwa kiwango kikubwa kutoka laki 794,337 mwaka 2019/20 hadi kufikia abiria laki  347,757 katika kipindi Cha mwaka 2020/21 ikiwa ni punguzo la abiria kwa asilimia 56.

"Kupunguza kwa shughuli za uendeshaji KIA kuliathiri mapato,ikizingatiwa kwa chanzo kikuu Cha mapato ya KADCO ni tozo zinazotokana na abiria wanaopita KIA pamoja na kutua na kuruka kwa ndege kiwanjani,hali hii ilipelekea menejimenti ya KADCO kuchukua hatua ya kubana matumizi na kusimamisha kwa muda baadhi ya shughuli za maendeleo ili iweze kupita Katika kipindi hiki kigumu ikiwa inaendelea kujiendesha,

Hata hivyo nikiri kuwa kipindi hiki tukiendelea kutoa huduma kwa kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa wakati wa janga la Uviko-19 na kutambuliwa kama moja ya viwanja kilichofanya vizuri zaidi katika kipindi hicho kwa kuzingatia maelekezo ya kujikinga yaliyokuwa yanatolewa kupitia Wizara yetu ya Afya,"amefafanua.

Ikumbukwe kuwa Usafiri wa anga ni chachu ya kuwezesha kukua kwa sekta nyingine mtambuka ikiwemo sekta ya Utalii, mifugo,kilimo na biashara ambapo huimarisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia mnyororo wa thamani unaotokana na shughuli za uendeshaji wa KIA,mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo hupitia KIA kwa ajili ya kwenda kwenye masoko ya nje ya nchi,hii inafaida kubwa katika uchumi wa kanda ya kaskazini na Taifa kwa ujumla.

Mwisho
 
 
 

 
 Mtendaji Mkuu wa  Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) Christine Mwakatobe,akizungumza na waandishi wa habari
 
 
 

 

UBORA WA KOROSHO UMEONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 95 HADI KUFIKIA ASILIMIA 97.

Na Moreen Rojas Dodoma

Jumla ya tani 8,959.023 za korosho ghafi zilibanguliwa ndani ya nchi kati ya tani 240,158.753 zilizozalishwa sawa na 3.7% na jumla ya leseni 55 za ununuzi wa korosho kwa ajili ya kusafishia nje ya nchi zilizotolewa ikiwa ni ongezeko la kampuni 5 ukilinganisha na leseni katika msimu wa 2020/2021.

Hayo yamesemwa na Fransis Afred Mkurugenzi wa bodi ya Korosho wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dodoma lengo ni kutoa taarifa ya itekelezaji wa shughuli mbalimbali za bodi hiyo kwa mwaka 2021/2022 na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2022/2023.

Aidha ameongeza kuwa kiasi cha kilo 91,764 za mbegu bora za korosho zenye thamani ya shilingi 275,292,000 zimesambazwa katika halmashauri 87 zinazolima korosho hapa  nchini ikiwa ni mkakati mojawapo wa kufikia uzalishaji wa korosho ghafi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/2026.

Wakulima 281,200 walisajiliwa kati ya wakulima 318,407 waliotarajiwa kusajiliwa sawa na 88% jumla ya wakulima na wapuliziaji 1,304, Viongozi wa Amcos 703 pamoja na maafisa ugani 1,923 wamepatiwa mafunzo bora ya kilimo cha korosho kwa kushirikiana na Tari _Naliendele "Amesema Afred.

Pikipiki 95 zenye thamani ya shilingi 297,514,236 zilizotolewa kwa maafisa ugani ikiwa ni nyezo muhimu katika kuwafikia na kuwahudumia wakulima kwa wakati.

Pamoja na hayo jumla ya maafisa ugani 536 kutoka mikoa ya Mtwara,Lindi,Ruvuma,Pwani na Tanga waliweza kunufaika na mpango wa motisha ya shilingi 100,000 kwa mwezi juu ya utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima takribani shilingi milioni 200 zilitengwa kwa ajili hiyo.

