Na Mwandishi Wetu,Mtwara.
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC)limetoa elimu kwa wananchi kuhusu namna Shirika linavyotekeleza Majukumu yake kwa Mujibu wa Sheria.
Elimu hiyo imetolewa katika maonesho ya Bishara, Uwekezaji na Fursa yanayofanyika katika viwanja vya Mashujaa kuanzia tarehe 19 hadi 31 Machi, 2023 Mkoani Mtwara.
Akizungumza na Vyombo ya habari Kaimu Afisa Mfawidhi wa Mkoa wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Mkoa wa Mtwara, Mha. Jospeh Myaka amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao Shirika hilo limejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shirika hilo linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo pia TASAC imeshiriki maonesho hayo ili kuwapa elimu wananchi kuhusu fursa za biashara zilizopo katika Sekta ya Usafiri kwa njia ya Maji sambamba na elimu kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira majini jukumu linalotekelezwa na Shirika hilo.
“TASAC tunashiriki maonesho haya ya Biashara Uwekezaji na Fursa mkoani Mtwara ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yanayotekezwa Kisheria. kama mdhibiti wa shughuli za usafiri kwa njia ya maji tunasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, tunadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba majini”
“Pia tunatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na wadau wa usafiri kwa njia ya maji katika jukumu letu la Udhibiti wa Safari kwa njia ya Maji na udhibiti Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira majini, wanaweza kufanya shughuli zao kwa usalama na kupata maendeleo na kuongeza pato la Taifa.” Ameeleza Myaka.
Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.
Maonesho hayo ya Biashara, Uwekezaji na Fursa ni maonesho ya Kwanza kufanyika Mkoani Mtwara yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza biashara na uwekezaji wa kisasa pamoja na fursa zilizopo katika sekta hiyo na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla.
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
TASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI MTWARA.
NAIBU WAZIRI NISHATI AMEWATAKA TANESCO KUWA NA KITENGO CHA MASUALA YA JINSIA.
Na Masala Komba Dodoma
Naibu waziri wizara ya nishati Steven Byabato ameagiza shirika la umeme Tanzania kuwa na kitengo cha masuala ya jinsia (dawati la jinsia).
Mhe.Byabato ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habati pamoja na wadau mbalimbali ambapo amezindua programu ya usawa kazini katika ukumbi wa morena jijini Dodoma.
Aidha amesema ni wajibu wa shirika kuweka mazingira rafiki na kuboresha mazingira kwa vijana wa like na wanawake ili kuweza kuwarahisishia kufanya kazi kwa urahisi bila kupata changamoto yoyote pindi wanapokuwa kazini.
Aidha amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo chama kitahakikisha kinaisimamia serikali katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
"Ili kufikia hadma hii chama kitaelekeza serikali kuhakikisha sekta zote zinazingatia masuala ya jinsia katika shughuli zao pamoja na kuimarisha madawati ya kijinsia ili kuzuia ukatili wa kijinsia,kubuni,kuendeleza na kutekeleza mikakati ya ushiriki wa wanawake katika kufanya maamuzi ya kiuchumi hadi kufikia 50/50" Amesisitiza Naibu waziri Byabato.
Aidha amesema kifungu cha 230 cha ilani ya chama cha mapinduzi(CCM) ya 2020_2025 inasema chama kinatambua kuwa na usawa wa kijinsia kama sehemu ya utekelezaji wa ilani yake kwa binadamu wote sawa na wanastahili heshima na fursa sawa.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2015_2020 miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuweka na kuimarisha mifumo ya haki za wanawake kwa kuanzisha madawati ya jinsia na watoto 420 katika vituo vya polisi pamoja na kuanzisha madawati hayo vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu madawati ya jinsia 162 yameanzishwa katika jeshi la magereza.
"Kumekuwa na juhudi za kupambana na vitendo vya rushwa ya ngono kupitia kampeni ya VUNJA UKIMYA iliyoratibiwa na taasisi ya kupambana na rushwa takukuru" Amesema Naibu waziri Byabato.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji Tanesco Ndg.Maharage chande amesema suala ya usawa wa kijinsia liko juu sana ambapo kipaumbele chao kama taasisi ni kuhakikisha wanawake wanaongezeka kwa kasi katika shirika lao.
