Home »
» MKUU WA MKOA DODOMA MHE. ROSEMARY SENYAMULE AMEPOKEA HATI YA PONGEZI KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI GEITA
MKUU WA MKOA DODOMA MHE. ROSEMARY SENYAMULE AMEPOKEA HATI YA PONGEZI KUTOKA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI GEITA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea hati ya pongezi kutoka kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita kwa kutambua mchango wake na kuleta mageuzi katika kipindi ambacho amekua Mkuu wa Mkoa huo.
Hati hiyo imewasilishwa leo tarehe 19/12/2022 na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita Bw. Renatus Masuguliko akiambatana na Katibu wake Bw. Novatus Lyaruu.
Bw. Masuguliko amesema kwa takribani mwaka mmoja ambao Mhe. Mkuu wa Mkoa Bi. Senyamule amekuwa mkoani Geita, amefanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika sekta zote na kumpongeza kwa kusimamia kwa vitendo kaulimbiu aliyoianzisha ya “Geita ya dhahabu, Utajiri wa heshima”
“Mkuu wetu wa Mkoa Mhe. Senyamule alivyokuja na hii kaulimbiu mwanzoni hatukumuelewa, lakini kwa kipindi kifupi amefanya mengi katika sekta ya elimu, afya, miundombinu, maji, uchumi na uzalishaji, hivyo watu wa Dodoma mna bahati ya kupata kiongozi mahiri” Amesisitiza Bw. Masuguliko.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amekishukuru Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Geita kwa kumpa tuzo ya heshima kwa kutambua mchango alioutoa akiwa Geita.
Amepongeza uongozi wa Chama hicho kwa kuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi kwa weledi na maarifa na kusisitiza kuwa kazi hiyo iwe endelevu ili jamii iweze kunufaika na kufahamu mambo ambayo Serikali imekuwa ikitekeleza katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma Bw. Mussa Yusuph na Katibu wake Bw. Ben Bago ambao pia waliambatana na ugeni huo kutoka Geita, wamesema jitahada zinaendelea ili Makao Makuu ya Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania yahamie katika Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipokea hati ya pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita Bw. Renatus Masuguliko kwa kutambua mchango wake na kuleta mageuzi kwa kipindi ambacho alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Hati hiyo ya pongezi amekabidhiwa leo tarehe 19/12/2022 Ofisini kwake Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita na Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kupokea hati ya pongezi ya kutambua mchango wake na kuleta mageuzi kwa kipindi ambacho alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita Bw. Renatus Masuguliko, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma Bw. Mussa Yusuph, Bw. Novatus Lyaruu Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita na Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma Ben Bago.
Related Posts:
BAJETI YA MWAKA 2025\2026 SHILING BILION 35.9 YAPITISHWA BAHI KWA KISHINDO Kusho ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Bahi Zaina Mlawa katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Joachim Nyingo mwisho ni Donald Mejiti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi [MNEC] Kikao cha Baraza la Madiwani cha kupokea ,ku… Read More
MKURUGENZI WA FEMAPO MATHIAS LYAMUNDA AMECHANGIA MILIONI 1 SHULE YA MSINGI BAHINa. Kadala Komba Bahi Mathias Lyamunda Mkurungenzi wa Shirika la Foundation for environmental Management and Campaign Against Poverty-(FEMAPO), amechangia Shilingi Milioni moja (1,000,000/: taslimu kwajili ya maendeleo ya shu… Read More
NOTISI YA KUONDOA KWENYE MZUNGUKO NOTI ZA ZAMANI ZA SHILINGI ZILIZOTOLEWA KUANZIA MWAKA 1985 HADI 2003 NA NOTI YA SHILINGI MIA TANO ILIYOTOLEWAMWAKA 2010, YA MWAKA 2024 … Read More
MAKATIBU WAKUU NA WADAU WA TANZANIA SAFARI CHANNEL WAKUTANA DODOMA Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na wadau wa televisheni ya Tanzania Safari Channel wamekutana kuzungumzia uendeshaji wa Chaneli ya Utalii ya Tanzania Safari Channel inayomilikiwa na Shirika la Utang… Read More
*FURSA KWA WANAWAKE KUKOPA DOWOSA RIBA ASILIMIA 1 KWA MWEZI*Na. Kadala Komba Dodoma Mhe. Mbonipaye Mpango Mwenza wa Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Amewataka wanawake kujiunga na DODOMA WOMEN SACCOS (DOWOSA) kwa maendeleo ya uchumi wetu Dowosa ni Saccos ya ku… Read More
0 Comments:
Post a Comment