Kiasi cha tani 30,000 kinatarajiwa kubanguliwa hapa nchini kati ya tani 400,000 zinazotarajiwa kuzalishwa,jumla ya leseni 60 zinatarajiwa kutolewa kwa msimu huu ambapo hadi sasa jumla ya kampuni 25 zimewasilisha maombi ya leseni " Amesema Afred.

Bodi ya Korosho Tanzania inaendelea na maandalizi ya usimamizi wa masoko na mauzo ya korosho ghafi ili kuhakikisha msimu wa mwaka 2022/2023 unakuwa na mafanikio kwa wadau wa Tasnia ya korosho nchini.

Bodi tayari imeanza kusajili na kutoa leseni kwa wanunuzi wa korosho ghafi kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi na kubangua nchini ambapo hadi kufukia tarehe 07 oktoba 2022,jumla ya kampuni 48 zimesajiliwa na kati yake kampuni 18 tayari zimepata leseni na zilizosalia zipo katika hatua mbalimbali za kukamilisha upatikanaji wa leseni "Amesema Afred.

 Bodi itaendelea kushirikina na wadau wote katika mnyororo wa zao la korosho kuhakikisha mkulima anazalisha na kuuza korosho zake kwa tija kwa maendeleo ya tasnia ya korosho nchini.
 
 

 

 

*”WANANCHI CHANGAMKIENI MBOLEA YA RUZUKU” RC DODOMA*

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati ametembelea kiwanda cha mbolea cha Intracom Tanzania 
, kiwanda kinachozalisha mbolea kilichopo eneo la Nala Jijini Dodoma.

Mhe. Senyamule ametembelea kiwanda hicho akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na baadhi ya wataalam wa idara mbalimbali.

Mhe. Senyamule ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa ya zoezi la usajili kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku kwani zoezi bado linaendelea
“Wananchi endeleeni na usajili kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku kutoka Serikalini kwani Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa kwenye kilimo hasa kupitia kiwanda hiki, tutapata mbolea ya kutosha kwa kilimo bora” .

Akizungumzia uwekezaji wa viwanda katika Mkoa wa Dodoma, RC Senyamule amesema;
“Nawapongeza sana Kiwanda cha Intracom kwa kuwa wa kwanza kuwekeza katika eneo hili la Nala kwani hili ni eneo limetengwa maalumu kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na nyinyi hamukuhofia kuwa wa kwanza kuwekeza hapa licha ya changamoto kadhaa, mumeona muwe njia kwa wengine. Natoa wito kwa wawekezaji wengine wote waliochukua maeneo hapa eneo la Viwanda Nala kuja kuwekeza kwani tunatamani tuanze kuiona dhamira hasa ya eneo hili na Serikali ya Mkoa imejipanga kuhakikisha wawekezaji wanakaa katika mazingira mazuri hapa Dodoma kwani Dodoma ni Fahari ya Watanzania”. Amesisitiza Senyamule.

Kadhalika, Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bw. Nduwimana Wazaire, akielezea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda mpaka sasa, amesema kuwa ujenzi unafanyika kwa awamu na kwa sasa tayari awamu ya kwanza imekamilika yenye uwezo wa kuzalisha mbolea tani laki mbili na wanatarajia kuanza ujenzi wa awamu ya pili mwishoni mwa Oktoba . Ujenzi kamili wa awamu ya tatu ambayo ndiyo itakua ya mwisho unatarajiwa kukamilika mwaka 2023.

Kiwanda cha Intracom Tanzania Ltd. kilianza ujenzi wake mapema mwaka jana na kinatarajiwa kuzalisha mbolea kiasi cha tani laki sita kwa mwaka. Kiwanda hiki  kinazalisha aina tatu za mbolea ambazo ni mbolea ya kuoteshea mazao (Fomi otesha), mbolea ya kukuzia (Fomi kuzia) pamoja na mbolea ya kunenepesha mazao (Fomi nenepesha). 

