Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

DIWANI NDONU AMETOA SIKU SABA KWA WAZAZI WA WANAFUNZI AMBAO HAWAJARIPOTI SHULE

Na. Kadala Komba Dodoma Diwani Kata ya Bahi Mkoa wa Dodoma Mhe.Augustino Ndonu ametoa siku saba kwa wazazi wa wanafunzi ambao bado hawajaripoti shule hadi sasa baada ya kufaulu darasa la saba na kuchanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 kuhakikisha wanafanya hivyo na atakae kaidi agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Mhe Ndonu ametoa agizo hilo wakati akitoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi 59 kwenye kata hiyo kwa wanafunzi wanaohishi mazingira magumu, Miongoni mwa vifaa alivyotoa kwa wanafunzi hao ni pamoja na vitambaa vya kushona sare za shule ikiwa ni kaptula sketi, shati ,viatu,daftari soksi,pamoja na kalamu. “Zaidi ya Million Tatu zimetumika kununua vifaa hivi fedha ambazo zimetoka kwenye Halmashauri yetu kwenye mfuko wa Elimu kwa lengo la kuboresha mzingira ya kupata Elimu Bora leo tumegawa shule 5 zilizopo kwenye kata yetu ,hivyo naagiza kuanzia leo January 24,2023 hadi ifikapo January 30 ,2023 watoto hao wawe wamekwisha ripoti shule na kuanza masomo. Mhe Ndonu amesema baada ya siku hizo wataanza msako na kukamata wazazi wote ambao watakeuka agizo hilo na kulipa faini ya Elfu 50. Pia nakuwaeleza faida za kusomesha mtoto kwamba akifanikia mtoto faida itakua ya mzazi na familia nzima. Kwaupande wake Afisa Elimu Sekondary Bahi Mery Chakupewa amesema kupitia mfuko wa Elimu Bahi ambao umeanzishwa na Halmashauri kwa lengo la kusaidia wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu, mfuko umewezesha wanafunzi kuwa na ufaulu mzuri katika mitihani ya shule za msingi na secondary, sababu wazazi wanatambua uwepo wa mfuko huo hivyo wanaimiza watoto kuanza shule na kumaliza. Aidha Mamos Longoye Mkuu wa shule Bahi B sekondari ameishukuru serikali kwa kuanzisha mfuko huo ambao unawasaidi sana watoto wanaotoka mazingira magumu kuna wanafunzi wanashindwa kuja shule hawana sare za shule na viatu kupitia mfuko huu watoto hao wameludi shule na sasa wanaendelea na masomo. Hapines Sevelina mwanafunzi wa kidato cha kwanza secondary B mnufaika wa mfuko huo ameshukuru kwa serikali kuwasaidi na kuahidi kufanya vizuri katika masomo yake.
Diwani Kata ya Bahi Mkoa wa Dodoma Mhe.Augustino Ndonu wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wanaoishi mazingira magumu.
Diwani Kata ya Bahi Mkoa wa Dodoma Mhe.Augustino Ndonu wakati akikabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi
wazazi wa wanafunzi wanaoishi mszingira magumu

