Subscribe Us

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

MAAFISA ELIMU KATA, WALIMU WAKUU, WALIMU WA MAZINGIRA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA KATA WAJENGEWA UWEZO JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI KATIKA MAZINGIRA YA SHULE BAHI

Na. Kadala Komba Bahi 
 
 
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndugu Boniphace Wilson akifunga mafunzo hayo  kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji  wa Halmshauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Zaina Mlawa  ametoa maagizo kwa walimu wa mazingira na  wakuu wa shule za msingi kutunza mazingira ya shule na kupanda miti ya kutosha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya shule zao. Akitoa maagizo hayo ameeleza umuhimu  wa uwepo wa miti shuleni na ujenzi wa madarasa  unaozingatia vigezo vya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndugu Boniphace Wilson
            akifunga semina ya mazingira  ya siku tatu
 
 
 
Hayo yamejiri wakati wa semina ya mazingira  ya siku tatu iliyohusu mafunzo kwa walimu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika shule zao. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi.

"Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Boniphace Wilson akifunga mafunzo hayo ametumia nafasi hiyo  kuishukuru serikali kupitia OR TAMISEMI kwa kuleta mafunzo hayo Bahi pia amewashukuru  wafadhili wa program hiyo ambao ni  Shule Bora kwa kutoa zaidi ya Milioni mia tatu,  kwajili kukamilisha maboma kumi na nane yaliyojengwa kwa kuzingatia vigezo vya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuwezesha  mafunzo mbali mbali kwa walimu yakiwepo haya ya mazingira
 
 
picha ya pamoja meza kuu 

 








Kwa upande wa walimu wakiongea kwa niaba, walimu wenzao wa wilaya ya Bahi  mwalimu Kondo,  Mwashi Benedict Cheo na Mkuu wa shule  Bahi English medium bi Farida Aloyce  Wameishukuru serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuwaletea mradi wa mazingira chini ya program ya shule bora  ambao utaenda kubadilisha mazingira ya shule zetu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

.Naye Afisa maendeleo ya jamii kata ya Babayu wilaya ya Bahi Nasibu Saidi Amewashukuru wafadhili wa mradi wa mazingira Shule bora kwa kuwakumbuka kata ya Babayu.




RC SENYAMULE AIPA KONGOLE BAHI USIMAMIZI WA FEDHA ZA UJENZI WA MIRADI

 Ikiwa ni miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan kwenye kiti cha Urais na yamefanyika Maendeleo makubwa chanya
Kupitia shamlashamla hizo za miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amefanya ziara  Wilaya ya Bahi na kukagua Miundombinu ya hospitali ya Wilaya pamoja na miradi inayotekelezwa Katika Hospitali hiyo ikiwemo ukamilishaji wa mochuali ambao tayari lipo jokofu moja kwaajili ya kuhifadhia miili,pia amekagua jengo la kulazwa wanaume na jengo la kulazwa wanawake,

Kupitia ziara hiyo mkuu wa Mkoa ametembelea pia Zahanati ndogo iliyopo Nagulo kata ya Bahi ambayo ilizindiliwa siku za karibuni na kupitia ukaguzi wake ameridhishwa na huduma kwani Zahanati hiyo kwani imekua msaada mkubwa wa kuwahudumia Wananchi wa Nagulo Bahi waliokua wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule ameipongeza sana Wilaya ya Bahi na uongozi wake kwa jitihada kubwa wanayoifanya ikiwemo usimamizi mzuri wa fedha za ujenzi wa miradi zinazotolewa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, na kupitia ziara hiyo amesisitiza kuwa dhana ya uwajibikaji bora iwe nguzo kuu kwa watumishi wote ili kuweza kuchochea maendeleo chanya ndani ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.


WAZIRI ULEGA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WA MIZANI KUPISHA UCHUNGUZI

 
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Balozi Aisha Amour, kuwasimamisha kazi wasimamizi wote wa Mizani waliokuwa zamu katika Mizani zilizopo katika barabara kuu ya T1 inayoanzia Dar es Salaam – Zambia kupitia mpaka wa Tunduma kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa malalamiko katika Mizani hizo.