Aidha amesema maeneo ya kimkakati yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kuiboresha sera ya shirika na kujenga uwezo ili sera iende sambamba na masuala ya kijinsia,kuwepo na taarifa sahihi zinazohusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye taasisi,kuruhusu fursa ya ukuzaji wa taaluma kwa wafanyakazi wanawake hasa wanaofanya kazi kwenye miradi pamoja na kuwepo kwa nafasi ya mafunzo kwa vitendo(intership)kwa wafanyakazi wanawake waliopo kazini ili kuwajengea uwezo kuelekea kwenye ajira kamili.
Naye Balozi Mwanaidi Sinare Maajar ambaye ni makamu mwenyekiti wa bodi amesema kuwa ni kweli kwamba masuala ya haki za jinsia inawahusu wanaume na wanawake yako katika nyanja mbalimbali ya serikali yetu.
Sanjari na hayo amesema kuwa hatutafikia maendeleo kama hatutazingatia wanawake has wa kwa kuzingatia sensa ya watu na makazi ambayo inaonyesha idadi kubwa ya wanawake ili kuleta usawa kazini.
Ameongeza kuwa ni wajibu wa kula mtu kuhakikisha kuwa hakuna vitendo vya kumdhoofisha mwanamke akashindwa kufanya kazi yake na pia kuhakikisha mifumo yote ni rafiki kwa wanawake ili kuwapa morali na wengine kuwa sekta ya nishati wanawake nao wanaweza na sio sekta ya nishati pekee bali nyanja zote.
Programu ya usawa kazini (Gender work program) kwa miaka minne 2023_2026 ni mradi uliofadhiliwa na benki ya Tanzania kupitia mkopo wa dunia wa gharama nafuu.
MCHUNGAJI DANIEL MGOGO HIZI NDOA HAZIWEZI KUDUMU
Mchungaji na Mhubiri maarufu kutoka Tanzania Pastor Daniel Mgogo ametaja aina ya ndoa ambazo kwa mujibu wa mafundisho yake ndoa hizo haziwezi kudumu hata iweje.
Kwa mujibu wa Mchungaji Mgogo amesema ndoa lazima zibarikiwe na kiongozi wa kidini la sivyo ndoa hizo zitasambaratika tu. Mchungaji huyo alisema kuwa baadhi ya watu tayari wameoana bila ndoa zao kubarikiwa na sasa wanakimbilia kanisani kuwahadaa viongozi wa kidini ili kupata vyeti vya ndoa. "Msingi wa ndoa yako ni nini kama si uzinzi na uasherati? Na wakati mwingine mnatudanganya wachungaji, mnakuja mnasema tunataka kufunga ndoa. Kumbe mnataka kupata uhalali wa wizi wenu," Mgogo alisema.
Mhubiri huyo amewashauri vijana na wanandoa kuwa na subira na kufuata taratibu zote zinazohitajika kabla ya kufunga ndoa.
Pastor Mgogo aliwaasa wanandoa ambayo hawajaona kihalali kanisani kuweka wazi mahusiano yao kwa viongozi wa kidini na wakubali kuongozwa sala ya toba.
"Mchungaji awaongoze kwa sala ya toba. Awarudishe kundini abariki ndoa yenu, mfunge ndio mwende kwa mbwembwe. Mnakomaa na dhambi,Hamna hata aibu," Pasta Mgogo alishauri.
KAGERA NI SHWARI HAKUNA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA MARBURG
Na. WAF - Ziara Mkoani Kagera, Bukoba
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea katika Kijiji cha Ntoma Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera kwa lengo la kujionea hali inavyoendelea baada ya kutangazwa kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Mkoani humo.
Katika Ziara hiyo, Waziri Ummy ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Zabron Yoti pamoja na Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Bi. Shalini Bahuguna.
Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa hali ni salama na kuwataka Wananchi wa kijiji hicho na watanzania kwa ujumla kuondoa hofu kwa kuwa Serikali inawajali Wananchi wake.
“Niwatoe hofu Watanzania tuendelee kufanya kazi zetu lakini tuzingatie maelekezo ya Serikali ya kujikinga na ugonjwa huu kwa kuepuka kushikana mikono hususan kipindi hiki lakini pia tujitahidi kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.” amesema Waziri Ummy
Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na juhudi za kuhakikisha ugonjwa huo unamalizika na hautatokea tena katika maeneo hayo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kanyangele Bw. Hamim Hassan ameishukuru Serikali kwa kufanya juhudi kubwa ambapo hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeongezeka kwa kuthibitika kuwa na ugonjwa huo.
