Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekemea Vikali kuhusu upotoshaji mbalimbali unaosambaa kwenye mtandao ya kijamii kuhusu Jeshi la kujenga Taifa na kuwahakikishia Watanzania kuwa JKT ni mahali sahihi na muhimu kwa vijana kuongeza tija katika Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 13,2023 wakati akifunga mafunzo ya 19 kwa mujibu wa Sheria Operesheni ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa, katika viwanja vya 834 KJ Makutupora Jijini Dodoma.
Amesema lengo kuu la vijana kuhudhuria mafunzo hayo ya mujibu wa Sheria ni kuwajengea Uzalendo, Moyo wa Kupenda kazi, kuwapa mbinu za kujitegemea, kujenga umoja na mshikamano utakao imarisha umoja wa kitaifa ili kuwa na Taifa bora lenye ustawi mzuri na viongozi bora wenye fikra chanya kwa Taifa .
"Nimefurahishwa na tamko lenu mlilolitoa leo juu ya upotoshaji mbalimbali juu ya Jeshi la Kujenga Taifa, Nami nawahakikishia Watanzania JKT ni mahali sahihi na muhimu kwa vijana wetu ili kuongeza tija ya utaifa wetu, hivyo mtoto akipata nafasi ya kujiunga na JKT ni fursa nzuri na aitumie" amesisita Senyamule
Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule amewaasa vijana wahitimu hao kuwa na matumizi bora ya mitandao ya kijamii kwa kupata elimu na kufanya biashara za njia ya mtandao.
"Napenda kuwasihi sana mkaitumie mitandao kwa ajili ya kujielimisha na siyo kutumia kuangalia mambo yasiyofaa ambayo ni kinyume na maadili yetu hivyo kuchangia mmomonyoko wa maadili
"Amesisitiza Senyamule
Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo ametumia jukwaa hilo kuwaasa wananchi wanaochoma moto ovyo katika eneo la Kikosi ambalo pia ni eneo oevu la bonde la Mzakwe ambacho ndicho chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatunza mazingira yake.
"Wananchi tunaoishi maeneo ya kuzunguka bonde tafadhali sana tutunze maeneo haya ili tuweze kuwa na uhakika wa maji kwani maji ni Uhai, yeyote atakaye kutwa anafanya shughuli ambazo zinachangia kuharibu mazingira kama uchomaji mkaa, kukata miti na Kilimo atachukuliwa hatua za sheria "amehimiza Senyamule
Kwa Upande Wake, Kaimu Kamanda Kikosi Meja James Andrew Macheta amesema wahitimu hao wamefanikiwa kujifunza Ukakamavu, Utii, Ujasiri, Stadi za Maisha, Ujasiriamali pamoja na ulinzi wa Taifa sambamba na kufanya kazi bila kuchoka sehemu yeyote hivyo wako tayari kutumika kama walinzi sehemu yeyote watakapo hitajika .
Vilevile, amewahasa vijana hao kuwa mabalozi wazuri kwa yote waliyojifunza kwa muda wa miezi mitatu kwa kuwa Wachapakazi na Kutekeleza kwa vitendo yote waliyofunzwa .
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
JKT NI MAHALI SAHIHI NA MUHIMU KWA VIJANA-MHE SENYAMULE
SERIKALI IMEWATAKA WANANCHI KUEPUKA KUINGIZA NA KUTUMIA MAJOKOFU NA VIYOYOZI VYA MTUMBA.
Na Moreen Rojas,
Dodoma.
Sekali imewataka wananchi kuepuka kuingiza nchini na kutumia majokofu au viyoyozi vilivyokiwshatumika (mtumba) ambavyo vinatumia gesi haribifu kwa tabaka la ozoni na badala yake watumie bidhaa zenye uwezo mdogo wa kuchangia ongezeko la joto duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Rais (Muungano Na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo wakati akitoa Tamko kuhusu Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni jijini Dodoma leo Septemba 13, 2023.
Amesema hayo wakati Tanzania ikitarajia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni Septemba 16, 2023 kama kumbukumbu ya tarehe ya kutiwa saini Itifaki ya Montreal ya mwaka 1987 kuhusu kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni ambalo kazi yake kubwa ni kuchuja sehemu kubwa ya mionzi ya jua isifike kwenye uso wa dunia.
Akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa katika utekelezaji wa Mkataba wa Montreal Serikali ilitoa mafunzo kwa maafisa wa mipakani kuwa kutambua vifaa vinavyotumia kemikali haribifu kwa tabaka la ozoni ambalo linapoharibiwa huruhusu mionzi ya jua kufika kwenye uso wa dunia na hivyo kusababisha madhara.