LENGO LA BIMA YA AFYA KWA WOTE NI KUCHANGIANA GHARAMA ZA MATIBABU - WAZIRI UMMY

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema lengo la Bima ya Afya kwa Wote ni kuchangiana kwa gharama za matibabu kwa wananchi wote ikiwemo wale ambao hawana uwezo ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaohangaika kutafuta huduma za matibabu wanapougua. Waziri Ummy amesema hayo leo tarehe 23 Januari 2023 wakati alipokutana na Wahariri wa Vyombo vya habari pamoja na Wakurugenzi wa taasisi mbalimbali katika kikao cha kujengewa uelewa kuhusu Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote kilichofanyika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam. Waziri Ummy amesema kuwa asilimia 15 tu ya watanzania ndio wamejiunga na kunufaika na bima afya ambapo asilimia 99 wamejiunga na bima wakati wakiwa wagonjwa kitu kinachoondoa dhana ya bima kwani mtu anatakiwa ajiunge kabla ya kuugua. “Japo muswada huu unapendekeza kila mtanzania ajiunge na bima ya afya kwa kufungamanisha na baadhi ya huduma za kijamii lakini hakuna mtu atakayekamatwa kwa kuwa hajajiunga na bima ndio maana serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya na kuweza kujiunga ili kuwa na uhakika wa matibabu kabla ya kuugua”. Ameongeza Mhe. Ummy. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii ili kujenga uelewa mpana wa umuhimu wa kila mwananchi kuwa na bima ya afya kama nyenzo itakayomsaidia kupata matibabu wakati wote bila kujali hali yake ya kipato kwa wakati huo. pamoja na kutoa elimu, Wizara imeendelea pia kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na kufanya maboresho katika maeneo hayo, kwa mfano katika eneo la ufungamanishaji baada ya kupokea maoni baadhi ya maeneo yamepungua kutoka tisa hadi kufikia matano. Akiwasilisha mada katika mkutano huo kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Benard Konga kwa niaba ya kamati inayoratibu muswada huo, ametaja baadhi ya huduma ambazo wananchi watakazonufaika nazo ikiwemo ada ya kuandikisha na kumuona daktari, gharama za vipimo, dawa na gharama za kulazwa. Huduma zingine ni gharama za dawa zote kama zilivyoainishwa katika orodha ya taifa ya dawa muhimu (NEMLIT), gharama za upasuaji mdogo, mkubwa na ule wa kitaalamu zaidi unaofanywa na madaktari bingwa, huduma ya afya kinywa na meno, huduma za matibabu ya macho, vifaa saidizi (medical/ othopaedic appliances) na huduma ya mazoezi ya viungo. Naye, Msemaji Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Gerson Msigwa amesema waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika kutoa elimu na kuwaomba kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa bima hii kwa watanzania na kuongeza kuwa bima hii inakwenda kuwa mwarobaini wa changamoto za matibabu kwa watanzania. Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Deodutus Balile amemhakikishia Mh. Waziri kuwa watatoa elimu kuhusu umuhimu wa bima hiyo, na kuomba pale watakapohitaji wataalam kutoa ufafanuzi watoe ushirikiano ili lengo la kutoa elimu liweze kufanikiwa
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari pamoja na Wakurugenzi wa taasisi mbalimbali katika kikao cha kujengewa uelewa kuhusu Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote kilichofanyika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi

SHAKA AKABIDHI RASMI OFISI KWA MJEMA

Picha zikionesha matukio mbalimbali ya makabidhiano ya ofisi baina ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg Sophia Edward Mjema na aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka Jana Tarehe 21 Januari, 2023 Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba, Dar es Salaam. #CCMImara #UongoziImara #KaziIendelee

