Subscribe Us

RC SENYAMULE AIPA KONGOLE BAHI USIMAMIZI WA FEDHA ZA UJENZI WA MIRADI

 Ikiwa ni miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan kwenye kiti cha Urais na yamefanyika Maendeleo makubwa chanya
Kupitia shamlashamla hizo za miaka minne ya Daktari Samia Suluhu Hassan Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amefanya ziara  Wilaya ya Bahi na kukagua Miundombinu ya hospitali ya Wilaya pamoja na miradi inayotekelezwa Katika Hospitali hiyo ikiwemo ukamilishaji wa mochuali ambao tayari lipo jokofu moja kwaajili ya kuhifadhia miili,pia amekagua jengo la kulazwa wanaume na jengo la kulazwa wanawake,

Kupitia ziara hiyo mkuu wa Mkoa ametembelea pia Zahanati ndogo iliyopo Nagulo kata ya Bahi ambayo ilizindiliwa siku za karibuni na kupitia ukaguzi wake ameridhishwa na huduma kwani Zahanati hiyo kwani imekua msaada mkubwa wa kuwahudumia Wananchi wa Nagulo Bahi waliokua wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule ameipongeza sana Wilaya ya Bahi na uongozi wake kwa jitihada kubwa wanayoifanya ikiwemo usimamizi mzuri wa fedha za ujenzi wa miradi zinazotolewa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, na kupitia ziara hiyo amesisitiza kuwa dhana ya uwajibikaji bora iwe nguzo kuu kwa watumishi wote ili kuweza kuchochea maendeleo chanya ndani ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.


Related Posts:

0 Comments:

Post a Comment