Dkt. Jafo alisema tabaka la ozoni linapoharibiwa husababisha saratani ya ngozi, mtoto wa jicho, upungufu wa kinga dhidi ya maradhi, kujikunja kwa ngozi, kuathirika kwa ukuaji wa mimea pamoja na kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.
Hivyo, alitoa wito kwa wananchi kununua bidhaa zilizowekwa nembo rasmi isemayo “Ozone friendly” au “low global warming potential” au yaani “sahibu wa Ozoni” au “uwezo mdogo wa kuchangia ongezeko la joto duniani”.
Madhara mengine aliyataja kuwa ni kuathirika kwa ukuaji wa mimea vile vile, baadhi ya kemikali hizi husababisha kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.
“Ukiangalia mwaka juzi (2021) kuna kazi mbalimbali zilikuwa zikifanyika kwa mafundi wa majokofu pamoja na kutembelea maduka ili kuhamasisha na kutoa mafunzo kwa mafundi ili waweze kutambua madhara yake na kuchukua hatua,” alisema Jafo.
Mafunzo hayo yalilenga namna ya kudhibiti uingizaji wa kemikali nchini kwa Maafisa wa Idara za Serikali zilizopo katika Mpaka wa Namanga na kutoa elimu kwa wanafunzi wa fani ya viyoyozi katika Chuo cha Ufundi Arusha pamoja na mafundi wa viyoyozi na majokofu kwa mkoa wa Arusha kuhusu namna bora ya kukarabati vifaa hivyo pasipo kuachia angani kemikali na hivyo kuharibu mazingira.
Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni mwaka huu ni “Hifadhi ya tabaka la ozoni na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi” ambayo imechaguliwa kutokana na mafanikio ya kimataifa kupitia utekelezaji wa Itifaki ya Montreal katika kuchangia jitihada za kuhifadhi tabaka la ozoni na kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
VIJANA WAHIMIZWA KUTOKUBALI KUTUMIKA KUVUNJA AMANI.
Na Mwandishi wetu - Dar es salaam
Vijana nchini wamehimizwa kuepuka kutumika na baadhi ya watu wasio na nia njema ili kuvunja Amani ya Nchi hatua itakayosababisha maendeleo ya Taifa kuzorota.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiwasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoshughulikia masuala ya Demokrasia ya Vyama vingi nchini katika Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini na Wadau wa Demokrasia Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na hali ya Siasa Nchini uliofanyika Jijini Dar es salaam.
Dkt. Yonazi amesema vijana wana sehemu kubwa ya kuwajibika kuhakikisha Taifa husika linapata maendeleo na siyo kutumika kwa lengo la kuvunja mshikamano, umoja na upendo ulioanzishwa na waasisi.
“Kuhusu ushiriki wa vijana katika Siasa, Demokrasia na Uongozi Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa, juhudi zinazofanywa na Serikali kuhusu ushiriki wa vijana katika siasa, demokrasia, uongozi, uchumi, ulinzi na usalama wa nchi yetu ziendelee na mikakati mipya ibuniwe ili kuongeza ufanisi na tija,” Amesema Dkt. Yonazi.
Pia ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha Mikakati iliyopo na mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Vijana pamoja na mipango ya kuhamasisha ushiriki wa vijana katika siasa, demokrasia, uongozi, uchumi, ulinzi na usalama wa nchi.
Kuhusu elimu ya uraia Katibu MKuu huyo amebainisha kwamba ipo haja ya elimu ya uraia kutolewa kwa wananchi ili kuwajengea uwezo kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa na kuwa na uelewa wa pamoja wa walengwa na elimu ya mpiga kura ifundishwe katika ngazi zote za mfumo wa elimu kuanzia shule za awali mpaka katika vyuo vya elimu ya juu.
“Serikali na wadau wengine waongeze kiwango cha ufadhili katika kutoa elimu ya uraia ikiwemo elimu ya mpiga kura, ili kukabiliana na upungufu wa rasilimali fedha, watu na vifaa katika kutoa elimu hiyo,” Amebainisha Katibu Mkuu huyo.
Aidha amehimiza ushirikishwaji wa Watu Wenye Ulemavu katika Siasa, Demokrasia na Uongozi kwa kuzifanyia maboresho Sheria zisizozingatia ujumuishwaji wa Watu Wenye Ulemavu akisema huzuia ushiriki wao katika siasa, demokrasia na uongozi ndani ya vyama siasa.
MWISHO
Rais
wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mara baada ya kufungua Mkutano Maalum wa
Baraza la Vyama vya Siasa Nchini na Wadau wa Demikrasia Kutathmini Utekelezaji
wa Mpaendekezo ya Kikosi Kazi na hali ya
Siasa Nchini uliofanyika Jijini Dar es salaam.
