Home »
» “UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA” DK. JINGU
“UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA” DK. JINGU
“UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA” DK. JINGU
NA MWANDISHI WETU - DODOMA
Watafiti wa masuala ya kilimo nchini wametakiwa kutumia matokeo ya utafiti wao wanaofanya katika kuboresha mbegu bora za mazao zinazoendana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwa na tija katika sekta .
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu wakati akifungua warsha ya kuelimisha wadau kuhusu Kazi za Muunganiko wa Taasisi za Kimataifa za Utafiti wa Kilimo (CGIAR) Jijini Dodoma.
Dk. Jingu amesema lengo kuu la warsha hiyo ni kuongeza kasi ya utekelezaji wa programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kwa kuboresha uratibu wa miradi ya OneCGIAR kwa kuzingatia utafiti utakaongeza uzalishaji.
“Kupitia Mkakati wa Utafiti na Ubunifu wa Mwaka 2030 CGIAR imeanzisha mkakati unaojulikana kama OneCGIAR ambao unalenga kufanya utafiti na maendeleo sasa ili tukuze sekta zetu za kilimo, mifugo na uvuvi lazima tuwekeze katika utafiti na maendeleo hivyo mkakati huu utasaidia katika uzalishaji na tija,” Amesema Katibu Mkuu huyo.
Pia alihimiza kwamba utafiti wa mbegu unaofanyika usaidie kuleta tija na faida katika shughuli za wakulima, wavuvi na wafugaji pamoja na kuendeleza ugunduzi wa mbegu mpya hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa.
“Hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo utafiti tunaoufanya uendane na hali ya hewa ya kipindi husika ukizingatia sasa hivi misimu ya mvua imebadilika kwahiyo tunahitaji mbegu zinazoendana na mazingira na namna ya kukabiliana na wadudu waharibifu,”Alieleza .
Katika hatua nyingine alisisitiza ushirikishwaji wa vijana katika sekta ya kilimo akisema licha ya uwepo wa sekta zingine kilimo kitaweza kustawi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi endapo vijana watawezeshwa kikamilifu.
“Vijana ili washiriki vizuri kilimo wanahitaji elimu , mafunzo kwa vitendo na namna ya kutumia fursa ya ukuaji wa teknolojia katika shughuli zao za uzalishaji wenye matokeo chanya na wafanye kwa tija itasaidia vijana kujikwamua kiuchumi wao wenyewe na kushiriki katika pato la Taifa,”Alisisistza Dk. Jingu.
Aidha alishauri uwepo wa ushirikiano kati ya Wizara za kisekta na wadau wa maendeleo kwa kuanzisha miradi mikubwa itakayoleta matokeo chanya katika sekta hizo muhimu kupitia mkakati huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Dk. Geoffrey Mkamilo alibainisha kwamba kufanyika kwa utafiti wa mbegu kunasaidia kubaini hali ya mbegu, changamoto na namna ya kuboresha uzalishaji wake utakaoendana na kipindi husika.
“Warsha hii inatuweka pamoja kama wataalamu na wizara za kisekta kubalishana uzoefu na namna ya kufanya utafiti wenye manufaa katika sekta zote za kilimo. Mifugo na uvuvi kubaini mbegu bora na wakati husika wa kuzifanyia kazi ziweze kuzalisha mazao bora kwa jili ya kuimarisha lishe na kipato,”alieleza Mkurugenzi.
Naye Mtaalamu kutoka OneCGIAR Dk. Regina Kapinga alifafanua kwamba licha ya kufanya utafiti unaowezesha mazao kuhimili mabadiliko ya tabia nchi pia unazingatia uboreshaji wa virutubishi katika mazao ya uvuvi, mifugo na mimea.
MWISHO
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya kuelimisha wadau kuhusu Kazi za Muunganiko wa Taasisi za Kimataifa za Utafiti wa Kilimo (CGIAR) iliyofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akitembelea mabanda baada ya kufungua warsha hiyo
Related Posts:
TUENDELEE KUUNGANA KUKABILIANA NA MAAFA NCHINI” MKURUGENZI MSAIDIZI JANE NA. MWANDISHI WETUMkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Jane Kikunya amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikia… Read More
TUNAIOMBA SERIKALI ITUSAIDIE KUFUNGIA MAKAMPUNI BUBU(UKUTA). Na Moreen Rojas,Dodoma.Umoja wa makampuni binafsi ya ulinzi Tanzania (UKUTA) wameiomba serikali kufungia makampuni bubu kwani wanafungua kampuni hizo bila kufuata sheria jambo ambalo ni sawasawa na kuhujumu uchumi… Read More
UNDP YAZINDUA WAZO LA KIBUNIFU LA MATUMIZI BORA YA NISHATI NCHINI. Na Moreen Rojas,Dodoma.Shirika la Maendeleo la Kimataifa UNDP limezindua wazo la kibunifu la matumizi bora ya Nishati nchini.Akizungumza na vyombo vya habari Machi 15,2024 jijini Dodoma Mtaalamu mshauri wa Shirika hilo … Read More
REA YATOA ELIMU YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA. Na Moreen Rojas,Dodoma.Viongozi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB); Mhe. Balozi na Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu, Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Hassan Saidy … Read More
HATUKUBALIANI NA SHERIA YA WENZA WA VIONGOZI KULIPWA MAFAO "CHADEMA". Na Moreen Rojas,DodomaCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepinga kitendo cha Bunge kupitisha sheria ya wenza wa viongozi kulipwa mafao huku kikishauri kufanyiwa kwa marejeo ya sheria ya Kikokotoo ambacho kime… Read More
0 Comments:
Post a Comment