WAZIRI MKENDA ANAYELETA UDANGANYIFU WA MITIHANI TUTAMKAMATA

Na. Kadala Komba Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Amesema mitihani imekuwa ikienda vizuri kwenye Baraza la Mitihani la Tanzania isipokuwa inapokwenda shuleni wamekuwepo watu wachache sana ambao wanajihusisha na udanganyifu na kwamba Serikali haitavumilia udanganyifu huo. “Anayeleta udanganyifu kwenye mitihani tutamkamata, walimu hakikisheni mnakataa kujiingiza katika udanganyifu huo na kuwa makini zaidi kwenye masuala ya mtihani,” amesisitiza Waziri Mkenda. Waziri Mkenda ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 17 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA) ambapo amesema kwa kufanya hivyo ni kuandaa taifa ambalo litashindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Amesema Shule zitakazofungiwa Kwa Udanganyifu Wa Mitihani Sio za Watu Binafsi Peke Yake Bali hata Zile Za Umma Endapo Tu Mtu atabainika amehusika Kufanya Jambo Hilo na Atafukuzwa Kazi na Kushtakiwa Mahakamani" Waziri Mkenda amekemea vikali udanyanyifu wa mitihani unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu na kuwataka Wakuu wa shule kutojiingiza katika udanganyifu huo. Na kuongeza kuwa "Kwa sasa kuna kesi zinaendelea kwa wale ambao walituhumiwa kwa kuvujisha mitihani na nawaahidi pindi hukumu zao zitakopotolewa na Mahakama, tutaweka majina yao hadharani ili kila mmoja asijaribu kujihusisha na udanganyifu huo." Akizungumzia suala la malezi shuleni Waziri Mkenda amewataka walimu kufuata Mwongozo wa Malezi, Unasihi na Ulinzi wa Mtoto katika Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu wa 2020 na kwamba kama kuna changamoto zibainishwe. “Tushirikiane kufanya ulinzi wa watoto, hakikisheni shuleni hawalali watoto wawili kitanda kimoja na kama kuna changamoto ya vyoo toeni taarifa kwa Mkurugenzi kuhusu changamoto hizo, lengo ni kuhakikisha kunakuwepo na mazingira salama ya utoaji elimu na kuwalinda watoto,” amesisitiza Waziri Mkenda. Amewataka Walimu kuangalia maudhui ya vitabu vinavyoingia shuleni ili visiharibu wanafunzi lakini pia kutumia Skauti na Viongozi wa dini katika kuendeleza malezi mazuri ya watoto shuleni. Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Dkt. Charles Msonde amewataka Wakuu wa Shule kufuatilia utendaji wa walimu shuleni ili kuondoa alama F kwenye masomo wanayofundisha. “Naendelea kusisitiza kufuatilia utendaji wa walimu, lakini pia wanafunzi wanapoingia shuleni tuanze na kuhakikisha wanakuwa vizuri katika lugha, wanapoilewa na kuweza kuiandika inakuwa rahisi kwao kuelewa masomo,” amesisitiza Dkt. Msonde. Kwa upande wake Rais wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSA), Frank Mahenge ameishukuru Serikali kwa namna inavyoshirikiana na Umoja huo na kuiomba pamoja na kazi nzuri wanayoifanya ya kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu nchini kujenga pia nyumba za walimu. Awake Aidha Katibu wa Elimu Jimbo Mkuu Katoliki la Dodoma Father Chrisant Mganga,amezitaka taasisi kuwa makini na vitu vinavyoletwa na Haki za Binadamu kunavitu vya hovyo vinaingizwa kwetu na baadhi wanatete vitu hivyo ambavyo vimetufikisha hapa tulipo leo , vijana wanafanya mambo ya hovyo mashuleni utasikia maadili ya memomonyoko hayo yote yamesababishwa na baadhi ya watu kuto kuwa waaminifu na kushindwa kujitambua wenyewe. @wizara_elimutanzania
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Akizungumza na Wadau wa Elimu
Katibu wa Elimu Jimbo Mkuu Katoliki la Dodoma Father Chrisant Mganga,
Khamis Ali Naibu Mkurugenzi Elimu (BAKWATA)
Waziri Mkenda na Wadau wa Elimu

MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 40 AMEKUTWA KANISANI BIRA NGUO ( MTUPU)

Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni Mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye Madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe huku sababu zikiwa bado hazijajulikana. Katibu wa Kanisa hilo, Elias Ngailo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Mwanaume huyo amekutwa akiwa mtupu amelala na kulazimika kumsaidia kumvalisha nguo na kumpeleka Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako huku wakiwa hawajui kama anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili. "Tumemuhoji baadhi ya maswali amesema yeye ni wa Morogoro sasa umekujaje huku hawezi kujieleza ila tulifadhaika tukaona walau tumsaidie kwa kumtafutia nguo asitiri mwili wake baada ya hapo tukampeleka kwenye Vyombi vya Usalama ili wajue namna ya kumsaidia" Mwinjilisti wa Kanisa hilo John Kisogo amesema awali baada ya kumkuta Mtu huyo katika madhabahu walilazimika pia kumfanyia maombi "Huyu Mtu alisema alijikuta tu yupo Madhabahuni tukamuuliza ulikuwa peke yako akasema nilikuwa na mwenzangu" Credit: Millard Ayo Kwa habari kemkem za kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha tembelea Shine News kila wakati hakika hutopitwa na chochote saa 24.

*CCM YATOA AGIZO KUHUSU WALIMU KUPEWA VISHIKWAMBI*

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa wiki moja kwa Wizara ya Elimu kuanzia leo Januari 20, 2023, kuhakikisha vishikwambi vilivyotolewa na serika kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa. CCM Imesema imepokea malalamiko ya kutotekelezwa kikamilifu kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji wa vishikwambi hivyo. Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, alisema wakati akizundua ugawaji wa vishikwambi hivyo Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kuhakikisha vifaa hivyo vinakwenda kwa walengwa. "Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivi ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini Chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo. "Kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane wawili wanaachwa. "Chama kinatoa maelekezo, kinaielekeza wizara husika (Wizara ya Elimu) kuhakikisha zoezi hili linakamilika na walengwa wote wanaostahili kuhakikisha wameipata vishikwambi hivyo, lakini so hivyo tu bali pia wahakikishe malalamiko haya hayapo na wasimamie zoezi kuona makundi yaliyopaswa kupewa yanafikiwa na wale ambao hawajapata wapate. Baada ya wiki moja tupate taarifa zoezi hili limekwendaje," amesema. ====