MHE. KATAMBI VIJANA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU NA UAMINIFU
Na. Mwandishi wetu – Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amewataka vijana kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kujiepusha na athari za kuwa kwenye kumbukumbu mbaya za utumishi wao.
Aidha, amesema kuwa hali hiyo inakwamisha jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi na kushiriki katika ujenzi wa taifa.
Mhe. Katambi amesema hayo Septemba 8, 2023 Bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Geita Mjini Costantine John Kanyasu lilihoji, Serikali inatambua utaratibu wa Mgodi wa GGML wa ku-blacklist vijana nchini na ni vijana wangapi wapo blacklisted.
Akijibu swali hilo, Mhe. Katambi, amesema Serikali imewahi kupata malalamiko kuhusu vijana ambao wamesitishiwa ajira zao katika mgodi huo na ufuatiliaji uliofanyika haukubaini suala hilo.
Amesema kilichobainika ni kuwa mgodi huo umeweka utaratibu wa kutunza taarifa za kiutendaji na mienendo ya wafanyakazi wake ikiwemo matendo na matukio ya ukiukwaji wa kanuni na taratibu ambayo mfanyakazi anakuwa amefanya katika kipindi cha ajira yake.
Kwa upande mwengine, Mhe. Katambi amewataka vijana ambao wana uhakika utumishi wao katika Mgodi huo bila dosari na wanaweza kuthibitisha kuwa wamekuwa black-listed, kuwasiliana na Ofisi yake ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
MWISHO
WATOTO ZAIDI YA MILIONI 3 KUPATA CHANJO YA POLIO KWENYE MIKOA 6 NCHINI.
Na WAF, Dodoma.
Wizara ya Afya kwa kushirikiana Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wadau wa Sekta ya Afya inatarajia kuendesha Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio kwa watoto zaidi ya Milioni 3,250,598 walio chini ya miaka 8 kwenye Mkoa wa Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Jijini Dodoma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio ambayo inatarajiwa kuanza kufanyika nchini kuanzia Septemba 21 hadi 24, 2023.
Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania inaendesha Kampeni hiyo ya chanjo kutokana na Wizara kupokea taarifa mnamo Mei 26, 2023 za uwepo wa mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja ambaye alionyesha dalili za kupooza kwa ghafla.
Mtoto huyo ambaye alitolewa taarifa kutoka Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa. Uchunguzi wa Maabara ulithibitisha kuwa mtoto huyu ana maambukizi ya virusi cha Polio.
Waziri Ummy amesema kuwa maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Polio yametolewa taarifa pia katika nchi zinazopakana na Tanzania mfano Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia hivyo hali hii inaongeza tishio na hatari ya maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Polio kwa nchi yetu hususani katika Mikoa inayopakana moja kwa moja na nchi hizo.
“Napenda nichukue fursa hii kuwataarifu kuwa tutakuwa na Kampeni maalum ya utoaji wa chanjo ya matone dhidi ya Polio (nOPV2) kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka nane (8). Kampeni hii itafanyika kwa siku nne (4) kuanzia tarehe 21 – 24 Septemba, 2023 katika Mikoa sita (6) inayopakana na nchi zenye mlipuko wa Polio ambayo ni Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya”. Amesema Waziri Ummy.
“Lengo la kampeni hii ni kuwafikia watoto 3,250,598 waliozaliwa baada ya mwaka 2016 ili kuwakinga dhidi ya Kirusi cha Polio aina ya pili (Polio Virus Type 2) kinachoweza kusababisha ulemavu wa kudumu. Kwa Mkoa wa Rukwa tunatarajia kufikia watoto 391,883 Kagera 729,387 Kigoma 884,477 Mbeya 614,346 Katavi 227,862 na Songwe 402,643”. Amefafanua Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema Ili kufanikisha Kampeni hii, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI pamoja na Wadau wa chanjo imeshafanya maandalizi kwa ajili ya kuwezesha zoezi bila kuathiri shughuli zingine za wananchi.
“Wakati wa Kampeni kutakuwa na jumla ya timu yenye jumla ya watoa huduma za afya 5,291 kwa Mikoa yote sita (6) itakayofikiwa na zoezi hili ambapo kila timu itakuwa na watoa huduma watatu. Timu hizi zitakuwa zinatoa huduma ya chanjo kwa walengwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya, nyumba kwa nyumba, shuleni na maeneo mbalimbali ya mikusanyiko ikiwemo Nyumba za Ibada”. ameeleza Waziri Ummy na kutoa rai kwa wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa watoa huduma za afya ili kuwezesha watoto wao kuchanjwa kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amesema katika kuendeleza mikakati ya kutoa chanjo dhidi ya Polio, imeundwa timu ya watu waliopata mafunzo ya kutoa chanjo hiyo katika Mikoa hiyo sita.