Aina zote hizi tatu zinapotumiwa na mkulima zitasaidia kupata matokeo chanya kwenye kilimo na mbolea inayozalishwa na kiwanda hiki ni (Organo-minerals) yaani mchanganyiko wa samadi na madawa.

MWISHO
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati ametembelea kiwanda cha mbolea cha Intracom Tanzania

 

 kiwanda kinachozalisha mbolea kilichopo eneo la Nala Jijini Dodoma

 

VIJANA WAKATAA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO 19 KWA KUHOFIA KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME.

Na Moreen Rojas Dodoma



Vijana wengi wameingiwa na hofu ya kukataa kuchanjwa chanjo ya uviko 19 kwa kuhisi watapunguza nguvu za kiume pamoja na kuhisi watajiingiza katika imani za kishirikina.


Hayo yamesemwa na Bi.Flora Kimaro mratibu msaidizi wa chanjo jiji la Dodoma wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya nala jijini Dodoma.

Aidha ameongeza kuwa vituo vya afya zaidi ya 65 vinaendelea kutoa chanjo ya uviko 19 katika jiji la Dodoma ambapo kiuhalisia watu wazima ndio wanaochanja zaidi,waliowengi wanaochanja ni wazee na sio vijana "Amesema Bi Kimaro.

Mikakati ambayo Serikali inayo ni kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari na sasahivi ni kupita nyumba hadi nyumba kuendelea kuelimisha jamii kuhusu uviko 19  " Amesema Bi Kimaro.

Kwa makundi hatarishi jiji la Dodoma wameyafikia kwa kiasi kikubwa sana kwa wanaoishi na HIV,TIB na Kisukari ambayo kinga zao zinashuka kwa hiyo wameendelea kuyafuatilia ikiwemo wazee ambao kinga yao ya mwili imeshuka "Amesema Bi Kimaro.

Ameongeza kuwa endapo tutafikia asilimia 80% kama nchi zingine zilizofanikiwa hakutakuwa na umuhimu wa kuzingatia uviko 19 ikiwemo suala zima la kuvaa barakoa kwani tutakuwa tumejikinga kwa eneo kubwa " Amesema Bi Kimaro.

Kwa upande wake shuhuda wa kwanza wa  chanjo ya uviko 19 Jane Shemndolwa ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata kutoka halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kata ya Chitemo amesema kuwa alikuwa haamini kwenye kuchanja kutokana na maneno kwamba ukichanja unageuka kuwa zombi,kama kiongozi kwenye jamii ameamua kuchanja ili kuwa mfano kwa jamii yake ili waweze kuhamasika kuchanja na binafsi hajawahi kupata madhara yoyote "Amesema Shemndolwa.

Shuhuda wa pili wa chanjo ya uviko 19 Jovery Tairo ambaye ni mwakilishi wa mchungaji kutoka kanisa la M.R.B Prophetic Ministry amesema kuwa kwake ilikuwa ngumu kama kijana mwenye imaani kupata chanjo ya uviko 19 kwani walikuwa wakiambiwa kuwa ni mpango wa kishetani wa kupunguza watu lakini baada ya kuhudhuria semina amepata elimu ya chanjo na ameona mambo hayo hayahusiani na chanjo nakuwashauri vijana kujitokeza  waweze kupata chanjo " Amesema Tairo.

Naye Mwenyekiti wa mafunzo Shekhe.Musa Kalasa amesema alichanja kwa utata sana kwa sababu alikuwa anafikiri ukichanja damu inaganda,lakini alipopata elimu akaona hizi ni fikra tu fikra kama hizi zipo lakini yeye amekuwa balozi kwa waumini wake wanaume kwa wanawake, ikiwa Rais Samia ameweza kuchanja na damu haijaganda mimi ni nani nisichanje? "Amesema shekhe Kalasa.