MWALIMU MWAKASEGE AINGILIA KATI VITA YA MCHUNGAJI KIMARO

VITA YA MCHUNGAJI KIMARO: MWALIMU MWAKASEGE AMESEMA KATIKA SOMO LAKE LA “MAHAKAMA INAYOMPA MUNGU UHALALI WA KUHUKUMU MIUNGU” KWAMBA PAULO KATIKA UTUMISHI WAKE , KILA ALIPOKUWA AKIPINGWA AU AKIZUIWA, ALIKUWA NA UWEZO WA KUJUA NI NANI ALIEKUWA ANAMPINGA AU ANAMZUIA. SHETANI ALIPOMZUIA PAULO ASIENDE MIJI FULANI, PAULO ALIJUA NI SHETANI ANAMPINGA. NA PIA KUNA WAKATI PAULO ALIKUWA AKIZUIWA NA ROHO MTAKATIFU ASIENDE MIJI FULANI, PAULO ALIJUA NI ROHO MTAKATIFU. KABLA YA KUANZA KUPIGANA VITA YOYOTE, NI VEMA SAANA TUANZE KUPIGANA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KWANZA KWA KUOMBA SANA MPAKA TUPATE KIBALI CHA “OK” YA MUNGU KAMA DAUDI (1 Samuel 30:8) “So David inquired of the LORD, saying, "Shall I pursue this troop? Shall I overtake them?" And He answered him, "Pursue, for you shall surely overtake them and without fail recover all." VITA YA WATUMISHI WA KWELI WA MUNGU INAPOKUWA IMEANZISHWA NA SHETANI KWA KUMTUMIA MKUU, TUSIKULUPUKE TUKAANZA KUPAMBANA BILA KUMUULIZA MUNGU KWANZA ATUPE MAELEKEZO (INSTRUCTIONS) TUANZIE WAPI. TUTAPIGWA VIBAYA SANA TUSIPOPATA OK YA MUNGU. MWALIMU MWAKASEGE NI MIONGONI MWA WATUMISHI AMBAO WAMETOA MACHOZI MENGI KATIKA UTUMISHI WAO. NI MUHIMU SAAANAA SANA KWETU WAPENDWA TUJUE KUWAOMBEA SAAANA NA KUWATIA MOYO WATUMISHI WOOTE WA KWELI WA MUNGU. WATUMISHI HAWA WANAPOPIGWA NA SHETANI, FAMILIA ZAO PIA ZINATESEKA SANA. TUMSIFU YESU KRISTO

PSPTB YACHUKUA HATUA KWA WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI UGAVI

Na. Kadala Komba Dodoma MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesem kuwa Bodi hiyo imekuwa ikichukua hatua katika madhaifu ambayo yanaweza kuleta hasara kwa serikali na kuathiri Miradi mikubwa kwa wakuu wa vitengo vya Ununuzi na Ugavi. Akizungumza jijini hapa leo Januari 19,2023 wakati wa kutoa taarifa ya matokeo ya mitihani ya 25 ya Bodi hiyo Mkurugenzi huyo amesema wanachosisitiza ni somo la hebabu na ni dhana ambayo imejengwa tangu chini kuwa somo hilo ni gumu kitu ambacho sio sahihi hesabu inafaulika. Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mtaalamu wa manunuzi ni vizuri ajue hesabu ambayo itamsaidia kujianini na kuandika ripoti katika shughuli zake na kwamba Ununuzi na Ugavi unaakisi zaidi katika uelewa wa manunuzi,uelewa wa dhana nzima mtambuka katika ule mzunguko wa shughuli za kimanunuzi kwa kuwa anatakiwa kupiga hesabu katika uwiano mbalimbali. "Tunachukua hatua pale tunaona kuna madhaifu ambao yanaweza kuleta hasara kwa serikali na pia inaweza kuathiri utoaji huduma kwa watu hasa katika miradi mikubwa," amesema Mbanyi. Ameongeza kuwa kumekuwa na mamalamiko kwa baadhi ya wanunuzi na kwamba wao kama Bodi mwaka wa fedha uliopita waliamru Wakuu wa vitengo 20 kuondolewa kwenye nafasi zao baada ya kutathimini taarifa ya matumizi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari wameshatuma barua 73 kuwaeleza makosa waliyoyafanya,udhaifu na makosa yaliyoonekana kwenye maunuzi na wanunuzi 68 kupeleka utetezi wao katika Ofisi ya Bodi. Akizungumzia matokeo hayo amesema jumla ya watahiniwa 1,216 walisajiliwa kufanya mitihani ambapo watahiniwa 1,135 sawa na asilimia 93.3 walifanya mitihani hiyo na kwamba kumekuwa na ongezeko la watahiniwa 1,031, ikilinganishwa na msimu uliopita. "Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 452 ni wapya na waliobaki 683 ni watahiniwa waliokuwa wanarudia baadhi ya masomo," amesema Mkurugenzi huyo. Mbanyi ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 613 sawa na asilimia 54.0 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 474 sawa na asilimia 41.8 watarudia baadhi ya masomo kuanzia moja hadi masomo matatu kutegemeana na idadi ya masomo aliyofeli na watahiniwa 48 sawa na asilimia 4.2 wamefeli masomo yote katika ngazi mbalimbali. "Katika masomo 34 waliyopimwa watahiniwa, masomo 18 yalifanywa vizuri, masomo 10 yalifanywa kwa wastani na matokeo ya masomo 6 yalikuwa mabaya kwa maana ya kuwa chini ya wastani. Huku watahiniwa watatu wakiibuka kama watahiniwa bora katika ngazi za mitihani za Professional I,iii na CPSP," amesema. Mwisho
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi

