Na. Kadala Komba Bahi
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndugu Boniphace Wilson
akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri
ya Wilaya ya Bahi Bi. Zaina Mlawa ametoa maagizo kwa walimu wa
mazingira na wakuu wa shule za msingi kutunza mazingira ya shule na
kupanda miti ya kutosha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
katika maeneo ya shule zao. Akitoa maagizo hayo ameeleza umuhimu wa
uwepo wa miti shuleni na ujenzi wa madarasa unaozingatia vigezo vya
kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndugu Boniphace Wilson
![]() |
akifunga semina ya mazingira ya siku tatu
Hayo yamejiri wakati wa semina ya mazingira ya siku tatu iliyohusu
mafunzo kwa walimu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
katika shule zao. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya
wilaya ya Bahi.
"Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Boniphace Wilson akifunga mafunzo hayo ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kupitia OR TAMISEMI kwa kuleta mafunzo hayo Bahi pia amewashukuru wafadhili wa program hiyo ambao ni Shule Bora kwa kutoa zaidi ya Milioni mia tatu, kwajili kukamilisha maboma kumi na nane yaliyojengwa kwa kuzingatia vigezo vya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuwezesha mafunzo mbali mbali kwa walimu yakiwepo haya ya mazingira

![]() | |
picha ya pamoja meza kuu |
![]() |
![]() |
![]() |
.Naye Afisa maendeleo ya jamii kata ya Babayu wilaya ya Bahi Nasibu Saidi Amewashukuru wafadhili wa mradi wa mazingira Shule bora kwa kuwakumbuka kata ya Babayu.
0 Comments:
Post a Comment