Na Mwandishi Wetu,, Kondoa
MTU mmoja anashikikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kukamatwa aking'oa bendera na mabango ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa (Bara) Othman Dunga).
Wakizungumzia tukio hilo, Mjumbe wa kamati tendaji CUF wilaya ya Kondoa, Ayubu Hamisi alisema kuwa asubuhi ya Machi 7 mwaka huu, wakati wakiwa katika maandalizi ya kumpokea Makamu Mwenyekiti Othuman Dunga kulitokea jambo la kusikitisha ambapo vijana wanaosadikiwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliingia mitaani na kung'oa bendera 13 na mabango 25 .
Alisema kuwa baada ya kufanya msako waliweza kumkamata kijana mmoja ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliofanya uhalifu huo na sasa anashikiliwa na Jeshi la polisi.
Mwanachama wa Chama hicho, Hadija Selemani alisema kuwa kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimewasikitisha sana. "Tulikuwa tumejiandaa vizuri wanachama wamefika wakiwa wamevalia sare zao vizuri kwa ajili ya kumpokea kiongozi wao lakini kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimetusikitisha sana," alisema na kuongeza.
"Jambo hili limetusikitisha sana kwani kwa mara ya kwanza Kondoa inapata kiongozi mwenye wadhifa mkubwa, lakini wasiotutakia mema ,wameshusha bendera, waking'oa mabango ,kinachofanyiika ni mbinu za kuua siasa za upinzani jambo ambalo limeleta taharuki,"alisema
Mwanachama mwingine wa chama hicho Nassoro Junguke alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitaka kuendeshwa kwa siasa za kistaarabu lakini baadhii ya watu wamekuwa wakifanya vitendo vinavyohatarisha amani iliyopo.
"Wakishusha tena bendera za CUF sisi hatutaenda polisi wataenda wao ,Jambo kama hili halikubaliki katika demokrasia yetu, "alisema.
Pia alisema walifanya msako na kufika hadi nyumba inayoficha wahalifu, walibaini wahalifu waliofanya tukio hilo ambao wamekuwa wakitembea na kapu la kukusanyia bendera wanazong'oa.
Pia alisema Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Kondoa amewafuata na kuwataka waondoe bendera kwenye nguzo.
Alisema kuwa jambo hilo limewatafakarisha sana kwani nguzo nyingi hata mahali panye nyaya bendera za CCM zinapepea lakini bendera za CUF hazitakiwi.
"Watendaji wa serikali wasiingizwe kwenye mitego ya siasa wafanye kazi za kutoa huduma kwa wananchi,"alisema
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara baada ya kupokelewa wilayani Kondoa Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga,, alisema hiyo ni mara ya pili bendera za chama hicho zinang'olewa wakati chama hicho kikiwa na mikutano.
Alisema kuwa tukio kama hilo lilitokea Julai mwaka jana wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipofika Kondoa ambapo bendera zaidi ya 60 ziling'olewa siku moja kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano.
"Huo ni uoga tushindane kwa hoja na sio kung'oa mabango na kuleta taharuki, "Alisema
Dunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kondoa alisema kuwa bendera ni alama ya chama tu .
"Wakati wengine wakihangaika kushusha bendera sisi tunahangaika kutafuta wanachama wapya wajiunge na chama.
Nyie ng'oeni bendera sisi tutaiba nyoyo za watu ili wajiunge kwa wingi na CUF, "alisema.
Dunga alichaguiliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania bara Desemba mwaka jana.
Alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, George Katabazi alisema kuwa taarifa kamili hazijamfikia anafuatilia suala hilo na atatoa taarifa ..Kaption
1.Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa IBara) Othuman Dunga akizungumza na wanachama na wananchi wa wilaya ya Kondoa kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa kwa ajili ya kumpogeza kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ,mnkutano huo ulifanyika katika uwanja wa stendi ya zamani jana.,
2Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taiifa (Bara) Othuman Dunga akiwasalimia wanachama wa CUF wa wilaya ya Kondoa waliokuja kumpokea kwa ajili ya kufanya mkutano wa kumpongeza kwa kucahaguliwa kwake kushika wadhifa huo.
3.Wanawake wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Kondoa wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga (hayupo pichani) baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa kwa ajili ya kupongeza uliofanyika jana
Home »
» ALIYENG'OA BENDERA YA CUF ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
ALIYENG'OA BENDERA YA CUF ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
Related Posts:
MCHUNGAJI DANIEL MGOGO HIZI NDOA HAZIWEZI KUDUMU Mchungaji na Mhubiri maarufu kutoka Tanzania Pastor Daniel Mgogo ametaja aina ya ndoa ambazo kwa mujibu wa mafundisho yake ndoa hizo haziwezi kudumu hata iweje.Kwa mujibu wa Mchungaji Mgogo amesema ndoa lazima zibarikiw… Read More
KAGERA NI SHWARI HAKUNA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA MARBURG Na. WAF - Ziara Mkoani Kagera, BukobaWaziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea katika Kijiji cha Ntoma Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera kwa lengo la kujionea hali inavyoendelea baada ya kutangazwa kuto… Read More
TANZANIA YAKABIDHI MISAADA YA KIBINADAMU KWA SERIKALI YA MALAWINA mwandishi wetuBalozi wa Tanzania Nchini Malawi Mhe. Humphrey Polepole ameshiriki katIka zoezi la kukabidhi misaada ya Kibinadamu kutoka Tanzania kwa Serikali ya Malawi ili kusaidia wahanga wa Kimbunga Freddy.Balozi amekabi… Read More
*TANZANIA NA UNESCO KUDUMISHA MASHIRIKIANO SEKTA YA MAJI*UNESCO- NEW YORKWaziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amekutana na Naibu Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO Bwana Xing Qu ofisi za UNESCO New York kwa lengo la kujadiliana juu ya mahusiano na mashairikiano katika … Read More
*KINANA AWATAKA WAISLAM KUZINGATIA MAADILI MEMA.*Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amewataka Waislamu kuzingatia mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) hususan kuhusu uchamungu na tabia njema.Kinana ameyasema hayo leo Machi 25, 2023 waka… Read More
0 Comments:
Post a Comment