MAPYA YAIBUKA: MBEYA KIJANA MMOJA AGAWA HELA MTAA KWA MTAA

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Jack au [ZOMBIE MGAWA HELA] ameibua maswali mengi kwa wakazi wa Mbeya Juu ya Hela anazogawa kwa watu kila mtaa anaopita. Na wengine wakitaka Kujua Ratiba ya wapi maeneo atakayokuwepo na wengine wakiogopa wakihusisha Imani za kishirikina kwamba watatolewa kafara. Wananchi wengi wameendelea kutoa maoni yao juu ya Utajiri wa ajabu wa kijana huyo anayegawa hela bira masharti yoyote. Huku akiwajazia mafuta wamiliki wa vyombo vya moto inasadikika Zaidi ya milioni 50 anatumia kugawa kwa watu kila siku. Inasemekana kijana huyo miaka 3 iliyopita alikuwa msaidizi wa mganga wa kienyeji jina maarufu Dk Manyaunyau baada ya kitambo akibuka na hili .
ZOMBIE MGAWA HELA KATIKA PICHA

WANAWAKE 15 WAMEFANYIWA UPASUAJI WA UGONJWA WA FISTULA

Na. Mwandishi wetu Mbeya Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi Amezindua Rasmi kambi ya matibabu ya Fistula katika Hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya ,amesema Ugonjwa wa Fistula unawasababishia maumivu makali wanawake huku ukiwahathiri kisikolojia hasa pale wanaponyanyapaliwa na jamii pamoja kukimbiwa na wenza. Aidha Naibu Waziri amesema tangu kuanzishwa kwa kambi hiyo Januari 16 mwaka huu mpaka sasa ni wanawake 15 pekee ndio waliofanyiwa upasuaji kati ya wanawake 60 wanaolengwa kunufaika na huduma hiyo ambayo inatolewa bure. “Kambi hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Hospital kanda ya Mbeya na Ofisi ya Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Kwaupande wake mwakilishi wa chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania ,Dk.Peter Majige amesema wanawake 3000 huugua kila mwaka ugonjwa huo nchini huku 1500 pekee wakitibiwa kutokana na matatizo mbalimbali . Amesema matibabu ya ugonjwa huo huwa yana gharama kubwa hali ambayo wananchi wengi wanashindwa kumudu na hivyo kukilazimu chama hicho kuomba ufadhili kutoka kwenye mashirika mbalimbali ya kitaifa. Ameiomba serikali kusamehe baadhi ya gharama za matibabu ya ugonjwa huo ili kuwasaidia wagonjwa wengi Zaidi kupata matibabu na kuondokana na tatizo hilo. Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Francis Rwegoshora amesema Hospital hiyo inatoa huduma ya matibabu ya ugonjwa huo lakini wagonjwa wengi wanashindwa kufika kutokana na uchumi mdogo pamoja na kutopata Taarifa . Amesema kambi hiyo iliyopelekwa katika Hospitali hiyo itasaidia kuwatambulisha matibabu hayo kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ili waende wakatibiwe.
Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi Akiwa na mwakilishi wa chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania
MATUKIO KATIKA PICHA YA UZINDUZI RASMI WA KAMBI YA MATIBABU YA FISTULA MBEYA

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA UTAKOSAIDIA MIJI YA TINDE NA SHELUI