Ulega amefanya maamuzi hayo mara baada ya kadhia iliyojitokeza hivi karibuni kwa msafirishaji Bi. Pamela James Bukumbi mwenye gari ya mizigo namba T 137 DLQ likiwa na tela T 567 CUR iliyotokea katika kituo cha Mizani ya Vigwaza akilalamika kuhusu kutozwa faini ya kuzidisha uzito katika Mizani hiyo wakati mizani nyingine alizopita gari yake haikuwa imezidisha uzito.

Ulega ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma leo tarehe 20 Machi, 2025 mara baada ya kupata taarifa hiyo na kusikiliza pande zote mbili kutoka kwa mlalamikaji na mlalamikiwa ambaye ni Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kubaini kuwa lipo tatizo la wazi ambalo limesababisha kadhia hiyo na kutoa maelekezo makuu matano.

“Baada ya kugundua liko tatizo, Nimeamua kuchukua hatua zifuatazo moja ni kuwasimamisha wale wasimamizi wetu wa Mizani wa hii T1 barabara nzima kuanzia Tunduma mpaka inafika pale Vigwaza waliokuwa kwenye zamu kwa siku ile wakati tukio linatokea”, amesema Ulega.

Ulega ameeleza kuwa amewasimamisha wasimamizi hao kwa lengo la kufanya uchunguzi ambapo tayari timu ya wataalam ya kuchunguza tukio hilo imeundwa ili kufuatilia safari nzima ya gari hilo ili kupata hali halisi na kuwasilisha mapendekezo mengine ili hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi ya wale wote ambao watabainika na vitendo visivyoridhisha.

Aidha, Waziri Ulega ameuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuanza hatua za kubadilisha mifumo ya uendeshaji wa Mizani 78 zote nchini haraka iwezekanavyo kwa kutangaza kwa watoa huduma wenye nia kuja na teknolojia ambazo ni ‘automated’ ili kupunguza muingiliano baina ya watu na watu na hivyo kumuwezesha dereva kujihudumia kwa kutumia mifumo jambo ambalo ni mkakati wa Wizara wa muda mrefu.

Aidha Ulega ameielekeza TANROADS kuhakikisha mifumo ya Mizani zote inasomana kutoka Mizani moja hadi nyingine ambapo jambo hilo limekuwa likisemwa na kusisitizwa mara kwa mara na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu mifumo katika Serikali kusomana na kuagiza utekelekezaji huo ufanyike haraka iwezekanavyo.

Ulega amewalekeza Mameneja wote wa TANROADS nchini kuwa nambari moja katika usimamizi wa Mizani zilizopo katika mikoa yao na sio kuwaachia wasimamizi peke yake na Mizani zitakazolalamikiwa na Mameneja husika pia watachukuliwa hatua.

“Kwa muda mrefu Mameneja wamekuwa wakijiweka kando sana katika usimamizi wa Mizani lakini hapo mbele tutaanza mara moja mizani zitakazokuwa zikilalamikiwa tutaanza kuwachukulia hatua na Mameneja na sio wasimamizi tu”, amesisitiza Ulega.

Vilevile, Ulega ameeleza kuwa Serikali inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ambayo kwa ujenzi wa kilometa moja unaigharimu Bilioni moja hadi mbili kutegemea mazingira ya eneo husika ambazo zinahusisha fedha za umma na hivyo kutoa rai kwa wananchi kuona umuhimu wa kuilinda rasilimali hiyo kwa kutokana na uwekezaji wake pamoja na usalama wa watumiaji wa miundombinu hiyo.



MBUNGE WA JIMBO LA BAHI MHE. KENNETH NOLLO AMSHUKURU MHE.RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO BAHI

 
Na. Kadala Komba Bahi

Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe. Kenneth Nollo amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya Maendeleo  kwa wananchi wa wilaya ya Bahi.

Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma Mhe. Rosemary  Senyamule  akikagua  miradi ya maendeleo  katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi katika hospitali ya wilaya Bahi,  tar 19/03/2025  alisema Hospitali hii nikama ndoto kwa wana Bahi ni ukombozi mkubwa sana sisi watu wa Bahi yunasababu zote kumshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan rais wetu kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea katika Halmashauri ya Bahi.

Katika sekta ya afya katika mwaka 2021hadi sasa mwaka 2025 vijiji kumi na saba vimepata  vituo vya Afya (Zahanati) ambapo awali vijiji kumi na tisa vilikuwa havina kituo cha afya  (Zahanati)


MSAKO MKALI WALIOGUSHI VYETI VYA JKT

 
Na. Angel Haule Dodoma

Jeshi la kujenga taifa JKT kimetoa onyo kwa watu wanaogushi vyeti vya Jeshi Hilo vinavyoonesha wamepitia mafunzo ya JKT na kutumia kama sifa ya kuombea kazi sehemu mbalimba Nchini, wakati watu hao hawajawahi Kupitia mafunzo yoyote ndani ya jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari  katika Makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Jijini Dodoma Kaimu mkuu wa tawi la utawala JKT KANALI JUMA MRAI amesema,

Hivi karibuni JKT imebaini uwepo wa vyeti vya kugushi vilivyotumika na baadhi ya vijana ambao sio waaminifu ili kujipatia ajira katika taasisi na makampuni yanayohitaji watendaji waliopitia mafunzo ya JKT.

Kaimu  Mkuu huyo wa tawi la utawala JKT ameongeza kuwa JKT inapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa, wale wote waliobainika na watakaobainika kugushi cheti Cha JKT kwa matumizi yoyote yale na hatua Kali za kisheria zitachukukiwa dhidi yao

Aidhi KANALI JUMA MRAI amesisitiza kuwa Jeshi la JKT lipo teyale kutoa ushirikiano kwa taasisi na makampuni yote yanayohitaji uhakiki wa vyeti vya JKT kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya jeshi hilo.

Katika hatua nyingine Jeshi la kujenga Taifa JKT Kupitia Kaimu huyo wa tawi la utawala JKT JUMA MRAI limesema jeshi hilo kinaendelea nafasi za kujiunga na mfunzo ya JKT zinatolewa Kila mwaka kwa vijana wa kitanzania wenye sifa , ili wamalizapo mafunzo ya JKT waweze kupata cheti Cha kuhitimu mafunzo hayo kihalali.


Akizungumza na waandishi wa Habari  katika Makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Jijini Dodoma Kaimu mkuu wa tawi la utawala JKT KANALI JUMA MRAI 


 


Baadhi ya waandishi wa Habari  katika Mkutano makuu na  KANALI JUMA MRAI Jijini Dodoma

WANACHAMA WAPYA 20 WA CUF WAKABIDHIWA KADI

 


Na Mwandishi Wetu, Kondoa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara)  Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua  wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho ili wakazuie bajeti zinazowakandamiza Watanzania.

Akizungumza na wananchi katika uwanja wa stendi ya zamani Dunga aliwataka wananchi kuchagua wabunge na madiwani ili wakazuie bajeti zinaxowakabili wananchi.
Alisema kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.

Alisema kuwa kwa sasa asilimia 99 ya wabunge wanatatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Alisema kuwa iwapo wananchi watakichagua chama hicho, watauza mazao yao vizuri,tofauti na sasa wananchi wanalazimishwa kuuza mazso kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo wamekuwa wakiuza kwa mkopo.


"Hospitali nyingi zimejengwa lakini  hakuna huduma,hakuna dawa  lakini CUF itahakikisha huduma zinaboreshwa hasa vijijini ambapo wananchi wamekuwa wakipata adha kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, "alisema

Alisema kuwa umaskini wa wananchi sio laana ya Mungu , CUF  ikishika dola itafanikisha mambo mengi ikiwemo wazee watapata posho ya kujikimu kila mwezi, "alisema.

