Subscribe Us

WANACHAMA WAPYA 20 WA CUF WAKABIDHIWA KADI

 


Na Mwandishi Wetu, Kondoa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara)  Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua  wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho ili wakazuie bajeti zinazowakandamiza Watanzania.

Akizungumza na wananchi katika uwanja wa stendi ya zamani Dunga aliwataka wananchi kuchagua wabunge na madiwani ili wakazuie bajeti zinaxowakabili wananchi.
Alisema kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.

Alisema kuwa kwa sasa asilimia 99 ya wabunge wanatatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Alisema kuwa iwapo wananchi watakichagua chama hicho, watauza mazao yao vizuri,tofauti na sasa wananchi wanalazimishwa kuuza mazso kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo wamekuwa wakiuza kwa mkopo.


"Hospitali nyingi zimejengwa lakini  hakuna huduma,hakuna dawa  lakini CUF itahakikisha huduma zinaboreshwa hasa vijijini ambapo wananchi wamekuwa wakipata adha kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, "alisema

Alisema kuwa umaskini wa wananchi sio laana ya Mungu , CUF  ikishika dola itafanikisha mambo mengi ikiwemo wazee watapata posho ya kujikimu kila mwezi, "alisema.

Alisema kuwa elimu bure haijaleta matokeo mazuri kwa wananchi kutokana na shule nyingi kuwa na michango mingi inayozidi hata ada zilizoondolewa.


Katika mkutano huo zaidi ya wanachama wapya 20 walikabidhiwa kadi.
Mkazi wa Kondoa, Hamidu Mkopi alitaka wananchi kuziishi 4R za Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwisho




Related Posts:

0 Comments:

Post a Comment