“Tumeunda timu nzuri ambayo imepata mafunzo ya kutoa chanjo ambayo ina watoa huduma Elfu Tano Mia Mbili Tisini na Moja (5,291) katika Mikoa hiyo Sita ili kuhakikisha watoto wote wanafikiwa katika kupatiwa Chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio” amesema Prof. Nagu.
“Tunawapa hamasa wazazi wahakikishe kwamba, wanawatoa watoto wao kupata chanjo hii ili kuwaepusha watoto wetu kupata ulemavu ambao kwakweli unakingika kwa kutumia chanjo”. Ameongezea Prof. Nagu.
VIFAA VYA KUJIPIMA UKIMWI MILIONI 1.6 VIMESAMBAZWA NCHINI
Na. WAF - Dodoma
Wizara ya Afya kwa Kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI hadi sasa imeweza kusambaza vifaa vya mtu kujipima mwenyewe maambukizi ya Virusi vya UKIMWI zaidi ya Mil. 1.6 kuanzia Mwaka 2021 nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo kwenye kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi alikua ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuongeza nguvu za kusambaza vifaa hivyo vya watu kujipima wenyewe Virusi vya UKIMWI ili kuweza kutambua hali zao wenyewe na kwa haraka kuhusu ugonjwa huo.
Waziri Ummy amebainisha kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kupanua wigo wa vituo vya kupima na kutoa huduma za matunzo (CTC) kwa watu wenye UKIMWI ambapo hadi sasa tuna vituo 8,529.
“Nitoe rai kwa watu wote wanaoishi na VVU kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI ili kuweza kujilinda wao wenyewe lakini pia kuwalinda wengine” amesisitiza Waziri Ummy.
Pia, Waziri Ummy amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kutoa huduma za kupima, tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU hapa nchini ili vituo vyote vinavyotoa huduma za Afya viwe pia vituo vya kupima na kutoa matunzo (CTC) kwa 95% ifikapo Mwaka 2025.
Aidha, Waziri Ummy amesema chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia, Serikali itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vitendanishi kwaajili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kuendelea kufuatilia taarifa zote kuhusu uwepo wa dawa mpya ambazo ni bora zaidi.
Mwisho, Waziri Ummy amelipongeza Baraza la Taifa la watu wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA) kwa kuanzaa mdahalo wa kuadhimisha Miaka 20, “Sekta ya Afya inatambua mchango wao mkubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI”. Amesema Waziri Ummy
CHUO KIKUU CHA UDOM KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA COLONY
Na Sifa Lubasi, Dodoma
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Colony kilichopo Ujerumani kimefanya
warsha ya watafiti wa kuhifadhi maarifa asilia kwa kuwashirikisha
wataalam kutoka nchi tisa duniani kwa lengo la kubadilishana uzoefu
katika uhifadhi kumbukumbu Kwa vizazi vijavyo.
Makamu Mkuu wa
Chuo hicho Profesa Lughano Kusiluka akizungumza na Waandishi wa habari
kuhusu warsha hiyo alisema kuwa warsha hiyo ina matarajio makubwa katika
kusaidia kuhifadhi maarifa asilia ambayo kwa namna moja au nyingine
yameanza kusahaulika.
Alisemakuwa hilo kutokana na jamii kujikita zaidi Katika elimu ya magharibi.
Alisema
kuwa moja ya mikakati ya kufanikisha hilo kuwa ni pamoja na kufanya
utafiti na kukusanya maarifa ya asili ya Kiafrika kutoka kwa wazee na
jamii za asili na hiyo itasaidia kuhifadhi maarifa na desturi ambazo
zimekuwepo kwa muda mrefu.
Alisema kuwa jamii inatakiwa
kuweka kumbukumbu za mila na desturi za Kiafrika kwa njia ya hadithi,
nyimbo, na ngonjera,kumbukumbu hizo zitatusaidia kuelewa na kuheshimu
urithi na kujifunza kuelewa kalenda za Kiafrika na matukio ya
kihistoria yaliyotokea katika bara la Afrika.
“Watanzania
tunatakiwa kujua kuwa tunaishi katika bara tajiri lenye historia ndefu,
na ni muhimu kuelimisha na kuenzi historia hii,” alisema
Profesa
Kusiluka akielezea kuhusu maono ya UDOM kwa miaka ijayo alisema kuwa
Chuo hicho kinatarajia kulitumia Jengo la Chimwaga kama hifadhi ya lugha
asili za Tanzania na tamaduni mbalimbali jambo litakalo wavutia wengi
na kuwa kivutio cha utalii.