Alisema kuwa elimu bure haijaleta matokeo mazuri kwa wananchi kutokana na shule nyingi kuwa na michango mingi inayozidi hata ada zilizoondolewa.


Katika mkutano huo zaidi ya wanachama wapya 20 walikabidhiwa kadi.
Mkazi wa Kondoa, Hamidu Mkopi alitaka wananchi kuziishi 4R za Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwisho




ALIYENG'OA BENDERA YA CUF ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

 
Na Mwandishi Wetu,, Kondoa

MTU mmoja anashikikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kukamatwa aking'oa  bendera na mabango ya Chama cha Wananchi (CUF)   wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa (Bara)  Othman Dunga).

Wakizungumzia tukio hilo,  Mjumbe wa kamati tendaji CUF wilaya ya Kondoa, Ayubu Hamisi alisema kuwa asubuhi ya Machi 7 mwaka huu, wakati wakiwa katika maandalizi ya kumpokea Makamu Mwenyekiti Othuman Dunga kulitokea  jambo la kusikitisha ambapo  vijana wanaosadikiwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  waliingia mitaani na kung'oa bendera 13 na mabango 25 .

Alisema kuwa baada ya kufanya msako waliweza kumkamata kijana mmoja ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliofanya uhalifu huo na sasa anashikiliwa na Jeshi la polisi.

Mwanachama wa Chama hicho, Hadija Selemani alisema kuwa kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimewasikitisha sana. "Tulikuwa tumejiandaa vizuri wanachama wamefika wakiwa wamevalia sare zao vizuri kwa ajili ya kumpokea kiongozi wao lakini kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimetusikitisha sana," alisema na kuongeza.

"Jambo hili limetusikitisha sana kwani kwa mara ya kwanza Kondoa inapata kiongozi  mwenye wadhifa mkubwa, lakini wasiotutakia mema ,wameshusha bendera, waking'oa mabango  ,kinachofanyiika ni mbinu za kuua siasa za upinzani jambo ambalo  limeleta taharuki,"alisema

Mwanachama mwingine wa chama hicho Nassoro  Junguke  alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitaka kuendeshwa kwa siasa za kistaarabu lakini baadhii ya watu wamekuwa wakifanya vitendo vinavyohatarisha amani iliyopo.

"Wakishusha tena bendera za CUF sisi hatutaenda polisi wataenda wao ,Jambo kama hili halikubaliki katika demokrasia yetu, "alisema.
Pia alisema walifanya msako na kufika hadi nyumba inayoficha wahalifu, walibaini wahalifu waliofanya tukio hilo ambao wamekuwa wakitembea na kapu la kukusanyia bendera wanazong'oa.

Pia alisema Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Kondoa amewafuata na kuwataka waondoe bendera kwenye nguzo.
Alisema kuwa jambo hilo limewatafakarisha   sana kwani nguzo nyingi hata mahali panye nyaya bendera za CCM zinapepea lakini bendera za CUF hazitakiwi.
"Watendaji wa serikali wasiingizwe kwenye mitego ya siasa wafanye kazi za kutoa huduma kwa wananchi,"alisema
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara baada ya kupokelewa wilayani Kondoa Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga,, alisema hiyo ni mara ya pili bendera za chama hicho zinang'olewa wakati chama hicho kikiwa na mikutano.
Alisema kuwa tukio  kama hilo lilitokea Julai mwaka jana wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipofika Kondoa ambapo bendera zaidi ya 60 ziling'olewa siku moja kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano.
"Huo ni uoga tushindane kwa hoja na sio kung'oa mabango na kuleta taharuki, "Alisema
Dunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kondoa alisema kuwa bendera ni alama ya chama tu .
"Wakati wengine wakihangaika kushusha bendera sisi  tunahangaika kutafuta wanachama wapya wajiunge na chama.
Nyie ng'oeni bendera  sisi tutaiba nyoyo za watu ili wajiunge kwa wingi na CUF, "alisema.
Dunga alichaguiliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania bara Desemba mwaka jana.

Alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, George Katabazi alisema kuwa taarifa kamili hazijamfikia anafuatilia suala hilo na atatoa taarifa ..Kaption




1.Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Wananchi (CUF) Taifa IBara)  Othuman Dunga akizungumza na wanachama na wananchi wa wilaya ya Kondoa kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa kwa ajili ya kumpogeza kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ,mnkutano huo ulifanyika katika uwanja wa stendi ya zamani jana.,


2Makamu Mwenyekiti  wa Chama cha Wananchi (CUF) Taiifa (Bara) Othuman Dunga akiwasalimia wanachama wa CUF wa wilaya ya Kondoa waliokuja kumpokea kwa ajili ya kufanya mkutano wa kumpongeza  kwa kucahaguliwa kwake kushika wadhifa huo.


3.Wanawake wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kondoa  wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga (hayupo pichani) baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa kwa ajili ya kupongeza uliofanyika jana



MAJIKO YA GESI 3,250 KUTOLEWA KWA BEI YA RUZUKU BAHI

 

Na. Kadala Komba Bahi

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza usambazaji wa majiko ya gesi (LAKE ) kwa bei ya ruzuku Wilayani Bahi Mkoani wa Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034.

Hayo yameelezwa Februari 19, 2025 Wilayani Bahi na Afisa mauzo lake gesi campan ,Kisajli Nehemia  wakati wa zoezi la uuzaji wa mitungi ya ges kwa wananchi na watumishi wa Serikali katika ofisi ya mtendaji wa  kata amesema majiko ya gesi 3250 kutolewa katika Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwa bei ya ruzuku na zoezi hili litaendeshwa kwa siku mbili.

Kwa upande  wa Mheshimiwa Diwani kata ya Bahi Augustino Ndonu amemshukuru Rais Samia kwa kuwasogezea nishati safi na salama kwajili ya utunzaji wa mazingira na bei nafuu hii nishati ukienda dukani kununua utauziwa Sh. 45000 Helfu leo wananchi wa kata yangu wananunua kwa Sh. 20800, Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita inahakikisha Watanzania wanaachana na matumizi ya nishati isiyo safi na salama kama ambavyo imeelekezwa katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Habiba Omar mkazi wa kata ya Bahi  amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaondolea kero wananchi wa Bahi  hususan wanawake na watoto ya kutembea umbali mrefu kusaka kuni kwa ajili ya kupikia.  wakizungumza kwa nyakati tofauti, Habiba Omar wamepongeza jitihada za Serikali za kuwasambazia nishati safi ya kupikia mbayo wamesema ni hatua nzuri ya kulinda afya zao na mazingira kwa ujumla.


Naye Miraji Bakar mkazi wa Kata ya Bahi amesema uwepo wa nishati safi ya kupikia wilayani hapo ni hatua ya kupongezwa kwani inakwenda kuimarisha afya za wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia kuni kupikia.

"Tulikuwa tunasikia tuu nishati safi lakini leo tumeelimishwa na pia tumeshuhudia majiko ya gesi yaliyotolewa na Serikali kwa ruzuku," amesema .

Wananchi waliyojitokeza kununua gesi









MAAFISA ELIMU KATA,WALIMU WAKUU WAJENGEWA UWEZO BAHI

 BAHI


Kupitia Mpango wa Shule bora leo tarehe 10/02/2025 yamefanyika Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Shule Wilayani Bahi .

Mafunzo haya yana lengo la kuongeza ushirikiano baina ya Walimu Wakuu,Maafisa Elimu Kata na watumishi walio chini yao ili kuboresha utendaji kazi  na kufanikisha dhana nzima ufundishaji na ujifunzaji ili kupata matokeo bora.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Afisa Elimu Wilaya Ndg.Boniface Wilson na yatafanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuanzia leo na kutamatika siku juma tano tarehe 13/02/2025.

Aidha,mafunzo haya yatakua endelevu kwa kuanzisha jumuiya za ujifunzaji ngazi ya Shule lengo kuu ikiwa ni kuzidi kupeana uzoefu katika usimamizi wa shule.


