Home »
» TIMU YA MBEYA CITY YAKABIDHI ZAWADI KWA WAGONJWA KATIKA KITENGO CHA WAZAZI META.
TIMU YA MBEYA CITY YAKABIDHI ZAWADI KWA WAGONJWA KATIKA KITENGO CHA WAZAZI META.
Na.Mwandishi wetu Mbeya
Katika kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka, ikiwemo Krismas na Mwaka mpya timu ya Mpira wa Miguu ya Mbeya City ikiongozwa na viongozi wake wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Kitengo cha Wazazi META kwaajili ya kutoa zawadi na kuwafariji wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kurudusha kwa jamii.
Akiongea kwa niaba ya Uongozi wa Timu ya Mbeya City, Paul Nonga mcheza wa timu hiyo amesema hii ni sehemu ya utaratibu wao kama timu lengo likiwa ni kurudisha kwa jamii, hivyo wametembelea Hospitalini hapo kwa lengo la kuwafariji wagonjwa pamoja na kutoa zawadi zikiwemo Sabuni, Mashuka 50, Dawa za Meno, mafuta, pamoja na Mifuko maalumu kwaajili ya kubebea vitu.
“Timu ya Mbeya City pamoja na Mdhamini wetu (Peri March) tumeweza kukabidhi Mashuka 50, na hii ni moja ya vitu huwa tunavifanya kwaajili ya Kurudisha kwa jamii.” – Paul Nonga.
Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha Wazazi Meta, Muuguzi wa Zamu Bi. Fatuma Saimoni ameushuru uongozi wa Timu hiyo na kuwasihi wandelee kuwa na moyo huo wa upendo wa jamii.
“Kwa hiyo tunashukuru kwa watu wa Mbeya City kwa kweli mna upendo, sisi kama wana META tunawashukuru sana Mungu aendelee kuwabariki kwa upendo huu.” - Fatuma Saimoni
MATUKIO YA PICHA TIMU YA MPIRA WA MIGUU MBEYA CITY WAKIWA NA VIONGOZI WAKITEMBELEA HOSPITAL YA RUFAA KANDA YA KATI KITENGO CHA WAZAZI
0 Comments:
Post a Comment