"Kupitia uhifadhi huu
tunategemea kuwashirikisha vijana wetu katika shughuli za kijamii ambazo
zinahusisha tamaduni na urithi wa Kiafrika na Kuwafundisha na
kuwahusisha vijana wetu kutahakikisha kuwa maarifa haya
hayapotei,"amesisitiza Prof.Kusiluka.
Naye mwakilishi wa
Chuo Kikuu cha Colony, Getrude Shnerider alisema kuwa warsha hiyo
inaangazia pia namna ya uhifadhi wa viumbe hai na wanyama
lengo
ni kusaidia jamii kutenga maeneo ya asili kama vile misitu, mabonde na
maeneo mengine ambayo ni muhimu kwa tamaduni na urithi .
Mmoja
wa washiriki katika warsha hiyo ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya
uzamivu(PhD)Adriano Utenga alisema kuwa maarifa ya watu yanatunzwa na
watu wenyewe hivyo kutoa wito kwa watanzania kuungana na nchi nyingine
za Kiafrika kwa njia ya ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa ili kudumisha
umoja na kulinda tamaduni.
Akitoa mfano alisema nchi za Ghana na Senegal zimefanya jitihada kubwa za kuhifadhi tamaduni na urithi zao.
Mwisho
ANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUUWA NCHI WANACHAMA
Na Mwandishi wetu- Dodoma
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika utakaofanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 23 hadi 27 mwaka 2023.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano huo kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu masuala muhimu yatakayojadiliwa.
Dkt. Yonazi amesema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema Nchi wanachama wa jukwaa hilo ni pamoja na Kenya, Uganda, Namibia, Zimbabwe, Eswatini, Msumbiji, Seychelles, Botswana.
Nchi nyingine ni Angola, Zanzibar, Malawi, Lesotho, Mauritius, Zambia na Afrika ya Kusini ambapo mkutano huo utafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Jukumu la Mahakama za Nchi Wanachama katika Utatuzi wa Migogoro chini ya Utangamano wa eneo Huru la Biashara la Afrika: Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa kwa Ufanisi katika Utoaji Haki”
WOWAP WATOA FEDHA TASLIMU KWA WANAFUNZI IKIWA NI MWENDELEZO WA KUSAIDIA WATOTO WA KIKE
Na. Kadala Komba Chemba
Mratibu wa Miradi Women Wake Up(WOWAP) Nasra Sulemani amesema Shirika linajihusisha na utetezi wa haki za wanawake na Watoto pamoja na kuwawezesha watoto vifaa mbalimbali ambavyo huwa tunatoa kwa awamu tofauti kama tulivyofanya katika shule zingine tumetoa mabegi, taa kwa wale wasio na umeme na chupa za kubebea maji pia tunategemea Watoto hao watakua ni wanufaika wa mradi huo ambao wanaenda kuuanza katika shule hiyo kwaiyo kupitia mradi huo tunaomba ushilikiano wenu wananchi na wadau mbalimbali kutoa matokeo mazuri ya mtoto Alisema.
Mratibu Nasra ameyasema hayo alipokuwa kwenye sherehe za kuhitimu wanafunzi wa darasa la saba Wilaya ya Chemba shule ya msingi kelema Balai ikiwa ni mwendelezo wa kutoa Eilimu kwa wazazi namna ya bora ya kuwasaidia Watoto wa kike, leo tumekusanyika hapa kwajili ya shughuli ya maafali ya Watoto wetu kama shirika tumeona ni vyema na sisi kuwa sehemu ya sherehe hizi kwa kuchangia kiasi cha fedha taslimu Elfu Hamsini (50,000 ) ambayo tutamkabidhi mkuu wa shule hii Khalfan Hassan Pamoja na boksi la Biskuti kwa wahitimu wa darasa la saba.