Wanachi wameendelea kuhamasishwa kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa uviko 19 ikiwemo kuchanja chanjo zote ili kupunguza kasi ya ugonjwa huo.
 
 
 
 

Bi.Flora Kimaro mratibu msaidizi wa chanjo jiji la Dodoma wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya na waandishi wa habari
       

 
 
Waandishi wa habari wakipatiwa mafunzo namna ya kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha Jamii juu ya kujikinga na Uviko 19



 
 
 

 

WATOTO YATIMA WAIOMBA BAKWATA KUWAWEKEA UZIO

 

Na Peter Mkwavila KONDOA

WATOTO wa Kituo cha yatima kinachomilikiwa na taasisi ya All Hafidhu Islamic Orphans Centre kilichopo Bicha wilaya ya Kondoa.

Wameliomba Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuwajengea uzio utakao wawezesha kudhibiti uharibufu wa vibaka ikiwemo na ulinzi wa mipaka ya kituo hicho  na jamii inayowazunguka.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Ukht Aisha Nobe,kwa niaba yao watoto mbele ya Shekhe wa mkoa wa Dodoma (BAKWATA) Mustaph Rajabu wakati alipokuwa akifunga kongamano la wanawake wakiislamu la siku 3 lililofanyika kituoni hapo.

Aisha,alisema kituo hicho kwa muda mrefu toka kujengwa hakina uzio ambao unaoweza kudhibiti vibaka na hata mipaka ya maeneo yanayozunguka.

“Mbali na kituo hicho kuwa na wanafunzi wa shule ya msingi,pia tunawatunza watoto wenye mahitaji maalumu,ila hakuna uzio ambao unaoweza kulinda mipaka na usalama wa mali na wao wenyewe”alisema.

Akizungumza kwenye kongamano hilo lililowashirikisha wanawake kutoka dini ya kiislamu  kwa ajili mafunzo,pia maada mbalimbali zilitolewa ikiwemo ya elimu kwa wanawake,malezi kwa watoto ndoa,ibada na ndoa ya mitaala.

Kwa upande wao washiriki ambao ni wanawake wametakiwa kuwa mabalozi wa elimu waliyoipata kwa wengine ili dini hiyo iweze kuondokana na changamoto zinazowakabiri.

Naye Shekhe wa Mkoa wa Dodoma wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mustapha Rajabu,alisema Kituo hicho kinatakiwa kuwa kwenye usalama zaidi ukizingatia kuna watoto wadogo wanaohitaji usalama mkubwa.

Alisema kutokana na umuhimu huo Bakwata kwa kushirikiana na taasisi zingine na wadau wa elimu watahakikisha wanasaidia kuondoa kero hiyo ya kukosa uzio ambao umesababisha kuwepo kwa mwingiliano.

“Nimesikia kilio chenu sisi kama Bakwata tutahakikisha tunashirikiana na wadau wengine tunatatua kero hii ili watoto wetu wasome kwenye hali ya usalama na hata mali zao ziwe salama pia na hata kwenye mipaka nayo ijulikane pia”alisema.

MWISHO.

 

 


 


BODI YA FILAMU TANZANIA IMEUNDA KAMATI MAALUM YA KURUDISHA UTAMADUNI WA KUTAZAMA FILAMU KATIKA KUMBI ZA SINEMA

Na Moreen Rojas Dodoma


 

Hatua hiyo inatarajiwa pia kutoa mchango stahiki katika uchumi wa wadau wa Sekta na Taifa kupitia viingilio vya mlangoni. 

Kwa upande wa usambazaji Serikali ina makubaliano ya kimataifa Televisheni Mtando ya Nuella (Nuella Online TV) ya nchini Uholanzi kununua na kuonesha Filamu za Kitanzania, na hadi sasa kuna filamu tisa (9) zinaonyeshwa huko.

