Home »
» WACHAKATAJI WA MAZAO YA UVUVI WAPIGWA MSASA
WACHAKATAJI WA MAZAO YA UVUVI WAPIGWA MSASA
WACHAKATAJI WA MAZAO YA UVUVI WAPIGWA MSASA.
Wachakataji wa mazao ya uvuvi nchini wametakiwa kutumia fursa ya teknolojia katika shughuli zao ili kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi na kukabiliana na upotevu wa mazao hayo katika Ziwa Tanganyika.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wachakataji, wavuvi na wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kupitia miradi yake ya FISH4ACP na Flexible Multi-partner Mechanism (FMM) mafunzo ambayo yamefanyika mkoani Kigoma.
Afisa huyo amesema mradi wa FISH4ACP unatekelezwa katika nchi 12 za Africa, Caribbean na Pacific ambapo nchini Tanzania unafanyika katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ukilenga kukabiliana na changamoto za upotevu wa mazao ya samaki kabla na baada ya shughuli za uvuvi, wakati wa uchakataji wa samaki na wakati wa kusafirishwa kwenda kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
“Mafunzo haya yamefanyika kwa njia ya filamu zilizonakiliwa kutoka Kenya, Uganda na Ghana lengo ni kuwawezesha wachakataji kujifunza njia bora za kuchakata mazao yao kama tulivyoona kwa wenzetu wanatumia majiko banifu, chanja rafiki na salama za kuanikia dagaa,”Amesema Afisa huyo.
Pia ameongeza kuwa kupitia miradi hiyo wanatarajia kujenga miundo mbinu ya kuchakatia dagaa na samaki itakayoendana na mabadiliko ya tabia Nchi ambapo kwa sasa hatua zilizochukuliwa ni ufuatiliaji wa maeneo sahihi ya kuchakatia.
“Kama mradi tutatengeneza majiko ya kubanikia samaki tupate bidhaa nzuri kutoka Ziwa Tanganyika na tutaendelea na ufuatiliaji kuona kama mafunzo haya yanatafanya kazi kama tulivyokusudia na yatasaidia changamoto iliyopo sasa ya mabadiliko ya tabianchi ,”Ameeleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia masuala la Udhibiti Ubora wa Mazao ya Uvuvi na Masoko, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bw. Steven Lukanga amebainsiha kuwa sekta ya uvuvi inachangia karibu asilimia 1.8 ya pato la Taifa wakati ulaji ukichangia asilimi 30 ya virutubishi vitokanavyo na wanyama.
“Ulaji wetu unaonekana tunakula wastani wa kilo 8. 5 badala ya kilo 20.5 kwa mwaka hivyo mafunzo haya yamekuja wakati muafaka yatasaidia kuboresha shughuli zetu tunazofanya hasa unapovua samaki wako au dagaa uhakikishe unawahifadhi sehemu salama na hata ukaushaji wetu uwe wenye manufaa kimasoko,”Amefafanua.
Naye Afisa Uvuvi anayesimamia Wilaya ya Uvinza Bw. Venance Msongambele amesema elimu hiyo itawasaidia wadau wa uvuvi na wachakataji kuepuka kufanya kazi kwa mazoea, na badala yake watakausha samaki kwa kutumia mkaa hatua inayoongeza thamani ya mazao hayo na kuvutia wateja.
“Kuna maboresho ambayo yakifanyika yatatusaidia sana kama kupata barafu kuhifadhi samaki na dagaa, majiko ya mkaa kwa sababu kuni siyo salama kwa afya kutokana na moshi na kupitia mafunzo haya tumejifunza kufanya uchakataji kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira,”Ameeleza Afisa huyo.
Akitoa shukrani zake Mchakataji kutoka Mwalo wa Katonga mkoani Kigoma Selestina Silvester ameipongeza FAO kwa kuandaa semina hiyo kwani itawasaidia katika uhifadhi wa rasilimali za Ziwa Tanganyika kwa manufaa yao na Nchi kwa ujumla.
“Tunaishukuru sana FAO kwa kutoa na elimu hii inatusogeza kutoka hapa tulipo hadi sehemu nyingine kwa sasa uchakataji tunafanya kienyeji sasa unakuta samaki au dagaa wanaharibika haraka kabla ya kufika sokoni na wanapungua ubora,”Amesema Selestina. Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin
Aidha Mwenyekiti wa Vyama vya Wavuvi Mkoa wa Kigoma Bwa. Francis John amewahimiza wadau hao kutumia ujio wa mradi huo kama fursa muhimu kwao kuongeza thamani ya bidhaa zao ili kuendana na hali ya soko la sasa.
MWISHO
Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia masuala la Udhibiti Ubora wa Mazao ya Uvuvi na Masoko, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bw. Steven Lukanga akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wachakataji wa mazao ya uvuvi Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma (kulia ) ni Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin .
Picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo.
Baadhi ya wadau wa sekta ya uvuvi wakiafuatilia mafunzo hayo kutoka kwa wawezeshaji(hawapo pichani).
Afisa Mtaalam Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji Hashim Muumin akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wachakataji wa mazao ya uvuvi mkoani Kigoma.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mwalo wa Kibirizi mkoani Kigoma wakiendelea na biashara zao.
Related Posts:
BAHI YAFUNGUA MILANGO KWA WANAFUNZI WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU. Na Kadala Komba- Dodoma Diwani wa Kata ya Mpamatwa, Sosthenes Mpandu amewataka wanafunzi kusoma kwa juhudi na kujiamini ili kufanya vizuri katika mitihani yao hatimaye waweze kujiunga na masomo ya elimu ya juu.… Read More
NAIBU WAZIRI MERYPRICA MAHUNDI AMETOA OYO KALI KWA WALE WANAOCHEPUSHA MAJI Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akizungumza kwenye kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta inayoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 na wanan… Read More
RAIS SAMIA KUZINDUA MATOKEO YA SENSA NA MUONGOZO WA MATUMIZI YA MATOKEO HAYO JIJINI DODOMANa. Kadala Komba Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo … Read More
NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAJI ATEMBELEA MKOA WA KIGOMA Na Mwandishi wetu Kigoma Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea Mradi wa Kuboresha Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Kigoma. Mradi huu unatumia ziwa Tanganyika kama chanzo cha maji, katik… Read More
KATAMBI AMEWATAKA VIJANA KUJITAMBUA NA KUTHUBUTUNa. Kadala Komba Dodoma Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, amewataka vijana kujitabua ,kuwa na uthubutu pamoja na kujiwekea malengo ,Amesema uwezi ku… Read More
0 Comments:
Post a Comment