Home »
» JAMII YAHIMIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA DAWA
JAMII YAHIMIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA DAWA
Na Kadala Komba- Dodoma
JAMII YAHIMIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA DAWA
Jamii imeaswa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya utumiaji dawa za binadamu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo usugu wa dawa hizo mwilini.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali (RBA-Initiative), Michael Mosha, Jijini Dodoma wakati wa mwendelezo wa kampeni ya kuongeza uelewa kuhusu Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa ambayo hufanyika Duniani kote kila ifikapo Novemba 18 hadi 24 Novemba kila mwaka.
Amesema kama shirika limekuwa likifanya hivyo mara kwa mara kwa kuwashirikiana na Shule mbalimbali na watoa huduma za Afya, wakulima na wafugaji, akisema kuwa Vimelea vya magonjwa havina mipaka vinampata kila mtu bila kujali kabila wala rangi.
“Tunatoa elimu hii kwa njia mbalimbali kama vipeperushi, usafiri wa Bajaji ambapo zimebandikwa vipeperushi vinavyozungumzia Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa lugha ya kiswahili na maeneo ya kimkakati kama stendi ya mabasi Nane Nane, Soko kuu la Machinga Complex Dodoma na maeneo mengine tukitoa elimu,”Amesema Mratibu huyo.
Pia Mratibu huyo ametoa wito kwa wananchi na jamii kwa ujumla kufuata kanuni nzuri ya matumizi ya dawa kwa wakati sahihi na ulioshauriwa na daktari.
Kwa upande wake Mfamasia kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Bakir Hussen ameeleza kuwa kampeni hii inafanyika Dunia nzima kwa kutoa elimu ya uelewa kuhusu usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa,
“Kupitia shirika hili tunatumia vyombo vya moto kama daladala, bajaji na kugawa vipeperushi maeneo sambamba na mashuleni kwa kuanzisha Club kwenye shule hizo kwa lengo moja kila mtu apate elimu hii,”Ameeleza Mfamasia huyo.
Aidha Mwalimu mlezi wa RBA-Club kutoka Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege Bwa. Musa Sulemani amesema tangu kuanzishwa kwa Programu hiyo shuleni imesaidia kuleta mabadiliko kitabia kwa wanafunzi kuanzia wanafunzi wa shule za Msingi hadi Sekondari.
Naye Mwalimu wa Shule ya Meriwa, Bw. Brighton Nashon amesema mwanzoni kulikuwa na mwitikio mdogo lakini baada ya kuendelea kuwapatia Elimu sasa wanafunzi wamekuwa na mwitikio mzuri uliyopelekea baadhi yao kutunga nyimbo zenye ujumbe juu ya matumizi sahihi ya Dawa
Nao Madereva Bajiji Haule Mkwasa na Abusasani Bundala wamelipongeza shirika la RBA Kwa kuwathamini na kutambua mchango wao katika jamii kwa kuwapatia mafunzo kwa vitendo iliyoambatana na matembezi katika jiji la Dodoma.
“Matembezi yamefanyika kuzunguka Dodoma na viunga vyake tukiendesha bajaji zetu zilizobandikwa mabango yaliyobeba ujumbe kwa lengo la kuigusa jamii moja kwa moja kuchukua tahadhari,” Wameeleza madereva hayo.
Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali (RBA-Initiative), Michael Mosha Akitoa Elimu kuhusu Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa
Mfamasia kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Bakir Hussen akieleza Madhara ambayo Binadamu anawedha kupata asipofuata ushauri wa daktari
Mwalimu mlezi wa RBA-Club kutoka Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege Bwa. Musa Suleman Akielezia faida ya Elimu hii mashuleni
Mwalimu wa Shule ya Meriwa, Bw. Brighton Nashon mwitikio mzuri kwa wanafunzi
Madereva Bajiji Haule Mkwasa na Abusasani Bundala Wakilipongeza shirika la RBA kwa kuwakumbuka Madereva Bajaji
PICHA YA PAMOJA VIONGOZI WA RBA NA MADEREVA BAJAJI KATIKA UKUMBI WA DEA MAMA JIJINI DODOMA
DAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WALIYOTUNUKIWA VYETI KWA KUTAMBUA MCHONGO WA VYOMBO VYA HABARI
WANANCHI WA DODOMA WAKIPATIWA VIPEPERUSHI KATIKA MAENENO TOFAUTI
0 Comments:
Post a Comment