MAKATIBU WAKUU NA WADAU WA TANZANIA SAFARI CHANNEL WAKUTANA DODOMA

 





Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na wadau wa televisheni ya Tanzania Safari Channel wamekutana kuzungumzia uendeshaji wa Chaneli ya Utalii ya Tanzania Safari Channel inayomilikiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Akizungumza mara baada ya Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara Wadau wa Tanzania Safari Channel kilichofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi Makatibu Wakuu hao wamekutana kwa lengo la Kupokea na Kujadili taarifa ya kikao cha Wakuu wa taasisi.

Dkt. Yonazi ipo haja ya yakuendelea kuboresha chaneli hiyo ili iendelee kuwa bora na kuwavutia watazamaji wa makundi yote ndani na nje ya Nchi.

Ameongeza kuwa chaneli hiyo itakuwa yakuigwa barani Afrika ambayo itaitangaza Afrika kutokea Tanzania.

Pamoja na hayo kikao hicho kimejadili mikakati mbalimbali ya kuiwezesha chaneli hiyo kuendelea kuendesha shughuli zake za uzalishaji wa vipindi vya utalii vyenye maudhui ya ubunifu zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza kuwa wizara yake katika kuisimamia TBC inayo dhima ya kuhakikisha kuwa tija ya chaneli hiyo inapatikana na changamoto zote zinatatuliwa ili jamii iweze kunufaika na uwepo wa chaneli hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi. Fatma Hamad Rajab ameishauri TBC kufanya kazi kwa ukaribu na Kamisheni ya Utalii Zanzibar ili kutangaza vivutio vingi vya utalii vilivyopo Zanzibar.




BAJETI YA MWAKA 2025\2026 SHILING BILION 35.9 YAPITISHWA BAHI KWA KISHINDO

Kusho ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Bahi Zaina Mlawa katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Joachim Nyingo mwisho ni Donald Mejiti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi [MNEC]


 Kikao cha Baraza la Madiwani cha kupokea ,kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2025\2026 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi   

Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Bahi Stuwart Masima akiwa na Paulina Bupamba katibu Ccm wilaya ya Bahi



Mbunge wa Jimbo la Bahi mkoani Dodoma, Kenneth Nollo kwenye mkutano wa Bajeti 

Diwani kata ya Ibugule Blandina Magawa akielezea changamoto ya maji kwenye kata yake


 

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAHI BI.ZAINA MLAWA 

Diwani kata ya Mpamantwa Sosthenes Mpandu Akipongeza kamati ya elimu Bahi kwa matokeo mazuri ya darasa la saba

 

Wajumbe wa mkutano wa bajeti 2025\2026

KATIBU TAWALA WA WILAYA YA BAHI NDUGU. MWANAMVUA BAKARI AKIJITAMBULISHA KWENYE BARAZA LA MADIWA 
Donald Mejiti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi [MNEC]


ENG. HOPENESS LIUNDI MENEJA RUWASA AJIKIBU HOJA ZA MADIWANI WILAYA YA BAHI

HONORINA MKUNDA AFISA MIPANGO HALMASHAURI YA WILAYA YA BAHI AKISOMA TAARIFA YA BAJETI YA MWAKA 2025\2026 KWA NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA BAHI ZAINA MLAWA

 

Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tarehe 29\01\2025  kupitia mkutano wa baraza ,wamejadili na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti mwaka wa fedha 2025\2026

   Tsh.35,977,869,837. Bajeti hii ambayo imelenga kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi ya maendeleo viporo,Utoaji mikopo ya asilimia 10 kupitia mapato ya ndani kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ,kuboresha miundombinu mbalimbali ya Afya na elimu na kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi kwakuviongezea thamani vyanzo vitokanavyo na kilimo Kilimo ,mifugo na Uvuvi ili kuimarisha mapato ya Halmashauri na Wananchi wa wilaya ya Bahi kwa ujumla wake alisema  itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2025\2026

Honorina  Mkunda Afisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Bahi  alisema hayo  wakati akiwakilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi  mtendaji Zaina Mlawa 

      Na. Kadala Komba Bahi

MWISHO