“Hatua za Serikali kupitia Wizara ya Afya zilizochukuliwa za kuwaweka sehemu maalumu waliokuwa karibu na wagonjwa imesaidia sana kutoendeleza maambukizi kwingine na hali ni shwari kwa sasa.” amesema Bw. Hassan
*KINANA AWATAKA WAISLAM KUZINGATIA MAADILI MEMA.*
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amewataka Waislamu kuzingatia mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) hususan kuhusu uchamungu na tabia njema.
Kinana ameyasema hayo leo Machi 25, 2023 wakati wa hafla ya mashindano ya Kuraani tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Faraja Foundation ya jijini Dar es Salaam.
""Tunaagizwa na Kuraani, pia tunaagizwa na Mtume wetu (Muhammad - S A.W) kuwa kila Mwislamu anapaswa kuzingatia mambo mawili lakwanza 'takwa' (uchamungu) na lapili 'akhlaki' tabia njema).
"Kwahiyo ukizingatia 'takwa' ukazingatia na maadili mema hakuna namna utapotoka, itakuwa hakuna haja hata ya sisi kuwa na wasiwasi kwamba maadili mabaya yanaweza yakatupitia," amesema Kinana.
Aidha, aliwahamasisha Waislamu nchini kuwapeleka watoto wao madrasa wakajifunze imani na maadili ya dini yao na kumjua Mwenyezi Mungu.
===
TANZANIA YAKABIDHI MISAADA YA KIBINADAMU KWA SERIKALI YA MALAWI
NA mwandishi wetu
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Mhe. Humphrey Polepole ameshiriki katIka zoezi la kukabidhi misaada ya Kibinadamu kutoka Tanzania kwa Serikali ya Malawi ili kusaidia wahanga wa Kimbunga Freddy.
Balozi amekabidhi misaada hiyo ya kibinadamu inayojumuisha Mablanket, Mahema, Unga wa Mahindi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Mhe. Nancy Tembo katika Mji wa Blantrey Nchini Malawi mapema leo 25/03/2023.
Balozi Polepole alibainisha kuwa wa watanzania, na watu wa Malawi ni jamii moja, na Nia ni kuendekeza umoja uliojengwa na waasisi wa Nchi zetu.
" Msaada huu wa kibinadamu utasaidia, katika jitihada za kurejesha matumaini na ustawi kwa ndugu zetu Wananchi wa Malawi", Alisisitiza Balozi Polepole.
Aliongeza kusema kuwa ana imani na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania walioenda Nchini Malawi watashirikiana na wenzao Wanajeshi wa Malawi, kuhakikisha kwamba misaada iliyotolewa inawafikia Wahanga wa Kimbunga Freddy.
Aidha, Tanzania imetoa madawa ya binadamu, ambayo yataweza kusaidia kwenye maeneo ambayo vituo vya afya vimeathirika. Hizi zote ni jitihada za kusaidia Nchi ya Malawi katika kurejesha huduma za afya.
"Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Msaada aliotoa kwa Nchi ya Malawi, kwa uwezeshaji wa fedha na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Wahandisi wa Medani) ambao watasaidia katika kurejesha hali ya miundo mbinu Nchini Malawi," alisema Balozi.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje wa Nchi ya Malawi Mhe. Nancy Tembo amesema ameshukuru Nchi ya Tanzania kwa Msaada wa kibinadamu iliowapatia, ambao umefika katika wakati muafaka.
“Msaada huu ni muhimu kwetu kwa sababu tunao Wanachi wengi ambao makazi yao yameharibika, na tunahitaji msaada wa kila mtu ili kuhakikisha wahanga wa Kimbunga Freddy wanapatiwa huduma za msingi kwa wakati,” alisema Waziri Nancy
Aliongeza kusema Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamekuja kutusaidia na wataungana na askari wetu wa Nchini Malawi katika kurudisha miundo mbinu iliyoharibika katika hali ya kawaida.
“Nachukua fursa hii kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutusaidia katika wakati ambao tunahitaji msaada sana, janga hili ambalo limeathiri Nchi ya Malawi, limegharimu maisha ya watu, na limeharibu miundo mbinu” alisema Waziri Nancy.