Na. Mwandishi wetu Shinyanga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango ameweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria utakaohudumia Tinde na Shelui unaogharimu shilingi bilioni 24.4, hafla iliofanyika eneo la Tinde mkoani Shinyanga leo tarehe 19 Januari 2023.  Dkt Mpango Amewataka kuongeza ufanisi katika matumizi ya maji, hususani kwenye kilimo pamoja na kuwaagiza kutunza vyanzo vya maji ikiwemochanzo cha Ziwa Victoria kilichopo Ihelele Wilayani Misungwi, ambacho ni tegemeo kwa upatikanaji wa huduma za maji katika Miji ya Wilaya za Misungwi, Kahama, Shinyanga, Tabora, Kahama, Nzega, Igunga, Shelui na Tinde.   Aidha Dkt. Mpango amesema dhamira ya Serikali ni kuona mradi huo unatoa maji na kuwa endelevu kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na pia juhudi za kupeleka maji katika maeneo yaliyopo karibu na mradi huo zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maeneo yote yanapata majisafi na salama na yanatosheleza mahitaji.   Makamu wa Rais ameongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutoa kipaumbele cha juu kugharamia miradi ya maji ili itoe huduma endelevu ya majisafi na salama pamoja na elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi wote. Amesema Sekta hiyo ni miongoni mwa Sekta za kipaumbele katika Mkakati wa kukuza Uchumi wa Viwanda na kupambana na umaskini nchini. Amesema kuboresha huduma ya maji kutapunguza muda wa kutafuta na kuchota maji ili kuwawezesha Wananchi kufanya kazi nyingine za maendeleo,kuongezeka kwa muda wa Wanafunzi kuhudhuria masomo, kuimarisha afya za Wananchi na kuepusha magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.   Halikadhalika Makamu wa Rais amekemea tabia ya wizi wa maji inayofanywa na baadhi ya watu nchini wakiwemo wawekezaji wakubwa. Amezitaka mamlaka kuacha kutoza faini ndogo kwa wanaokutwa na hatia za wizi wa maji. Aidha amevitaka vyombo vyote husika kufuatilia na kuwachukulia hatua wezi wote pamoja na wale wanaochepusha maji kutoka kwenye mito bila vibali halali na wengine kuharibu vyanzo vya maji.   Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema Wizara hiyo inatekeleza miradi ya maji ya kimkakati katika mkoa wa Shinyanga inayogharimu shilingi bilioni 35 itakayosaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa mkoa huo kuondokana na changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama.   Aweso amesema pamoja na wananchi wa kata ya Tinde kunufaika na mradi huo pia vijiji 22 vya Jirani vitaweza kufikiwa na mradi utakaowasaidia wananchi kupata maji safi na salama. Ameongeza kwamba Wizara hiyo itaendelea kufuatilia na kusimamia kwa makini utekelezwaji wa miradi ya maji ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kutoka huduma kwa wananchi katika kufikia adhma ya kufikisha maji kwa asilimia 95 maeneo ya mijini na asilimia 85 maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango akiweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria
Waziri wa Maji Jumaa Awes akitoa ufafanuzi utekelezaji wa miradi ya maji

WAZIRI WA ELIMU, PROF. MKENDA AMEZINDUA BODI YA TUME YA VYUO VIKUU 2023-2026

Na. Kadala Komba Dodoma WAZIRI Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Ameitaka Tume Ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) kushirikiana na Vyuo Vikuu Vyote Kwa kuwasikiliza, Kuwapa Muda Wa Kutosha, Kuhakikisha wanasaidiwa na Sehemu yenye Vikwazo wapewe Ushauri Wa haraka Kabla ya Kuchukua Sheria Nyingine Muhimu. . Mkenda Ameyasema hayo Leo January 19,2023 Alipokuwa kwenye Akizinduzi Bodi Ya Tume ya Vyuo Vikuu kuanzia mwaka 2023 hadi mwaka 2026 Jijini Dodoma. . Amesema wanahitaji Watanzania wengi waende Nje Ya Nchi Wakasome Na Sio Masomo ya Sayansi Tu hata Na Masomo Mengine Kwa Sababu hawawezi kutarajia Watu Ndani ya Nchi ikiwa Hawana Walimu Wa Kutosha. . Mkenda Ameitaka Pia TCU Kujaribu Kuvitambua Vyuo vinavyofundisha Nje Ya Nchi na Kuvielewa Vizuri Hasa Medicine. . Aidha, Mkenda Amesema Vyuo Vikuu ni Muhimu Sana kusimamia Ubora Wake Kwa Sababu vitakuwa Chachu Ya Kuwasaidia Kuongeza Ubora Kwa Ngazi ya Chini. . Nae Mwenyekiti Wa Bodi Ya Tume Hiyo Prof. Penina Mlama Amemuahidi Waziri Mkenda Kwamba watakuwa Began Kwa Bega Na wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Katika Juhudi zake Za Kupaisha Sekta Ya Elimu Juu Ili Watanzania Wote wanaopita Katika Vyuo Vyao Vikuu wapate Elimu Yenye Tija na Ya Viwango Vya Juu Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.
WAZIRI Wa Elimu, Sayansi Na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda,