“Tukiwa kama wadau na watetezi wa Watoto wa kike kupitia mradi huu hapa wilaya ya Chemba na kata zake tumekuwa tukifanya hivi takribani miaka mitatu katika shule mbalimbali katika kata mbalimbali kwa awamu tunaona mahitaji yameongezeka kata zimeongezeka wahitaji wameongeza kata ambazo zimeongezeka ni Pranga,Soya kupitia kata hizi tumechangua shule ya Kelema Balai kama shule ya kuanza nayo tunategemea kwamba katika shughuli za utekelezaji wa mradi tutafanya kazi kwa karibu sana na Watoto wa shule hii kwa kuanzisha klabu ya shule kupitia klabu watawapa mafunzo ambayo yatawajenga katika namna ambayo wataendelea kukaa shule kwa muda unaoitajika”
Sambamba na hilo Mratibu wa Miradi Women Wake Up Nasra Sulemani amesema tunatengemea kupata matokeo mazuri sehemu zote ambazo zimepitiwa na mradi , tunasema hivi kwa sababu maeneo ambayo tumefanya mradi tumepata matokeo makubwa ambayo yametupa nguvu ya kusonga mbele kwenye maeneo mengine, tumeona Watoto walio pata elimu kupitia mradi wamefanya vizuri sana katika matokeo yao ya mitihani lakini pia wamejengewa uwezo mzuri wa kujiamini na kujieleza kwasabau wamefanikiwa kuwapeleka kwenye platform mbalimbali ambazo ni za kitaifa na kimataifa na kuwakutanisha na watu muhimu ambao wanaweza kuwajenga wengine walipata nafasi ya kuwenda Bunge na kuhuzulia vipindi mbalimbali vya Bunge, wameenda kwenye mikutano mbalimbali ya kimataifa Dar es salaam, kwaiyo wanategemea kwamba kadri wanavyoendelea kufanya mambo hayo tunaenda kuyafanya na Watoto wa shule hii hivyo basi tunatamani sana wazazi washiriki ili kuona namna gani wanakua ni sehemu muhimu sana ya kusimamia maswara hayo wanayoenda kuyafanya alisema .
Kwaupande wake Mwzeshaji wa mradi Luhaga Makunja Miradi Women Wake Up(WOWAP) ameipongeza shule ya msingi Kelema kwa kuendelea kuwasapoti wanafunzi kwenye vipaji leo tumeona Watoto wadogo walivyoonesha vipaji vyao inamaamisha Kelema kwa siku zijazo tutakuwa na watu wakubwa na tegemezi kwenye nchi yetu ila kama watawatunza Watoto hawa vizuri wataleta mabadiliko makubwa sana, itakuwa ni ajabu miaka 15 mbele kusikia shule hii ya Kelema hakuna madaktari au viongozi wakubwa wanaotoka kwenye shule hii.
“hili safari ya hawa Watoto Kwenda kutimiza ndoto zao hususani Watoto wa kike sio rahisi kama wanavyoichukulia wanasema wamekuwa na vikwazo wao kuweza kutimiza ndoto zao na kila mtoto anandoto na kipaji lakini wanapoanza safari za ndoto zao wanakutana na vikwazo vingi hususani Watoto wa kike wengi wanakatiza masomo”
Mwzeshaji wa mradi Luhaga alisema leo hii itasikitishwa sana tutakaporudi miaka miwili na kusikia yule binti aliekua anaongea pale sana ameacha shule, Lengo kubwa la sisi kufika hapa ni kuhamasisha wazazi na jamii kuchukua hatua kuweza kupunguza hivyo vikwazo ambavyo vinafanya hao Watoto wanaacha shule na Kwenda kuishi Maisha ya utu uzima kabla ya umri wao.
![]() | |
| Mratibu wa Miradi Women Wake Up(WOWAP) Nasra Sulemani akizungumza na wazazi kwenye mahafali ya darasa la saba |
Mwzeshaji wa mradi Luhaga Makunja Miradi Women Wake Up(WOWAP)Mkuu wa shule ya msingi kelema Balai Khalfan Hassan
![]() |
| MATUKIO YA PICHA WANAFUNZI SHULE YA KELEMA |
WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA NAIBU WAZIRI MKUU CHANGAMOTO YA MAFUTA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.
Dotto Biteko aendelee kushughulikia suala la changamoto ya upatikanaji
wa nishati ya mafuta katika maeneo mbalimbali nchini.
“...Watanzania
wapate hii huduma, upatikanaji huu ni muhimu kuhusisha taasisi zote za
mafuta na wanunuaji mafuta kwa pamoja ‘bulk’ wakae pamoja na Wizara
zinazohusika ikiwemo Wizara ya Fedha na Idara ya Ofisi ya Uratibu Ofisi
ya Waziri Mkuu waone namna ya upatikanaji wa mafuta.”
Ametoa
maagizo hayo leo (Alhamisi, Septemba 7, 2023) wakati akijibu swali la
Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi katika kipindi cha maswali kwa Waziri
Mkuu Bungeni Jijini Dodoma. Mbunge huyo alitaka kufahamu ni upi mkakati
wa Serikali katika kuhakikisha Taifa linakuwa na mafuta ya kutosha.