Hayo yamesemwa  na Dkt.Kiagho Kilonzo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika kuelekeza utekelezaji wa mwaka wa fedha 2022/2023.

Aidha ameongeza kuwa Dira ya Bodi ya Filamu ni: Kuwa na Tasnia ya Filamu Shindani kwa Maendeleo ya Taifa na kupunguza umasikini (Vibrant and competitive Film industry for national development and poverty alleviation). 

Dhima ya Bodi ya Filamu ni: Kuweka mazingira bora na wezeshi kwa ukuaji wa Tasnia ya Filamu. (To create conducive and enabling environment for film industry prosperity).

Malengo ya bodi ya filamu ni kukuza Tasnia ya Filamu kwa:
- kuweka miongozo ya uundwaji wa Sera na Sheria za kuisimamia Sekta ya Filamu nchini,
- Kuongeza uzalishaji wa filamu za kitanzania na za kimataifa nchini Tanzania
- Kuimarisha uwekezaji katika Sekta ya Filamu
Kuendeleza uhifadhi wa kazi za filamu nchini.

Majukumu ya bodi ya filamu.
Kuishauri Serikali masuala yote yanayohusu Filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na kuratibu Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza;
Kusimamia na kuratibu utayarishaji/uandaaji, uhakiki wa Filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na kuzipangia madaraja na kuzipa vibali; na
Kuandaa, kuratibu na kuendesha warsha, vikao, mijadala na mafunzo ya kujenga weledi kwa wadau wa filamu, utoaji wa tuzo na uendeshaji wa matamasha mbalimbali.


Fursa za Ajira
Kwa kipindi cha Januari hadi Disemba, 2021 pekee inakadiriwa kuwa ilichangia takriban ajira 30,000 zilizotokana na Filamu (waigizaji, waandaaji na watoa huduma). Kwa mazingira ya Kitanzania, Filamu moja (wastani wa watu 20, tamthilya moja wastani wa watu 100). 
Kiasi hicho ni ongezeko la nafasi 5,000 kutoka 25,000 kiasi kinachokadiriwa kuzalishwa mwaka 2020. 
 

Mfumo wa Kutoa Huduma za Bodi KIDIJITALI.
Taasisi imeanzisha mfumo ambao unatoa huduma karibia zote za Bodi kwa wadau wake (bila kulazimika kufika katika ofisi za Bodi) ikiwemo:
- vibali mbalimbali (uandaaji wa filamu, uhakiki, vitambulisho, nk)
- kuhifadhi taarifa za wadau,
- kuwatambua kupitia vitambulisho vinavyotolewa na Bodi.


Filamu za Kimkakati
Program hii ina lengo la kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia (maeneo mahsusi) ya nchi kwa lengo la kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali waliyonayo. Programu hii itasaidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa kuhusisha taarifa za viongozi wetu mbalimbali waliofanya mambo makubwa kama vile Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye alisaidia ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika.

Dkt.Kiagho wakati akujibu maswali ya waandishi wa habari amesema kuwa kama bodi wamejipanga kuhakikisha wanatoa maudhui mazuri kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuwapa semina wasanii chipukizi namna gani ya kujiuza kimataifa ili kuweza kukua kibiashara kuendana na kasi ya ulimwengu ikiwa ni pamoja na kulinda tamaduni zetu kama taifa kwa kuwa na vijana wanaojielewa.


Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ameipongeza bodi ya filamu Tanzania kwa kazi nzuri wanayoifanya ambayo imepelekea Tanzania kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji wa filamu Afrika na kuwaomba wawekezaji wa ndani na nje kuungana na sekta hiyo ili kuweza kufika mbali zaidi kwani tayari filamu zetu zimeshashinda tuzo mbalimbali nje ya nchi hii ni kuonyesha ni kwa namna gani sekta ya filamu nchini inazidi kwenda kimataifa.