MKULIMA WA KARANGA NA MTAMA ANAYETUMIA VIFAA VYA KISASA KULIMA NA KUPANDA

Na. Kadala Komba Dodoma Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula amesema Hapa naendesha kilimo cha karanga na mtama kwa kutumia teknolojia mbalimbali katika kuandaa mashamba, kulima, kuvuna na sasa nategemea kuwa na teknolojia mpya ya mashine ya kuchambua karanga kulingana na madaraja na kutumia teknolojia rahisi," álisema Alizungumza wakati wa mahojiano na Shinenews walipotembelea katika shamba lake lililopo katika eneo la Zinje, Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula álisema kuwa matumizi ya teknolojia yanafanya kilimo kiwe rahisi na uzalishaji kuwa mkubwa. Álisema kuwa katika kuandaa mashamba anatumia trekta dogo la mkono (power tiller) ambapo hutumia lita mbili na nusu kulima shamba la ekari moja, jambo anbalo hupunguza gharama kwani unapolima kwa kutumia treka ekari moja hugharimu kati ya Sh 30,000 hadi Sh 50,000," álisema. "Ukiwa na power tiller unatumia dizeli ya Sh 7,500 inapunguza gharama kwa kiasi kikubwa, wakati wa kupanda tunatumia mshine ambayo huchimba shimo na kufukiia mbegu, mashine hiyo niliinunua kwa Sh 350,000 ina uwezo wa kupanda eneo kubwa kwa muda mfupi" Álisema kuwa wakati mashine hiyo ndogo ikiwa na kontena lililojaa mbegu za karanga mpandaji huipitisha pembeni ya Kamba ambapo ina uwezo wa kupanda karanga nmstari kwa mstari kwa sentiometa 50 na shimo kwa shimo ni sentimita 10. “Unapoanza kupanda unatakiwa ukakikishe Kamba imefungwa kwa kunyooka hii hurahisisha hata wakati wa kuvuna karanga kwa kutumia mashine usiruke mstari,” alisema Aidha alisema kuwa wakati wa kupalilia hutumia teknolojia ya kuua magugu na kuacha karanga ikiwa salama. Álisema kuwa hata kwenye uvunaji wamekuwa wakitumia mashine na kwenye kupura mazao,' álisema. Aliwataka wakuliwa na wale wanaotaka kuingia kwenye kilimo kuwa ua utararibu wa kuwatembelea wakulima wanaotumia teknolojia ili kujifunza na kuboresha kilimo. Alisema kuwa mpango wa Sserikali wa kuwezesha vijana kuingia kwenye kilimio utakuwa na manufaa makubwa kama vijana watakuwa na utayari wa kuingia kwenye kilimo. “Tunatakiwa kuhakikisha vijana wanaelimishwa ili wafahamu kilimo ni nini nina amini kilimo cha teknolojia kitawavutia vijana wengi,” alisena. Mmoja wa kibarua katika shamba hilo, Maneno Paulo alisema kuwa matumizi yam ashine yanmepelekea kazi yao kuwa nyepesi. “Hapa tunapanda kwa kutumia mashine, tunavuna kwa mashine kazi yetu inakuwa rahisi tifauti na kufanya kazi kwa kutumia mikono. Aliwataka vijana kujiajiri kupitia kilimo kwani kuna fursa nyingi. Agostine Ng’ambi mkazi wa Zinje ambaye pia ni kibarua katika shamba hilo alisema kuwa upandaji ni rahisi na wanatumia muda mfupi katika kazi zao za kila siku. mwisho
Ukiwa na power tiller Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula Akiwa na Power Tiller akiandaa shamba la Karanga
Agostine Ng’ambi mkazi wa Zinje ambaye pia ni kibarua katika shamba hilo
Mmoja wa kibarua katika shamba hilo, Maneno Paulo
mashine hiyo ndogo ikiwa na kontena lililojaa mbegu za karanga mpandaji huipitisha pembeni ya Kamba ambapo ina uwezo wa kupanda karanga nmstari kwa mstari kwa sentiometa 50 na shimo kwa shimo ni sentimita 10.
Katibu Mtendaji wa Shirika la Agriculture Seeds Production Association (DASPA), Aithan Chaula Akitoa maelekezo kwa Vibarua

