Home »
» MKURUGENZI WA MASHTAKA MWAKITALU AMETEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA DODOMA
MKURUGENZI WA MASHTAKA MWAKITALU AMETEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA DODOMA
Na. Mwandishi wetu Dodoma
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ametembelea Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Maafisa wa Magereza katika kuwatunza wafungwa pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili mahabusu.
Akizungumza baada ya kutembelea Gereza Kuu la Isanga Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa lengo la kutembelea wafungwa na mahabusu ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa misingi ya sheria na kanuni zake.
'’kufanya haya yote ni kuona haki jinai inasimamiwa ipasavyo lakini tukipata hizi changamoto na kuzisikiliza tunaenda kuzifanyia kazi na kuzishughulikia. Changamoto tulizozipokea ambazo hazipo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka tunazichukua na kuzipeleka ofisi ambazo zinahusika lengo ikiwa ni kuona Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo.Amesema DPP Mwakitalu
Hata hivyo,Mwakitalu amezitaja changamoto ambazo amezipokea katika ziara yake ambapo mahabusu wamezieleza ikiwa ni sula zima la ucheleweshwaji wa kesi na kuchelewa kwa upelelezi ambapo ameeleza kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kuzishughulikia changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa wameshasajili Hati za Mashtaka Mahakama Kuu ambazo hivi sasa zipo katika mchakato wa kusikilizwa.
'’Mahabusu wengi ambao nimewasikiliza wamesema kesi zao zimechelewa upelelezi ,lakini hali halisi ni kwamba kesi zao hazijachelewa upelelezi kwa kuwa tayari zimekamilika na kinachosubiriwa ni utaratibu wa kisheria ambao utawezesha kesi hizo kusikilizwa na Mahakama Kuu Amesema DPP Mwakitalu.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka nchini imeanza mwendelezo wa ziara zake katika Magereza mbalimbali nchini kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa wa Magereza, wafungwa pamoja na mahabusu ili kuhakikisha Haki Jinai inasimamiwa ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Mwisho.
Related Posts:
JIFUNZE KUHUSU MTI UNAFUNDISHA MENGI Na.Mwl Triple J. "Basi *KWA MTINI JIFUNZENI* mfano; *TAWI LAKE likiisha KUCHIPUKA NA KUCHANUA MAJANI* , mwatambua ya kuwa *WAKATI WA MAVUNO U KARIBU"*(Mathayo 24:32) ...MAISHA Ya MWANADAMU ni Kama MTI, Matendo Yake … Read More
CHAMWINO YAJIWEKEA MPANGO MKAKATI WA KUONDOA ZIRO MASHULENINa Peter Mkwavila CHAMWINO. MKUU wa wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Gift Msuya amesema kuwa ili kuepukana na ziro shule za masingi na sekondari wamejiwekea mpango mkakati wa kuwasaka watoto wasioenda shule na ikiwemo na k… Read More
NBS IDADI YA WATALII WALIOINGIA NCHINI YAONGEZEKA HADI ASLIMIA 62.7. Na.Kadala Komba Dodoma OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema kuwa idadi ya watalii walioingia nchini kuanzia Januari hadi Julai yaongezeka hadi kufikia 742,133 ikilinganishwa na 456,266 kwa kipindi Cha mwaka 2021, saw… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 17, 2022… Read More
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 18, 2022… Read More
0 Comments:
Post a Comment