Naye Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulika na Operesheni pamoja na Uratibu wa shughuli za Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu Luteni Kanali Selestine Masalamado ametoa pole kwa wananchi wa Malawi kwa Maafa ya Kimbunga Freddy.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maafa kuratibu swala la misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Wahanga wa Kimbunga Freddy Nchini Malawi, ambapo kwa awamu ya kwanza helikopta mbili kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania zilisafiri kuja Malawi kufanya kazi za wokozi, lakini msaada wa pili ilikuwa ni msaada wa fedha kwa serikali ya Malawi na tatu ni kutoa msaada wa kibinadamu
kwa Wahanga wa Kimbunga Freddy.
*TANZANIA NA UNESCO KUDUMISHA MASHIRIKIANO SEKTA YA MAJI*
UNESCO- NEW YORK
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amekutana na Naibu Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO Bwana Xing Qu ofisi za UNESCO New York kwa lengo la kujadiliana juu ya mahusiano na mashairikiano katika usimamizi wa uendelezani wa Rasilimali za Maji na ushirikiano katika usimamizi wa Maji Shirikishi.
Waziri Aweso amewasilisha ombi la Tanzania kujengewa uwezo na UNESCO katika usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji na utekelezaji wa miradi ya Maji, uandaaji wa maandiko ya Miradi na utafutaji wa fedha.
MCHUNGAJI WAKRISTO TUMEZIDIWA MAARIFA NA WACHAWI
Na. Kadala Komba Bahi
Daniel David Kikunile Mchungaji Kiongozi Mchungaji Daniel Kikunile wa Kanisa la Ufunuo na Uzima lililopo karibu na shule ya Msingi Bahi Misheni Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Amesema Sisi wakristo ni wazembe tunazidiwa maarifa na wachawi, Mfano Mchungaji,Mwinjilisti Ametumika kikamilifu katika huduma au karama aliyupowe na Mungu kwa Kazi aliyotumwa hapa Dunia tatizo linakuja pale Kazi yake ikiisha anakufa bila kuacha Mrithi wa huduma au karama aliyonayo.
hayo alipokuwa Akihubiri kanisani hapo Jumapili wakati Akifundisha Somo la Fimbo ya Enzi ya Kitaifa ya Kichawi Sambamba na kuhitimisha Mfungo wa siku Saba wa kuombea Wilaya ya Bahi na vijiji vyake. UFUNUO 12:5
Mchungaji Kikunile Alisema njia pekee ya kufurahia wokovu na karama tulizopewa na Mungu ni kuwarithisha watu wetu wa karibu kile ulichopewa na Mungu amekupa bure na wewe toa bure, Maono ya Viongozi wengi wa Dini wamebeba Maono mengi juu ya huduma namna ya kufanya Kazi ya Mungu tatizo linakuja wanapotwaliwa basi na Maono yamekufa hakuna mtu wa kuyaendeleza wanaobaki wanashindwa sababu ahakufundishwa, kama ni huduma inayumba nyingine zinakufa kabisa na kusaulika kama kulikuwa na huduma ya namuna hiyo.
"Tofauti na Wachawi mchawi kabla ajafa anatafuta mtu wa kumrithi Kazi aliyokuwa anafanya ya kuloga watu, kama ni Mganga anatafuta mtu wa kumwachia tunguli, Mikoba yake na irizi zake Ili kile alichokuwa anakufa ya yeye kuendelee kufanyika hata kama yeye hayupo Tena katika Dunia Kazi aliyokuwa nayo ya kuharibu maisha ya watu inaendelea kufanywa na warithi wake Tena na kuzidi Alisema .
Aidha Mchungaji Kikunile Alisema Wakristo Mungu ametupa Neema Kubwa katika huduma zetu,tunacho chakula cha kutosha kulisha kondoo zetu sababu sisi ni Wachungaji ni haki yetu kulisha kondoo waliopo kwenye Zizi letu hata tukitwaliwa na Bwana leo tunakuwa hatuna mashaka kwa kile tulichokianzisha kinaendelea,Mavuno hayatakauka Shambani mwa Bwana maana Watendakazi wanafanya Kazi ile ile kama miujiza inaendelea kutendeka uponyaji unaendelea kama Yesu Kristo alivyofanya kwa Wanafunzi wake Aliwafundisha hata Yesu alipowaacha Wanafunzi waliendeleza Kazi ile ile aliyokuwa Anafanya Yesu.