WAZIRI WA ELIMU, PROF. MKENDA AMEWATAKA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU KUWAPELEKA SHULE

Na WyEST Masasi, MTWARA Wito umetolewa kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kutowaficha watoto ndani badala yake wawapeleke shule kwa kuwa zipo shule maalum kwa ajili ya watoto hao. Hayo yamesemwa na Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokuwa akizindua majengo mapya ya Shule Jumuishi ya Mfano ya Msingi Lukuledi iliyojengwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa Elimu na Kuendeleza Ujuzi na Stadi za Kazi (ESPJ) na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi ya kupata elimu. "Nipende kuwaasa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum popote nchini kutowaficha watoto ndani kwani Serikali iko tayari kuhakikisha watoto wote wanapata elimu stahiki," amefafanua Prof. Mkenda. Waziri Mkenda ameongeza kuwa katika mchakato unaoendelea wa mapitio ya Sera na mabadiliko ya mitaala, wanafunzi wenye mahitaji maalum wamepewa kipaumbele cha pekee katika kuhakikisha elimu wanayopata inawapa ujuzi kulingana na mahitaji waliyonayo pamoja na kuongeza walimu wenye taaluma hiyo. "Katika mchakato wa mapitio ya Sera na mabadiliko ya mitaala, suala la elimu jumuishi limetiliwa mkazo na tutaendelea kutilia mkazo hadi katika utekelezaji, ndio maana tunaendelea kuwekeza katika miundombinu stahiki kwao kwa kujenga shule jumuishi za Mfano na ninashukuru Benki ya Dunia kwa ufadhili wa mradi uliowezesha ujenzi huu sasa wanafunzi wetu wako katika mazingira bora ya kielimu," amesema Waziri Mkenda. Waziri Mkenda pia amewaasa wadau wa maendeleo kuendelea kuona umuhimu wa kuchangia juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ujifunzaji katika ngazi zote za elimu. Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo, Dkt. Magreth Matonya, Mkurugenzi wa Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema shule hiyo ni Jumuishi ikiwa na maana inachukua wanafunzi wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji maalum na kwamba awali ilikuwa katika majengo ambayo yalichakaa na finyu kulingana na idadi ya wanafunzi. Ameongeza kuwa ujenzi wa shule hiyo umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 1.4 na kwamba ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 320 kwa mara moja ambapo wanafunzi wenye mahitaji maalum watakaa bweni. Ametaja baadhi ya majengo yaliyopo kwenye shule hiyo kuwa ni mabweni 4, madarasa 12, ofisi 6, nyumba za watumishi 8, karakana 3, bwalo na jiko. Mengine ni jengo la Utawala, nyumba ya mkuu wa shule 1, matundu ya vyoo 9, na chumba cha maalum upimaji usikivu. Naye Mratibu wa Mradi wa ESPJ, waliofadhili mradi, Margaret Mussai amewataka walimu, wanafunzi na wanajumuiya wa shule hiyo kuhakikisha wanatunza miundombinu ya shule hiyo ili iweze kutumika mpaka vizazi vijavyo ikiwa kwenye hali nzuri. "Serikali imetumia fedha nyingi sana kujenga majengo haya hivyo niwaase walimu, wanafunzi na wanajumuiya wa shule hii kuitunza na kuienzi hii miundombinu ili itumike na kizazi cha sasa na cha baadae," amefafanua Mussai. Katika hafla hiyo Waziri Mkenda pia alikabidhi rasmi shule hiyo kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Abdalla Malela alipokea Hati ya Makabidhiano ya shule hiyo.
Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokuwa akizindua majengo mapya ya Shule Jumuishi ya Mfano ya Msingi Lukuledi iliyojengwa na Wizara ya Elimu
Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi na viongozi wa Shule
majengo yaliyopo kwenye shule hiyo kuwa ni mabweni 4, madarasa 12, ofisi 6, nyumba za watumishi 8, karakana 3, bwalo na jiko.