Na. Angel Haule Dodoma
Jeshi la kujenga taifa JKT kimetoa onyo kwa watu wanaogushi vyeti vya Jeshi Hilo vinavyoonesha wamepitia mafunzo ya JKT na kutumia kama sifa ya kuombea kazi sehemu mbalimba Nchini, wakati watu hao hawajawahi Kupitia mafunzo yoyote ndani ya jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Jijini Dodoma Kaimu mkuu wa tawi la utawala JKT KANALI JUMA MRAI amesema,
Hivi karibuni JKT imebaini uwepo wa vyeti vya kugushi vilivyotumika na baadhi ya vijana ambao sio waaminifu ili kujipatia ajira katika taasisi na makampuni yanayohitaji watendaji waliopitia mafunzo ya JKT.
Kaimu Mkuu huyo wa tawi la utawala JKT ameongeza kuwa JKT inapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa, wale wote waliobainika na watakaobainika kugushi cheti Cha JKT kwa matumizi yoyote yale na hatua Kali za kisheria zitachukukiwa dhidi yao
Aidhi KANALI JUMA MRAI amesisitiza kuwa Jeshi la JKT lipo teyale kutoa ushirikiano kwa taasisi na makampuni yote yanayohitaji uhakiki wa vyeti vya JKT kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya jeshi hilo.
Katika hatua nyingine Jeshi la kujenga Taifa JKT Kupitia Kaimu huyo wa tawi la utawala JKT JUMA MRAI limesema jeshi hilo kinaendelea nafasi za kujiunga na mfunzo ya JKT zinatolewa Kila mwaka kwa vijana wa kitanzania wenye sifa , ili wamalizapo mafunzo ya JKT waweze kupata cheti Cha kuhitimu mafunzo hayo kihalali.
![]() |
![]() |
Baadhi ya waandishi wa Habari katika Mkutano makuu na KANALI JUMA MRAI Jijini Dodoma
0 Comments:
Post a Comment