“Lakini
pia tupanue wigo wa waagizaji wa mafuta ili tuwe na mafuta mengi
nchini kwa usalama wa Taifa letu. Na kama hili litafanyika ndani ya wiki
moja tutakuwa tumeshapata majibu na kuwapa taarifa
Watanzania.Tutahakikisha nishati hii ya mafuta inapatikana na Naibu
Waziri Mkuu atashughulikia hilo.”
Wakati huo huo, Waziri Mkuu
ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI iendelee na utaratibu wa kubaini maboma
yote kwenye sekta ya afya na elimu ambayo waliyajenga na
hayakukamilika, wahakikishe wanaendelea kutenga fedha kwa ajili ya
kuyakamilisha kwa sababu yametokana na bajeti zao.
Waziri Mkuu
amesema suala la ujenzi wa miradi ya elimu au afya ambayo inahusisha
majengo ni mkakati ulioelekezwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa
kupitia fedha zinazopelekwa kutoka Serikali Kuu ambazo zinapelekwa
kujenga majengo hayo kwa thamani ya jengo kutokana na makadirio
waliyoyatoa, hivyo wanatakiwa wasimame ujenzi ukamilike kama
ilivyokusudiwa.
Aidha, Waziri Mkuu amesema chanzo kingine ni
fedha inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri zenyewe ambapo wao
hupanga mipango ya maendeo yao kupitia bajeti yao na kwenda kujenga,
maboma mengi yanatokana na mipango yao, hivyo wayakamilishe.
“Uzoefu
tulioupata wakati wa ukaguzi wa miradi hii, majengo ambayo
yametekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu yamekwenda kama yalivyo na
pale ambapo hayakukamilika hatua kali zimechukuliwa. Sasa kwa kuwa
maboma mengi yanatokana na mipango yao na kushindwa kuyaendeleza,
mkakati wa Serikali ni kuhakikisha maboma yote yanakamilika.“
Ametumia
fursa hiyo kuziagiza zifanye tathmini ya miradi yake ione maeneo gani
ambayo walianza miradi na wameshindwa kukamilisha na yamebaki maboma ili
wapange bajeti ya kila mwaka kuhakikisha maboma hayo yanakamilika.
“Halmashauri haziwezi kushindwa kupata shilingi milioni 50 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa zahanati.“
Ameyasema hayo wakati akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga aliyetaka kujua ni nini
mpango wa Serikali katika kuhakikisha inakamilisha maboma ya kutolea
huduma za elimu na afya nchini, miradi iliyoanzishwa na Serikali na
nguvu za wananchi ili wananchi hao waweze kuona thamani ya nguvu yao na
ya fedha za Serikali zinazopelekwa katika maeneo yao.
WOWAP IMEWATAKA WAZAZI KUHAKIKISHA WANASAIDIA KUTIMIZA NDOTO ZA WATOTO WA KIKE.
Mratibu wa Miradi Women Wake Up(WOWAP) Nasra Suleimani ameiasa jamii
kuhakikisha wanasaidia kutimiza ndoto za watoto wa kike ikiwa ni pamoja
na kutokomeza mimba za utotoni na vikwazo vyote ambavyo vinamkuta mtoto
wa kike katika kukwamisha ndoto zake za kufikia kielimu.
Bi.Nasra
ameyasema hayo wilaya ya chemba katika kijiji cha kwamtoro kata ya
kwamtoro kwenye mkutano wa nje na Wazazi wa kijiji hicho kwa lengo la
kuhamasishaji jamii pamoja na kuwapatia Elimu namna bora ya kuwasaidia
watoto wa kike kutimiza ndoto zao kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa
ujumla.
"Tumekuwa tukiufanya mradi huu kwa nguvu kubwa katika
mashule lakini kutoka na ambavyo tumekuwa tukipata mrejesho kutoka kwa
wanafunzi namna ambavyo wazazi wamekuwa hawana ukaribu na watoto wao,
hivyo tukasema tunahaja ya kuhakikisha kwamba sasa tunakwenda kuwafikia
wazazi hivyo leo tuko hapa kuhakikisha tunaongea na wazazi na tumefanya
mkutano wa hadhara na wazazi na wamepata elimu vizuri na tunategemea
basi kupitia elimu hii waliyoipata leo wataenda kuwa sehemu ya chachu ya
kuhakikisha kwamba wanaweza kuzifanyia kazi zile changamoto za mtoto wa
kike ambazo wanazipata katika majumba yao na katika ngazi ya familia
ili kuhakikisha mtoto wa kike anafanya vizuri katika kutimiza ndoto
zake" Amesisitiza Bi.Nasra
Aidha ametoa Wito kwa jamii
kuhakikisha wanalea watoto wa kike vizuri kwani suala la malezi sio la
shule peke yake wala mashirika peke yake bali wazazi ndio watu wa kwanza
kabisa na wao ndio wanatumia nafasi kubwa ya kuaminika na watoto hivyo
imani yangu kupitia mkutano huu utaleta mabadiliko makubwa na watoto
watakuwa wamefurahi kwani ni sehemu ambayo wamekwenda kutekeleza zile
changamoto ambazo wamekuwa wakiwaletea katika mradi huu tangu wameuanza.