" Viongozi wezangu Ambao tumepewa Neema ya kuchunga Kondoo nawakumbusha tuache Urithi kwajili ya Ukombozi wa Kizazi hiki na kijacho kama sisi tulivyo rithishwa kutoka kwa Adamu na Musa kwa jili ya Utukufu wa Bwana na Kazi yake Alisema .
a Yesu kupata wokovu Ili uende Mbinguni Alisema .
Picha Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Akifundisha Somo la Fimbo ya Enzi ya Kitaifa ya Kichawi.
Washarika wa Kanisa hilo wakipiga makofi wakionekana kupendezwa na Somo hilo
MEJA JENERALI MBUGE “MIKOA IANZISHE TIMU YA WATAALAM YA KUKABILIANA NA MAAFA”
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge amewataka Wataalam kuanzisha Timu Mtambuka ya Wataalam ya Kukabiliana wa Maafa kila Mkoa ambayo itarahisisha mawasiliano ndani ya Mkoa wakati wa kukabiliana na dhahrura.
Meja Jenerali Mbuge ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha Kuweka Mkakati wa Kuanzisha Timu ya Wataalam ya Kukabilianana Maafa Mkoa wa Dodoma (Dodoma Mult Agency Emergency Response Team – DoMAERT) kilichofanyika Jijini Dodoma.
Amesema uwepo wa timu hiyo pia itasaidia kuunganisha nguvu kwa wadau waliopo ndani ya Mkoa na kuweza kutumia rasilimali zilizopo kuhakikisha maafa yanakabiliwa na wananchi kuwa katika mazingira salama.
“Nchi yetu imekuwa ikipata maafa mara kwa mara ambayo uratibu wake unahitaji kila Mkoa kuwa na Timu Mtambuka ya Wataalam ya Kukabiliana wa Maafa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi ya Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 na kanuni zake hivyo uundwaji wa timu hizo ni muhimu kwa usalama wa wananchi na mali zao,” Amesema Meja Jenerali Mbuge.
Pia Mkurugenzi huyo amewasisitiza washiriki kupitia kikao kazi hicho kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anafahamu jukumu lake na kulitekeleza kikamilifu pamoja na tayari kwa ajili ya kukabiliana na maafa ndani ya Mkoa.
Katika hatua nyingine ameeleza Meja Jenerali Mbuge kwamba Idara ya Menejimeti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa kuhakikisha usimamizi na uratibu wa maafa na huduma za dharura zinatolewa kwa wakati kwa kuzingatia mipango, miongozo na mikakati ya kitaifa na kisekta.
“Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Na. 6 ya mwaka 2022 inaratibu na kusimamia masuala ya maafa nchini,”Amebainisha Mkurugenzi huyo.
CHRISTINA SHUSHO AZIKWAPUA MILIONI 10 ZA NABII MKUU GEORDAVIE, AMUITA MFALME.
March 13, 2023 Staa wa muziki wa Injili nchini Christina Shusho alifika Kanisani kwa Nabii Mkuu Geordavie jijini Arusha kwa ajili ya Ibada, lakini akiwa katikati ya mazungumzo Shusho alianza kum-mwagia sifa Nabii huyo na baadae akamuomba kiasi cha pesa ili zimsaidie kwenye shughuli yake ya uzinduzi wa Album yake mpya itakayozinduliwa April 9, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City akiwa yeye Rose Muhando, Martha Mwaipaja na wanainjili wengine.
Naye Nabii Mkuu Geordavie bila kupepesa macho aliinuka upesi ambapo kabla ya kutoa dau aliloombwa alimuomba Shusho aimbe kionjo cha wimbo wa "Nipe macho nione" ili asikie umwororo wa sauti yake, na baada ya Shusho kutii maamuzi hayo papohapo alipewa milioni 10 huku akisifiwa kuwa kilichomsukuma zaidi nabii kukubali kukwapuliwa pesa hizo ni sauti nyororo ya mwanainjili huyo.
"Wewe ni Mfalme, wewe ni Baba na si kwamba ni kujifanya wala kujipendekeza ila mimi ni mtoto wako mimi ni binti yako ninasikia Fahari nazungumza maneno haya kwa baba na nasikia nina nguvu ninaposema kitu kwa baba, siyo kitu kingine ni kazi ileile uliyotutia moyo kuendelea ndo hiyo tunaifanya, Baba natamani unipe nguvu"- alisema Christina Shusho.