Kwa upande wake Luhaga Makunja ambaye ni mwezeshaji women wake
up amesema kuwa dhumuni la mkutano huo ni kuwahamasisha wazazi kutatua
vikwazo vinavyosababisha watoto wadogo hususani ni wasichana kukatiza
masomo yao ambapo wameweza kuongelea vikwazo vilivyopo katika jamii
wanaposhindwa kuwaunga mkono watoto wa kike waliokatisha masomo
kutokana na ujauzito ambapo hivi sasa sharia inawaruhusu kuendelea na
masomo baada ya miaka miwili lakini bado changamoto kubwa imekuwa upande
wa wazazi na jamii.
"Kumekuwa na dhana mbaya kwa jamii na
mtazamo hasi kwa jamii kwamba mwanafunzi ambaye alishapata mimba
anaporudi shuleni kunakuwa na mazingira yakukatisha tamaa wenzao
kuwazomea na kukosa mahitaji muhimu na kuweza kuboresha mazingira ya
shuleni ili waendelee na masomo na kutimiza ndoto zao"
Aidha
ameongeza kuwa wazazi wanaunga mkono hili jambo ila wanashauri Serikali
kuwatengea shule maalumu na madarasa maalumu ili kuepuka mazingira
ambayo yanafanya washindwe kuchangamana na wale wanafunzi wengine ambao
wako shuleni hivyo wazazi wamesema watahimizana kuweza kuwafikia watoto
wa kike mashuleni ikiwa ni nia ya kutoa elimu kuhusiana na stadi za
maisha na kuweza kuchukua hatua stahiki na kuweza kuepuka mimba
zisizotarajiwa na makundi yanayoweza kuwapotosha.
Sambamba na
hilo Afisa Mtendaji wa kata ya kwamtoro Evaresto Mahenge amesema
wanaishukuru team ya women wake up kwa mafunzo waliyofanya kwenye kata
yake anaimani yatawasaidia watoto wa kike kufikia ndoto zao
kielimu,elimu hii itaenda kuwa chachu kwa wazazi kwa sababu elimu hii
imewahamasisha wazazi hivyo wataenda kupambana kuhakikisha wanamsimamia
mtoto wa kike katika harakati zake za masomo,itakuwa ni chachu kwa
wanafunzi wengine ambao waliacha shule kwa muda kutokana na changamoto
mbalimbali ambao watafutiliwa na kurudishwa mashuleni na kutimiza
malengo yao.
Kwa upande wake Mwasiti Issa ambaye ni mzazi katika
kijiji cha kwa mtoro amelishukuru shirika la women wake up kwa kutoa
elimu ya kuelimisha watoto wa kike kujizua kujihususha na anasa pamoja
na mambo mabaya na kuhakikisha wanongea nao na kuwakusanya kuongea nao
na kuwaelimisha madhara ya mimba za utotoni.
Sanjari na hayo
Tizo Wambura ambaye ni mkazi wa kijiji cha kwamtoro ambaye pia ni
mwanakamati wa shule ya msingi kwamtoro wamelishukuru shirika hilo kwa
semina ya malezi au makuzi ya mtoto wa kike katika jamii na kama
kiongozi anaahidi kuendelea kutoa semina mashuleni lakini pia mahali
popote ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa watu katika viahatarishi ambapo
wakipata elimu hii itaweza kuwasaidia na kuweza kuijenga jamii iliyo
bora.
![]() | |
| Mratibu wa Miradi Women Wake Up (WOWAP) Nasra Suleimani akizungumza na wazazi wilaya ya Chemba katika kijiji cha kwamtoro kata ya kwamtoro kwenye mkutano |
![]() |
Mratibu wa Miradi Women Wake Up (WOWAP) Nasra SuleimaniAkiwa amesimama mkono wake wa kushoto ni Alwino Alois Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwamtoro na kulia kwake ni Hassan Hussen Mwenyekiti wa mtaa wa kwamtoro akifatiwa na Afisa Mtendaji wa kata ya kwamtoro Evaresto Mahenge mwisho kabisa ni Luhaga Makunja ambaye ni mwezeshaji women wake up
Wazazi wakichangia jambo kwanye mkutano wa Shirika la Women Wake Up







































